Manumba alazwa ICU Aga Khan

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Posts
19,021
Reaction score
9,177
Manumba alazwa ICU Aga Khan

HALI ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, DCI Robert Manumba ni mbaya na amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, kwenye wodi ya wgonjwa Mahututi (ICU) jijini Dar es Salaam akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria.

Kwa mujibu wa taarifa zilizonaswa na Habarimpya.com hivi punde ni kwamba Manumba amelazwa katika Hospitali hiyo tangu juzi.
Hata hivyo vyanzo vya kuaminika ndani ya Jeshi la Polisi nchini zinadai kwamba hali ya Mkurugenzi huyo wa makosa ya jinai nchini ni mbaya.......

MY TAKE:
Eah Mwenyezi Mungu Msaidie Kiumbe wako huyu apone haraka aje atutumikie Watanzania kama alivyotutumikia Jana na juzi na kesho afanye hivyo,
Umzidishie maisha marefu aishi ili aine kesho na kesho kutwa.
Amin!

 
 
Jamani mtu akiumwa tunasahau maovu yake! Mgonjwa na maiti hawana adui!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Tumuachie Mungu amhukumu . Najua kuwa huyu ni shetani wa haki za wanyonge, lakini tumwachie Mungu!
 
Kaka, duh, kumbe hata wewe huwapendi hawa jamaa...ama kweli sasa tumekamilika!Aende kama vp, labda atavpunguzia watu wa kuwa-prosecute baada ya maccm kuwa chama cha upinzani..
 
Mzee wa Mabwepande na Kauli Tata za Maandamano ya CDM.
 
Pole Manumba ila pia jua kifo si mchezo, kama ni hivyo kumbuka sana marehemu Mwangosi (Rest in Peace), na mateso ya Dr. Ulimboka Mungu alimnusuru hadi leo unashindwa kumhoji na hata wale waliohusika kumwokota, waliokuwa naye usiku wa utekaji, etc!! Usiwaze kumuua au kupanga kutoa kumwaga na kutoa uhai wa watu!! Roho zao zitatutafuna, na majonzi ya familia zao yatatufuata!!!
 
 
kibanga Ampiga Mkoloni, Wewe ndio una roho ya kinyama kabisa! ni sidhani kama una imani yoyote Juu ya Mungu! kwani uliambiwa kufa ni adhabu? jipange upya!
 
Jamani mtu akiumwa tunasahau maovu yake! Mgonjwa na maiti hawana adui!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Tumuachie Mungu amhukumu . Najua kuwa huyu ni shetani wa haki za wanyonge, lakini tumwachie Mungu!

umeanza vizuri unamaliza vibaya.....!!!mwanadamu ni mwanadamu,hata akiwa mbaya vipi hawezi kuwa shetani hata akiwa mzuri vip hawez kuwa malaika....
 
Duh,unamuombe mwenzako afe? Wewe sio binadamu. Amekukosea nini mpaka useme hivyo?

I thought binadamu wote sawa...inanikumbusha wale waliokuwa wanaombea Dr.ulimboka afe baada ya kuteswa vile. I realize we somehow live double standard life when it comes to our interest
 
Mkuu, kifo hakina formula.Mtamuombea mwenzio afe ukaishia kutangulia wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…