Manji afanya ufisadi manispaa ya Kinondoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manji afanya ufisadi manispaa ya Kinondoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Nov 26, 2009.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Manji akumbwa na balaa• Manispaa Kinondoni kumfikisha mahakamaniNa Betty Kangonga, Tanzania DaimaHALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni, inatarajia kumfikisha mahakamani mfanyabiashara maarufu nchini na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Manji, kwa kukabidhidhi matela ya kubebea takataka yaliyo chini ya kiwango.Nia hiyo ya Manispaa ya Kinondoni, ilitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Manispaa hiyo na Diwani wa Kata ya Magomeni, Julian Bujugo, ambaye alibainisha kuwa, halmashauri hiyo ilimpatia zabuni ya kuagiza matela mfanyabiashara huyo, lakini ameshindwa kulinda makubaliano ya mkataba.Alisema wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona Manji hana nia ya kupeleka matela yenye viwango vinavyohitajika au kurejesha kiasi cha shilingi milioni 324 alichopewa kwa ajili ya kazi hiyo.Bujugo alisema matela 27 yalikusudiwa kusambazwa katika kata zote za wilaya hiyo ili kuiweka manispaa hiyo katika hali ya usafi.Alisema Manji alitakiwa kukabidhi matela hayo katika muda usiopungua miezi mitatu (Septemba – Desemba 2008), lakini alikiuka taratibu ambapo aliwakabidhi Novemba mwaka huu.“Zabuni hiyo ilikuwa ni ya kipindi cha miezi mitatu, lakini Manji alikiuka utaratibu huo ambapo imepita zaidi ya mwaka ndiyo anatuletea matela hayo yasiyo na ubora,” alifafanua Bujugo.Aidha, alisema halmashauri katika mkataba wake na Manji, ilitaka matela yenye matairi manane, lakini mfanyabiashara huyo aliwapelekea matela yenye matairi manne.“Sisi tuna ushahidi wa kile tulichokiagiza katika makubaliano yetu. Tulihitaji kuletewa matela yenye matairi manane, amechukua muda mrefu anatuletea matela ya matairi manne, hatuyataki,” alieleza.Alisisitiza kuwa, kamati yake na halmashauri haikuwa tayari kupokea matela hayo na kumshauri Manji kutimiza kile walichokubaliana katika mkataba husika.Alisema hivi sasa kuna mbinu chafu na ushawishi unaofanywa na mfanyabiashara huyo kwa baadhi ya madiwani ili wakubali kuyapokea matela hayo.Alibainisha kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilitoa siku saba kwa Manji kuyaondoa katika eneo yalipowekwa matela hayo na kuleta yale yanayokidhi viwango.Alidai kwamba pamoja na agizo hilo, mfanyabiashara huyo alishindwa kutimiza masharti aliyopewa, jambo lilioifanya manispaa kufikiria kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha jambo hilo linamalizika.Tanzania Daima Jumatano lilijaribu kumtafuta Manji ili kuzungumzia sakata hilo, lakini simu yake ya mkononi ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni msaidizi wake.Msaidizi huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema Manji hakuwepo ofisini huku akilitaka gazeti limuachie maagizo ili akirudi ampe.“Ninaomba uniachie ujumbe nitamfikishia na kama atakuwa tayari najua lazima atakupigia,” alieleza msaidizi huyo.Hata hivyo, msaidizi huyo alishindwa kutimiza ahadi hiyo ambapo hadi Tanzania Daima Jumatano linakwenda mtamboni, hakuna simu yoyote iliyopigwa na Manji.Source: Tanzania Daima.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,807
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mkuu hii tayari ipo hewani humu JF tangu juzi!!:D
   
 3. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  kaka naona leo upo kwenye mud kwelikweli maana kila thread unakua wakwanza nuipokea.GIG UP.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,807
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  mkuu nimenyimwa kale kamchezo napotezea kiaina
   
 5. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  hahahahahahahahah
  Umeudhi kitu gani leo?.
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,807
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ni hutu tupombepombe twa after hour!!
   
Loading...