MANYARA: RC Mnyeti avunja Baraza la Kata

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amelivunja baraza la ardhi la Kata ya Murray wilayani Mbulu mkoani Manyara baada ya wananchi kulalamika kunyanyaswa, kuombwa rushwa na kunyimwa haki zao.

Akizungumza jana Februari 12, 2018 baada ya kulivunja baraza hilo, Mnyeti amesema hawezi kuliacha liendelee kufanya kazi kwenye eneo hilo wakati wananchi wanalalamikia kukosa haki zao.

Amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Mbulu, Anna Mbogo kuanza mchakato wa kupatikana viongozi wapya, waadilifu wa baraza la kata hiyo ili waendelee kuwatumikia wananchi.

Amesema mikutano ya wananchi kuwachagua wajumbe wengine inatakiwa kuanza upya ili nafasi za wajumbe wapya zipatikane na kuhudumia jamii ya eneo hilo.

"Tafuteni watu waadilifu, wenye weledi na hofu ya Mungu ambao wanaweza kuwahudumia wananchi ili washike nafasi hizo na kutekeleza majukumu yao ipasavyo," amesema Mnyeti.

Amesema kuwa baada ya kuwaondoa viongozi wa baraza hilo linalodaiwa kupokea rushwa wananchi waendeshe zoezi la kupatikana majina mapya kisha yapelekwe kwenye vyombo vya uchunguzi.

Mkazi wa kata ya Murray, Michael Amme amelalamikia baraza hilo akidai kuwa halitendi haki na kuwaonea wananchi wanyonge.

Amme amesema kwa muda mrefu walikuwa wanalalamikia uamuzi wenye harufu ya rushwa kwa maelezo kuwa familia yao iliporwa eneo kutokana na maamuzi mabovu ya baraza hilo.

Soma: Mkuu wa Mkoa Dar aheshimu sheria zilizopo
Hata hivyo, mjumbe wa baraza hilo Verani Anthony amesema wananchi wa eneo hilo wanapaswa kupatiwa elimu juu ya utendaji kazi wao.
Amesema wananchi hao wangepatiwa semina juu ya baraza hilo wasingelalamika kwani wao hutekeleza wajibu wao ipasavyo.

Pia, Mnyeti amemuagiza mkuu wa polisi wilaya ya Mbulu, kumkamata Mwenyekiti wa kijiji cha Murray, John Amme kwa kuwanyanyasa wananchi yakiwamo madai ya kuwapiga.

"OCD mkamate huyo mwenyekiti wa kijiji hiki ili akaeleze huko polisi kwa nini amemvunja mkono mwananchi kwa sababu kupiga watu si wajibu wake," alisema Mnyeti.
 
Mnyeti hapendi rushwa kwa kweli. Amejawa hofu ya mungu
KWELI KABISA

screenshot_20171209-155734-png.647023
 
kila mkuu wa mkoa na wilaya ni hakimu na jaji.wanasikiliza upande mmoja bila mashahidi nakutoa hukumu.safari ni ndefu tunakoenda ipo watajitangaza kuwa rais kwa mamlaka waliokuwanao KWENYE MIKOA YAO
 
Haya.........wanaiga kutoka juuu hawa...ila poa tu...fresh...tutapnana motoni mamaeee
 
Naona awamu hii
Hapa kazi tu

Itanyoosha wengi waliokuwa na mazoea mabaya na wengineo
 
Kuna mdada anaishi Usagara Misungwi akikupa issue za huyu bwana kabla hajateuliwa ukuu wa Wilaya utakaa chini.

By the way ni shwahiba mkubwa wa Kitwanga
 
Leo nimesoma Mwananchi kuwa ilibidi Wizara ya Tamisemi ilimwandikia barua Makonda afafanue kuhusu kufuta mabaraza ya kata.

Makonda amekanusha kufuta mabaraza ya ardhi kwa mjibu wa msemaji wa Tamisemi.

Sasa na huyu anarudia yale yale, kweli baba ukipoteana hata watoto ni rahisi kupoteana.
 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amelivunja baraza la ardhi la Kata ya Murray wilayani Mbulu mkoani Manyara baada ya wananchi kulalamika kunyanyaswa, kuombwa rushwa na kunyimwa haki zao.

Akizungumza jana Februari 12, 2018 baada ya kulivunja baraza hilo, Mnyeti amesema hawezi kuliacha liendelee kufanya kazi kwenye eneo hilo wakati wananchi wanalalamikia kukosa haki zao.

Amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Mbulu, Anna Mbogo kuanza mchakato wa kupatikana viongozi wapya, waadilifu wa baraza la kata hiyo ili waendelee kuwatumikia wananchi.

Amesema mikutano ya wananchi kuwachagua wajumbe wengine inatakiwa kuanza upya ili nafasi za wajumbe wapya zipatikane na kuhudumia jamii ya eneo hilo.

"Tafuteni watu waadilifu, wenye weledi na hofu ya Mungu ambao wanaweza kuwahudumia wananchi ili washike nafasi hizo na kutekeleza majukumu yao ipasavyo," amesema Mnyeti.

Amesema kuwa baada ya kuwaondoa viongozi wa baraza hilo linalodaiwa kupokea rushwa wananchi waendeshe zoezi la kupatikana majina mapya kisha yapelekwe kwenye vyombo vya uchunguzi.

Mkazi wa kata ya Murray, Michael Amme amelalamikia baraza hilo akidai kuwa halitendi haki na kuwaonea wananchi wanyonge.

Amme amesema kwa muda mrefu walikuwa wanalalamikia uamuzi wenye harufu ya rushwa kwa maelezo kuwa familia yao iliporwa eneo kutokana na maamuzi mabovu ya baraza hilo.

Soma: Mkuu wa Mkoa Dar aheshimu sheria zilizopo
Hata hivyo, mjumbe wa baraza hilo Verani Anthony amesema wananchi wa eneo hilo wanapaswa kupatiwa elimu juu ya utendaji kazi wao.
Amesema wananchi hao wangepatiwa semina juu ya baraza hilo wasingelalamika kwani wao hutekeleza wajibu wao ipasavyo.

Pia, Mnyeti amemuagiza mkuu wa polisi wilaya ya Mbulu, kumkamata Mwenyekiti wa kijiji cha Murray, John Amme kwa kuwanyanyasa wananchi yakiwamo madai ya kuwapiga.

"OCD mkamate huyo mwenyekiti wa kijiji hiki ili akaeleze huko polisi kwa nini amemvunja mkono mwananchi kwa sababu kupiga watu si wajibu wake," alisema Mnyeti.
Dunia ina mambo! Utafikiri yeye nyeti ni muadilifu na mwenye hofu ya Mungu..Mungu ikimbize miaka haraka we are tired with thuis people!
 
Litakuwa lina chembechembe za uchadema hili.
Huyu ni kati ya wakuu wa mikoa wa hovyo kabisa Na wapumvavu kuwahi kutokea
 
Back
Top Bottom