Manispaa ilala; deci nyingine?

AG

Member
Jun 11, 2007
82
55
Manispaa ya ilala imetoa tangazo kuhusu ugawaji wa viwanja eneo la Kinyerezi. Katika tangazo hilo unatakiwa ulipe shilingi 20,000.00 kupitia benki ya DCB akaunti 011005000075. Manispaa wameamua kuchaji sqm 1 kwa shilingi 10,000.00 hadi 15,000.00. Swali la kujiuliza hivyo viwanja ambavyo viko 3000 watavigawaje wakati wananchi kwa maelfu wamefurika kwenye hiyo benki wakitaka kupatiwa viwanja? Kama watalipa watu 100,000 hivyo viwanja 3000 itakuwaje? Je pesa zitakazo kusanywa itakuwaje? Hii si DECI nyingine? Maswali ni mengi sana.
 
Kwa kweli ni deci kabisa wana toa form zaidi 100,000 yaani wanaiba pesa za bure kabisa,na hiyo bei utadhani sio viwanja vya serikali yaani sasa mfano 25x25 unalipa 6.2m na unatakiwa ulipe ndani siku 14 hawa wanajua ugumu wa pesa hawa kweli??
 
Hii ni zaidi ya DECI, kwa haraka haraka ukichukua 100,000xTSHS 20,000=TSHS 2,000,000,000; Aliyegundua hii anastahili sifa. Fomu kwenye attachment
 
i warned something last week kabla ya hili tangazo... we have a person there who only care about money, hana morals wala social responsibilities... hata ukisema vitanda vya uzaizi vinahitajika anaweza kuuliza hivi keko hatuwezi kununua kwa elfu tisini hadi tununue kwa milioni moja?? anasahau its more than laying on your back kuoanua miguu na kutoa mtoto
 
yalitokea burka........ the government thorugh local authority is cheating again
 
Hii ishu bana itakuja kubackfire siku za mbeleni.. kuna mtu wa huko jikoni anasema viwanja vyenyewe vina wenyewe sasa sijui wanachukua hela za watu za nini...
 
Kuna haja ya serikali kupiga marufuku wizi wa hela za wananchi kwa mtindo huu. Siyo haki kabisa ukusanye elfu 20,000 kwa watu 100,000 ukiwaahidi kuwapa viwanja kumbe una viwanja vya kutosha watu 3000 tu. Nasema tena huu ni wizi kabisa na serikali ikatae wizi wa namna hii
 
We si uache kulipia wenye pesa zao acha wanunue.We kama huwezi kulipia kiwanja acha wenye uwezo wachukue viwanja,we sogea kisarawe au kwingine kwa saizi yako.Kinyerezi hupawezi hapo si kwa kila saizi,tafuta saizi yako ya kiwanja cha sh.100/= kwa mita
 
Manispaa ya ilala imetoa tangazo kuhusu ugawaji wa viwanja eneo la Kinyerezi. Katika tangazo hilo unatakiwa ulipe shilingi 20,000.00 kupitia benki ya DCB akaunti 011005000075. Manispaa wameamua kuchaji sqm 1 kwa shilingi 10,000.00 hadi 15,000.00. Swali la kujiuliza hivyo viwanja ambavyo viko 3000 watavigawaje wakati wananchi kwa maelfu wamefurika kwenye hiyo benki wakitaka kupatiwa viwanja? Kama watalipa watu 100,000 hivyo viwanja 3000 itakuwaje? Je pesa zitakazo kusanywa itakuwaje? Hii si DECI nyingine? Maswali ni mengi sana.

Mkuu hilo limekuwa likiniumiza sana maana yalinikuta kule Arusha kwenye shamba la burka ambapo tulichangishwa elfu 20 lakini viwanja walipewa wenye uwezo wao akiwemo Rizwani kikwete. Ndo maana nasema ccm si chama cha wanyonge tena
 
We si uache kulipia wenye pesa zao acha wanunue.We kama huwezi kulipia kiwanja acha wenye uwezo wachukue viwanja,we sogea kisarawe au kwingine kwa saizi yako.Kinyerezi hupawezi hapo si kwa kila saizi,tafuta saizi yako ya kiwanja cha sh.100/= kwa mita

Fikiria kwanza mbona unashindwa kufikiria? Ni vigumu wananchi wanavyolipia kujua kama idadi ya watu imefkia sawa na viwanja vilivyopo cha muhimu cha haki ilikuwa serikali kukubali kuwarejeshea wale wote watakaokuwa wamekosa kiwanja
 
weye si fikiriakwanza jina likufalo fikiriamwisho,hao manispaa wezi wanauza viwanja bila kuwalipa fidia wahusika kwan walifanya valuation 02,12,2009 had leo asilmia kubwa hawajalipwa fidia pia leo pana kikao cha wadai fidia na mkuu wa wilaya kuzungumzia juu ya fidia zao,nitawajulishe nn kimeazungumzwa.
 
Kuna haja ya serikali kupiga marufuku wizi wa hela za wananchi kwa mtindo huu. Siyo haki kabisa ukusanye elfu 20,000 kwa watu 100,000 ukiwaahidi kuwapa viwanja kumbe una viwanja vya kutosha watu 3000 tu. Nasema tena huu ni wizi kabisa na serikali ikatae wizi wa namna hii

Mkuu, Serikali ndo inaiba, sasa itajipigaji marufuku? Au umesahau Kule Arusha walikuwepo mawaziri na Rizwani walipogawana eneo la Burka- wananchi wa Arusha wakakosa kwa mtindo wa Deci. Vingenevyo, Kikwete awaweke ndani mawaziri wake na Rizwani kwa sababu ndo miongoni mwa wahusika. Inawezekana?
 
Back
Top Bottom