Manji apokwa jengo la Quality Plaza

Mwitongo

JF-Expert Member
Jan 30, 2009
312
360
Wadau yule tajiri Yusuf Manji, ameshindwa kesi na kupokwa jengo la Quality Plaza ambalo alilijenga, akaliuza kwa shirika moja la hifadhi, na kisha akawa mpangaji. Tangu alipopanga hakupata kulipa pango. Bado Tanesco nao wanamdai umeme wa mabilioni. Uamuzi umetolewa na Mahakama wiki hii, lakini jambo la ajabu ni kwamba vyombo vya habari vimekaa kimya kabisa. Hapa kuna nini? Huenda ukimya huu unatokana pia na Manji kutumia nguvu ya Mahakama kuzuia magazeti zaidi ya 10 yasimwandike kwa mazuri wala kwa mabaya! Ebu tujadili jambo hili.
 
Pigo kwa watani zngu Yanga na wana ccm mafisadi na hatimae nguvu ya hela imeshindwa kazi
 
Kwenye kichwa cha habari yako neno APOKWA umemaanisha nini mkuu?
 
Wadau yule tajiri Yusuf Manji, ameshindwa kesi na kupokwa jengo la Quality Plaza ambalo alilijenga, akaliuza kwa shirika moja la hifadhi, na kisha akawa mpangaji. Tangu alipopanga hakupata kulipa pango. Bado Tanesco nao wanamdai umeme wa mabilioni. Uamuzi umetolewa na Mahakama wiki hii, lakini jambo la ajabu ni kwamba vyombo vya habari vimekaa kimya kabisa. Hapa kuna nini? Huenda ukimya huu unatokana pia na Manji kutumia nguvu ya Mahakama kuzuia magazeti zaidi ya 10 yasimwandike kwa mazuri wala kwa mabaya! Ebu tujadili jambo hili.
..mbn anaandikwa kuhusu kugombea YANGA na hajashtaki?
 
..mbn anaandikwa kuhusu kugombea YANGA na hajashtaki?

Hii ilikuwa habari njema kwake maana anaitaka Yanga kwa muda mrefu sana na ndiye aliyeigawa Yanga maana alitaka iwe company aimiliki na wale wote waliopinga walijigawa na ndiyo maana hadi leo yanga ina makundi mawili na migogoro haitakaa imalizike. Kwa sasa anaingia kwa mgongo wa uongozi ili akamilishe azma yake. Subirini mambo mtayaona.
 
Wadau yule tajiri Yusuf Manji, ameshindwa kesi na kupokwa jengo la Quality Plaza ambalo alilijenga, akaliuza kwa shirika moja la hifadhi, na kisha akawa mpangaji. Tangu alipopanga hakupata kulipa pango. Bado Tanesco nao wanamdai umeme wa mabilioni. Uamuzi umetolewa na Mahakama wiki hii, lakini jambo la ajabu ni kwamba vyombo vya habari vimekaa kimya kabisa. Hapa kuna nini? Huenda ukimya huu unatokana pia na Manji kutumia nguvu ya Mahakama kuzuia magazeti zaidi ya 10 yasimwandike kwa mazuri wala kwa mabaya! Ebu tujadili jambo hili.

Mahakama ipi iliyotoa uamuzi huo? na ni shirika lipi la hifadhi lilomshtaki? Toa taarifa zilizokamilika hii JF inatumika na wengi kama chanzo cha habari, sasa habari ikiwa sio kamili haipendezi
 
sasa waadnishi wa habari wataandikaje hilo wakati kila tarehe 30 wanakwenda kwa Sabrina pale Quality Centre ofisi za Nexus Consulting Agency kukamata mpunga..wanavuta kilo 4 kila mwezi ...hahaaaa
 
  • Thanks
Reactions: Edo
Huyu Shafii Dauda huyu atatuua wana Yanga jamani! Yaani ameshafika mpaka huku jameniiiii....

Tumemfanya nn au ndiye akiyefanya mpaka Manji ashindwe kumleta Maximo nn?

Halafu tena mm nimesikia ni yeye ndiye aliyemteka Yondani pale mtaa wa twiga na jangwani. Mweeeeeh.
 
Nchi hii ni ya wenye pesa, kama unabisha utaona? Hilo jengo ataendelea kulitumia na kodi hatalipa na hakuna gazeti lolote litakaloandika habari hizo.
 
Wezi wa kalamu,na wanaotumia madaraka vibaya siku zao zinahesabika.Na kimvuli chao tunakifaham.
 
