Manunuzi ya nguo zimwi linalomaliza pesa za wanawake

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,513
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari tajwa hapo juu, Kama ilivyo katika watu wanaoongoza kuwa na nguo ni wanawake.

Hii yote hutokana na kutaka kuwa na muonekano mzuri na utanashati.

Pia mavazi hayo yanafanya mwanamke kuwa mrembo zaidi kulingana na aina ya mavazi.

Kuna aina nyingi za mavazi yanayopendwa sana na wanawake.

Mojawapo ya mavazi hayo ni yale ya casual, official na wedding guest.

Leo tutazungumzia mavazi ya aina mbili ya casual ambayo ni suruali za aina mbalimbali, blouse za aina mbali mbali, vigauni.

Haya mavazi ya mitoko ya weekend yaani casual na mitoko ya hapa na pale ni moja ya mavazi yanayonunuliwa bila mpangilio wa pesa, maana mwanamke akiiona tu nguo ukute ni blouse au jeans, zimwi linaamka hata kama hakupanga kununua atanunua tu.

Nguo zingine ananunua lakini havai kabisa utakuta kabati limejaa akitaka kuvaa anavurugwa kichwa mpaka avuruge kabati.

Mavazi mengine ni pamoja na mavazi ya sherehe, ambayo ni yale magauni ambayo wanavaa kama wedding guest.

Huwa magauni hayo yanatumia gharama nyingi sana, ila hata kama pesa akupangilia ananunua wala hajali.

Mbaya zaidi magauni haya yanaendana na rangi husika ya wakati huo au rangi ya ukumbi, pia na fashion husika hivyo humlazimu kila sherehe kununua nguo.

Zimwi hili la kununua nguo limekuwa likiwatesa sana mabinti wengi na wengine wamejikuta wakidanga ili wanunue nguo zinazokwenda na wakati.

Ukija katika ndoa yani wanawake hasa wale wa uswahilini pamoja na mama wa nyumbani ambao hawana kazi wamekuwa wakibana pesa za waume zao za matumizi kama mlo kamili ambazo wanaachiwa wanabana ili wanunue nguo.

Zimwi hili halijaishia hapo linawafanya wanawake kuwa watumwa wa kwenda na wakati ambao wakati huo hauendi na wao.

Isipokuwa wakati huo umegeuka zimwi ambalo limekuwa likipoteza pesa zao.
View attachment 2320322
 
Waafrika wengi tumeiaga Western Consumerism.....
Kitu ambacho hakishabihiani kabisa na uhalisia wa chumi zetu hapa Afrika....
Walau wenzetu vile viwanda vya nguo huwepo nchini kwao hivyo bei huwa chini, sisi huwa tunaagiza!
Dada anataka Balenciaga, Michael Kors, Givenchy, Ralph Lauren, Prade halafu mshahara tsh 600,000/=

Hapo kwenye sherehe wanawake wa uswahilini wameweza sana.....
Wao ni full kushonesha sare ya madera ya tsh 10000/=.............

Lakini pia wanawake wa kiislamu wameweza sana,.......
Wao huvaa hijab 24/7, kitu cha gharama kwao ni Perfume tu.......
 
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari tajwa hapo juu, Kama ilivyo katika watu wanaoongoza kuwa na nguo ni wanawake.
Yaani Donatila jinsi nyie wanawake mnavyopagawa na kuchanganyikiwa pindi mkiona nguo nzuri, pochi au kiatu dukani, na mnahakikisha lazima mkipate ndio ivyo ivyo na sisi wanaume tunajisikia tunapomuona demu mkali njiani. So mkome na maswali yenu eti " kwanini unatamani mwanamke wa nje wakati una mke mzuri ndani?" 😄😄😄
 
Yaani Donatila jinsi nyie wanawake mnavyopagawa na kuchanganyikiwa pindi mkiona nguo nzuri, pochi au kiatu dukani, na mnahakikisha lazima mkipate ndio ivyo ivyo na sisi wanaume tunajisikia tunapomuona demu mkali njiani. So mkome na maswali yenu eti " kwanini unatamani mwanamke wa nje wakati una mke mzuri ndani?"
Tumekoma
 
Tabia ya kutokuridhika Ni Asili yenu.
Yani akiona jua anaitaka ila akiangalia jua haipo kichwan labda afosi tuuh.
 
zaidi ya saa nzima mtu aliniweka eti anatafuta nguo ya kuvaa..

mtu kabati limejaa na kuna nguo zina zaidi ya mwaka hazijavaliwa.

Kimbembe siku nikamwambia embu chambua ambazo hazitakiwi tukazigawe alipata sijui mbili tu.😂 Kila hiyo anaiona nzuri tena, kiruuu....😀
 
Back
Top Bottom