Manumba asema kile chama cha Kiislam kinachunguzwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manumba asema kile chama cha Kiislam kinachunguzwa

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Lunyungu, Jul 23, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Date::7/22/2009Polisi wafufua kitengo cha kuchunguza uhalifu mtandaoni[​IMG]Na Patricia Kimelemeta

  JESHI la Polisi limeunda timu ya kuchunguza matukio ya uhalifu kwa njia ya mitandao, simu za mikononi, ATM za mabenki na huduma nyingine za mitandao cha Ant cyber crime Unity ili waweze kubaini watu wanaotumia mitandao hiyo, kinyume na taratibu.

  Hatua hiyo, imekuja baada ya kutokea matukio ya wizi katika ATM za benki, wananchi kutumiana ujumbe wa matusi kupitia mtandao na simu za mikononi na kusababisha usumbufu kwa wananchi.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, (DCI) Robert Manumba alisema matukio hayo, yameibuka nchini hivi karibuni na kusababisha baadhi ya wananchi kupata matatizo.

  Alisema wananchi wengi wamekuwa wakitumia mitandao hiyo, kinyume na taratibu, na kusababisha upotevu wa fedha.

  Alisema kutokana na hali hiyo, jeshi hilo litawashughulikia wananchi wote watakaobainika kufanya vitendo hivyo, kinyume na taratibu.

  “Kuna baadhi ya wananchi wanatumia mitandao vibaya, baadhi ya wanatumia ili waweze kuwatukana wenzao, wengine kuiba na kusababisha malalamiko mengi kutokea,” lisema Manumba.

  Alisema timu hiyo, itahakikisha wanaofanya vitendo hivyo, wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.

  Manumba alisema hivi sasa wanaboresha timu hiyo ili iweze kufanya kazi na kwamba anaamini mpango huo, utafanikiwa.

  Alisema timu hiyo, ilikuwepo muda mrefu, lakini ilishindwa kufanya kazi kwa sababu matukio ya wizi kwa kutumia mitandao, haikuwepo.

  Wakati huo huo, Manumba alisema hivi sasa wanakichunguza chama cha kiislamu kinachojishughulisha na kutetea haki na maslahi ya waislamu nchini.
  “Kuna baadhi ya kundi la watu linalojishughulisha na masuala ya siasa ndani ya dini, jambo ambalo linaweza kusababisha mvutano kwa wananchi, kutokana na hali hiyo, tunatakichunguza kwanza ili tuweze kubaini undani wake na kazi wanazozifanya na ikabainika wamekiuka taratibu, watachukuliwa hatua za kisheria,”alisema.
  Tuma maoni kwa Mhariri
   
 2. H

  Haki JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2009
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanini asiende kuchuguza wanaokula kula Rushwa Serikalini?
   
 3. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wangapi wamechunguzwa na kukutwa na makosa lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yao?.
   
 4. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ataweza wapi kuchunguza wakati haya mambo ya udini Kikwete mwenyewe kayakalia kimya maana anajua kuwa yanamnufaisha yeye binafsi.
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ni ajabu sana, nilidhani kuwa tayari tuna set of rules and regulations in these matters. Chama hicho ni wazi kinakuja kwa lengo la kuwagawa watanzania mpaka sasa DCI hajui aseme nini. Tangu lini uchunguzi wa issue kubwa umefanyika kwa mafanikio hapa bongo. Ni kutuzuga tu.
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Jul 23, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kama akina nani?
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jul 23, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hiki chama hakina tofauti na Al-Qaida!
   
 8. B

  Bull JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2009
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Kuna connection gani?
   
 9. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0


  Huwezi tofautisha dini na siasa, kwani vyote ni vitu vinavyoathiri mfumo wa wananchi kila siku ya maisha yao. Haya ni yale mawazo ya kizamani ya kina Kingunge. Binadamu ni siasa ni dini ni maisha yake ya kila siku. hebu sasa polisi wafunguke akili zao waache kutumiwa na wanasiasa wachumia tumbo.​
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huyu Manumbu ana matatizo makubwa sana au kubwa sana ,Hivi aulizwe ,matajiri kuibiwa kunamhuzunisha sana ? Sasa atueleze kwanini mabasi ya humu ndani Tanzania hayasafiri usiku ? Au hawayaruhusu kusafiri usiku ?

  Kule mikoa ya magharibi kuna njia kuu za kuingia na kutoka mikoani ni lazima upewe escort na polisi ? Kuna wizi wa kuyaibia magari makubwa matrela six wheels ambao hufanyika wakati magari haya yakipandisha milima mikubwa ,Manumba anatwambia nini kwa haya ? Waandishi wetu humu wanayaona masuali haya muulizeni huyo Manumba ,sio anakwenda kujificha katika cyber crimes ,wizi ambao ni wa mtu kujitakia.

  Manumba mauaji ya Maalbino mpaka tumeshayazoea ,toka mlikuwa yanatangazwa mpaka sasa hivi ,hayatangazwi tena ,waliokamatwa mumewatrace mpaka wapi ? Maana wauaji na wateja na mganga pana utatu hapo !! eei ndio maana yake . Mumekamata wauaji ,mganga yupo wapi alietoa utabiri huo ,na mhusika mkuu aliekwenda kwa Mganga ni nani ? Mauaji ya Maalbino ni mauaji ya kukodi na yamekuwa kama ni serial killings ,mlikuwa msilale wala msipate usingizi mpaka mmehakikisha ni nani huyo mteja ?

  Huko kwenye mambo ya dini sina haja nako ,maana wewe utakuwa unatumika kwenye kazi yako upo sawa kabisa ,tatizo isije kuwa unatumiliwa ,maana waraka wa Zanzibar wa Wakiristo uliokamatwa ,kuna madai kuwa kwa kuwatumia watu wao wanahakikisha mambo ya Kiislamu hayapiti kiurahisi na ikiwezekana yanazuiwa kabisa ,kama tunavyoona.

  Mheshimiwa Manumba una kazi kubwa sana kuliko hiyo ya cyber Crimes ,tunahitaji Tanzania inayotembeleka wakati na saa yeyote ile ,iwe hata mtu peke yake anaweza kukatisha mikoa na kutembea ndani ya nchi yake ,kwanza kutembelea mikoani hakuhitaji fedha kubwa au uwe tajiri ,ela ndogo tu unaweza kuipangiza na kutembelea mikoa ambayo mtu Mzalendo atatamani kuenda ,lakini ukiritimba wa ujambazi ndani ya nchi hii ndio unaturudisha nyuma.
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,375
  Likes Received: 19,621
  Trophy Points: 280
  ccm ni miyeyusho sana
   
Loading...