Mansour: Tusimame Pamoja Kuitetea Zanzibar

mrelbattawy

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
564
195
WAZIRI wa zamani wa serikali ya Zanzibar, Mansour Yussuf Himid amesema Zanzibar ni ya Wazanzibari na ametaka wananchi kujielewa katika kusimamia hilo.

Amesema wananchi wanapaswa kujielewa kuwa Zanzibar ni mali yao wenyewe na hakuna ubia na watu wengine wasiyokuwa Wazanzibari.

Akizungumza jana Chaani, Mkoa wa Kaskazini Unguja kwenye mkutano wa hadhara wa Chama cha Wananchi (CUF) Mansour, alisisitiza kwa Wazanzibari kutokurudi nyuma katika kutetea Zanzibar, yenye MAMLAKA kamili:

“Napenda kusisitiza kwenu wananchi kutokukubali kurudi nyuma katika suala zima la kuitetea Zanzibar…bila ubaguzi wa aina yoyote,” alisema Masour.

Mansour ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano, katika mkutano huo alialikwa kama mjumbe wa Kamati hiyo, ambapo alisema wakati Mzee Karume ametuhakikishia urithi wa Nchi hii basi kila mmoja wetu ana haki sawa na mwengine.

Alitaka Wananchi hususan vijana kutokukubali kurudi tena nyuma kwa sasa katika suala zima la kuitetea Zanzibar, yenye MAMLAKA kamili.

Alisema wananchi wa Zanzibar ni waungwana sana lakini vile vile si wajinga, wanapodai haki yao, hakuna sababu ya kudharauliwa: “Tusilazimishane tunapokataa mfumo wa Muungano wa serikali mbili,” alisema Mansour.

Aidha, alisema anawashangaa sana baadhi ya viongozi wanaotoa kauli za kuwatisha wananchi wanaotaka Zanzibar, yenye MAMLAKA kamili.

Mansour ambaye alifukuzwa uanachama wa CCM miezi michache iliyopita, alimsifu Maalim Seif Sharif Hamad, huku akisema hajawahi kumsikia kutoa lugha ya matusi si kwa wananchi wala kwa viongozi.

‘’Binafsi sijawahi kumsikia Maalim Seif akikemea wananchi juu ya maamuzi yao wanayotaka…Iweje leo wengine watumie nafasi za uongozi kuwatisha wananchi?,’’alihoji Mansour.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano, Hassan Nassor Moyo alisema madai ya sasa ya Wazanzibari, si mambo mageni kwa sababu yalikuwapo kabla ya kuja kwa Muungano:

“Tunayodai sasa kwa nchi yetu si mageni yote tulikuwa nayo hapo awali kabla ya Muungano,” alisema Mzee Moyo.

Mkutano wa CUF Chaani 28.12.2013
 
ferre.g

JF-Expert Member
Mar 3, 2013
2,215
1,195
Ni kweli kanena Zanzibar imetengwa sana..... tazama hili.Baada ya mkapa angefuata mgombea toka Zanzibar lakini wapi Dr. Salim akapakwa matope mazito ya mauaji.....

Ni awamu mbili tumetoswa Zanzibar hii ni sawa na miaka 20 sasa na awamu hii tena sioni tambo toka huko zaidi ni bara tuu.

Jitambueni mdai Zanzibar yenu kamili.
 
fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,449
2,000
Ni hapo Zanzibar itakapojitambua kwa ukweli sio chuki itafanikiwa, mfano wazanzibar wangecheza karata safi kwa kuunga mkono CDM ili uchukue nchi, harafu wao CUF na CDM anandoto moja ya serikali 3, ambayo ingetimia.
 
Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,208
2,000
Matamshi ya Nahodha jana atapona kweli kuvuliwa uanachama?

Nahodha kachukia sana kuvuliwa madaraka sasa kaamua lolote na liwe!Wao Bara wamemwaga mboga na yy sasa kaamua kumwaga mboga!Wa ZNZ kwa nn wanalazimishwa Muungano wasio upenda?
 
Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
7,272
2,000
Ni kweli kanena Zanzibar imetengwa sana..... tazama hili.Baada ya mkapa angefuata mgombea toka Zanzibar lakini wapi Dr. Salim akapakwa matope mazito ya mauaji.....

Ni awamu mbili tumetoswa Zanzibar hii ni sawa na miaka 20 sasa na awamu hii tena sioni tambo toka huko zaidi ni bara tuu.

Jitambueni mdai Zanzibar yenu kamili.

Mbona haueleweki? Mara TUmetoswa mara YEnu! Na ni nani aliyempaka matope Salim A Salim kama si mzanzibari mwenzake?

Matatizo yenu msiyalete kwetu.

Amandla.....
 
mpemba mbishi

JF-Expert Member
Nov 27, 2011
1,132
1,195
himid.jpg mansour.jpg
 
SlaaSlaala

Senior Member
Apr 30, 2013
107
170
Mbona haueleweki? Mara TUmetoswa mara YEnu! Na ni nani aliyempaka matope Salim A Salim kama si mzanzibari mwenzake?

