Manyara: Watu 6 wafariki dunia na 20 wajeruhiwa katika ajali ya basi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,114
Watu sita wamefariki na wengine 20 kujeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya Kiteto Mkoani Manyara, kufuatia ajali ya Basi lililoanguka katika Kijiji cha Chekanao likitokea Matui Wilayani Kiteto kuelekea Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara ACP George Katabazi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo September 19, 2022 na kusema kati ya majeruhi hao 20, watatu wamesafirishwa kwenda Dodoma kwa ajili ya matibabu zaidi, huku akitaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendo kasi ambapo Dereva alishindwa kumudu gari hilo na kuanguka.
 
Hilo eneo kwanini lisimegwe na kuwa Dodoma
 
Back
Top Bottom