Mbunge Conjesta: Manispaa ya Temeke ilijipangia Kukusanya tsh bilioni 60 lakini Wizara ya Fedha ikawaambia Wakusanye tsh 42 bilioni!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,114
Mbunge wa viti maalumu mh Conjesta amemtaka Waziri wa Fedha kuacha kuwapunguzia Malengo ya Makusanyo ya Ushuru Halmashauri mbalimbali kwani Tabia hiyo inatengeneza Taifa Maskini na tegemezi

Conjesta amesema kwa mfano Manispaa ya Temeke ilijipangia Kukusanya tsh bilioni 60 lakini Wizara ya Fedha ikawaambia Wakusanye tsh 42 bilioni

Wizara ikadai kwa mujibu wa rates za IMF Manispaa ya Temeke wanapaswa Kukusanya tsh bilioni 42

Hapo ndio Wizi na Ufisadi unapoanza, amesisitiza

Source: Bunge Tv
 
Kwani ukikusanya juu ya Lengo, pesa inayozidi haiandikwi.
Mara nyingi nasikia kuwa Halmashauri fulani imevuka lengo na kukusanya kwa mfano 15% ZAIDI ya lengo. Hizo pesa huandikwa kwenye vitabu kama zile nyingine. Shida iko wapi?
 
Mbunge wa viti maalumu mh Conjesta amemtaka Waziri wa Fedha kuacha kuwapunguzia Malengo ya Makusanyo ya Ushuru Halmashauri mbalimbali kwani Tabia hiyo inatengeneza Taifa Maskini na tegemezi

Conjesta amesema kwa mfano Manispaa ya Temeke ilijipangia Kukusanya tsh bilioni 60 lakini Wizara ya Fedha ikawaambia Wakusanye tsh 42 bilioni

Wizara ikadai kwa mujibu wa rates za IMF Manispaa ya Temeke wanapaswa Kukusanya tsh bilioni 42

Hapo ndio Wizi na Ufisadi unapoanza, amesisitiza

Source: Bunge Tv
Made in Tanzania.
 
Back
Top Bottom