Maofisa polisi 120 watimuliwa CCP

Eistein

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
1,107
482
igip_mangu.gif

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu

Moshi. Maofisa wa Polisi wapatao 120 wa Jeshi la Polisi, waliokuwa wakihudhuria mafunzo ya kupandishwa vyeo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi (MPA), wametimuliwa chuoni hapo.

Habari za uhakika zilizopatikana jana kutoka ndani ya chuo hicho zamani kikijulikana kama CCP, zimedai uamuzi wa kuwaondoa chuoni ulitangazwa jana na mkuu wa chuo hicho, Matanga Mbushi.

Vyanzo mbalimbali vililidokeza gazeti hili kuwa, waliotimuliwa chuoni hapo ni maofisa ambao wana ulemavu wa aina mbalimbali walioupata wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kazi.

Habari hizo zilisema hadi jana saa 9:00 alasiri, maofisa hao walikuwa ofisi za mkuu wa chuo hicho wakisubiri kupatiwa maelekezo ya namna ya kurejea katika vituo vyao vya kazi mikoa mbalimbali.

"Wako 120 hivi walikuja hapa (MPA) kwa ajili ya kuchukua kozi za Koplo, Sajenti, Meja na ‘Assistant Inspector' (wakaguzi wasaidizi), lakini ndiyo hivyo wametuambia tuondoke," kilidokeza chanzo chetu.

Hata hivyo, ofisa mmoja alilidokeza gazeti hili kwamba mkuu wa zamani Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, ambaye amestaafu, ndiye wa kulaumiwa kwa kutoheshimu mapendekezo ya wataalamu.

"Tulimwambia IGP Mwema kwamba ni vizuri kama maofisa wenye ulemavu kama baadhi ya vigezo wanavyo basi wapewe vyeo huko huko mikoani, lakini wasiende chuoni," alidokeza na kuongeza;

"Tulipendekeza yafunguliwe madarasa ya kanda wakishafanya mtihani wa kawaida wapewe vyeo huko huko, lakini wakija chuoni ni lazima wahudhurie vipindi vyote ambavyo vinafanya chuo kiitwe chuo.

"Chuo chochote kile kina vigezo vyake na kwamba ili mtu apate cheo alichokwenda kukisomea ni lazima ahudhurie asimilia 95 ya vipindi ikiwamo kwata, medani za kivita na kuzuia vurugu,"alisema.

Chanzo kingine kililidokeza gazeti hili kuwa maofisa hao waliripoti chuoni hapo wiki mbili zilizopita na katika uchunguzi, walibainika wana ulemavu ambao hawawezi kumudu mafunzo ya ukakamavu.

Mmoja wa maofisa hao waliotimuliwa alilalamika kuwa kitendo hicho siyo cha kiungwana kwa kuwa ulemavu huo waliupata wakiwa kazini wakilitumikia Taifa na hawajashindwa kuingia darasani.

"Baadhi yetu tumefanya kazi miaka 20 wengine 25. Wamekatika miguu. Wako trafiki wamegongwa na polisi wengine wamepigwa risasi na majambazi wakapata ulemavu si sawa kutunyima vyeo," alidai.

Ofisa huyo alisema pamoja na ulemavu huo, lakini wamekuwa wakipangiwa kazi na kuzimudu kama kawaida isipokuwa zile za ukakamavu na kwamba hata wakati wakipendekezwa, walikuwa wanajulikana matatizo yao.

Alipoulizwa na gazeti hili jana, Mbushi alithibitisha kuwapo kwa uamuzi wa kuwaondoa chuoni maofisa hao, lakini akasema wanasubiri maelekezo zaidi kutoka makao makuu ya polisi.

"Bado hatujawaondoa lakini ukweli ni kwamba kama mtu hawezi kumudu mafunzo lazima aondolewe. Kama mtu hawezi kuingia kwenye paredi anakosa vigezo vya chuo," alisema na kuongeza;

"Tunawasiliana na makao makuu ili tuone wataamua nini, lakini kwa kweli hawawezi kumudu mafunzo ni wagonjwa wameumia, wengine miguu mibovu na mafunzo ni ya kijeshi siyo darasani pekee," alisema na kuongeza:

"Ni lazima tuchukue kila aina ya tahadhari unaweza kulazimisha halafu mtu akafa kwa sababu mafunzo hasa ya ujasiri ni magumu, lakini kumbe mtu amekuja ni mgonjwa," alisisitiza Mbushi na kuongeza;

"Kwa hiyo wamependekezwa kupata vyeo kwa utaratibu wa kawaida kabisa ndani ya Jeshi la Polisi wanaingia darasani kama kawaida, lakini gwaride ambalo ni sehemu ya mafunzo hawawezi."


