BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,109
Na Veronica Mheta | Daily News | June 21, 2008
Serikali imesema kuwa baadhi ya maofisa habari wamekuwa wakivujisha siri za serikali kwa kuziuza kwenye magazeti wapate fedha kama mgawo kwa kufanikisha uuzwaji wa siri hizo, na kwamba sasa itachukua hatua za kisheria kukomesha hali hiyo.
Inadaiwa kuwa maofisa habari wengine huwapigia simu wahusika wa magazeti na kuwapatia siri hizo wazichapishe magazetini. Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Kassim Mpenda, wakati akitoa maazimio ya mkutano uliofanyika mjini Morogoro hivi karibuni mbele ya maofisa habari kutoka wizara zote za serikali.
Mpenda alisema kutokana na udhaifu wa maofisa hao, magazeti yamekuwa yakinunua siri za serikali na kuzichapisha kutokana na uuzaji wa siri hizo unaofanywa na maofisa hao. Alisema ofisa habari yeyote atakayebainika kuuza au kutoa siri za serikali ili ziandikwe magazetini atachukuliwa hatua kali za kisheria.
"Jamani tushirikiane kuhakikisha siri za serikali hazitoki nje au kwenye magazeti hivyo tuhakikishe tunazilinda siri hizo. Si vyema kuandikwa magazetini na kama kuna ofisa atabainika kuuza siri hizo atachukuliwa hatua kali za sheria," alisema Mpenda.
Alisema baadhi ya mapendekezo yaliyopendekezwa na maofisa habari ni kuimarisha Idara ya Habari (MAELEZO) ili iratibu shughuli za vitengo vya Habari, Elimu na Mawasiliano ili kufanikisha utoaji taarifa za serikali kwa umma.
Aliwataka maofisa habari kuhakikisha wanaandaa taarifa za mipango watakayoifanya kwa mwaka mzima kurahisisha kutoa habari zinazohusu maendeleo ya kila wizara husika.
Aliiomba serikali iangalie jinsi ya kushughulikia vyombo vya habari binafsi vinavyoipinga serikali kwa kupotosha umma na alizitaka wizara zitumie vyombo vya habari vya serikali kutoa taarifa zake kwa umma.