Maofisa wa JWTZ kuhusishwa na fedha za Uswisi ni pigo kubwa sana kwa nchi

Mkuu Bukyanagandi hupo? Au utasema na hii ni 'kutoa siri za jeshi'... Kusema kweli jeshi limeoza, kama tuonavyo MSD wanavyotuuzi ARV feki, huko jeshini ni mara 10... Kwa hali hii ndio tunataka kupigana vita, kwa hakika jeshi letu litadhalilishwa...
 
CCM na Jeshi lao moja tu,ndio maana CCM wanakiburi wanajua wakuwalinda wapo
 
Kile kibabu kilicho jiuzulu siku za karibuni si kilitajwa kuwa kina trilioni tatu?
Hivi kwanini JF iliuondoa uzi ule??
NAIKATAA CCM NA MAMBO YAKE YOTE NA WATU WAKE WOTE EEE MWENYEZI MUNGU NISAIDIE!!!!!!!!
Taarifa ya kuwepo maafisa watatu wastaafu wa JWTZ katika orodha ya vigogo walioficha fedha uswisi ni pigo kubwa sana kwa nchi kwani hii taasisi ni moja ya taasisi ambazo Watanzania tulikuwa na imani nayo bado lakini pia linaweza kuwa pigo kwa nchi kwani inawezekana kabisa hali ya jeshi letu kivifaa sio nzuri sana kwani kuna uwezekano pesa za kununulia vifaa/Silaha zilichakachuliwa na hivyo aidha hatuna silaha nzuri na za kutosha au tuna silaha duni/zilichochakachuliwa.

Kama tulivyoona ajali kadhaa ya choppers cha jeshi zinazoaminika tuliuziwa zikiwa zimeshachoka lakini inawezekana pia hela hizo zilizofichwa uswisi ni matokeo ya kudhulimiwa kwa wapiganaji wetu na hivyo kuua morali ya vijana wetu.

Kwangu kuwepo kwenye orodha hii maafisa nyeti na wanaopaswa kuwa na uzalendo wa hali ya juu hata kujitolea maisha yao kutulinda ni Pigo kubwa sana kwa nchi yetu.
 
Hiyo List inakera kila siku mara, mawaziri, mara maofisa wa jeshi tutasikia mara madaktari, viongozi wa vyama vya siasa, mara watendaji wa kijiji, tunataka majina hapa...thats all
Hiyo list serikali haiwezi kuwa na dhamira ya kuitaja. Tukumbuke mwezi wa 6 benki kuu ya uswisi iltoa rasmi taarifa ya viongozi wa ngazi za juu wa serkali yetu kuwa wameficha shilingi bilioni 313 huko uswisi. Hivi sasa ni miezi minne hayo majina yameendelea kuwekwa siri kubwa. Lakini hilo linafanyika kwa kusudi moja tu kuwa angalau serikali ya CCM iendelee kuwa madarakani hadi mwaka 2015. Kwa kuwa kama list hiyo inatajwa rasmi leo, maana yake tujiandae kwenda kwenye uchaguzi mkuu sasa. Kwa kuwa serkali yote itabidi ijiuzulu. Kwa kuwa mkulu mwenyewe, mkuu wa nchi, jina lake naye limo katika hao walioficha pesa hizo huko uswisi. Kwa mazingira hayo hakuna uwezekano wa serikali kuwa na uhalali wa kuendelea kuongoza, iwapo tu majina hayo yatayamkwa hadharani. Kwa maana watuwe tayari kusubiri hadi mwisho wa Dunia, bila kuyasikia majina hayo yakitamkwa na serikali ya CCM!!
 
T215ZZK....asifanye usanii safari hii lazima atutajie hayo majina isije ikawa ni bra bra za kila siku kila mtu akiibuka nina orodha ya watu fulani,mara majambazi,mara wauza madawa ya kulevya..halafu hamuwataji...plz plz...safari hii tutakuwajibisha mwenyewe msitufanye watanzania ni watu wa kudanganywadanganywa tu kila siku

...mkuu mimi nadhani majina si issue,issue ni je hata kama yakitajwa hatua stahiki zitachukuliwa?...hadi hivi leo ni majina magapi ya mafisadi yameishatajwa?,je kuna hatua zozote zilishachuliwa?!...zaidi ya-kuambiwa...1."mwacheni mzee apumzike"...2.hakuna hushahidi...3.mwanyeushahidi alete(wakati serikali ndo inavyombo na wataalam wenyeuwezo wa kutafuta na pata ushahidi,mfano usalama wa taifa,polisi na takokukulu)...tumeisha tajiwa majina ya akina Rostam,Lowassa,Chenge,Karamagi nk,wamechuliwa hatua gani?,angalau hata kuhojiwa walishahojiwa?,kwa hiyo na-hata haya majina tunayotaka yatajwe "ndugu yangu" utayasikia tu alfu mambo yataendelea kama kawaida...
...hii list pamoja na yawale wote waliotajwa kwe kashfa ya EPA,RECHMOND,KAGODA,MEREMETA,MADAWA YA KULEVYA na WALA RUSHWA,walisha pewa muda na mr dhaifu wajirekebishe...
 
Hiyo List inakera kila siku mara, mawaziri, mara maofisa wa jeshi tutasikia mara madaktari, viongozi wa vyama vya siasa, mara watendaji wa kijiji, tunataka majina hapa...thats all

Na mwishowe utasikia "ni chadema"
watatumia njia niliyoipendekeza ya kutatua mgogoro wa mpaka baina yetu na malawi, yaani kuitwaa 'blantaya' ili ombi lao (wamalawi) liwe kurudishiwa makao makuu ya nchi yao sio ziwa tena. Nadhani iko haja ya wabunge wa upinzani kusimama kidete bungeni kuibana serikali hata ikilazimu kutolewa nje na makinda + ndugai & zungu watolewe wote kwa mpigo tujue moja, wenye m4c waende kuwaambia wananchi kwa njia hiyo, wenye ile nyingine ya kafu nao wajimwage na makosta yao waueleze umma.
 
si afadhari kajenda Tanzania, kuliko angekwenda kuyaweka njeeee

kuna brigedia jenerali mmoja anajenga lijumba la kifahari huko oysterbay hua najiulizaga hela katoa wapi haiwezi kua ni hela yake ya kustaafu ndio inamuwezesha kujenga jumba la kifahari hivyo...hawa wanajeshi ogopa...
 
...kama RPC Barlow alikuwa na utajiri wakutisha si shangai kusikia maofisa wa JWTZ kuwa na account-zenye mabilioni ya fedha zilizopatikana kifisadi uko Uswiz,na wala sitoshtuka kama kesho nikisia tena ya kwamba moja kati ya hizo accounta ni ya jaji wa mahakama ya rufaa...
 
...mkuu mimi nadhani majina si issue,issue ni je hata kama yakitajwa hatua stahiki zitachukuliwa?...hadi hivi leo ni majina magapi ya mafisadi yameishatajwa?,je kuna hatua zozote zilishachuliwa?!...zaidi ya-kuambiwa...1."mwacheni mzee apumzike"...2.hakuna hushahidi...3.mwanyeushahidi alete(wakati serikali ndo inavyombo na wataalam wenyeuwezo wa kutafuta na pata ushahidi,mfano usalama wa taifa,polisi na takokukulu)...tumeisha tajiwa majina ya akina Rostam,Lowassa,Chenge,Karamagi nk,wamechuliwa hatua gani?,angalau hata kuhojiwa walishahojiwa?,kwa hiyo na-hata haya majina tunayotaka yatajwe "ndugu yangu" utayasikia tu alfu mambo yataendelea kama kawaida...
Na hao ndio wanajiandaa kuchukua madaraka ya nchi - Lowassa ni mjumbe wa nec, Karamagi ni mjumbe wa nec nk. Ina maana tutasubiri hadi 2025!
 
Kile kibabu kilicho jiuzulu siku za karibuni si kilitajwa kuwa kina trilioni tatu?
Hivi kwanini JF iliuondoa uzi ule??
NAIKATAA CCM NA MAMBO YAKE YOTE NA WATU WAKE WOTE EEE MWENYEZI MUNGU NISAIDIE!!!!!!!!
alijiuzulu au alistaafu
 
Na hao ndio wanajiandaa kuchukua madaraka ya nchi - Lowassa ni mjumbe wa nec, Karamagi ni mjumbe wa nec nk. Ina maana tutasubiri hadi 2025!

God forbid..Hapo nipo sawa rafiki hakatizi mtu..Washukuru Mungu iwapo watafika hata hiyo 2015 ....Siyo vyote uonavyo vyafaa mbele ya macho yako vina nguvu zingine ni mabua tu!
 
Hiyo list serikali haiwezi kuwa na dhamira ya kuitaja. Tukumbuke mwezi wa 6 benki kuu ya uswisi iltoa rasmi taarifa ya viongozi wa ngazi za juu wa serkali yetu kuwa wameficha shilingi bilioni 313 huko uswisi. Hivi sasa ni miezi minne hayo majina yameendelea kuwekwa siri kubwa. Lakini hilo linafanyika kwa kusudi moja tu kuwa angalau serikali ya CCM iendelee kuwa madarakani hadi mwaka 2015. Kwa kuwa kama list hiyo inatajwa rasmi leo, maana yake tujiandae kwenda kwenye uchaguzi mkuu sasa. Kwa kuwa serkali yote itabidi ijiuzulu. Kwa kuwa mkulu mwenyewe, mkuu wa nchi, jina lake naye limo katika hao walioficha pesa hizo huko uswisi. Kwa mazingira hayo hakuna uwezekano wa serikali kuwa na uhalali wa kuendelea kuongoza, iwapo tu majina hayo yatayamkwa hadharani. Kwa maana watuwe tayari kusubiri hadi mwisho wa Dunia, bila kuyasikia majina hayo yakitamkwa na serikali ya CCM!!
You are right!! But this is where our mistakes kill us. We currently lack dedicated citizens to die for our country!! Katika hili tungekuwa tumeshapata hiyo list siku nyingi na pengine watu wangekuwa washakuwa na aibu kila kona.
 
VIGOGO 10 wametajwa kuhusika katika kashfa ya kuficha Sh303.7 bilioni katika benki mbalimbali nchini Uswisi.

Katika orodha hiyo inadaiwa kuwa yupo kiongozi mmoja mwandamizi mstaafu, maofisa watatu wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), mawaziri wastaafu ambao baadhi yao bado ni wabunge na aliyewahi kuwa kiongozi mwandamizi wa Benki Kuu Tanzania (BoT).

Majina hayo ambayo mwandishi wetu amefanikiwa kuyaona, yamo katika orodha ya mchunguzi mmoja wa kimataifa wa masuala ya ufisadi (jina tunalo).

Juzi, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alimshukia Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah akimtuhumu kuandika barua Uswisi akisema Tanzania haina masilahi na mabilioni ya fedha yaliyofichwa katika benki zilizopo nchini humo. Hata hivyo, Dk Hoseah alikanusha madai hayo akisema hajawahi kufanya hivyo.

Akizungumza jana Zitto alisisitiza kauli yake akisema: “Sijawahi kumsema Dk Hoseah kwa lolote, kwa nini leo nimsingizie? Yeye mwenyewe anajua ushirikiano niliompa wakati wabunge wanapinga yeye asichunguze malipo ya posho mara mbili kwa wabunge.”

“Nilisimama kidete kusema Takukuru wapo sahihi na mimi nilikwenda mwenyewe kwao kuhojiwa na kuagiza wajumbe wa kamati yangu (Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma), waende kuhojiwa. Spika aliyestaafu (Samuel Sitta) akaizima kashfa ya wabunge kupokea posho mara mbilimbili. Mwulizeni amesahau? Sasa leo nimzushie ili iwe nini?.”

Alisema orodha ya Watanzania wenye fedha huko Uswisi, ipo na ameiona na nyaraka zinaweza kutolewa kwa taasisi za Serikali tu.
“Dk Hoseah kazuia nyaraka hizo. Akitaka nimwonyeshe mtu anayeweza kutoa nyaraka hizo, nipo tayari isipokuwa aahidi kuiweka wazi,” alisema Zitto.

