Maokoto, maokotaji na maokotezi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,929
Mwenda tezi na omo marejeo ngamani.. Ni rahisi kwa ngamia(sio mnyama) kupenya kwenye tundu la sindano (kwa waamini na waaminio) kuliko tajiri kuingia kwenye ufalme wa Mungu...!

Maokoto
Haya yako kila mahali.. Zamani tuliaswa si kila kitu ni cha kuokota japo waswahel walisema cha kuokota si cha kukwiba bali mwenye mali ni mjinga! Je akiwa mwerevu?
Kuna maokoto hayaokotwi, mengine ni matego, mengine ni magunia ya chawa mengine ni mimba zilizoharibika na mengine ni ya wezi huku mengine yakiwa ni ulimbo kwenye ndoano unasiane ushindwe kujua pa kutokea
Maokoto mabaya yote ni yale yatembeayo majini, maana hayana nyayo

Maokotaji
Zamani tuliambiwa angalia usije ukalaaniwa/ukalaanika ukawa muokota makopo! Siku hizi maokotaji yako kila kona.. Je yamelaaniwa? Yanaokota chochote, lolote, popote! Yanaokota nyikani, yanaokota mawandani, yanaokota barabarani yanaokota majalalani lakini yanapofiks majini.. Hayaokoti! Ama huokota kwa hofu kubwa maana majini hakuna nyayo wala hakuna mbawa..!

Maokotezi
Kwenye fuko la maokoto, kuna maokotezi ya kila aina aina.. Mabaya na mabaya zaidi, machafu na machafu zaidi. Yanukayo na yenye kunuka zaidi, yenye kutoa uvundo na yaliyovunda kabisa...!

Maokotaji yameenda majalalani kufanya maokoto na yamepata maokotezi ya kuyaingiza nyuani mwetu.. Kibaya na kibaya zaidi sana sana..yameokoteza majini sasa kaya nzima ni mavundo na uvundo
Tulioaswa zamani kuhusu maokoto hatukukimbilia maokoto.. Tuliwaasa msiyaokote mlikaza shingo msitusikilize.. Sasa mmeokoteza mpaka majini.. Uvundo wa shombo lililooza ni akheri mara mia uvundo wa msalani wa jumuiya...

Sasa tunanukiwa wote.. Uvundo haubagui pua.. Hata kama umeikata na kuunga wajihi
Tunpojaribu kuwaambia maokoto yenu ni uvundo mtupu..
Msitubambikie yasiyofaa
Msitutese bila sababu
Msitunyamazishe kwa mashtaka ya kutunga
Msitusingizie tusiyotamka..

Tunapenda maisha kama nyie
Tuna watoto kama nyie
Tuna wapendwa kama nyie
Tuna wazazi, ndugu na jamaa kama nyie

Haya maokoto toka majini ikiwapendeza yaondoni yananuka uvundo mkali sana na hofu yetu uvundo wake usije kutuletea masahibu ya kimwili na kiroho.. Tutaangamizana kwa ubishi na ubabe wa kijinga
6c54ecd89f683f38ce912c3835bcfde1.jpg
 
Mwenda tozi na omo marejeo ngamani.. Ni rahisi kwa ngamia(sio mnyama) kupenya kwenye tundu la sindano (kwa waamini na waaminio) kuliko tajiri kuingia kwenye ufalme wa Mungu...!

na kwa ubishi na ubabe wa kijingaView attachment 2717146

Lkn mbona Muokotaji Umemzidishia tumbo , inaonekana la muokotaji halijashiba bado so ataendelea kuokota tu hata kama ushauri huu sahihi ataupata.
 
Mwenda tozi na omo marejeo ngamani.. Ni rahisi kwa ngamia(sio mnyama) kupenya kwenye tundu la sindano (kwa waamini na waaminio) kuliko tajiri kuingia kwenye ufalme wa Mungu...!

Maokoto
Hondoni yananuka uvundo mkali sana na hofu yetu uvundo wake usije kutuletea masahibu ya kimwili na kiroho.. Tutaangamizana kwa ubishi na ubabe wa kijingaView attachment 2717146
Umewahi kuwa mwalimu wa fasihi?

Andiko mujarabu, msg sent🙏🙏
 
Back
Top Bottom