Maofisa wa JWTZ kuhusishwa na fedha za Uswisi ni pigo kubwa sana kwa nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maofisa wa JWTZ kuhusishwa na fedha za Uswisi ni pigo kubwa sana kwa nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sabayi, Oct 29, 2012.

 1. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Taarifa ya kuwepo maafisa watatu wastaafu wa JWTZ katika orodha ya vigogo walioficha fedha uswisi ni pigo kubwa sana kwa nchi kwani hii taasisi ni moja ya taasisi ambazo Watanzania tulikuwa na imani nayo bado lakini pia linaweza kuwa pigo kwa nchi kwani inawezekana kabisa hali ya jeshi letu kivifaa sio nzuri sana kwani kuna uwezekano pesa za kununulia vifaa/Silaha zilichakachuliwa na hivyo aidha hatuna silaha nzuri na za kutosha au tuna silaha duni/zilichochakachuliwa.

  Kama tulivyoona ajali kadhaa ya choppers cha jeshi zinazoaminika tuliuziwa zikiwa zimeshachoka lakini inawezekana pia hela hizo zilizofichwa uswisi ni matokeo ya kudhulimiwa kwa wapiganaji wetu na hivyo kuua morali ya vijana wetu.

  Kwangu kuwepo kwenye orodha hii maafisa nyeti na wanaopaswa kuwa na uzalendo wa hali ya juu hata kujitolea maisha yao kutulinda ni Pigo kubwa sana kwa nchi yetu.
   
 2. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,139
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  wengine hatuwafahamu hao maofisa,embu funguka majina yao tuwajue.
   
 3. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Nani katoa hiyo orodha?
   
 4. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  ZK anayo list
   
 5. m

  malaka JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Sio vifaa tu hapo kaka. Ni mafunzo, hela za makambi ya makomandoo pia. HIvi nani atamnyoooshea kidole mwenzie hapa tanzania sasa?
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  vipi safari hii Abdallah Shimbo yupo tena..
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  kuna brigedia jenerali mmoja anajenga lijumba la kifahari huko oysterbay hua najiulizaga hela katoa wapi haiwezi kua ni hela yake ya kustaafu ndio inamuwezesha kujenga jumba la kifahari hivyo...hawa wanajeshi ogopa...
   
 8. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Lets wait.......
   
 9. C

  Concious Senior Member

  #9
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  T215ZZK....asifanye usanii safari hii lazima atutajie hayo majina isije ikawa ni bra bra za kila siku kila mtu akiibuka nina orodha ya watu fulani,mara majambazi,mara wauza madawa ya kulevya..halafu hamuwataji...plz plz...safari hii tutakuwajibisha mwenyewe msitufanye watanzania ni watu wa kudanganywadanganywa tu kila siku
   
 10. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,399
  Likes Received: 1,524
  Trophy Points: 280
  ........moja kastaafu hivi karibuni, alimpiga mkwara Slaa wakati wa uchaguzi....
   
 11. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,399
  Likes Received: 1,524
  Trophy Points: 280
  ........Hm!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 12. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Tukisema hapa watu wanaanza kutoka mapovu. Kimsingi hakuna ufisadi uliotukuka kama jeshini, ukisia mishahara hewa ndo huko, ukisikia fedha za UN zinapigwa panga kwa ajili ya kununua vifaa wakati hawanunui ndiyo huko, ukisikia fedha za kujikimu kwa wanajeshi hazilipwi lakini kwenye budget zipo ndiyo huko, ukisikia makato ya ajabu ajabu kwenye mishahara ya wanajeshi ndiyo huko. Yaani kuna mengi, ila kwa kuwa wanajiita wenye nchi, we just have to be patients and wait for the principle of natural selection to take place.
   
 13. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Picha iko wapi, isitoshe ile ni Jumba au kibanda? Umeiona nyumba ya mchungaji wa mungu na mmiliki wa St. Marys?
   
 14. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mbona haiweki? ama ndio ile tantalira ya barua ya Takokuru?
   
 15. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  VIGOGO 10 wametajwa kuhusika katika kashfa ya kuficha Sh303.7 bilioni katika benki mbalimbali nchini Uswisi.

  Katika orodha hiyo inadaiwa kuwa yupo kiongozi mmoja mwandamizi mstaafu, maofisa watatu wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), mawaziri wastaafu ambao baadhi yao bado ni wabunge na aliyewahi kuwa kiongozi mwandamizi wa Benki Kuu Tanzania (BoT).

  Majina hayo ambayo mwandishi wetu amefanikiwa kuyaona, yamo katika orodha ya mchunguzi mmoja wa kimataifa wa masuala ya ufisadi (jina tunalo).

  Juzi, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alimshukia Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah akimtuhumu kuandika barua Uswisi akisema Tanzania haina masilahi na mabilioni ya fedha yaliyofichwa katika benki zilizopo nchini humo. Hata hivyo, Dk Hoseah alikanusha madai hayo akisema hajawahi kufanya hivyo.

  Akizungumza jana Zitto alisisitiza kauli yake akisema: "Sijawahi kumsema Dk Hoseah kwa lolote, kwa nini leo nimsingizie? Yeye mwenyewe anajua ushirikiano niliompa wakati wabunge wanapinga yeye asichunguze malipo ya posho mara mbili kwa wabunge."

  "Nilisimama kidete kusema Takukuru wapo sahihi na mimi nilikwenda mwenyewe kwao kuhojiwa na kuagiza wajumbe wa kamati yangu (Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma), waende kuhojiwa. Spika aliyestaafu (Samuel Sitta) akaizima kashfa ya wabunge kupokea posho mara mbilimbili. Mwulizeni amesahau? Sasa leo nimzushie ili iwe nini?."

  Alisema orodha ya Watanzania wenye fedha huko Uswisi, ipo na ameiona na nyaraka zinaweza kutolewa kwa taasisi za Serikali tu.
  "Dk Hoseah kazuia nyaraka hizo. Akitaka nimwonyeshe mtu anayeweza kutoa nyaraka hizo, nipo tayari isipokuwa aahidi kuiweka wazi," alisema Zitto.

  Alisema katika orodha ambayo Waziri wa Fedha wa Ufaransa anayo, kuna Watanzania lakini akaituhumu Serikali akisema haitaki kufuata njia halali za kupata orodha hiyo kwa kuwa viongozi wengi na wafanyabiashara wakubwa wana akaunti katika benki za Uswisi.

  Juni 26, mwaka huu gazeti hili lilichapisha habari kuhusu utoroshwaji wa fedha hizo na kueleza kuwa Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini kwa kushirikiana na Takukuru inachunguza suala hilo.

  Kiasi hicho cha fedha kimedaiwa kuingizwa katika akaunti za Watanzania na kampuni moja ya uchimbaji mafuta na kampuni kadhaa za uchimbaji madini ambazo zinafanya kazi Tanzania.

  Chanzo hicho kiliongeza kwamba kiasi hicho cha fedha kipo katika akaunti sita tofauti zinazomilikiwa na Watanzania wakiwamo wanasiasa wakubwa.

  Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa tangu akaunti hizo zifunguliwe, wamiliki wake halali hawajawahi kuingiza hata shilingi.

  "Uchunguzi wetu unaonyesha kuwa fedha hizo zipo katika akaunti sita tofauti ambazo zinamilikiwa na wanasiasa wakubwa nchini na wenzetu wa Uswisi wameeleza fedha hizo zimeingizwa na kampuni kadhaa ambazo zinahusika na mafuta pamoja na madini hapa nchini," kilidokeza chanzo hicho.

  Kugundulika kwa kiasi hicho cha fedha katika benki za Uswisi ni kutokana na ripoti ya Benki ya Taifa ya Uswisi (SNB) iliyotolewa mwaka huu.
   
 16. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hiyo List inakera kila siku mara, mawaziri, mara maofisa wa jeshi tutasikia mara madaktari, viongozi wa vyama vya siasa, mara watendaji wa kijiji, tunataka majina hapa...thats all
   
 17. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Uko sahihi kabisa mkuu.
   
 18. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Watanzania tuamke sasa! Mafisadi wanaanzisha issue za kidini ili kutuhamisha mind zetu! wahenga walisema miluzi mingi humpoteza mbwa.
   
 19. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Wekeni majina yao kuficha haisadii
   
 20. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #20
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,969
  Likes Received: 6,747
  Trophy Points: 280
  Umesema kweli kabisa! Hatutaki usanii kwa jambo kubwa kama hili. Wakati mamilioni ya wa-TZ, wanaishi kwa kula mlo mmoja kwa siku, hawa wenzetu wachache wanaogelea kwenye utajiri wa kutisha kwa kuwekewa mabilioni ya shilingi, kama rushwa kwenye mabenki hayo ya uswisi, na kampuni za kigeni zinazochimba mafuta na gesi.

  Kwa bahati mbaya sana, hiyo list ya waliowekewa hizo pesa, itakuwa jambo lisilowezekana kutangazwa na serikali hii ya CCM. Kwa kuwa inahusisha watu wenye madaraka makubwa sana kwenye serikali ya awamu hii na iliyopita. Kwa uchache tu miongoni ya majina hayo ni JK, Mkapa, Hosea, Lowasa, Mwema, Chagonja,Shimbo, Membe,Balali na Mkulo!!

  Sasa kwa list hiyo ni wazi juhudi zote zitafanywa na serikali ya CCM, hadi mwisho wa Dunia, kuhakikisha list hiyo haijulikani kwa walalahoi wa nchi hii, maana ikitolewa rasmi ripoti hiyo kwa wananchi, maana yake huo ndiyo utakuwa mwisho rasmi wa chama cha magamba!!
   
Loading...