Source:Mwananchi
 
Nadhani ni uamuzi mzuri..warudi huko mpaka madarasa ya kikanda yatakapo funguliwa wasome huko na kupatiwa vyeo vyao.tunaheshimu mchango wao kwa taifa hili..ila kwa pale CCP kwakweli haifai kuwepo bila hata kwenda kwenye field craft sasa hayo siyo mafunzo
 
KUTIMULIWA MAAFISA POLISI CHUONI kwa wepesi laweza onkana swala dogo, lakini ni picha kamili ya hali iliomo jeshini! kulindana na kupinda kanuni that is the law of the day! hata watoto wanaoingia form 1 wana medical exam, police chuoni waingia tu! kuna uozo mkubwa jeshi hilo, yanayofanikiwa kuonekana is just a tip of the ice berg! au ndio dalili ya mfumo? au kiwakilishi cha jamhuri ya kambale?
 
Nadhani huo ni uamuzi mzuri ingawa ulipaswa kufanyika mapema kuepusha usumbufu......huwezi kwenda MPA alafu ukaepuka mafunzo muhimu ya medani za kivita , kwata n.k yanayohitaji utimamu wa kimwili .....kile ni chuo ambacho huwezi kuvunja taratibu bila kuwepo na utaratibu wa kuingiza mtaala utaokubalika na wataalamu wa mambo ya Kipolisi ....
 
Ulemavu mmewatia wenyewe halfu mnawafukuza kama vipi si wana bima ya ulemavu walipwe mshahara kila mwezi.
 
mi sifahamu jamani, kwa hiyo walioumia kazini uwezekano wa kupanda vyeo ni hakuna?!! mbona wanawaonea sasa, sasa hao wakistaafu si ataonddoka na milioni kumi tu!
 
Polisi wana mambo..Matanga Mbushi anasema anasubiri maelekezo kutoka Makao Makuu..ikumbukwe hao makao makuu ndio waliowatoa majina
 
This heading is quite misleading and conveys wrong information! It is as if they have been sacked from police force due to criminal acts, or disciplinary grounds which is not!
correct reporting may be could have .....................have terminated/(have been terminated) their training due to......

Ndio waandishi/wahitimu wetu toka vyuo vikuu utitiri vilivyoota kama uyoga !
 
KUTIMULIWA MAAFISA POLISI CHUONI kwa wepesi laweza onkana swala dogo, lakini ni picha kamili ya hali iliomo jeshini! kulindana na kupinda kanuni that is the law of the day! hata watoto wanaoingia form 1 wana medical exam, police chuoni waingia tu! kuna uozo mkubwa jeshi hilo, yanayofanikiwa kuonekana is just a tip of the ice berg! au ndio dalili ya mfumo? au kiwakilishi cha jamhuri ya kambale?

Nachukia mtu anaecomment bila kuelewa mada husika halafu anajifanya mjuaji kupitiliza.
Umembiwa hao wamepata ulemamavu na matatizo wakiwa ktk majukumu humohumo ndani ya utumishi wao. Fungua akili kenge we!
 
Mwema nae elimu ni finyu
nani mwenye elimu/akili finyu. yule ambaye hakuanzisha hivyo vyuo mikoani vya vyeo bandia lakini hakuwapeleka ccp au huyu ambaye hakuanzisha hivyo vyuo na kuwapeleka ccp?
kwani kilichomzuia mangu kuanzisha hiyo kitu ni nini wakati ana madaraka yaleyale aliyokuwa nayo Mwema?
sio ajabu Mwema aliona hawana sifa ndo maana hakuwapeleka ccp na wala hakuanzisha hivyo vyuo vya bandia. ila mangu kwa uelewa wake mdogo ameona wana sifa lakini wamefika ccp wakakuta mkuu wa chuo ana akili zinazooana na za Mwema ndo maana kawatimua.
tumia akili kinyesi wewe.
 
Kama una ulemavu huwa wanafanyiwa bodi halafu wanastaafishwa kwa ugonjwa!

Itakuwa hawa hawakutaka kufanyiwa bodi na kustaafu,, sasa wewe mlemavu utafanya kozi gani?

Huo ndo utaratibu wa polisi force!
 
Back
Top Bottom