Manispaa ya Shinyanga, Kero ya bodaboda kutoa excos kusababisha makelele hamuioni?

luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
6,325
6,871
Najiuliza Jeshi la Polisi usalama barabaran kama wapo macho kweli? Ukifika Shinyanga mjini bodaboda nyingi zimetobolewa excos kitendo ambacho hupelekea kelele kwa wananchi wanaoishi pembezoni ya barabara mfano, Nkulila road.

Kero nyingine, zipo baadhi ya izi pikipiki guta zimefunga honi zile za mabasi (honi za tembo) unakuta unapigiwa honi mpaka mtu unachanganyikiwa. Yaani Jeshi la Polisi lina shindwa kweli kukagua dereva wa hizi bodaboda kama kweli wana leseni?

Majuzi tu hapa bodaboda mmoja kagongwa na lori mpaka kifo palepale kwa uzembe tu, sasa kwanini Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani msiwe wakali ili kuzuia matukio kama haya? Ukipita pale mataa ya phantom yaani bodaboda haelewi taa nyekundu inamtaka afanye nini, wao wanapita tu.

Kero nyingine, majira ya usiku barabara kuu ya kwenda Mwanza karibu na TTCL pale katika ile Bar and Grill, unakuta gari zinapaki pembezoni mwa highway na ikiwa chaki za mstari wa njano zinakataza parking eneo hilo lakini ajabu tabia hii inaonekana kushamiri.

Ukipita pale usiku kuanzia saa 2 hivi lazima utakuta gari mbili zimepaki. Mamlaka husika amkeni, chukueni hatua. Mbona Mwanza Jeshi la polisi limezuia utoboaji wa excos?
 
Najiuliza Jeshi la Polisi usalama barabaran kama wapo macho kweli? Ukifika Shinyanga mjini bodaboda nyingi

Ukipita pale usiku kuanzia saa 2 hivi lazima utakuta gari mbili zimepaki. Mamlaka husika amkeni, chukueni hatua. Mbona Mwanza Jeshi la polisi limezuia utoboaji wa excos?
Zifungiwe kama mbovu,maana sio mtengenezaji alivyopangia mlio!
 
Kuna kipindi nikiwa mwanza nilikuwa naishi kwenye nyumba iliyopo barabarani aisee nilikoma na kelele za pikipiki zilizofanyiwa mafekeche ya kuondolewa exzos yaani sometimes unashtuka hadi saa nane usiku kutokana na makelele ya pikipiki
 
Yaan ss iv Shinyanga ni kero kubwa, kwa mtu ambaye haja experience hii kadhia kwake ataona ni kama masihara tu

Yaan huwezi lala , imagine izi barabara zilizopo pembezon ya makazi ya watu unakuta gari inapita above 50 speed .. tena hapo akikukuta unavuka basi lzm uambulie matusi
 
Kama magari ya serikali baadhi yao wanavunja sheria za barabara, wananchi wa kawaida watashindwa kuvunja sheria!!
 
Yaan ss iv Shinyanga ni kero kubwa, kwa mtu ambaye haja experience hii kadhia kwake ataona ni kama masihara tu

Yaan huwezi lala , imagine izi barabara zilizopo pembezon ya makazi ya watu unakuta gari inapita above 50 speed .. tena hapo akikukuta unavuka basi lzm uambulie matusi
Dah pole sana chief
 
Back
Top Bottom