Manyanyaso ya TRA kwa wafanyabiashara wa Mbao

Manyanyaso ya TRA kwa wafanyabiashara wa Mbao

Hardrock2019

Member
Joined
Feb 26, 2019
Posts
10
Reaction score
14
TRA ni kero kubwa sana katika kukuza mazingira ya biashara.Unakuta mtu una kijiwe cha biashara ya mbao katika mji fulani, huko unakuwa umelipia leseni ya biashara, kibali cha TFS na kodi za tra pia umelipa.

Unakuta mtu unaenda iringa kufata mbao ambazo hununui kwa mtu ni kwamba kule iringa unakuwa unanunua mashamba ya miti ambayo bado haijakomaa ikikomaa unakuwa unavuna mbao zako mwenyewe.

Ukivuna mbao ukiwa unazisafirisha TRA barabarani wanakukamata wanataka uwape risiti ya manunuzi kuonesha ni wapi uliponunua huo mzigo na gharama yake.

Ukiwaonesha barua ya Mtendaji wa kijiji ulikotoka kuonesha huo mzigo umevuna kwenye shamba lako hawakubali wanakamata mzigo.

Na hapo unakuwa una vibali vyote kibali cha maliasili kukutambuliasha wewe ni mtu unaedeal na mbao na kodi za TRA unalipa.

Kero yangu,TRA ukiwakuta njiani wanakusimamisha na kuzuia mzigo wako wanakudai risiti ya manunuzi ya mzigo unaotoka shamba,sasa hii risiti mimi ntaitoa wapi wakati mzigo nimetoka kuuvuna shambani?

Hii imekuwa ni kero kubwa sana.
 
Tax officers wa tiaraei wana matatizo sana. Wanajikuta miungu watu wale kama wana share na hii nchi what you’ve said is very deep and ingenious. Wananyanyasa wafanyabiashara sana
 
Tax officers wa tiaraei wana matatizo sana. Wanajikuta miungu watu wale kama wana share na hii nchi what you’ve said is very deep and ingenious. Wananyanyasa wafanyabiashara sana

Mkuu kuna vitu wanazingua sana kwa kweli,ivi ni sawa na mtu awe kabeba mahindi kutoka shamba unamwambia naomba risiti ya manunuzi ya hayo mahindi
 
Wanalazimisha kila kitu kiwe wanavyotaka wao. Biashara ni tofauti sana siku hizi hasa za mbao. Wanakijiji wengi waauza miti ikiwa nado midogo kwa uhitaji wa hela.

Sasa hizo risiti zinatoka wapi basi wapige kambi vijijini kujihakikishia.
 
Mlikataa wokovu ukaenda kwa mataifa kwa hiyo ni vyema na haki mkakiona cha mtema kuni!
 
Hawa tulishawasema lakini hawaelewi wewe umelipa ushuru na risiti unayo haya hiyo ya manunuzi kwa mali ya shambani utaipata wapi?
 
Tra sio watu friendly, ni jitu linalotisha sana jitu hilo alijari hisia za watu japo wakati fulani sisi watanzania ni watu wajanja wajanja sana so wanafahamu hilo ndy maana wanatumia nguvu nyingi
 
Kuna TRA wa ofisi na wamitaani hapo tunakuta vitu viwili kazi tofauti
 
Dawa ni kuwafungulia kesi mahakamani wanakutia hasara wakufidie, ukifanya hivo watajifunza
 
Ni sawa na Azam awe na risiti ya mzigo wa juisi anazotoa kule kiwandani
 
Siku hizi wanataka mzigo uwe na EFD receipt (VAT), gari unalosafirishia mzigo
waonyeshe receipt (VAT) ya nauli ya mzigo husika, etc etc.
 
Mkuu kuna vitu wanazingua sana kwa kweli,ivi ni sawa na mtu awe kabeba mahindi kutoka shamba unamwambia naomba risiti ya manunuzi ya hayo mahindi
Utaratibu uko hivi, pale unaponunua miti shambani kwa mtu tengeneza mkataba simple wa mauziano na mshirikushe VEO wa kijiji husika ili awe shahidi na agonge muhuri (kuna malipo kidogo utalipa kijijini na kupewa risiti but itakuwa msaada baadae). Hizo documents ndizo utaenda nazo TFS kupata TP na vibali vingine.
 
Nauliza.
Ni kitu gani hii serikali ya awamu ya tano imefanya kuinua Maisha ya mtanzania. Mimi naona nabanwa kila upande. Kila uchao wanabuni mbinu za kuniumiza zaidi. Walishanivunjia nyumba zangu bila fidia. Kwenye uchaguzi ndio waliniacha hoi. Mbunge waliomchagua anahitaji kuongozwa.
1. Ukisema wamejenga flyover Mimi nakaa Handeni hainisaidii.
2. SGR. kwanza nasikia haijaisha
3. Barabara ya baharini huko siitumii.
4. Sijawahi panda ndege hata hili Hajees nauli yake ziiwezi nikija Dar napanda fuso.

Wenzangu Kama Kuna aliyefanyiwa wepesi na hii awamu atuambie I could be missing something.
 
Umenichekesha mzee wa "Chanika".
 
Pole tumia transfer pricing...
Fungua kampuni mbili.. Moja ya uzalishaji nyingine ya trading.. Mfano unaweza kuwa na ABC plantation and Forestation Ltd na nyingine ikawa ABC general trading ltd.
Hiyo ya plantation inamuuzia mzigo hiyo ya trading at transfer price!
 
Back
Top Bottom