Mansour: Tusimame Pamoja Kuitetea Zanzibar

Mansour: Tusimame Pamoja Kuitetea Zanzibar

Ndugu, hii ni sehemu ya habari mbali mbali, ukiona habari haikufurahishi achana nayo.loo

Hongereni wazanzibari kwa kudai mamlaka yenu na sisi tunaidai Tanganyika yetu.

Umemwambia ukweli ---- huyu anapuuza yetu Zanzibar........ mjini wanena umemchana peupeeee
 
Wanasiasa wa Zanzibar wanashangaza linapokuja suala la muungano. Marehemu Karume si ndiye alikubali kuwepo muungano huu na akaridhia mamlaka hayo 'kamili' yanayodaiwa yatwaliwe na serkali ya muungano! Sasa wanapotumia Jina lake kudai hayo hayo aliyoridhia inatia Shaka Kama kweli wanamtendea haki.

Kuna wengine wanadai Zanzibar haiwezi kumudu gharama nje ya muungano, lakini wakati huo huo wanadai mamlaka kamili ndani ya muundo wa serikali mbili za muungano. Hii nayo ni ajabu, utakuwa na mamlaka kamili kwa serikali kugharamiwa na nani? Mamlaka kamili yanakuja na gharama zake na nafikiri Kila mtu anajua kuwa 'unajikuna' kwa kadri ya urefu wa mkono wako.
 
Katika maneno ya Karume umeyaona hayo tu?

Haya kwa hoja ya hayo nami nakukumbusha kuungia maneno yake mangine alinena hivi:-

MUUNGANO HUU NI KAMA KOTI LIKIKUBANA WAEZALIVUA,

Mkuu hayo uliayasahau kidogo lakini ndo haki ya ukamilifu wa maneno yake,

Haya okoteleza mengine tena tukusahihishe na fikra zako za upotoshaji.
 
Ukiangalia maandishi yangu sijaandika maneno yoyote allyotamka marehemu Karume. Ni wanasiasa wanaochukua wayatakayo kwa mtazamo wake - Kama unavyofanya wewe hapa.
 
Ukiangalia maandishi yangu sijaandika maneno yoyote allyotamka marehemu Karume. Ni wanasiasa wanaochukua wayatakayo kwa mtazamo wake - Kama unavyofanya wewe hapa.

Hao wanasiasa wanarithi/wanafuata manenovya kiongozi wao Abeid Aman Karume,

Sasa kosa lao li wapi ama nawe umeamua tu kuwaanda?

Na hata kama wamegeuka si inakuja baada ya kugundua kuwa wanabanwa na koti pia kosa liwapi?
 
Umemwambia ukweli ---- huyu anapuuza yetu Zanzibar........ mjini wanena umemchana peupeeee

Huu unafik ndio unaowaharibia. Sasa kama wewe ndio mkekereketwa wa uzanzibari yenu, unafanya nini Mwanza? Mwenzako unayemsifia nae hivyo hivyo, mara mzanzibari, mara chogo. Ndio maana hata katika hili mmeweka unafik mbele. Hamtaki kusema Muungano uvunjwe, mnabakia kuomba mfukuzwe. Mmesikia wapi sovereign states mbili ndani ya Muungano? Mnadai mlilazimishwa kuungana, mkisahau kuwa muasisi wenu alitaka serikali moja na ni Nyerere aliyekataa kuimeza Zanzibar. Mnasema tunawapandikizia chuki, mkisahau kuwa Sultan wenu baada ya Mapinduzi alipewa hifadhi Tanganyika. Mnasahau kuwa baada ya kumuua muasisi wenu, wakina Babu walipewa hifadhi Bara. Mnasahau kuwa wakati mnalazimisha kuwaoa waarabu, waarabu koko hao hao walipewa hifadhi bara ambako hakuna aliyewabughudhi. Mnasahau kuwa hao vikongwe ambao leo wanajifanya kudai mamlaka kamili Zanzubar, wamewekeza na wengi wao wanaishi kwa muda mwingi kwa huyo ambae wanadai ni mkoloni wao.

Hamna lolote. Unafik umewajaa. Si mna serikali yenu? Mnashindwa nini kufanya referendum kuhusu Muungano halafu kuiambia serikali dhalimu ya JMT kuwa hamna mpango nao? Mnaogopa nini? Gharama inawatisha nini wakati mna mafuta na karafuu na maankal wa Oman? Kuwa mtachinjana? Si mna serikali ya Kumbaya!

Amandla.....
 
Katika maneno ya Karume umeyaona hayo tu?

Haya kwa hoja ya hayo nami nakukumbusha kuungia maneno yake mangine alinena hivi:-

MUUNGANO HUU NI KAMA KOTI LIKIKUBANA WAEZALIVUA,

Mkuu hayo uliayasahau kidogo lakini ndo haki ya ukamilifu wa maneno yake,

Haya okoteleza mengine tena tukusahihishe na fikra zako za upotoshaji.

Kumbe mnaweza wenyewe kulivua koti linalowabana, sasa kwa nini mnakazania mvuliwe na mwengine?

Amandla......
 
Kumbe mnaweza wenyewe kulivua koti linalowabana, sasa kwa nini mnakazania mvuliwe na mwengine?

Amandla......

Ni nani mwenye kung'ang'aniza uendelee kuwepo ama nawe hujui huja ni nini?

Acha tabia ya kishetani ya kupinga kila kitu cha haki kisa wewe tu mlengo wa kushoto.
 
Ni nani mwenye kung'ang'aniza uendelee kuwepo ama nawe hujui huja ni nini?

Acha tabia ya kishetani ya kupinga kila kitu cha haki kisa wewe tu mlengo wa kushoto.

Nielimishe basi maana ya "huja"?

Nang'ang'ania kuwepo wapi? Kama ni kwenye hili jamvi, ulinikuta na utaniacha.

Hata nawe kuna wengine wanakuona una tabia ya kishetani kwa kuupinga Muungano ambao wao wanaona ni wa haki.

Unaelewa kweli maana ya mlengo wa kushoto? Kwangu mimi kuniita leftist ni badge of honour.

Matatizo yenu vijana wa leo mna-copy na ku-paste bila kuelewa maana yake. Maneno yako yamekusuta.

Amandla.....
 
Unaota huku umesimama .....jibu ni kikwete na timu yake 2005

Usimsingizie. Waunguja ndio waliomkataa Salim Ahmed Salim na sio machogo. Hao ndio uarabu wake ndio uliowakwaza. Machogo wamkatae vipi wakati heshima yote na vyeo vyote amevipata kwenye Muungano!

Amandla.....
 
Nilichokuuliza, umeketi tini na ikakutukua muda wote katika zako fikara na ukaonelea hilo ndo jawaba liso shaka katiko langu ulizo?

Ungeniuliza kwa lugha yetu machogo pengine ningekujibu. Hiyo lafudhi yako siielewi.

Amandla......
 
Ungeniuliza kwa lugha yetu machogo pengine ningekujibu. Hiyo lafudhi yako siielewi.

Amandla......

Endeleza kuvaa yako mawani ya mato usiku,

Niaminicho ni kuwa ulizo limekufika na limefahamika kwa wenye kufahamu ufahamu wa ulizo,

Sasa shida ya uelewa wako usinigeiye mie,
Kujivika upogo wa kuipambanua haki kwako ni dasturi,

Una huja nyangine nikusaidize?

Teh teh teh ...
 
Kwa nini hautaki kujitambulisha kama muunguja? Hivi unaamini machogo wote tunawaelewa? Ongea lugha tunayotumia wengine tutakuelewa. Kama hauwezi, basi baki kwenye jamvi lenu.

Ulimnukuu Karume kuwa" Muungano ni kama koti ambalo likimbana atalivua" bila kujua kuwa ndicho wengine tunachosema kila siku. Kama koti la Muungano linawabana wazanzibari wanashindwa nini kulivua? Mnachokitaka mvuliwe ili mkija sikia baridi mtulaumu kwa kuwavua.

Kwa hiyo hilo ndo hakiki la jibu lako au ndo mfumo wa suali juu ya suali?
 
WAZIRI wa zamani wa serikali ya Zanzibar, Mansour Yussuf Himid amesema Zanzibar ni ya Wazanzibari na ametaka wananchi kujielewa katika kusimamia hilo.

Amesema wananchi wanapaswa kujielewa kuwa Zanzibar ni mali yao wenyewe na hakuna ubia na watu wengine wasiyokuwa Wazanzibari.

Akizungumza jana Chaani, Mkoa wa Kaskazini Unguja kwenye mkutano wa hadhara wa Chama cha Wananchi (CUF) Mansour, alisisitiza kwa Wazanzibari kutokurudi nyuma katika kutetea Zanzibar, yenye MAMLAKA kamili:

“Napenda kusisitiza kwenu wananchi kutokukubali kurudi nyuma katika suala zima la kuitetea Zanzibar…bila ubaguzi wa aina yoyote,” alisema Masour.

Mansour ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano, katika mkutano huo alialikwa kama mjumbe wa Kamati hiyo, ambapo alisema wakati Mzee Karume ametuhakikishia urithi wa Nchi hii basi kila mmoja wetu ana haki sawa na mwengine.

Alitaka Wananchi hususan vijana kutokukubali kurudi tena nyuma kwa sasa katika suala zima la kuitetea Zanzibar, yenye MAMLAKA kamili.

Alisema wananchi wa Zanzibar ni waungwana sana lakini vile vile si wajinga, wanapodai haki yao, hakuna sababu ya kudharauliwa: “Tusilazimishane tunapokataa mfumo wa Muungano wa serikali mbili,” alisema Mansour.

Aidha, alisema anawashangaa sana baadhi ya viongozi wanaotoa kauli za kuwatisha wananchi wanaotaka Zanzibar, yenye MAMLAKA kamili.

Mansour ambaye alifukuzwa uanachama wa CCM miezi michache iliyopita, alimsifu Maalim Seif Sharif Hamad, huku akisema hajawahi kumsikia kutoa lugha ya matusi si kwa wananchi wala kwa viongozi.

‘’Binafsi sijawahi kumsikia Maalim Seif akikemea wananchi juu ya maamuzi yao wanayotaka…Iweje leo wengine watumie nafasi za uongozi kuwatisha wananchi?,’’alihoji Mansour.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano, Hassan Nassor Moyo alisema madai ya sasa ya Wazanzibari, si mambo mageni kwa sababu yalikuwapo kabla ya kuja kwa Muungano:

“Tunayodai sasa kwa nchi yetu si mageni yote tulikuwa nayo hapo awali kabla ya Muungano,” alisema Mzee Moyo.

Mkutano wa CUF Chaani 28.12.2013

Haiwezekani kwa kuwa serikali 2 zunawanufaisha wazanzibari viongozi wa ccm
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom