salaleeeee,jiografia ya darasa la 4Kumekucha na sura tofauti katika mji wetu mdogo Manispaa ya Manzese!!Kuna askari kila kona pale Manzese kati wanapofurika wafanya biashara wa kila aina,Ni siku chache tu Mkandarasi wa ujenzi wa barabara ya Morogoro STRABAG aliamua kusimama kujenga eneo hili maarufu la Manzese kwa sababu za kiusalama. Kwani wafanyabiashara walivamia eneo lote la ujenzi na kukata vizuizi vilivyowekwa.Ili hali wakijua hakuna wa kuwachukulia hatua. Mahindi yanachomwa katikati ya barabara nk Nadhani Dola ikaona haina haja ya kusukumana nao kwa kutumia nguvu.Leo kunako majira ya saa 11 alfajiri askari wamemwagwa eneo hilo na magari ya deraya yakiranda randa kwenye viunga vya mitaa hiyo. La kufurahisha kila mfanyabiashara akifika anajibebea frame yake na kuanza zake kusikojulikana. Kumbe basi Jiji letu linaweza kuwekwa katika mazingiora yanayostahili kwa kufuata mfumo huu.:kev:
Manzese si manispaa,,,,asante sana kwa ujumbe wako
Ubungo wamesharudi hao wamachinga! wenzetu uongozi hawauwezi!
nimewaona juzi,but kuelekea uchaguzi wa 2015 watawaacha tu
Hili ni tatizo kubwa kuliko tunavylidhania! hasa tatizo letu ni kukosa utaratibu katika majiji na miji yetu. watu wanahamia kila siku kutoka vijijini wengine wamezaliwa humu humu mijini na wamekua hakuna utaratibu mtu anaamua kuanzisha shughuli za kumuendeshea maisha popote iwe barabarani serikali haijali, alafu wanakurupuka siku moja eti wanataka kuweka utaratibu hii inasababisha machafuko, inazalisha vibaka na mengine maana kumzibia riziki mtu atafanya lolote ili aishi. mipango miji fanyeni kazi kubainisha maeneo ya biashara, maeneo ya makazi na shughuli nyingine na manispaa wayasimamie haya
Wameambiwa waende bunju