Maofisa habari waonywa kwa kuuza siri za serikali

Aaa,sijui kinachoendelea katika nchi yetu,lakini hali halisi inasikitisha.Katika watawala wetu wengi,Bwana Nkullo ni mmoja wa wale ambao nimetokea kumuona kama mtu asiye na busara na ambae anaelekea kutumikia mabwana fulani hivi.Sina haja ya kuwataja mabwana hao kwa vile wachunguzi makini wa mambo wanawaelewa.

Sasa katika siku chache zilizopita kulikuwa na mafunzo kule Morogoro ya watendaji wa Wizara yake na kama kawaida yake aliibuka na hoja ya kukemea wale ambao wana tabia ya kuvujisha siri za serikali hasa wafanyakazi wa ngazi za juu za utumishi katika Wizara yake.Tabia hii ya kulalamika kwamba siri sa serikali zinavujishwa sio ya kwake tu na ni ya siku nyingi.Ni tabia pia ya viongozi wengi wa ngazi za juu wa serikali.Mimi sina hakika siri hizi wanazo ziongelea ni siri gani.Lakini the baseline ni kwamba wote wanasukumwa na desire ya kuficha maovu.Mtendaji mzuri hawezi kuwa na kitu kinachoitwa siri,kwa vile huduma yake na utendaji wake wote ni kwa ajili ya wananchi.Kuna ubaya gani mwananchi ambaye ndiye focus ya utendaji wetu sisi wote akijua matatizo yaliyopo?By the way transparency tunayoiongelea kila kukicha ni ipi?

Naomba nimalizie kwa kumwambia Nkullo kwamba anacho jaribu kutuambia ni kwamba ni mtendaji duni na mwenye maovu mengi ambayo anajaribu kuyaficha by intimidating his surbodinates.Hiyo ilikuwa style ya EL,hata hivyo hakwenda mbali sana.Lakini napenda kumuonya kwamba hakuna jambo lisilo na na mwisho.Siku ya arobaini ipo na inakuja.
 
Wao ndio serikali kwa hiyo siri ni pamoja na ujaji wa fedha za mawizara kwa safari na matumizi nje ya bajeti kinyume cha taratibu (ufisadi halisi).
 
Hawa jamaaa mimi nahasira nao yani hata sijuhi nifanyeje inshort juu ya hili linchi,watu wanalimbikiza madeni huko kwnye mahotel ya kifahari huko zenji kwa umalaya wao halafu kodi zetu nd' zinalipa hayo matumizi ikiwa ni pamoja na visafari vyao vya matibabu ya kuchange da...... kila kukichaaaa!!!! Mungu Tusaidie na hili balaaa
 
Kila siku tunaambiwa "watumishi wa serikali" wanatoa SIRI za Serikali; wanapaswa kuzitunza.

Lakini, hatuambiwi siri za serikali ni zipi. Katika fuatilia yangu nimegundua kuwa HIZO zinazoitwa "SIRI za Serikali" sehemu kubwa ni taarifa za uhalifu na ufisadi wa watu binafsi ambao ni viongozi ima wa SERIKALI au wa chama TAWALA au taasisi za serikali.

SWALI: Je, hizi kweli ni siri za SERIKALI? Kweli?

1) KWELI, ufisadi wa MKURUGENZI au WAZIRI au hata RAIS ni siri za serikali! KWELI?

2) KWELI, wizi wa EPA, DEEP GREEN, RICHMOND, MAJENGO PACHA BOT nk ni siri za serikali! KWELI?

3) KWELI, HIVI TUSEME uzinzi wa GEN PATREUS ni siri za CIA au USA! KWELI? nk

HAPANA: SIYO KWELI ...

Labda KAMA tuNAkubalianA na KARL MARX & ENGELS kwamba siri za watawala ndizo siri za serikali na sheria zinatungwa kwa ajili ya watawaliwa siyo kwa ajili ya watawala ... vinginevyo lazima tuondokane na hii hali.

VYOVYOTE vile, ni wakati wa kupata tafsiri ya kisheria ya nini maana ya "msemo" HUU MAARUFU 'siri ya serikali': ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha hilo linatimia, ni muhimu. VIONGOZI wetu wamekuwa wakificha madudu yao "ndani ya uvungu wa kitanda" kinachoitwa siri za serikali. HILI TUSILIRUHUSU KUENDELEA ...
 
Hivi serikali ni ya nani?yani watu waliokuweka madarakani unawanyima taarifa,eti ni siri za serikali?Hiki nacho ni kituko.
CCM wajue kuwa watu wameshachoka.Hao maafisa habari wa wizara wataendelea kutoa habari becouse wanawajibika kwa wananchi(For the Public Interest)
Msiwasingizie maafisa habari tu,vilevile TISS kuna wazalendo ambao nao wamechoshwa na uozo unaoendelea nchini becoz nao wana ndugu,jamaa na marafiki wanaoathiriwa na mauzauza yanayofanywa na Magamba.
 
Siri kuu zilikuwa wizi wa EPA na wizi mwingine serikalini!! Mnatuibia halafu mnaita SIRI zenu pambaf!!
 
Umeona eeh! DHAIFU na Serikali yake DHAIFU...Wanakupua mabilioni kila kukicha halafu wanaita siri za Serikali!!!!

Siri kuu zilikuwa wizi wa EPA na wizi mwingine serikalini!! Mnatuibia halafu mnaita SIRI zenu pambaf!!
 
hapa asingetafuna maneno angesema tu. Ufisadi wa viongozi wa serikali unavujishwa basi.!
 
kwa kufunuliwa mikataba ya kuuza mali zetu kwa miaka 100 ndo kosa hlo?mmezoea sasa baaasi
 
Back
Top Bottom