Manumba: Polisi lipizeni kisasi

Manumba: Polisi lipizeni kisasi

Katka kile ambacho hata mm ckutarajia kukisikia kutoka kiongozi mkubwa kama Manumba n kauli yake ya jana wakati wa kukumuaga marehem Barlow kua watalipiza kisasi kwa yeyote aliyehusika!....

kama police wataanza kujichukulia sheria mkonon tena kwa kutanganza hadhari kuua raia n dhahiri kua hatuna viongoz wala sheria hazifuatwi tena hapa TZ

.
Kwa kauli hii ya Manumba ni wazi sasa Taifa limeruhusiwa rasmi kulipizana visasi.
Wakristo ruhsa sasa kulipiza kisasi kwa waislamu waliobomoa makanisa yao.
Waandishi wa habari nao walipize kisasi kwa jeshi la polisi lililomuua Mwangosi.
Ndugu wote waliouliwa jamaa zao na polisi kwa kisingizio cha kujibizana risasi nao walipize kisasi, kwani sii kazi ya polisi kuua bali kukamata wahalifu na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Nchi ya kulipizana visasi tutafika? Ngoja tuone!
Kwa yatakayotokea tanzania soon na hakuna tena namna ya kuzuia yasitokee, Manumba namwona akiwa miongoni mwa waliopelekwa kujibu mashtaka katika mahakama ya kimataifa.
 
Kama ni kweli alisema...basi hisia zilitawa zaidi ya akili yake baada ya kumwona kamanda mwenzake akiwa amelala milele kwa kupigwa risasi za shingo.
Mwenye mamlaka hatakiwi kuongozwa na hisia bali sheria. Mitaani mob justice, na polisi wanalipigia kelele tuache kuchukua sheria mkononi sasa leo wao wanatangaza kujikulia sheria mkononi!

Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo.
 
Katka kile ambacho hata mm ckutarajia kukisikia kutoka kiongozi mkubwa kama Manumba n kauli yake ya jana wakati wa kukumuaga marehem Barlow kua watalipiza kisasi kwa yeyote aliyehusika!....

kama police wataanza kujichukulia sheria mkonon tena kwa kutanganza hadhari kuua raia n dhahiri kua hatuna viongoz wala sheria hazifuatwi tena hapa TZ

Hata mimi sikuamini masikio yangu pale nilipomsikia kiongozi mwandamizi wa Jeshi la Polisi akijiapiza mbele ya umati wa waombolezaji kwamba WATALIPIZA KISASI.

Nikabaki najiuliza kwamba hivi Tanzania kweli tunalo Jeshi la POLISI or We have A BUNCH OF JANJAWEED!
 
Katka kile ambacho hata mm ckutarajia kukisikia kutoka kiongozi mkubwa kama Manumba n kauli yake ya jana wakati wa kukumuaga marehem Barlow kua watalipiza kisasi kwa yeyote aliyehusika!....

kama police wataanza kujichukulia sheria mkonon tena kwa kutanganza hadhari kuua raia n dhahiri kua hatuna viongoz wala sheria hazifuatwi tena hapa TZ

hii kauli hata mimi ilinistua. katika nchi zenye uadilifu jamaa angefutwa kazi mara moja
 
MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba amewataka Polisi kuhakikisha wanalipa kisasi dhidi ya mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow (53).

Akitoa salamu za polisi, wakati wa ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Barlow, DCI Manumba alisema polisi wamefundishwa kuwa watulivu wakati wa hatari, lakini kwa kifo cha kamanda huyo "wanatakiwa kulipiza kisasi" kwa kuwakamata waliohusika.
"Wakati wa hatari, askari tunafundishwa kutulia, ninawashukuru askari mlitulia, lakini katika hili ninawataka kuhakikisha mnalipa kisasi kwa waliohusika, kwa kuwakamata wote walioshiriki mauaji haya," alisema Manumba.

Mwili kwa Kamanda Barlow aliyeuawa na watu wasiojulikana usiku wa Oktoba 13, mwaka huu, uliagwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi katika ibada iliyofanyika katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.

Ibada hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo na viongozi mbalimbali, wakiwamo makamanda wa polisi wa mikoa ya Tabora, Shinyanga, Geita, Mara, Kagera na Simiyu.DCI Manumba alisema ulipizaji huo wa kisasi lazima ulenge kuwakamata washiriki wa matukio mengine ya mauaji kama yale ya albino pamoja na wazee vikongwe kwa sababu za imani za kishirikina.

Kuhusu upelelezi wa tukio hilo, Manumba alisema ushirikiano walioupata kutoka kwa wananchi umefanikisha kazi hiyo kufikia hatua nzuri kwani tayari wamewabaini baadhi ya watuhumiwa."Taarifa mlizotupa zimetusaidia na muda si mrefu tutakuwa tumemaliza kazi na wale wote waliotusaidia watakuwa wadau wetu," alisema DCI Manumba na kuongeza:

"Tabia mbovu za kutekeleza mauaji kwa kujichukulia hatua mikononi, yakiwamo yale ya vikongwe na albino bila ya kujali uwepo wa Mahakama ni changamoto, Watanzania wanatakiwa kutafakari wapi wanalipeleka taifa hili."

Alisema Jeshi la Polisi limejipanga kukabiliana na uhalifu wa namna hiyo kwa sababu wahalifu hawana dini wala kabila na kuwataka wananchi kuimarisha ulinzi shirikishi kutokana na uchache wa askari katika jeshi hilo.

Ibada ya kuaga
Ibada ya kuaga mwili wa kamanda huyo iliongozwa na Padri Raymond Manyanga wa Parokia ya Nyakahoja.

Akizungumza katika ibada hiyo, Waziri Lukuvi aliwataka wananchi wa Mwanza kuwa na imani na Serikali yao akisema ipo kwa ajili ya kuwalinda pamoja na mali zao.

Lukuvi alisema kuuawa kwa Barlow hakuwezi kusababisha kuvurugika kwa amani katika mkoa huo kwa kuwa Serikali ipo makini kulinda usalama wa nchi.

Katika salamu zake za Mkoa wa Mwanza, Ndikilo alisema katika kipindi hiki, polisi hawataweka silaha chini na watasonga mbele mpaka hapo ushindi wa kuwakamata wauaji utakapopatikana. Alisema vyombo vya usalama vimepanga kuhakikisha vinawawajibisha wahusika wa mauaji hayo ambayo aliyaita ya kinyama.

Alisema mkoa umepata pigo kwa kuwa Kamanda Barlow alikuwa mtu mwenye ushirikiano akimsifia kwa ushirikiano wake wa kuhakikisha Mkoa wa Mwanza unakuwa salama.

"Tangu Kamanda Barlow alipoteuliwa kuja katika mkoa huu, amefanya kazi nzuri ya kuhakikisha usalama wa Wana - Mwanza pamoja na mali zao na kukomesha mauaji ya albino, vikongwe pamoja na ujambazi wa majini na barabarani," alisema Ndikilo.

Padri Manyanga alimwombea msamaha marehemu kwa wale wote ambao aliwakosea na kuwataka wamwombee ili apumzike kwa amani.

Alisema hategemei katika kazi aliyokuwa akifanya marehemu asiwe na maadui kwa sababu yeye ni binadamu kama walivyo wengine... "Marehemu alijitahidi kuwatumikia Watanzania kwa kuhakikisha kuwa haki inatendeka. Kama alikuwa na upungufu, basi alikuwa kama watu wengine ila kwa uwezo wake Mungu alimjalia kufanya kazi yake. Maisha ya mwanadamu ni zawadi kutoka kwa Mungu, hakuna mtu ambaye ana haki ya kutoa uhai wa mtu yeyote."

Salaam za Kikwete
Rais Jakaya Kikwete ameliagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha linachukua hatua za lazima kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria watu wote wanaotuhumiwa kupanga na kutekeleza mauaji ya Kamanda Barlow.

Katika salamu za rambirambi alizompelekea Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Saidi Mwema, Rais Kikwete amesema ameshtushwa na kuhuzunishwa na mauaji hayo.

"Nimepokea kwa mshtuko mkubwa na huzuni nyingi taarifa za kifo cha ACP Barlow kilichotokea usiku wa Ijumaa katika jiji la Mwanza ambako watu wasiojulikana walimpiga risasi na kumuua ofisa huyo mwandamizi wa Jeshi letu la Polisi," alisema na kuongeza:

"Historia ya ACP Barlow ni ya mfano katika utumishi wa umma na hususan katika Jeshi la Polisi. Kwa hakika, Jeshi la Polisi limempoteza kamanda hodari na wananchi wa Tanzania, hususan wale wa Mkoa wa Mwanza, wamempoteza mlinzi shupavu wa usalama wao na mali zao."

