Manji kafanya aliyofanyiwa Muro, nani anamlinda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manji kafanya aliyofanyiwa Muro, nani anamlinda?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lunyungu, Dec 17, 2011.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Manji amgeuzia kibao aliyeibua upya Kagoda

  Mwanaharakati maarufu nchini, Kainerugaba Msemakweli, ameelezea kusakwa kwake na Jeshi la Polisi ili akamatwe, akisema kuwa kumetokana na kufunguliwa jalada katika kituo cha polisi cha Mabatini Kijitonyama, jijini Dar es Salaam na mfanyabiashara Yusufu Manji.

  Manji ambaye ni miongoni mwa watu waliotajwa kuhusika katika kashfa ya kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, anadai kuombwa na Msemakweli rushwa ya Sh milioni 100 ili aachane na harakati zake za kufuatilia kashfa inayoikabili kampuni hiyo.

  Kagoda inatuhumiwa kukwapua Sh. bilioni 40 katika Akaunti ya malipo ya Madeni ya Nje (Epa) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa njia za kifisadi.

  Akizungumza na NIPASHE, Msemakweli ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alisema taarifa za Manji kufungua jalada hilo zimefika kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba.

  Alisema jalada hilo lipo mikononi mwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Salum Kisai, wa Ofisi ya DCI, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

  Msemakweli alisema katika jalada hilo, Manji anadai kuwa aliombwa rushwa hiyo na Msemakweli Novemba 25, mwaka huu.

  “Ni kwamba, Manji alikwenda kituo cha polisi Kijitonyama. Akasema eti tarehe 25 mwezi wa 11 nilimuomba anipe rushwa ya Sh. milioni 100 ili niachane na mambo ya Kagoda,” alisema Msemakweli.

  Hata hivyo, alisema tarehe ambayo Manji ameitaja kituo cha polisi kuwa walionana na kumuomba hiyo rushwa, yeye hakuwapo Dar es Salaam.

  Alisema tarehe hiyo alikuwapo mjini Bukoba, mkoani Kagera, hivyo akasema madai ya Manji ni uzushi mtupu.

  “Tarehe 12 mwezi wa 11 nilitoka Dar es Salaam kwenda Bukoba kupitia Mwanza,” alisema Msemakweli.

  Alisema tangu Novemba 13 alikuwa Bukoba na Novemba 22 alikata tiketi kwa ajili ya safari ya kurudi jijini Dar es Salaam.

  Msemakweli alisema Novemba 29, aliondoka Bukoba na aliwasili Dar es Salaam asubuhi ya siku iliyofuatia (Novemba 30).

  “Hata simu yangu ilisoma tarehe 22 mwezi wa 11 nilikuwa Bukoba,” alisema Msemakweli.

  Alisema alipofika jijini Dar es Salaam, alionana na Kamishna Manumba na kumueleza mkasa wote wa kusakwa kwake na polisi wa Kituo cha Mabatini Kijitonyama kuhusiana na tuhuma zilizopelekwa na Manji dhidi yake.

  Msemakweli alisema Kamishna Manumba alimthibitishia kuwa yote alimueleza ni ya kweli kwa kuwa taarifa za kufunguliwa kwa jalada hilo na Manji alikuwa tayari anazo.

  Alisema baadaye, Kamishna Manumba alimtuma ACP Kisai kufuatilia suala hilo katika kituo hicho.

  Msemakweli alisema baadaye Kamishna Manumba aliagiza jalada hilo liondolewe katika kituo hicho na kupelekwa Makao Makuu ya Polisi.

  “ACP Kisai akalichukua jalada hilo, akalipeleka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi. Baadaye akamuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi Mabatini Kijitonyama nisikamatwe mpaka DCI atakapoagiza,” alisema Msemakweli.

  DCI ROBERT MANUMBA
  NIPASHE iliwasiliana na Kamishna Manumba ili kujua hatua zilizokwisha kuchukuliwa na polisi kuhusiana na tuhuma za Manji zilizomo kwenye jalada hilo, alisema kwa kifupi: “Mpigie Msemaji wa Jeshi la Polisi.”

  MSEMAJI WA POLISI
  Msemaji wa Jeshi hilo nchini, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Advera Senso, alipoulizwa na NIPASHE kwa njia ya simu jana, alimtaka mwandishi kuonana naye ofisini kwake.

  Hata hivyo, mmoja wa maofisa waandamizi wa makao makuu ya jeshi hilo, alithibitisha jalada hilo kuwapo ofisini kwao na kusema linaendelea kufanyiwa kazi.

  “Tulipata malalamiko kutoka kwa Msemakweli. Tukaitisha jalada kutoka Kijitonyama. Tukakuta kweli. Tukawaambia Kijitonyama wasimkamate Msemakweli mpaka upelelezi wa suala hili ukamilike. Kwa sababu kuna mambo tunazungumza naye, hivyo isije ikawa mambo haya yanapandana. Kwa hiyo, jalada linafanyiwa kazi. Tunaendelea na upelelezi,” alisema afisa huyo, ambaye hakutaka kutaja jina lake kwa vile yeye si msemaji wa polisi.

  Habari za polisi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Kituo hicho kumsaka kwa zaidi ya wiki mbili ili wamkamate Msemakweli zilipatikana kutoka Kituo cha Mabatini Kijitonyama Desemba 12, mwaka huu.

  Msemakweli alithibitisha kutafutwa na polisi, lakini siku hiyio alikataa kuzungumzia undani wa suala hilo, badala yake aliomba kupewa muda atakapokuwa katika nafasi nzuri ya kulizungumzia kwa undani baada ya kuwasiliana na wahusika.

  Msemakweli ni mmoja wa mashahidi muhimu katika uchunguzi mpya wa sakata la wizi wa fedha za Epa unaoendelea chini ya Kikosi Kazi (Task Force) ambacho polisi wamo ndani yake.

  Siku hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo, alisema raia kutafutwa na polisi ni jambo la kawaida kwa kuwa ni sehemu ya jeshi hilo kukamilisha upelelezi wa taarifa ambazo zinakuwa zimefika kituoni.

  Msemakweli ndiye aliyeibua upya sakata la Kagoda kwa kuwasilisha kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi, ushahidi unaowahusisha watu kadhaa ambao alikabidhiwa DCI Manumba, ambao alianza kuufanyia kazi.

  Hadi sasa haijafahamika ni watu wangapi wamekamatwa ama kuhojiwa kuhusiana na sakata hilo pamoja na kuwa ni dhahiri kwamba vigogo wengi hawajaguswa, jambo linalozidi kuwapa jeuri ya kuendelea kuwatisha watoa taarifa.

  Wiki iliyopita, DCI Manumba katika mkutano na waandishi wa habari uliokuwa umeitishwa na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema, alipoulizwa suala la ushahidi wa Msemakweli na kashfa ya Kagoda ilikofikia, alisisitiza kuwa uchunguzi bado unaendelea.

  Kagoda ilichota Sh. bilioni 40 katika wizi wa Epa wa jumla ya Sh. bilioni 133 zilizokwapuliwa na kampuni kadhaa, yakiwamo mengine hewa.

  Kumekuwa na woga mkubwa wa kuwachukulia hatua wamiliki wa Kagoda ingawa baadhi ya wamiliki wa kampuni nyingine zilizochota fedha za Epa wamefunguliwa kesi mahakamani na wengine wamekwisha kuhukumiwa vifungo.

  Msemakweli aliwasilisha kwa DPP rundo la nyaraka ambazo alidai zinafichua kwa kina wamiliki wa Kagoda ingawa kumekuwa na juhudi kubwa ndani ya serikali za kuficha wamiliki halali wa kampuni hiyo.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hawana ubavu wa kumkamata..mambo yamekwekwa hadharani mapema, hivyo hawatathubu maana wataumbuka
   
 3. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Msemakweli be very ver, very, careful. hao watu wanamtandao mkali sana. Usimwamini mtu yoyote, usile hoteli yaani hata sijui itakuwaje.

  Lakini, be very very careful.
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nani anamlinda Manji kwa nini dharau hii na manyanyaso kwa wazalendo ?
   