Alisema katika orodha ambayo Waziri wa Fedha wa Ufaransa anayo, kuna Watanzania lakini akaituhumu Serikali akisema haitaki kufuata njia halali za kupata orodha hiyo kwa kuwa viongozi wengi na wafanyabiashara wakubwa wana akaunti katika benki za Uswisi.

Juni 26, mwaka huu gazeti hili lilichapisha habari kuhusu utoroshwaji wa fedha hizo na kueleza kuwa Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini kwa kushirikiana na Takukuru inachunguza suala hilo.

Kiasi hicho cha fedha kimedaiwa kuingizwa katika akaunti za Watanzania na kampuni moja ya uchimbaji mafuta na kampuni kadhaa za uchimbaji madini ambazo zinafanya kazi Tanzania.

Chanzo hicho kiliongeza kwamba kiasi hicho cha fedha kipo katika akaunti sita tofauti zinazomilikiwa na Watanzania wakiwamo wanasiasa wakubwa.

Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa tangu akaunti hizo zifunguliwe, wamiliki wake halali hawajawahi kuingiza hata shilingi.

“Uchunguzi wetu unaonyesha kuwa fedha hizo zipo katika akaunti sita tofauti ambazo zinamilikiwa na wanasiasa wakubwa nchini na wenzetu wa Uswisi wameeleza fedha hizo zimeingizwa na kampuni kadhaa ambazo zinahusika na mafuta pamoja na madini hapa nchini,” kilidokeza chanzo hicho.

Kugundulika kwa kiasi hicho cha fedha katika benki za Uswisi ni kutokana na ripoti ya Benki ya Taifa ya Uswisi (SNB) iliyotolewa mwaka huu.

kama hamuwezi kuwataja, nyie ni wambea na wachochezi wakubwa
 
hii niwataje nisiwataje.. usipowataja tawataja... sasa imekuwa kama wimbo unaochosha kama kweli mtu ushahidi anao na yeye hawataji hao wezi hana tofauti na hao wezi
 
kama hamuwezi kuwataja, nyie ni wambea na wachochezi wakubwa

Nadhani Zitto anaiongelea hii list:

Kwamuda wa miaka miwili sasa tangu tulipoanza kazi nzito ya upelelezi wa wakubaini na kuzuia uingizaji na utoroshaji wa pesa nchini,
Juhudi zetu zimeanza kuzaa matunda baada ya kubaini majina halisi ya watanzania walioficha fedha nje ya nchi na wanaoingiza fedha haramu nchini.
Kwakushirikiana na mashirika ya kijasusi ya CIA-USA, M1-6-UK, RAW-India, DGSE-Ufaransa, FSB Urusi, ISI Pakistan, na MSS-China, ambayo yamekuwa yakifuatilia nyendo za fedha haramu hasa za kighaidi dunia, tumefanikiwa kutambua Watanzania, Wakenya, Waafrika kusini, Waganda na Wakongo wengi matajiri walioficha fedha uswisi.
Hapa nitawaorodhesha Watanzania tu;
Orodha ni ndefu ila hapa ni wale walioficha zaidi ya USD $3.5 mmilion kila moja. Wamo wanasiasa pamoja na wafanyabiashara kadhaa maarufu. Imebainikwa kwamba fedha nyingi za wanasiasa zimewekwa na makampuni ya nje yenye shughuli Tanzania. Wamo hata Makatibu Wakuu Wizarani na wakurugenzi ila hawajafikia USD3.5million ndio maana majina yao hayamo.
Orodha kamili ni:
Jakaya M. Kikwete, January Makamba, Abdalla Kighoda, Nimrod Mkono, Nazir Karamagi, Andrew Chenge, Yusuf Makamba, Edward Lowassa, Rostam Aziz, Yusuf Manji, Ridhiwani Kikwete, Mohamed Dewji, Bernard Membe, Paul Chagonja , Zitto Kabwe, William B. Mkapa, Said Mwema, Abdulrahman Shimbo, Edward Hosea, Daudi T.S Balali, Basil Mramba,Mustapha Mkullo, Grey Mgonja, Patrick Rutabanzibwa,Tanil Somaiya, Jeetu Patel, Onoko Okesukwu mwenye asili ya Kinigeria, Awadh Mohamed (mwenye uraia wa msomalia) na Subhash Patel
 
Back
Top Bottom