Mwili wa Barlow uliwasili Dar es Salaam jana na leo utaagwa nyumbani kwake Ukonga kuanzia saa 6:00 mchana kabla ya kupelekwa katika Kanisa Katoliki Majumba Sita kwa ajili ya misa na watu mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho.

Wasifu wa Barlow
Marehemu Barlow alizaliwa Desemba 26, 1959 mkoani Kilimanjaro na kusoma katika Shule ya Msingi Lombeta Moshi Vijijini na kuhitimu mwaka 1974.Mwaka 1979 alimaliza elimu ya sekondari katika Shule ya Seminari Maua na mwaka 1981 alijiunga na Shule ya Sekondari Mirambo, Tabora katika mchepuo wa Lugha.

Mwaka 1982 aliajiriwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Iringa na mwaka huohuo alijiunga na Chuo cha Polisi Moshi kusoma sheria ya uhamiaji. Baada ya kuhitimu, mwaka 1984 aliajiriwa katika Idara ya Uhamiaji na kupelekwa katika ofisi zake za Mkoa wa Mtwara.

1984 alitunukiwa shahada ya kwanza ya utawala mafunzo, Chuo cha Polisi Dar es Salaam na baadaye kupata mafunzo ya ukaguzi mnamo mwaka 1987.

Mwaka huohuo wa 1987 alihamishiwa Polisi na kuanza kazi katika makao makuu ya Idara ya Upelelezi.

Katika uhai wake, aliwahi kufanya kazi katika Wilaya ya Musoma, Mkoa wa Kigoma kabla ya kupandishwa cheo na kuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi na kufanya kazi ya kuongoza jeshi hilo katika mikoa ya Mara na Tabora kabla ya kuhamishiwa Mwanza.

Chanzo: Mwananchi
 
Sikutegemea Maneno Kama haya yangetolewa na Mtu yeyote Mwenye Busara Katika Hili Taifa
 
namlilia sana mwangosi, muuza magazeti moro, shujaa yule wa arusha! Mbona hakukuwa na kauli km hizi?
 
Wametuua vya kutosha hawa polisi,yaliyotokea kwa barlow ni sauti ya wananchi kuchoshwa na ukatili wa jeshi la polisi,na kibaya zaidi wanatetea serikali ambayo hata wao wenyewe haiwajali,haiji akilini msiba mkubwa kama huu umetokea rais ndo kwanza anaondoka kwenda kupanda farasi oman,hili ni funzo kwa mapolisi kuwa wanayemtetea hana habari nao,endeleeni kujikomba mtapukutika mmoja mmoja mpaka mtakwisha,wananchi wameshaamua

Tatizo Hawa Watu Hawajikombi ila wamekuwa ni Kundi la Maharamia!! Ukiona Gari la polisi ewe ndugu Yangu kimbia!! Kwani wametangaza Vita na raia wasiokuwa na Hatia!!
 
Nilisikiliza hiyo taarifa.
Nitakusahihisha kidogo mtoa mada. Manumba alisema watalipiza kisasi kwa kuhakikisha wale wote waliohusika kumuua kamanda wanakamatwa na kuchukuliwa hatua stahili.

Kama watawakamata na kuwapeleka kwenye sheria hapo kuna kisasi? Neno kisasi lina maana kumtenda adui kwa kiwango kilekile alichokitenda. Na hii ndo haki ya jino kwa jino. Manumba kwa kutumia neno 'kisasi' alimaanisha hilo, yaaani kummaliza muuaji.
 
Kuna uwezekano mkubwa sana wahusika halisi wasipatikane kabisa, ila raia wengine wasio na hatia watakamatwa na kuuwawa ili ku-sympathy situation.
Omba Mungu atakaye kamatwa usiwe wewe, ndugu yako, rafiki yako au jirani yako.