 5. S

  Shembago JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2011
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukweli utajulikana tu hata wakificha,ipo siku mambo haya yatakuwa wazi na sheria itachukua mkondo wake
   
 6. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 283
  Trophy Points: 160
  Wewe shembago,sheria ipi itachukua mkondo! Sheria ya magamba,sahau ilo ushaona mwenye pesa anafungwa tz?
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Dec 17, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Jina la Manji nimeisoma kwenye list of shame!
   
 8. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #8
  Dec 17, 2011
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu pesa, ukiwa nayo inakupatia kila aina ya ulinzi na hata wa kukufanyia unavyotaka,isipokuwa kifo.teh teh teh teh,hii ndo bongo dasalaam
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  manji katumia mbinu ya kitoto kwweli...
   
 10. Kiungani

  Kiungani JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2011
  Joined: Feb 2, 2007
  Messages: 274
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa nini Manumba na watu wake wanakataa kuwashirikisha TAKUKURU katika suala hili? Hili ni suala la rushwa.

  Manji kalipeleka Kijitonyama moja kwa moja kama kesi ya kuku, kufungua mashitaka bila kuwashirikisha TAKUKURU. TAKUKURU wanajaribu kulifuatilia lakini wanazungushwa na ofisi ya DCI, hawajajua kwa nini. Je, polisi wanaogopa nini kama kweli hilo suala limeletwa na Manji na wao hawana mkono wao hapo? Milioni 100 siyo rushwa ndogo hiyo (ingawa kwa Manji ni senti za juice tu kwa rushwa).

  Ile kesi ya Muro ilijulikana toka mwanzoni ni njama za Kova na vijana wake, na hata TAKUKURU hawakuwa na kasi nayo sana (mnakumbuka ushahidi wa video aliyosema Kova anao na wataonyesha mahakamani, na siyo kwa waandishi wa habari?). Hili la Msemakweli na Manji linagusa masuala ya EPA ambayo TAKUKURU, DCI, DPP na TISS tayari wanachunguza, na ushahidi mwingine wa Msemakweli uko kwao.

  Namwaminia Manumba, ila katika hili itabidi awe macho sana asije akaingizwa mkenge na vijana wake kwa mgongo wa Manji.
   
 11. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2011
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Angetumia mbinu ipi mkuu,kama hii ni ya kitoto?
   
 12. Biz2geza

  Biz2geza Senior Member

  #12
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  why mabatini post?sheria inasemaje kuhusu ufunguaji wa kesi kama hizi?
   
 13. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,654
  Likes Received: 3,301
  Trophy Points: 280
  Yap!ni kwa sababu anajua wazi kuwa wa tz pamoja na viongozi wao wengi ni kama tu watoto.
   
