Manyara: Wanachama 139 wa CHADEMA watimkia CCM

Manyara: Wanachama 139 wa CHADEMA watimkia CCM

Kumbe ndio lengo lao? Tulikuwa hatujashtuka!
Shtuka mkuu wamefungia ili polisi watembeze mkong'oto kwa raia halafu wawapitishe mamluki wao kwenye uchaguzi bila wananchi kuona kwenye vyombo vya habari.
 
Mimi namuunga mkono Magufuli,lakini vitendo vya kujiuzulu Ubunge,Udiwani nk na kukubaliwa kugombea tena si utamaduni wenye afya Kwa demokrasia na maana halisi ya siasa tunazohitaji.Ufike mahali wewe katibu uone hili na ulikemee Kwa ustawi wa siasa safi na zenye tija,tuachane Na ngonjera ,ukizingatia watu wanataka maji,Umeme,barabara,na hospitali havipatikani Kwa kutosheleza,Sasa wanapokuja wengine wanaleta siasa za maji taka na tunarudia chaguzi na wanakuwepo wanaoshangilia unaniuma saaaaaana.
 
Swafiiii sana walahi
E247FB2C-705F-4A08-88E4-6FA6811C6EAC.gif
 
Huyu m/kiti wa uvccm inawezekana upstairs hayuko sawa, yaani wananchi kuchagua Chadema kwake ni kosa, hili ni janga la taifa kuwa na vijana wa aina hii, Demokrasia ya vyama vingi inawapa uhuru wananchi kuchagua mtu /kiongozi wanayemtaka, yeye anakuja na huu upuuzi, vijana wa namna hata kuongoza ng'ombe hawafai
 
Hivi siku zote huwa wanahama wa chadema tuu wanaenda CCM ??
Hakuna wa vyama vingine wanao jiunga CCM ni chadema tuu ???
Hakuna wasio na vyama ambao Sasa wanajiunga CCM. Huwa chadema tuu ????
Inatia Shaka hii.
Kuna chama kimoja tuu ambacho watu wanahamia chama kimoja tuuuu. Na siyo vingine ??? Kweli ????
Basi Kama ni hivyo chadema no kubwa Sana Kila siku inahamwa na bado hawaishi. Bado ipo tuuuu
 
IMG-20180120-WA0019.jpg

Taarifa ambazo WALTER HABARI imezipata zinaeleza kuwa WANACHAMA 139 wa Chadema wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, wamejiunga na CCM na kupokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM wa Mkoa wa Manyara Mosses Komba.

Akizungumza wakati wa kuwapokea na kuwakabidhi kadi za CCM wanachama hao wapya, Komba alisema wamefanya uamuzi sahihi kwa wakati sahihi. Komba alisema hawatajuta kujiunga na CCM kwani hivi sasa chama hicho kinachoongozwa na Mwenyekiti wake Rais John Magufuli kinawatumikia wananchi kwa kutatua kero na kuufanikisha maendeleo.

Alisema wanakaribishwa CCM kwa moyo mmoja hivyo washirikiane na wanachama wengine ili kuhakikisha wanalirudisha jimbo hilo na kata sita zinazotawaliwa na Chadema. "Kati ya makosa tuliyofanya kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ni kuachia jimbo la Simanjiro liende Chadema na kata za Mirerani, Naberera, Loiborsiret, Ruvu Remit, Loiborsoit na Endiamtu zichukuliwe na wapinzani," alisema Komba.

Alisema ushabiki wa kufuata mkumbo ndiyo uliowagharimu wananchi wa wilaya hiyo na kata hizo, hadi kusababisha wakapatikana madiwani na mbunge wa kutoka upinzani badala ya CCM."Nakuagiza Mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya ya Simanjiro, Thomas Mollel na wenyeviti UVCCM wa kata husika ambazo madiwani wao ni wapinzani, mkishindwa tena 2020 mjiuzulu," alisema Komba.

Alisema vijana ndiyo nguzo kubwa ya ushindi kwenye chama hicho na wamepata mwamko wa kushiriki kuwajulisha wananchi kuwa CCM ndiyo chama cha kukimbilia. Mjumbe wa baraza la utekelezaji UVCCM mkoa wa Manyara, Elizah Ladis alisema tangu waanze ziara ya kutembelea wilaya za mkoa huo mwezi Desemba mwaka jana, hiyo ndiyo idadi kubwa ya wapinzani 139 kujiunga na CCM.
Hapo kabla nilikua napenda sana kuangalia Movie za Vita kati ya Marekani v/s Vietnam. Hawa Vietnam tulikua tukiwaitaga "Wavete". Hizi movie za "Wavete" sifa yao kuu ilikua kwamba movie moja wanaigiza wengi sana hawa "wavete".

Yaani Sterling anaweza akawa anamimina risasi sehemu moja wanakufa kama 30 hivi lakini akisonga mbele anaenda kuwakuta wengine nyomi vilevile. Au hata hapo hapo alipoawaua hao 30 wanatokea wengine tena wengi tu. Waweza kuta Wamarekani Masterling (Makomandoo) wako wachache lakini hawa "Wavete" walikua wa kumwaga tu.

Sasa bana nikawa najiuliza kwenye malipo "in reality" inakuaje. Yaani kama Movie moja wamekufa "Wavete" zaidi ya 200 watalipwaje sasa Moie ikishauzwa? Si wakigawana masterling na hao wavete 500 kutakua hakuna faida? Na wanawapata wapi watu wote hao 500 wa kuigiza? Hili swala nilikua nalifikiria sana kipindi hicho.

Sasa bana miaka ya hivi karibuni nkasema nifanye ka utafiti nini ilikua inatokea that time. Kumbe bana wale "Wavete" walikua labda 20 tu hivi moie nzima, sema kila wakiuliwa camera inavyohama nao wananyanyuka tena na kwenda kuigiza kwengine.

Movie mmoja inaweza kuonyeshwa "Wavete" hata 500 kumbe ni hao hao 20 tu labda, sema ndio wanahama hama tu location
sema sababu ya nyuma ya pazia hatuyajui ndio maana tunadhani wako wengi sana hao "Wavete"
.
Nimekumbuka sana huu mchezo baada ya kuisoma hii thread.
 
Back
Top Bottom