Mimi sijaelewa. Kama alishaliuza, amepokwa nini?

http://www.fikrapevu.com/biashara-na-uchumi/zitto-kabwe-amponza-manji-kutimuliwa-na-pspf-quality-plaza

SAKATA la kati ya Mfanyabiashara Yusuf Manji na mifuko ya hifadhi ya jamii limeendelea na sasa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), umemtaka mfanyabiashara huyo kuhama mara moja katika jengo la Quality Plaza ambalo aliuuzia mfuko huo katika mazingira tata.

Manji anadaiwa na PSPF karibu Sh bilioni 5, ambazo ni malimbikizo ya kodi ya pango.

Kwa muda mrefu sasa Manji amekua akitajwa kufanya biashara zenye utata na mifuko ya hifadhi ya jamii na alifanikiwa kuiuzia PSPF jengo la Quality Plaza na Mufuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuizua maghala kwa shilingi bilioni 46, ambayo aliyajenga kwa mkopo wa Sh bilioni 9 kutoka mfuko huo.

Habari za uhakika kutoka serikalini zinaeleza kwamba, uamuzi huo wa PSPF umefikiwa Ijumaa ya Aprili 1, 2011 baada ya mfuko huo kubanwa na Wabunge wa Kamati Hesabu za Mashirika ya Umma* (POAC), inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe .

Katika barua ya PSPF* kwenda kwa kampuni ya Image Properties & Estate inayosimamia uendeshaji wa Quality Plaza, mfuko huo umeitaka kampuni ya Quality Group Limited kuondoka mara moja katika jengo hilo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Hivi karibuni, Quality Group Limited iliiomba Mahakama kuzuia kuondolewa kwao katika jengo hilo, maombi ambayo muda wake ulishakwisha lakini PSPF wakawa wanachelewa kuchukua hatua wakati taasisi hiyo ilikua na hali mbaya ya kifedha kiasi cha serikali kuombwa na POAC kulinusuru kwa kuwekeza zaidi.

“Unaelekezwa kuitimua haraka Quality Group Limited kwa kushindwa kutimiza masharti ya mkataba wa pango,” inaeleza sehemu ya barua hiyo ya Aprili 1, 2011 iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi* Adamu Mayingu, kwenda kwa Image Properties & Estate.

Jengo hilo liko kitalu namba 182/2 barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam ni mali ya PSPF alipanga baada ya kuliuza lakini akawa halipi kodi.

Katika maelezo ya wakili wa PSPF, Benitho Mandele, ambayo iliwasilishwa mahakamani iilieleza kwamba Manji anadaiwa kodi ya kuanzia Aprili, 2009 hadi Desemba 2010, hivyo jumla ya deni lote ni dola 2,335,189.06 za Marekani, wakati shauri hilo lilipowasilishwa mahakamani na sasa limefikia Sh bilioni 5.

Makampuni mengine ya Manji yaliyomo katika jengo hilo ni pamoja na kampuni aliyoichukua kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mazingira tata ya Gaming Management Limited, Quality Ligistics Co. Limited, International Transit Ivestment Limited na Q-Consult Limited.
 
Wadau yule tajiri Yusuf Manji, ameshindwa kesi na kupokwa jengo la Quality Plaza ambalo alilijenga, akaliuza kwa shirika moja la hifadhi, na kisha akawa mpangaji. Tangu alipopanga hakupata kulipa pango. Bado Tanesco nao wanamdai umeme wa mabilioni. Uamuzi umetolewa na Mahakama wiki hii, lakini jambo la ajabu ni kwamba vyombo vya habari vimekaa kimya kabisa. Hapa kuna nini? Huenda ukimya huu unatokana pia na Manji kutumia nguvu ya Mahakama kuzuia magazeti zaidi ya 10 yasimwandike kwa mazuri wala kwa mabaya! Ebu tujadili jambo hili.
Mi naogopa kujadili hii humu na sisi JF tukafungiwa!, mwisho wa siku atakayeshinda ni Manji!, he who laugh last, laugh most!. Nchi hii ina wenyewe, na wenyewe ni hao!. Anaedhani wenyewe ni sisi!, anajifariji tuu !.
 
Pasco uko sahihi. Sina maneno ya kuongeza. Hii kesi inachekesha sana na inadhihirisha jinsi nchi ilivyo na watu wenye jeuri. Lolote linaweza kutokea. Mbowe anasema 90% Mp's wameingia kwa rushwa... Do u expect anything difference?
 
Manji utajiri wake mwingi umepitia njia za kitapeli na mfumo mbovu wa nchi, EPA, Mifuko ya Hifadhi na Mikataba ya Ujanja Ujanja, Tajiri Mengi alihainisha lakini akaishia kuombwa msamaha na kulipa sh.1
 
Back
Top Bottom