 14. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mwanaharakati maarufu nchini, Kainerugaba Msemakweli, ameelezea kusakwa kwake na Jeshi la Polisi ili akamatwe, akisema kuwa kumetokana na kufunguliwa jalada katika kituo cha polisi cha Mabatini Kijitonyama, jijini Dar es Salaam na mfanyabiashara Yusufu Manji.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Manji ambaye ni miongoni mwa watu waliotajwa kuhusika katika kashfa ya kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, anadai kuombwa na Msemakweli rushwa ya Sh milioni 100 ili aachane na harakati zake za kufuatilia kashfa inayoikabili kampuni hiyo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kagoda inatuhumiwa kukwapua Sh. bilioni 40 katika Akaunti ya malipo ya Madeni ya Nje (Epa) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa njia za kifisadi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumza na NIPASHE, Msemakweli ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alisema taarifa za Manji kufungua jalada hilo zimefika kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema jalada hilo lipo mikononi mwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Salum Kisai, wa Ofisi ya DCI, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Msemakweli alisema katika jalada hilo, Manji anadai kuwa aliombwa rushwa hiyo na Msemakweli Novemba 25, mwaka huu.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Ni kwamba, Manji alikwenda kituo cha polisi Kijitonyama. Akasema eti tarehe 25 mwezi wa 11 nilimuomba anipe rushwa ya Sh. milioni 100 ili niachane na mambo ya Kagoda,” alisema Msemakweli.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, alisema tarehe ambayo Manji ameitaja kituo cha polisi kuwa walionana na kumuomba hiyo rushwa, yeye hakuwapo Dar es Salaam.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema tarehe hiyo alikuwapo mjini Bukoba, mkoani Kagera, hivyo akasema madai ya Manji ni uzushi mtupu.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Tarehe 12 mwezi wa 11 nilitoka Dar es Salaam kwenda Bukoba kupitia Mwanza,” alisema Msemakweli.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema tangu Novemba 13 alikuwa Bukoba na Novemba 22 alikata tiketi kwa ajili ya safari ya kurudi jijini Dar es Salaam.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Msemakweli alisema Novemba 29, aliondoka Bukoba na aliwasili Dar es Salaam asubuhi ya siku iliyofuatia (Novemba 30).[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata simu yangu ilisoma tarehe 22 mwezi wa 11 nilikuwa Bukoba,” alisema Msemakweli.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema alipofika jijini Dar es Salaam, alionana na Kamishna Manumba na kumueleza mkasa wote wa kusakwa kwake na polisi wa Kituo cha Mabatini Kijitonyama kuhusiana na tuhuma zilizopelekwa na Manji dhidi yake.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Msemakweli alisema Kamishna Manumba alimthibitishia kuwa yote alimueleza ni ya kweli kwa kuwa taarifa za kufunguliwa kwa jalada hilo na Manji alikuwa tayari anazo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema baadaye, Kamishna Manumba alimtuma ACP Kisai kufuatilia suala hilo katika kituo hicho.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Msemakweli alisema baadaye Kamishna Manumba aliagiza jalada hilo liondolewe katika kituo hicho na kupelekwa Makao Makuu ya Polisi.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]ACP Kisai akalichukua jalada hilo, akalipeleka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi. Baadaye akamuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi Mabatini Kijitonyama nisikamatwe mpaka DCI atakapoagiza,” alisema Msemakweli.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]DCI ROBERT MANUMBA[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]NIPASHE iliwasiliana na Kamishna Manumba ili kujua hatua zilizokwisha kuchukuliwa na polisi kuhusiana na tuhuma za Manji zilizomo kwenye jalada hilo, alisema kwa kifupi: “Mpigie Msemaji wa Jeshi la Polisi.”[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]MSEMAJI WA POLISI[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Msemaji wa Jeshi hilo nchini, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Advera Senso, alipoulizwa na NIPASHE kwa njia ya simu jana, alimtaka mwandishi kuonana naye ofisini kwake. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, mmoja wa maofisa waandamizi wa makao makuu ya jeshi hilo, alithibitisha jalada hilo kuwapo ofisini kwao na kusema linaendelea kufanyiwa kazi.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Tulipata malalamiko kutoka kwa Msemakweli. Tukaitisha jalada kutoka Kijitonyama. Tukakuta kweli. Tukawaambia Kijitonyama wasimkamate Msemakweli mpaka upelelezi wa suala hili ukamilike. Kwa sababu kuna mambo tunazungumza naye, hivyo isije ikawa mambo haya yanapandana. Kwa hiyo, jalada linafanyiwa kazi. Tunaendelea na upelelezi,” alisema afisa huyo, ambaye hakutaka kutaja jina lake kwa vile yeye si msemaji wa polisi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Habari za polisi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Kituo hicho kumsaka kwa zaidi ya wiki mbili ili wamkamate Msemakweli zilipatikana kutoka Kituo cha Mabatini Kijitonyama Desemba 12, mwaka huu.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Msemakweli alithibitisha kutafutwa na polisi, lakini siku hiyio alikataa kuzungumzia undani wa suala hilo, badala yake aliomba kupewa muda atakapokuwa katika nafasi nzuri ya kulizungumzia kwa undani baada ya kuwasiliana na wahusika.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Msemakweli ni mmoja wa mashahidi muhimu katika uchunguzi mpya wa sakata la wizi wa fedha za Epa unaoendelea chini ya Kikosi Kazi (Task Force) ambacho polisi wamo ndani yake.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Siku hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo, alisema raia kutafutwa na polisi ni jambo la kawaida kwa kuwa ni sehemu ya jeshi hilo kukamilisha upelelezi wa taarifa ambazo zinakuwa zimefika kituoni.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Msemakweli ndiye aliyeibua upya sakata la Kagoda kwa kuwasilisha kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi, ushahidi unaowahusisha watu kadhaa ambao alikabidhiwa DCI Manumba, ambao alianza kuufanyia kazi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hadi sasa haijafahamika ni watu wangapi wamekamatwa ama kuhojiwa kuhusiana na sakata hilo pamoja na kuwa ni dhahiri kwamba vigogo wengi hawajaguswa, jambo linalozidi kuwapa jeuri ya kuendelea kuwatisha watoa taarifa.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wiki iliyopita, DCI Manumba katika mkutano na waandishi wa habari uliokuwa umeitishwa na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema, alipoulizwa suala la ushahidi wa Msemakweli na kashfa ya Kagoda ilikofikia, alisisitiza kuwa uchunguzi bado unaendelea. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kagoda ilichota Sh. bilioni 40 katika wizi wa Epa wa jumla ya Sh. bilioni 133 zilizokwapuliwa na kampuni kadhaa, yakiwamo mengine hewa.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kumekuwa na woga mkubwa wa kuwachukulia hatua wamiliki wa Kagoda ingawa baadhi ya wamiliki wa kampuni nyingine zilizochota fedha za Epa wamefunguliwa kesi mahakamani na wengine wamekwisha kuhukumiwa vifungo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Msemakwili aliwasilisha kwa DPP rundo la nyaraka ambazo alidai zinafichua kwa kina wamiliki wa Kagoda ingawa kumekuwa na juhudi kubwa ndani ya serikali za kuficha wamiliki halali wa kampuni hiyo.[/FONT]
  SOURCE: NIPASHE
   
