Manyanyaso kwenye ndoa

Mzee makoti

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2016
Posts
5,290
Reaction score
8,230
Wakuu kuna Binti ndoa yake Ina changamoto sana ye na mumewe....mumewe anamnyanyasa mno,kwa kushirikiana na mama mkwe,yaan mama mkwe katoka mkoani hadi mjini anapoishi mwanae wa kiume,ili tu aje kupambana na mke mwana ili aondoke!

Picha linaanza jamaa amuachii hela ya kula mkewe,watoto anawapa hela wakale kwa mama lishe, mama mkwe anamuambia mwanae kuwa Kijijinj tayari washamtafutia mke mwingine amtimue huyu wa sasa, na wamezaa watoto wawili! Na Wana nyumba!

Kesi yao ishafika serikali za mtaa lakini anasema wanamzingua tu, ni hatua gani anaweza kufuata huyu binti apate haki yake,. Alitegemea ujio wa mama mkwe utaleta suluhu ya mgogolo wao,lakini imekuwa ni kinyume chake!
Nini afanye! Hatua gani afuate labda?
 
Hii story y upande mmoja kiongozi. Lazima kuna chanzo kutoka kwa Dada yako sema ukweli. Ili wanajamii wakusaidie. From no whare achukiwe,ateswe na kunyanyasika Big NO kiongozi.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Hapa si suala la kuvumilia manyanyaso kwa sababu tu wameoana. Kama kweli hali iko hivyo, huyo dada aanze kuhifadhi ushahidi wa manyanyaso, vitisho, kunyimwa mahitaji ya msingi na matukio mengine muhimu.

Kwa kuwa tayari amefika Serikali ya Mtaa bila kupata suluhisho, anaweza kutafuta msaada wa ustawi wa jamii na dawati la jinsia la Polisi, hasa kama kuna vitisho au ukatili. Pia atafute ushauri wa kisheria kutoka kwa msaada wa sheria/wanasheria ili ajue haki zake kuhusu watoto, matunzo na mali ya ndoa.

Muhimu zaidi, asifanye uamuzi wa kukabiliana na mume au mama mkwe kwa nguvu. Kama kuna hatari ya usalama, aweke usalama wake na wa watoto kwanza. Mama mkwe kuwa upande wa mwanawe hakumpi haki ya kumtesa au kumfukuza mkwewe kwa vitisho.
 
Kweli kabisa
 
Abebe watoto arudi kwao, akiwa huko aende mahakamani kufile madai ya talaka ili apate mgao WA nyumba (maana ndio shida yake)..ajue sio kitu cha siku Moja, inaweza kuchukua miaka hata mitano. Hawamtaki wameshamchoka, anaweza Akawa yeye ndio sababu hatuwezi jua. Cha muhimu mapenzi yakiisha yameisha, hayalazimishwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…