Mimi mara nyingi najiuliza kwani hawa polisi baba zao,mama zao na ndugu zao wote ni mapolisi?
kama jibu ni la chuki hii polisi wanayokuwa nayo kwa raia inatoka wapi,maana kama si ndugu yake
yeye basi ni ndugu wa polisi mwingine mahali fulani."Polisi Think Twice"
 
nimegundua vilaza na aoga ni wengi, mbona kauli haikuishia hapo? amesema walipe kisasi kwa kuwakamata waliomuua xaxa we unaogopa nn kwani we ndo muuaji. au mnajisahaulisha kuwa hamjui kama moja ya kazi zao ni kukamata wahalifu?! najua kwa baadhi yenu wauaji wale si wahalifu ndo mana mnashangaa
 
hii n kaul yake mwenyew na amekaririwa hadi kwenye TV's na baadhi ya magazeti ya leo

Naona hiyo ni kauli mbiu yao baada ya hili tukio,kuna askari nafanya nae kazi ana cheo kikubwa tu aliposikia taarifa za kuuwawa Barlow alisema waliomuuwa lazima watapatikana na ni lazima watauwawa.
 

Habari nilizoipata kutoka chanzo cha uhakika kabisa zinasema aliyekuwa mchezaji wa kutumawa wa Pamba FC ya Mwanza Fumo Felicia pamoja na ndugu yake mwingine wametiwa mbaroni siku ya jana jioni kwa kuhishwa ktk 'mchongo' wa mauaji ya RCP,


Inasemekana Fumo ni mdau wa karibu sana na 'amewekeza' kwa mwalimu Doroth, mwanamama
ambaye mara kwa mara alikuwa ‘akisindikizwa vichochoroni' na marehem kamanda Barlow


Jitihada za ndugu na marafiki kujaribu kuwatoa akina Fumo ‘lockup' zinaendelea vizuri


Nitazidi kuwajulisha yanayojiri.
 
Hakuna utawala wa sheria! Manumba anafanya atakalo Waislam pia
 
jamani kweli the great thinkers tunajadili heading na kuacha maudhui? jamani dci kafunguka vizuri saana lazima tukubali kila jambo, lina mwanzo wake na mwisho wake.1.namaanisha mwanzo ktk maelezo yangu, hivi kweli kiongozi mkubwa wa mkoa anauwawa na wauwaji wanafanikiwa kujificha, khali ya usalama kwa wananchj wa kawaida inakuwaje? hapo lugha ya kikamanda lazima itumike na si kutumika tu ilete mrejesho wenye tija 2. hapa namaanisha mwisho jambo kama hili na mengine yasitokee na jeshi la polisi pamoja na wadau wake wajizatii kulinda na kutetea haki za wanyonge ahsanteni
 
Kwa habari za nyuma ya pazia uyu RPC ameuliwa na askari waliokua chini yake baada ya kuchoshwa na tabia yake ya kutembea na wake zao.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Watalipiza! Hii kauli sio nzuri! kazi ya polisi ni kulinda raia sio kuwaua! chondechonde Manumba msitumie vitu vizito kwa hao watuhumiwa wa mauaji.

Hapana, mimi nimemsikia LIVE. Amesema kuwa polisi "WALIPIZE KISASI KWA KUHAKIKISHA KUWA WANAWAKAMATA WALE WOTE AMBAO WAMEHUSIKA." Tafadhali musim-qupote vibaya.

After all, majeshi yetu yalivyojaa wasomi siku hizi unadhani kuna askari unaweza ukamwambia alipize kisasi na yeye akaondoka kichwa kichwa bila kuhoji kwa nini unamwambia hivyo? Siyo kweli hata kidogo!
 
na kawaida visasi haviishagi, kuna hatari zaidi huko tuendako. :hatari::hatari:
 
Anajuaje pengine hata hao wauaji nao walikuwa wanalipiza kisasi baada ya kudhulumiwa jambo?

Maisha ya dhuluma na maonevu ndio hupelekea haya. Tuishi kwa kiasi na haki hata kama tuna madaraka makubwa. Siamini watu wanaweza kumpiga mtu risasi halafu wasichukue kitu na bado tuseme hao ni majambazi.

WanaJF, kuna wafanyabiashara wa5 wa madini waliuawa msitu wa Mbande miaka kadhaa iliyopita tukiaminishwa kuwa walikuwa majambazi. Madini yao yaliporwa na maisha yao vilevile. Familia zao zimekumbwa na dhiki na hakuna msaada kwao. Hukumu wote tuliisikia. Je mambo kama haya hayatoshi kutufikisha kwenye matukio kama haya?
 
Back
Top Bottom