 15. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Viongozi wenyewe wote wamenunuliwa kwa pesa za haohao matajiri, kwanini wasiwalinde!
   
 16. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #16
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,110
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Kwa hili utaona kesi ya Manji itakwenda haraka ili Msemakweli hafungwe kabla ya maelezo yake hajafanyiwa kazi hii ndio Tanganyika mwenye pesa sio mwenzio tena mhindi anatuibia na kutunyanyasa na pesa aliotuibia. Rais, na timu yake wamewekwa mfukoni hapo usemi kitu uenda hata quality Rostam nae yumo. Hilo jengo ni la watanganyika ni pesa zetu ndio iliyoijenga hata waseme nini ni pesa zetu walizoiba. Zitarudi tu hata kama sio leo lakini wajukuu watazirudisha tu. Lazima watafuatilia hizo mabilioni yaliyojenga Quality yalitoka wapi? kama ni mfanyabiashara ni biashara gani alikuwa anafanya je kodi alikuwa analipia sawasawa. Muda ukifika yote yatafunguka watalinda lakini yana mwisho hakuna aliejua rais wa ufaransa au wa misri watapatikana na makosa. Ivyo tujipe moyo hata Tanganyika yana mwisho hata kama sio lakini itakuwa kesho.
   
 17. I

  ITSNOTOK Member

  #17
  Dec 18, 2011
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana. Lakini ni wakati wa sisi wananchi kuamka hata kwa maandamano kuwahoji polisi WAMEFIKISHIWA TAARIFA NA VIELELEZO JUU YA KAGODA mbona hayashughulikiwi. Hii inatosha kwanza kumpa support Mtanzania mwenzetu kwa kujitahidi kutaka kulinda mali ya mtanzania. Lakini pia ingempa kusita huyu ambaye anamgeuzia kibao anayemtuhumu.

  WATANZANIA, ITS TIME TO WORK UP, WORK UP NOW - UNTIL WHEN YOU WILL STAY JUST WATCHING HUMILIATION, MUWE WACHUNGU NA MALI ZENU, NANI WA KUWATETEA OTHERWISE.
   
 18. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #18
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa sifa za kijinga kiherehere kitamponza.
   
 19. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #19
  Dec 18, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,219
  Trophy Points: 280
  pesa, fedha, hela, money
   
 20. m

  mpigilie JF-Expert Member

  #20
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mzee una mawazo ya kizee...  Sichangii mada.
   
Loading...