Matatizo yenu msiyalete kwetu.

Amandla.....

Ndugu, hii ni sehemu ya habari mbali mbali, ukiona habari haikufurahishi achana nayo.

Hongereni wazanzibari kwa kudai mamlaka yenu na sisi tunaidai Tanganyika yetu.
 
gogo la shamba

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
6,670
2,000
WAZIRI wa zamani wa serikali ya Zanzibar, Mansour Yussuf Himid amesema Zanzibar ni ya Wazanzibari na ametaka wananchi kujielewa katika kusimamia hilo.

Amesema wananchi wanapaswa kujielewa kuwa Zanzibar ni mali yao wenyewe na hakuna ubia na watu wengine wasiyokuwa Wazanzibari.

Akizungumza jana Chaani, Mkoa wa Kaskazini Unguja kwenye mkutano wa hadhara wa Chama cha Wananchi (CUF) Mansour, alisisitiza kwa Wazanzibari kutokurudi nyuma katika kutetea Zanzibar, yenye MAMLAKA kamili:

“Napenda kusisitiza kwenu wananchi kutokukubali kurudi nyuma katika suala zima la kuitetea Zanzibar…bila ubaguzi wa aina yoyote,” alisema Masour.

i
Mansour ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano, katika mkutano huo alialikwa kama mjumbe wa Kamati hiyo, ambapo alisema wakati Mzee Karume ametuhakikishia urithi wa Nchi hii basi kila mmoja wetu ana haki sawa na mwengine.

Alitaka Wananchi hususan vijana kutokukubali kurudi tena nyuma kwa sasa katika suala zima la kuitetea Zanzibar, yenye MAMLAKA kamili.

Alisema wananchi wa Zanzibar ni waungwana sana lakini vile vile si wajinga, wanapodai haki yao, hakuna sababu ya kudharauliwa: “Tusilazimishane tunapokataa mfumo wa Muungano wa serikali mbili,” alisema Mansour.

Aidha, alisema anawashangaa sana baadhi ya viongozi wanaotoa kauli za kuwatisha wananchi wanaotaka Zanzibar, yenye MAMLAKA kamili.

Mansour ambaye alifukuzwa uanachama wa CCM miezi michache iliyopita, alimsifu Maalim Seif Sharif Hamad, huku akisema hajawahi kumsikia kutoa lugha ya matusi si kwa wananchi wala kwa viongozi.

‘’Binafsi sijawahi kumsikia Maalim Seif akikemea wananchi juu ya maamuzi yao wanayotaka…Iweje leo wengine watumie nafasi za uongozi kuwatisha wananchi?,’’alihoji Mansour.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano, Hassan Nassor Moyo alisema madai ya sasa ya Wazanzibari, si mambo mageni kwa sababu yalikuwapo kabla ya kuja kwa Muungano:

“Tunayodai sasa kwa nchi yetu si mageni yote tulikuwa nayo hapo awali kabla ya Muungano,” alisema Mzee Moyo.

Mkutano wa CUF Chaani 28.12.2013
mbona Karume asili yake ni mtu wa Kigoma,napendekeza baada ya kuvunja muungano watu wanaoishi Zanzibar wachague kuwa wazanzibari au wa watanganyika na wanaoishi Tanganyika pia wachague kuwa watanganyika au wazanzibar
 
Bocho

JF-Expert Member
Jan 6, 2013
1,489
1,195
Nasubiri Mansour atakapojiunga CUF 2015! Sijui itakuwae? Ila siku moja itakuwa kweli by Ali Nabwa!
 
Mshikawezi Mwizi

JF-Expert Member
Jul 24, 2013
751
500
ninyi wazanzibar ni watumwa wetu lazima tuwanyanyase hadi hapo mtakapojitambua na kuchukua hatua....na bado mtaipandeka!
 
ilboru1995

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,329
0
Naunga Mkono Hoja 100% Zanzibar ipewe madaraka kamili ... Wabara huwa tunainajisi Znz! Angalia wenye kuingia mikataba ya kishenzi wote ni wabara, MAFISADI wote wanatoka bara! Wenye kung'ang'ania rasilimali za nchi zimilikiwe na wageni kwa 100% ni wasomi wa kutoka bara! Wabara tumemaliza kugawa dhahabu, almasi, uranium, vitalu vya uwindaji sasa mnataka mafuta ya znz muendelee kumilikisha kwa wazungu! Kama mnarejeshewa thru makanisa sisi hatutaki! Zanzibar waachiwe wajiamulie mambo yao kwa 100%... Bara tayari tumeshindwa na hatuwezi chochote kinachoweza kuleta maendeleo katika nchi hii...
 
ferre.g

JF-Expert Member
Mar 3, 2013
2,215
1,195
Mbona haueleweki? Mara TUmetoswa mara YEnu! Na ni nani aliyempaka matope Salim A Salim kama si mzanzibari mwenzake?

Matatizo yenu msiyalete kwetu.

Amandla.....

Unaota huku umesimama .....jibu ni kikwete na timu yake 2005
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom