Julai mosi - Tumeanza mwaka Mpya wa fedha 2013/2014

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
Ndugu Waheshimiwa, itakumbukwa kwamba katika mwaka wa fedha 2013/14, Bunge lilipitisha sera mbalimbali za kodi ambazo zimetekelezwa na Serikali.
Azma ya sera hizo ni kuimarisha
ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kupanua wigo wa kodi, kuimarisha taratibu za kukusanya mapato pamoja na kupunguza misamaha ya kodi ili kuweza kugharamia kwa kiwango kikubwa matumizi ya
Serikali kwa kutumia mapato ya ndani.
Kwa kuzingatia azma hiyo, Serikali imechukua hatua zifuatazo katika eneo la mapato:-
(i) Kuboresha mifumo ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya kodi na yasiyo ya kodi kwa kupitia upya mfumo wa ukadiriaji kodi, utoaji wa stakabadhi na leseni, pamoja na kuboresha viwango vya
kubakiza maduhuli kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali;
(ii) Kupanua wigo wa kodi kwa kuendelea kurasimisha sekta isiyo rasmi ili iingie kwenye mfumo wa kodi;
(iii) Kufanya mapitio ya sheria za Wakala/Taasisi za Umma zinazokusanya maduhuli ili ziweze kuchangia zaidi kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali;
(iv) Kufanya mapitio ya sheria mbalimbali zinazotoa misamahaya kodi kwa lengo la kudhibiti na kupunguza misamaha hiyo;
(v) Kupitia upya mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya majengo katika majiji, manispaa, miji, wilaya na miji midogo ili kuuboresha zaidi;
(vi) Kufanya mapitio ya vyanzo vya mapato na mfumo wa ukusanyaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuongeza mapato; na
(vii) Kujenga uwezo wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania, Mamlaka ya Mapato Tanzania, na Wakala waUkaguzi wa Madini ili kuweza kusimamia
ukusanyaji wa mapato katika maeneo ya madini, gesi na petroli, nk.

Misingi ya Bajeti ya Serikali kwa kipindi cha mwaka 2013/14 ni UKUSANYAJI KODI - KWAHIYO BASI KUANZIA JULAI MOSI TUNAANZA KUTEKELEZA SERA NA MSINGI YA BAJETI YA SERIKALI KWA KIPINDI CHA MWAKA MPYA WA FEDHA 2013/14...

Naomba kuwakilishi...
===
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT. WILLIAM AUGUSTAOMGIMWA (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALIKUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2013/2014I. UTANGULIZI​
1.​
Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufulijadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka2013/14. Pamoja na hotuba hii, vimeandaliwa vitabu vinne vya Bajetivinavyoelezea takwimu mbalimbali za Bajeti. Kitabu cha Kwanza kinahusumakisio ya mapato; Kitabu cha Pili kinaelezea makisio ya matumizi ya kawaidakwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi na Wakala wa Serikali; Kitabu cha
Tatu​
kinahusu makisio ya matumizi ya kawaida kwa Mikoa na Mamlaka yaSerikali za Mitaa; na Kitabu cha Nne kinaainisha makadirio ya matumizi yamaendeleo kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi na Wakala za Serikali,Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, upo Muswada wa Sheria yaFedha wa mwaka 2013 ambao ni sehemu ya bajeti hii.2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwakutujalia afya njema na kutuwezesha kushiriki mkutano wa nane wa Bunge laKumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha namshukuru MheshimiwaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwauongozi wake thabiti. Vilevile, napenda kutumia fursa hii kukushukuru weweMheshimiwa Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wa vikao vya Bunge kwakuongoza majadiliano vizuri bungeni.3. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia mapendekezo ya Bunge yamzunguko mpya wa bajeti, Serikali imeridhia mapendekezo hayo ambayoyanatoa fursa ya kushirikisha wadau wengi zaidi na kuwezesha utekelezaji wabajeti kuanza tarehe 1 Julai kila mwaka. Serikali imetekeleza mapendekezohayo kwa kurekebisha muda na utaratibu wa hatua za uandaaji wa bajetiambazo zimezingatiwa wakati wa maandalizi ya bajeti ya mwaka 2013/14.4. Mheshimiwa Spika, kutokana na mabadiliko hayo, Serikali itakuwainatayarisha Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti mwezi Agosti hadiOktoba kila mwaka; kuidhinisha na kusambaza Mwongozo mwezi Novemba;kuandaa rasimu za mipango na bajeti za mafungu mwezi Novemba hadiJanuari; kufanya uchambuzi wa rasimu za Bajeti na kuingiza takwimu kwenyemfumo wa IFMS Mwezi Februari; kuwasilisha rasimu za Bajeti pamoja narandama kwenye Kamati za Bunge za Kisekta mwezi Machi; kuchapisha nakuwasilisha Bungeni vitabu vya bajeti mwezi Aprili; kuchambua na kuidhinishabajeti Bungeni mwezi Aprili hadi Juni; na kufanya ufuatiliaji na tathmini yashughuli zilizoidhinishwa muda wote wa utekelezaji wa bajeti.5. Mheshimiwa Spika, kufuatia mabadiliko hayo, Wizara zote zinatakiwakuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha na kuhitimishwa nahotuba hii ya bajeti ya Serikali.6. Mheshimiwa Spika, Ninazishukuru Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisina Wakala za Serikali, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na wadaumbalimbali walioshiriki kufanikisha matayarisho ya bajeti hii. Kwa namna yapekee, ninaishukuru Kamati ya Bunge ya Bajeti ikiongozwa na Mwenyekiti wakeMhe. Andrew John Chenge, Mbunge wa Bariadi Magharibi kwa kuchambua kwakina bajeti za mafungu yote na kutoa mapendekezo. Aidha, naishukuru KamatiMaalum ya Mheshimiwa Spika kuhusu mapendekezo ya mapato na matumizi yaSerikali; pamoja na Wenyeviti wa Kamati za kisekta kwa ushauri, mapendekezona maelekezo wakati wakichambua Bajeti hii. Vilevile, ninawashukuruWaheshimiwa Wabunge wote kwa ushauri na mapendekezo yao ambayoyamesaidia kuboresha Bajeti hii.7. Mheshimiwa Spika, ninampongeza kwa dhati Waziri Mkuu, Mhe. MizengoKayanza Peter Pinda (Mb), kwa hotuba yake ambayo imefanya majumuisho yamapitio ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2012/13 na kutoa mwelekeo washughuli za Serikali kwa mwaka 2013/14. Aidha, ninamshukuru Mhe. StephenMasatu Wasira (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu kwakuwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi ya mwaka 2012 na Mpango waMaendeleo wa mwaka 2013/14. Vilevile, ninawapongeza Mawaziri wenzangukwa kuwasilisha hotuba za bajeti za wizara zao ambazo zimejumuishwa katikaBajeti hii.8. Mheshimiwa Spika, ninawashukuru Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe.Janet Zebedayo Mbene (Mb) na Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb), Katibu Mkuu;Naibu Makatibu Wakuu; Gavana wa Benki Kuu; Kamishna Mkuu wa Mamlakaya Mapato; Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu; Viongozi wakuu wataasisi zilizo chini ya Wizara; wakuu wa idara na vitengo pamoja na watumishiwa Wizara ya Fedha na taasisi zake kwa michango yao katika maandalizi yaBajeti hii. Ninamshukuru pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kutayarishakwa wakati Muswada wa Fedha wa mwaka 2013 na nyaraka mbalimbali zasheria ambazo ni sehemu ya Bajeti hii. Aidha, ninamshukuru Mpiga ChapaMkuu wa Serikali kwa kuchapisha nyaraka zote za Bajeti kwa wakati.9. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya mwaka 2013/14 ni ya tatu katika utekelezajiwa Mpango wa kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano; Ilani ya UchaguziMkuu ya CCM ya mwaka 2010; na Awamu ya Pili ya Mkakati wa KukuzaUchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA II). Aidha, Bajeti hii inaendeleakutekeleza Malengo ya Maendeleo ya Milenia 2015. Madhumuni ya mipangona mikakati hii ni kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Vilevile,Bajeti hii inalenga kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kwa ajili ya maendeleoendelevu kupitia mfumo mpya wa utekelezaji wa miradi ya kipaumbele ambayoitaleta matokeo makubwa kwa haraka.10. Mheshimiwa Spika, kama ilivyoelezwa katika hotuba iliyowasilishwa naMhe. Stephen Masatu Wasira (Mb), kuhusu utaratibu mpya wa uibuaji wavipaumbele vya Taifa ambavyo vitaleta matokeo makubwa na ya haraka (BigResults Now –BRN), Bajeti ya mwaka 2013/14, imedhamiria kutekeleza maeneomakuu sita yaliyobainishwa kama vipaumbele vya kitaifa. Maeneo hayo ni maji,nishati, uchukuzi, kilimo, elimu na kuongeza mapato.11. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo ya awali, naomba sasakutoa taarifa kuhusu mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2012/13, namwelekeo wa makadirio ya mapato na matumizi kwa kipindi cha mwaka2013/14.
II. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA SERA ZA BAJETI YA MWAKA 2012/13​
12.​
Mheshimiwa Spika, shabaha na malengo ya Bajeti ya mwaka 2012/13yalijikita katika kukuza Pato halisi la Taifa kwa asilimia 6.8 mwaka 2012;kuongeza mapato ya ndani kufikia uwiano na Pato la Taifa wa asilimia 18.0;kudhibiti mfumuko wa bei na hatimaye kuurudisha kwenye kiwango chatarakimu moja; kuimarisha kiwango cha ubadilishaji wa fedha kitakachotokanana mwenendo wa soko la fedha pamoja na kuongeza mikopo kwa sekta binafsikwa asilimia 20 ya Pato la Taifa.13. Mheshimiwa Spika, maeneo mengine yaliyozingatiwa katika misingi nashabaha ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2012/13 yalikuwa: kuwepo kwa nishatiya umeme wa uhakika na kuhamasisha matumizi ya gesi asilia; kuimarika kwautekelezaji wa Sera za Fedha na Bajeti; kuimarika kwa mahusiano na Washirikawa Maendeleo; kutekeleza maboresho katika sekta ya umma ikiwa ni pamoja nakuendelea kuimarika kwa usimamizi wa fedha za umma; kuboresha mazingiraya biashara pamoja na kuongezeka kwa tija na fursa za uwekezaji; kulinda nakudumisha mafanikio yaliyopatikana katika Sekta za huduma za jamii;kuimarisha utawala bora na uwajibikaji; na kuimarisha utaratibu wa ubia kati yaSekta ya Umma na Binafsi (PPP).
Sera za Mapato​
14.​
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/13, Sera za mapatozilizotekelezwa na Serikali zililenga kuongeza mapato ya ndani yatokanayo nakodi na yasiyo ya kodi ili kuimarisha uwezo wa Serikali wa kutoa huduma kwaumma na kupunguza utegemezi wa bajeti. Sera zilizotekelezwa zililenga katikakuimarisha taratibu za kukadiria na kukusanya mapato; kuboresha sheria zakodi; kuongeza matumizi ya kielektroniki katika kukusanya kodi; kupunguzamisamaha ya kodi; na kuwianisha viwango vya kodi na tozo.15. Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kwamba katika mwaka wa fedha2012/13, Bunge lilipitisha sera mbalimbali za kodi ambazo zimetekelezwa naSerikali. Azma ya sera hizo ilikuwa ni kuimarisha ukusanyaji wa mapato yandani kwa kupanua wigo wa kodi, kuimarisha taratibu za kukusanya mapatopamoja na kupunguza misamaha ya kodi ili kuweza kugharamia kwa kiwangokikubwa matumizi ya Serikali kwa kutumia mapato ya ndani. Kwa kuzingatiaazma hiyo, Serikali imechukua hatua zifuatazo katika eneo la mapato:-(i) Kuboresha mifumo ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya kodina yasiyo ya kodi kwa kupitia upya mfumo wa ukadiriaji kodi, utoaji wastakabadhi na leseni, pamoja na kuboresha viwango vya kubakizamaduhuli kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali;(ii) Kupanua wigo wa kodi kwa kuendelea kurasimisha sekta isiyo rasmiili iingie kwenye mfumo wa kodi;(iii) Kufanya mapitio ya sheria za Wakala/Taasisi za Ummazinazokusanya maduhuli ili ziweze kuchangia zaidi kwenye Mfuko Mkuuwa Serikali;(iv) Kufanya mapitio ya sheria mbalimbali zinazotoa misamaha ya kodikwa lengo la kudhibiti na kupunguza misamaha hiyo;(v) Kupitia upya mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya majengo katika majiji,manispaa, miji, wilaya na miji midogo ili kuuboresha zaidi;(vi) Kufanya mapitio ya vyanzo vya mapato na mfumo wa ukusanyajikatika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuongeza mapato; na(vii) Kujenga uwezo wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati na Madini,Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania, Mamlaka ya Mapato Tanzania,na Wakala wa Ukaguzi wa Madini ili kuweza kusimamia ukusanyaji wamapato katika maeneo ya madini, gesi na petroli.
Mwenendo wa Ukusanyaji Mapato ya Ndani​
16.​
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Aprili 2013, jumla ya mapato yakodi na yasiyo ya kodi yalifikia kiasi cha shilingi bilioni 6,717.2, sawa na asilimia93.2 ya makadirio ya kukusanya shilingi bilioni 7,209.2 katika kipindi hicho naasilimia 77.1 ya makadirio ya mwaka ya shilingi bilioni 8,714.7. Kati yamakusanyo hayo, mapato ya kodi yalikuwa shilingi bilioni 6,371.3 ambayo nisawa na asilimia 96 ya makadirio ya kipindi hicho na asilimia 79.0 ya lengo lamwaka la shilingi bilioni 8,070.1 na mapato yasiyotokana na kodi yalikuwashilingi bilioni 357.8 ikiwa ni asilimia 55.5 ya lengo la mwaka la shilingi bilioni644.6.17. Mheshimiwa Spika, tathmini ya makusanyo ya mapato inaoneshamwenendo wa kuridhisha ambapo hadi kufikia mwezi Aprili 2013, makusanyo yaushuru wa forodha yalifikia shilingi bilioni 487.8, sawa na asilimia 84.6 yakukusanya shilingi bilioni 576.7; mapato kutokana na kodi ya ongezeko lathamani yalifikia shilingi bilioni 1,965.5, sawa na asilimia 90.3 ya lengo lakukusanya shilingi bilioni 2,176.4. Kwa upande wa ushuru wa bidhaa, hadikufikia mwezi Aprili 2013 jumla ya shilingi bilioni 1,050.7 zimekusanywa ambazoni sawa na asilimia 90.3 ya kukusanya shilingi bilioni 1,163.1. Kwa upande wakodi ya mapato kwa makampuni, makusanyo yalifikia shilingi bilioni 2,381.9 hadimwezi Aprili 2013, ambacho ni sawa na asilimia 105.4 ya lengo la kukusanyashilingi bilioni 2,260.718. Mheshimiwa Spika, kuongezeka kwa makusanyo ya kodi kulitokana,pamoja na sababu nyingine, na: kuongezeka kwa makusanyo ya kodi yamapato ya makampuni; kuongezeka kwa kodi ya zuio inayotokana na malipo yagawio katika makampuni ya madini; na ukusanyaji wa malimbikizo ya kodi.Hatua zingine za kiutawala zilizosababisha kuongezeka kwa mapatozinajumuisha: kuhakikisha mashine za kielektroniki zinatumika ipasavyo;kuendelea kuimarisha mfumo wa kusimamia vitalu vya kodi; kuboresha mfumowa uthamanishaji bidhaa; kuimarisha ukaguzi wa hesabu za walipa kodi;mapato kutokana ya mauzo ya hisa za kampuni ya M/S BP Tanzania;kuongezeka kwa ushuru wa bidhaa wa muda wa maongezi wa simu; na utozajiwa ushuru wa bidhaa katika bidhaa zote zisizo za petroli zinazostahili kutozwakodi hiyo.19. Mheshimiwa Spika, licha ya mafanikio hayo, baadhi ya kodi zimeoneshamwenendo usioridhisha tofauti na ilivyotarajiwa, hasa kwenye kodi ya ongezekola thamani, ushuru wa bidhaa kwenye bidhaa zisizo za petroli na kodi ya mapatoinayotokana na ajira. Aidha, uzalishaji katika baadhi ya viwanda ulipungua nahivyo kusababisha makusanyo ya ushuru wa bidhaa na kodi ya ongezeko lathamani kuwa chini ya matarajio. Vilevile, kumekuwa na ongezeko la uingizajibidhaa kupitia njia zisizo rasmi bila kulipia ushuru na kodi.20. Mheshimiwa Spika, makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi yamekuwahayaridhishi kutokana na: uwezo mdogo wa ukusanyaji na kukosa utaalam,vifaa duni na mifumo dhaifu ya ukusanyaji wa mapato ambayo inachangia katikaupotevu wa mapato. Wakala na Mashirika bado hayachangii ipasavyo kwenyeMfuko Mkuu wa Serikali. Aidha, baadhi ya Idara ambazo zilikuwa vyanzomuhimu zimegeuzwa kuwa Wakala zilizoundwa chini ya Wizara mbalimbalihivyo kupunguza michango yake kwenye mapato ya Mfuko Mkuu wa Serikali.21. Mheshimiwa Spika, hadi mwezi Aprili 2013, mapato yanayokusanywa naMamlaka za Serikali za Mitaa yalifikia shilingi bilioni 177.4, sawa na asilimia 49ya lengo la mwaka la kukusanya shilingi bilioni 362.2.
Misaada na Mikopo ya Nje yenye Masharti Nafuu​
22.​
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/13, Serikali ilikadiria kupatashilingi bilioni 842.5 kama misaada na mikopo ya kibajeti. Hadi kufikia Aprili,2013 Serikali ilipata misaada na mikopo ya kibajeti ya shilingi bilioni 645.4ambazo ni sawa na asilimia 77 ya makadirio ya mwaka. Kwa upande mwingine,shilingi bilioni 443.4 zilipokelewa kupitia mifuko ya kisekta, ikiwa ni sawa naasilimia 107 ya makadirio ya shilingi bilioni 415.1 kwa mwaka.23. Mheshimiwa Spika, misaada na mikopo nafuu iliyopokelewa kwa ajili yamiradi ya maendeleo kwa kipindi kilichoishia Aprili, 2013 ilifikia shilingi bilioni1,235.7 ambayo ni asilimia 65 ya ahadi ya shilingi bilioni 1,899.1 kwa mwaka.Upungufu huu umetokana na Washirika wa Maendeleo kuchelewa kutoa taarifawanapotuma fedha moja kwa moja kwenye miradi husika; kasi ndogo yautekelezaji wa baadhi ya miradi; ucheleweshwaji wa taarifa za utekelezaji wamiradi kutoka Wizara, Idara, Taasisi, Maaikoa na Serikali za mitaa; pamoja namchakato mrefu wa ununuzi, hususan inapohusisha kupata idhini ya mfadhili(no objection).
Mikopo ya Ndani​
24.​
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai hadi Aprili 2013, Serikaliilikopa shilingi bilioni 1,364.7 kutoka soko la ndani la mitaji kwa ajili ya kulipiadhamana za Serikali zilizoiva pamoja na shilingi bilioni 809.1 kwa ajili yakugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mikopo ya Nje yenye Masharti ya Kibiashara​
25.​
Mheshimiwa Spika, mwaka 2012/13 Serikali ilikadiria kukopa mikopoyenye masharti ya kibiashara shilingi bilioni 1,254.1, sawa na Dola zaKimarekani milioni 800 kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleokatika bajeti ya mwaka 2012/13 iliyopitishwa na Bunge lako tukufu. Hadi kufikiaMei 2013, Serikali ilipokea shilingi bilioni 947, sawa na dola milioni 600 kutokabenki ya Stanbic, na shilingi bilioni 59.2, sawa na dola milioni 37 kutoka benk yaCredit Suisse.
Sera za Matumizi​
26.​
Mheshimiwa Spika, Serikali ilitekeleza sera za matumizi kwa kuzingatiavipaumbele vilivyoainishwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2012/13,ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini. Aidha, sera zamatumizi zililenga kupunguza nakisi ya bajeti kwa kuwianisha mapato namatumizi; kuzingatia Sheria ya Fedha za Umma na Sheria ya Ununuzi waUmma; kusimamia ulipaji wa mishahara; na kuendelea kuhakiki na kulipa madaiya wakandarasi, wazabuni, watoa huduma na watumishi, pamoja na kufuatiliautekelezaji wa bajeti.27. Mheshimiwa Spika, Serikali ilikadiria kutumia shilingi bilioni 15,191.9katika mwaka 2012/13. Mgawanyo wa matumizi ya Serikali katika kipindi hikiulikuwa kama ifuatavyo: shilingi bilioni 10,597.1 zilitengwa kwa matumizi yakawaida na shilingi bilioni 4,594.8 zilikadiriwa kutumika kwa ajili ya matumizi yamaendeleo.
Mwenendo wa Matumizi​
28.​
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2013, matumizi ya kawaida bilakujumuisha malipo ya hatifungani zilizoiva (rollover) yalifikia shilingi bilioni7,582.6, sawa na asilimia 82 ya makadirio ya mwaka. Kati ya kiasi hicho, malipoya mishahara ya watumishi wa Serikali, katika wizara, Idara zinazojitegemea,Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Taasisi za Ummayalikuwa shilingi bilioni 3,209.2 sawa na asilimia 85 ya makadirio ya mwaka yashilingi bilioni 3,781.1.29. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2012/13 Serikali iliendelea na udhibiti waulipaji wa mishahara ya watumishi wa Serikali pamoja na taasisi zake. Kwamwaka 2012/13 Serikali imekamilisha uhakiki wa watumishi na malipo yamishahara kwenye Wizara pamoja na Sekretarieti za mikoa. Kazi hii ilianzamwaka 2011/12 kwa kufanya uhakiki wa watumishi wa Serikali kwenye Mamlakaza Serikali za Mitaa na taasisi zote. Matokeo ya uhakiki wa watumishiyalisambazwa kwa waajiri kwa ajili ya kuchukua hatua zinazostahili. Aidha,Serikali imechukua hatua ya kusambaza mfumo wa malipo kwa waajiri wote ilimarekebisho ya mishahara, waajiriwa wapya, kuondoa watumishi wanaomalizautumishi wao (wanaostaafu, wanaofukuzwa, wanaofariki, wanaocha kazi)yaweze kufanyika mara moja baada ya tukio hilo kutokea kwenye kituo cha kazi.Katika mwaka 2013/14 Serikali itaendelea na hatua za kudhibiti mishahara yawatumishi, ikiwa ni pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali kuendeleakukagua eneo hilo.
Maslahi ya Watumishi​
30.​
Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuboresha maslahi ya watumishiwa umma kulingana na uwezo wa mapato yake kwa lengo la kuwawezeshakumudu gharama za maisha. Maeneo ambayo yatatiliwa mkazo ni pamoja naongezeko la mshahara hasa kima cha chini, kupunguza kiwango cha kodi yamapato kwenye mishahara, malipo ya mshahara kwa wakati na kuhakikishawatumishi wanalipwa mafao yao mara baada ya kustaafu.31. Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea kutoa kipaumbele katika kulipaDeni la Taifa. Katika kipindi hicho, malipo ya riba kwa mikopo ya ndani na njeyalikuwa shilingi bilioni 438.8, sawa na asilimia 79 ya makadirio ya shilingi bilioni555.2 kwa mwaka. Malipo ya deni halisi la mikopo ya nje yalikuwa shilingi bilioni79.0, sawa na asilimia 34 ya makadirio ya mwaka. Aidha, Serikali ilitumia shilingibilioni 1,364 kwa ajili ya kulipia dhamana za Serikali za muda mfupi naHatifungani za Serikali zilizoiva. Vilevile, matumizi mengineyo katika Wizara,Idara, Taasisi za Serikali, Mikoa na Halmashauri yalifikia shilingi bilioni 3,000.8ikiwa ni asilimia 74 ya makadirio ya shilingi bilioni 4,070.9 kwa mwaka.32. Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2013, jumla ya shilingi bilioni 3,956.3zilitolewa katika miradi ya maendeleo ikilinganishwa na makadirio ya mwaka yakutumia shilingi bilioni 4,594.8. Kati ya hizo, fedha za ndani zilikuwa shilingibilioni 2.277.2 ikilinganishwa na makadirio ya mwaka ya shilingi bilioni 2,280.6,sawa na asilimia 99.9. Aidha, fedha za nje zilikuwa shilingi bilioni 1,679.1ikilinganishwa na makadirio ya shilingi bilioni 2,314.2 sawa na asilimia 73 yamakadirio ya mwaka.
Usimamizi wa Fedha za Umma​
33.​
Mheshimiwa Spika, mwaka 2012/13, Serikali ilianza kutekelezampangokazi wa miaka mitano wa kuiwezesha Serikali Kuu kuandaa hesabu kwaviwango vipya vya uhasibu vya Kimataifa (IPSAS Accrual Basis). Kwa mara yakwanza hesabu za Wizara, Idara za Serikali zinazojitegemea na Sekretarieti zaMikoa kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2013 zitaandaliwa kwakutumia viwango hivyo. Wizara imeandaa miongozo mbalimbali na kufanyamikutano elekezi ili kuwajengea uwezo wa uelewa wahasibu na wadaumbalimbali.34. Mheshimiwa Spika, katika kudhibiti mapato na matumizi, Serikaliimeandaa na kutoa miongozo ya usimamizi wa vihatarishi katika sekta ya ummapamoja na mwongozo wa uhakiki wa ubora wa ukaguzi wa ndani. Serikali piaimetayarisha mwongozo wa ukaguzi wa ndani kwa kuzingatia viwango vyakimataifa ambao unategemea kuanza kutumika rasmi Julai, 2013. Miongozohiyo ina lengo la kuboresha utendaji kazi wa ukaguzi wa ndani.
Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA II)​
35.​
Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa MKUKUTA II umeonesha mafanikiokatika maeneo mengi ingawa bado kuna changamoto. Mafanikio hayo ni pamojana kuendelea kukua kwa pato la Taifa, kuongezeka kwa mapato ya kodi, kukuakwa sekta ya fedha na mikopo kwa sekta binafsi, kuimarika kwa usimamizi wamatumizi ya Serikali na kuimarika kwa utoaji na upatikanaji wa huduma za jamii.36. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kutathmini hali ya umaskini hapanchini, Serikali imefanikiwa kukamilisha zoezi la ukusanyaji wa takwimu zaUtafiti wa Hali ya Mapato na Matumizi katika kaya binafsi ya mwaka 2012.Uchambuzi wa takwimu hizo unaendelea na unatarajia kukamilika kabla yaDesemba 2013. Aidha, takwimu za Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika 2012,na Utafiti wa Hali ya Ajira na Kipato wa mwaka 2012 vitafanyiwa uchambuzi wakina ili kutuwezesha kupata takwimu zitakazoonesha hali ya umaskini katikangazi mbalimbali.37. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa nguzo ya pili ya MKUKUTA yakuboresha hali ya maisha na ustawi wa jamii, viashiria vingi vilioneshamabadiliko chanya. Viwango vya uandikishaji katika ngazi za elimu ya msingi nasekondari vimeimarika. Aidha, uandikishaji katika ngazi ya vyuo vya ufundi naelimu ya juu uko katika kiwango cha kuridhisha. Matokeo haya yanatokana nautekelezaji wa juhudi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi yashule, vyuo, waalimu, upanuzi wa miundombinu ya ufundishaji na kuongezekakwa mikopo ya elimu ya juu. Changamoto iliyopo ni kuboresha mazingira yakufundishia na kujifunza katika ngazi zote. Katika mwaka 2011/12, Serikaliiliendelea pia kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha huduma za afya, lishe,upatikanaji wa maji safi na salama na utoaji elimu kwa umma kuhusu kinga yamalaria na athari za ugonjwa wa UKIMWI.38. Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha utawala bora na uwajibikaji, Serikaliimechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuimarisha mfumo wa usimamizi wa maliza umma, kuimarisha mfumo wa sheria na haki za binadamu, hususan katikangazi za chini kwa kuongeza idadi ya mahakimu. Hatua hii imeboresha kasi yautoaji maamuzi ya mashauri katika mahakama zetu. Aidha, programu yamaboresho ya sekta ya sheria nayo iliendelea kutekelezwa, lengo likiwa nikuhakikisha kuwa haki za raia zinaboreshwa na kulindwa, hususan wale waliokatika mazingira hatarishi.
Sensa ya Watu na Makazi​
39.​
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/13, Serikali ilifanya Sensa yaWatu na Makazi kama ilivyopangwa ambapo jumla ya shilingi bilioni 127.3zilitumika. Matokeo ya sensa hiyo, yalibainisha kuwa Tanzania ina jumla ya watumilioni 44.9 sawa na ongezeko la asilimia 2.6 kwa mwaka ikilinganishwa namatokeo ya Sensa ya mwaka 2002 ambapo ongezeko lilikuwa asilimia 2.9.(Picha ya sensa)40. Mheshimiwa Spika, kasi ya ongezeko la idadi ya watu ni kubwa kwamikoa ya Dar es Salaam na Mjini Magharibi ambapo kasi ya ongezeko la idadiya watu kwa mkoa wa Dar es Salaam ni asilimia 5.6 kwa mwaka, wakati MjiniMagharibi kasi hiyo ni asilimia 4.2. Aidha, mkoa wa Dar es salaam una idadikubwa ya watu ikilinganishwa na mikoa mingine ukiwa na asilimia 10 ya idadi yawakazi wote wa Tanzania Bara. Vilevile, wastani wa idadi ya watu kwa kaya kwamwaka 2012 umebakia karibu sawa na ule wa mwaka 2002. Wastani ulikuwawatu 4.9 kwa kaya mwaka 2012 ikilinganishwa na watu 4.8 mwaka 2002.Napenda niwajulishe waheshimiwa wabunge kwamba Serikali inatumia takwimuza sensa hii katika kuandaa sera, mikakati, mipango na kufanya tathmini yautekelezaji. Nashauri wadau wengine wafanye hivyo pia wakati wa kuandaamipango ya maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa Taifa letu.41. Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na uchambuzi wa kina wamatokeo ya Sensa ambayo yatahusisha viashiria vya kiuchumi na kijamii.Napenda nitumie nafasi hii kuwajulisha kuwa toleo linalofuata ni la mgawanyowa watu kwa umri na jinsia katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Wilaya ambalolitatolewa mwezi Julai, 2013. Matokeo yanayofuata ambayo yanahusu viashiriavya kiuchumi na kijamii yataendelea kutolewa kama yalivyoanishwa kwenyeratiba ya usambazaji na katika tovuti ya Serikali.
Sekta ya Fedha​
42.​
Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea kutekeleza progamu yamaboresho ya sekta ya fedha ili kuhakikisha kwamba sekta hii inachangiakikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kukuza Pato la Taifa. Katika mwaka2012, huduma ya sekta ya fedha ilichangia asilimia 1.8 ya pato la Taifaikilinganishwa na asilimia 1.7 mwaka 2011. Aidha, katika kipindi hicho, sekta yafedha ilikua kwa asilimia 13.2 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 10.7 mwaka2011. Ongezeko hilo lilitokana na mafanikio ya utekelezaji wa maboresho yasekta ya fedha ambayo yaliwezesha kuongezeka kwa idadi ya benki kutoka 49Februari 2012 hadi 51 Februari 2013; kampuni za bima kutoka 26 mwaka 2011hadi 28 mwaka 2012; na Idadi ya SACCOS kutoka 5,424 Machi 2012 hadi 5,559Machi 2013.43. Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea kutekeleza sera ya fedha yenyelengo la kupunguza ukwasi nchini ambapo Benki Kuu iliongeza mauzo ya fedhaza kigeni katika soko la fedha za kigeni pamoja na mauzo ya dhamana zaSerikali. Aidha, Benki Kuu ilipandisha kiwango cha chini cha fedha zinazotakiwakuhifadhiwa Benki Kuu kwa ajili ya akiba ya amana za serikali katika mabenkikutoka asilimia 30 hadi asilimia 40, pamoja na kupunguza kiwango cha kuhodhifedha za kigeni kulingana na mitaji yao kwa mabenki kutoka asilimia 10 hadiasilimia 7.5 kuanzia Desemba, 2012. Hatua hizo zilisaidia katika kupunguzakiwango cha mfumuko wa bei usiojumuisha chakula na nishati (core inflation)kutoka asilimia 9.0 Aprili, 2012 hadi asilimia 6.5 Aprili, 2013. Vilevile, hatua hizizilisaidia kuimarika kwa kiwango cha ubadilishanaji wa shilingi dhidi ya Dola yaKimarekani.44. Mheshimiwa Spika, Serikali ilifanya utafiti wa huduma ndogo ndogo zabima kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za bima kwa wananchiwalio wengi. Utafiti umebaini kwamba kiwango cha matumizi ya huduma zabima bado ni kidogo, ambapo ni asilimia 19 tu ya watu wazima wanatumiahuduma hizo (hii inajumuisha huduma za bima ya afya zinazotolewa na Mfukowa Taifa wa Bima ya Afya). Utafiti umebaini pia kwamba uhitaji wa hudumandogo ndogo za bima ni mkubwa na upatikanaji wa huduma hizo utasaidiakatika juhudi za Serikali za kukuza uchumi na kuondoa umaskini. Serikaliiliendelea kuwahamasisha wananchi ili waone umuhimu wa kujiunga na hudumaza bima.45. Mheshimiwa Spika, Serikali ilianzisha kampuni ya Tanzania MortgageRefinancing Company (TMRC) ili kuwezesha benki kutoa mikopo ya nyumba. Ilibenki ziweze kupata mikopo hiyo, zinapaswa ziwe na hisa kwenye kampunihiyo. Hadi kufikia Desemba 2012, benki 12 zimenunua hisa. Serikali kupitiaKampuni ya TMRC ilitoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 4.2 kwa benki12 wanachama, ambazo zilitoa mikopo 1,799 yenye thamani ya shilingi bilioni106.2.46. Mheshimiwa Spika, katika kutimiza azma ya Serikali ya kuimarishausimamizi na maendeleo ya Sekta ya Fedha, Serikali inaendelea kuwekamazingira mazuri kwa kuanzisha Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedhaambayo ndani yake kutakuwa na kitengo cha kusimamia sekta ya hudumandogo ndogo za fedha na kitengo cha sera za sekta ya fedha. Muundo huumpya kwa sasa uko katika hatua ya kuridhiwa. Miongoni mwa majukumu yaidara hii ni kuandaa sera ya sekta ya huduma ndogo ndogo za fedha.47. Mheshimiwa Spika, katika kuhamasisha uanzishwaji wa benki zawananchi, Benki kuu imekuwa ikitoa masharti nafuu yanayohusu mtaji wakatizinapoanza. Kwa mfano, wakati benki za biashara zinatakiwa kuwa na mtaji washilingi bilioni 15, benki za wananchi zinatakiwa kuwa na shilingi bilioni 2. Kwaupande mwingine, serikali imekuwa ikihimiza uanzishwaji wa SACCOS,VICOBA na benki za wananchi ili kuwawezesha wananchi kupata mitaji kwa ajiliya biashara na uzalishaji.
Ununuzi wa Umma​
48.​
Mheshimiwa Spika, Bunge lako tukufu limetunga Sheria mpya yaUnunuzi wa Umma Na. 7 ya mwaka 2011 baada ya kubaini upungufuuliokuwepo katika Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 21 ya mwaka 2004. Aidha,Bunge lako pia limetunga Sheria ya Ubia Na. 19 ya mwaka 2010 ambayoutekelezaji wake katika hatua ya kumpata Mbia unatumia Sheria ya Ununuzi waUmma. Hivyo kuna haja ya kufanya marekebisho ya Sheria ya Ununuzi waUmma Na. 7 ya mwaka 2011 ili kuzingatia maboresho na mabadilikoyanayohitajika. Mbali na kuleta uwiano wa Sheria ya Ununuzi na Sheria ya Ubia,maboresho yanalenga kuweka misingi imara ya taratibu za kusimamia ununuziwa umma; kufafanua majukumu ya Mamlaka za usimamizi wa ununuzi waumma; na kuongezea madaraka ya kiutendaji Taasisi za ununuzi na zilezinazosimamia ununuzi wa umma. Aidha, maboresho yanalenga kupunguzamuda wa kushughulikia malalamiko ya wazabuni, na kupunguza muda wamchakato wa ununuzi. Serikali inakusudia kufuta Sheria ya Ununuzi wa Ummana. 21 ya 2004 mara baada ya mabadiliko ya Sheria Na. 7 kukamilika na Kanunimpya kutangazwa katika gazeti la Serikali.
Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi​
49.​
Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kusimamamia sera yake yakushirikisha sekta binafsi ili iweze kuongeza Pato la Taifa. Katika mwaka2012/13, Serikali ilifanya uchambuzi wa awali wa baadhi ya miradi ya PPPkatika sekta za ujenzi wa barabara na bandari. Miradi hiyo ni pamoja na ujenziwa barabara ya Dar es Salaam – Chalinze, bandari ya Katanga, bandari yaMwambani, na bandari ya Mtwara.50. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Sheria ya Ubia ya mwaka 2010,changamoto iliyojitokeza ni kuwepo kwa vitengo na ofisi nyingizinazoshughulikia masuala ya PPP. Kwa kutambua hili, Serikali katika mwaka2013/14 itaunganisha vitengo vya PPP na kufanya mapitio ya sheria na kanuniza ubia kwa nia ya kufanya maboresho. Aidha, katika mwaka 2013/14, Serikaliimepanga kuanzisha mfuko maalumu utakaotumika kugharamia upembuziyakinifu ili kuendeleza miradi ya ubia hapa nchini.
Deni la Taifa​
51.​
Mheshimiwa Spika, hadi mwishoni mwa Machi 2013, Deni la Taifa(likijumuisha deni la umma na sekta binafsi) lilikuwa shilingi bilioni 23,673.53ikilinganishwa na deni la shilingi bilioni 20,276.6 likiwa ni ongezeko la asilimia17. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 18,282.02 ni deni la nje na shilingi bilioni5,397.50 ni deni la ndani. Deni la nje, linajumuisha deni la umma la shilingibilioni 15,203.34 na deni la sekta binafsi ni shilingi bilioni 3,078.69. Kiasi hichocha deni la nje kinajumuisha deni halisi shilingi bilioni 16,087.43 na malimbikizoya riba ya shilingi bilioni 2,194.59. Deni la ndani linajumuisha hati fungani zamuda mrefu kiasi cha shilingi bilioni 4,261.03 na dhamana za Serikali za mudamfupi kiasi cha shilingi bilioni 1,136.48. Mikopo hiyo iligharamia miradi yamaendeleo hususan miundombinu kwa kuzingatia vipaumbele vilivyopitishwa naBunge lako tukufu.
Uhimilivu wa Deni la Taifa​
52.​
Mheshimiwa Spika, Serikali inasimamia deni la taifa kwa kuzingatiaMkakati wa Taifa wa Kusimamia Deni la Taifa pamoja na Sheria ya Mikopo,Dhamana na Misaada ya mwaka 1974 kama ilivyorekebishwa mwaka 2004.Kwa kuzingatia Sheria hiyo, mwaka 2012 Serikali ilifanya tathmini ya kuangaliauhimilivu wa Deni la Taifa. Napenda kulijulisha bunge lako tukufu kwamba,viashiria vyote vya kupima uhimilivu wa deni vilivyokubalika kimataifavinaonesha kuwa, Deni la Taifa ni himilivu katika muda mfupi na muda wa kati.Mathalani, uwiano wa thamani ya sasa ya deni la Taifa kwa Pato la Taifa niasilimia 18.9, ikilinganishwa na ukomo wake wa asilimia 50 na kiashiria chauwiano wa thamani ya sasa ya deni la Taifa kwa mapato yanayotokana namauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi ilikuwa asilimia 53.6 ikilinganishwa naukomo wa asilimia 200.
Tathmini ya Uwezo wa Kukopa na Kulipa Madeni​
53.​
Mheshimiwa Spika, Serikali imepiga hatua kubwa katika kufanikishazoezi la nchi kufanyiwa tathmini ya uwezo wa kukopa na kulipa madeni na ipokwenye hatua ya kupata kampuni za kufanya tathmini. Kazi hii imepangwakukamilika mwaka 2013/14 ambapo itawezesha nchi kukopa kwa gharamanafuu katika masoko ya fedha ya kimataifa kwa ajili ya kugharamia miradimikubwa ya miundombinu. Aidha, kampuni za Tanzania nazo zitaweza kupatamitaji kwa urahisi zaidi kutoka kwenye masoko ya mitaji ya kimataifa.
Ushirikiano wa Kiuchumi wa Kikanda​
54.​
Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuimarisha ushiriki katikaJumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusinimwa Africa (SADC). Ushiriki wetu katika jumuiya hizi ni mojawapo ya mkakatiwa kuhakikisha tunaitumia jiografia ya nchi yetu kwa kukuza uchumi.55. Mheshimiwa Spika, mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Masharikiumefikia hatua ya kuanzisha Umoja wa Fedha na majadiliano ya Itifaki hiyoyanaendelea na yanatarajiwa kukamilika mwezi Novemba 2013. Aidha, hatuazinachukuliwa za kutekeleza Itifaki ya Soko la Pamoja ambapo yameainishwamaeneo katika sheria zetu yanayotakiwa kufanyiwa marekebisho ili kuwezeshaushiriki wa nchi katika soko hili. Baadhi ya sheria zitakazo rekebishwa ni zilezinazohusika na taratibu za kuwezesha watanzania kuwekeza mitaji yao katikanchi za Jumuiya; lengo likiwa kurahisisha biashara ya mitaji na huduma ilikuchochea uwekezaji.56. Mheshimiwa Spika, mwaka 2012/13, Serikali iliendelea na utekelezaji waMpango Mkakati wa Maendeleo wa SADC, ambapo taratibu za kuridhia Itifaki yaFedha na Uwekezaji ya SADC zimekamilika. Itifaki hii itarahisisha taratibu zauwekezaji katika nchi za SADC, kuwezesha nchi za SADC kuwianisha sera zakodi hasa eneo la vivutio vya uwekezaji. Kupitia Itifaki hii, nchi za SADCzitaweza kubuni na kutekeleza sera za kuimarisha uchumi na fedha kwa pamojakwa lengo la kuwa na utulivu wa uchumi katika ukanda huu na hivyo kuvutiauwekezaji. Ili kuhakikisha azma hii inatekelezwa kwa vitendo, nchi za SADCzinakamilisha utaratibu wa kuanzisha Mfuko wa Maendeleo.
III. MAFANIKIO NA CHANGAMOTO KATIKA UTEKELEZAJI WA BAJETIYA MWAKA 2012/13​
57.​
Mheshimiwa Spika, mafanikio na changamoto za utekelezaji wa bajetikwa mwaka 2012/13 kwa kila sekta yameelezwa kwa kina katika hotuba zabajeti za wizara husika ambazo bunge lako tukufu limepata fursa ya kuzijadili nakuzipitisha. Kwa kuzingatia hilo, nitaeleza kwa kifupi baadhi ya mafaniko nachangamoto hizo.
Ukusanyaji wa Mapato​
58.​
Mheshimiwa Spika, bajeti ya mwaka 2012/13 ilitekelezwa kwa mafanikio,hususan katika ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi; utoaji wa huduma za jamii;kuimarisha ulinzi na usalama, pamoja na utengamano wa kikanda na kimataifa.Aidha, Serikali imefanikiwa kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani, hususanmapato ya kodi kutoka wastani wa shilingi bilioni 540 kwa mwezi kwa mwaka2011/12 hadi shilingi bilioni 640 kwa mwezi kwa mwaka 2012/13. Pamoja nawastani huo wa mwezi, kiwango cha juu cha makusanyo kilifikiwa mweziDesemba 2012, ambapo makusanyo ya kodi na yasiyo ya kodi yalikuwa shilingibilioni 890.
Ukuaji wa Uchumi​
59.​
Mheshimiwa Spika, Pato la Taifa limeendelea kuimarika mwaka 2012ambapo ukuaji halisi ulikuwa asilimia 6.9 ikilinganishwa na asilimia 6.4 mwaka2011. Ongezeko hili la ukuaji lilitokana na kuboreshwa kwa miundombinu yausafirishaji na mawasiliano, pamoja na kuimarika kwa uzalishaji viwandanikutokana na jitihada za serikali za kuhakisha upatikanaji wa umeme wa uhakikasambamba na matumizi ya nishati mbadala katika uzalishaji viwandani.60. Mheshimiwa Spika, sekta ya mawasiliano ndiyo ilikuwa na kiwangokikubwa cha ukuaji wa asilimia 20.6 mwaka 2012. Pamoja na kuwa na kiwangokikubwa cha ukuaji, sekta ya mawasiliano ilichangia asilimia 2.3 tu katika Pato laTaifa ikilinganishwa na sekta ya kilimo ambayo pamoja na kukua kwa kiwangokidogo ilichangia asilimia 24.7 katika Pato la Taifa mwaka 2012. Zaidi ya asilimia70 ya watanzania wamejikita katika shughuli za kilimo, hivyo hii ni sekta ambayoserikali inaitilia mkazo ili kuhakikisha kuwa inaleta mafanikio yanayotarajiwa nawengi, ikiwemo kupunguza umaskini. Serikali imefanya jitihada kubwa zakuboresha sekta hii lakini bado imeendelea kukua kwa kiwango kisichozidiasilimia 5 kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.(picha ya Kilimo)61. Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na jitihada za kuimarisha sektaya kilimo ili ikue kwa kasi zaidi na kuongeza kipato na hivyo KupunguzaUmaskini kwa wananchi walio wengi. Juhudi hizo zinahusisha kuendelezamiundombinu ya umwagiliaji ili kuondokana na kilimo cha kutegemea mvua;kutoa ruzuku za pembejeo za kilimo kwa wakati zikiwemo mbolea, madawa nambegu bora; kuondoa kodi katika zana mbalimbali za sekta ya kilimo ilikuongeza tija; kuimarisha masoko ya mazao, kuongeza thamani ya mazao yakilimo, mifugo na uvuvi na uhifadhi; na kuimarisha barabara vijijini. Aidha,Serikali itaendeleza juhudi za upatikanaji wa umeme na maji vijijini. Vilevile,Serikali itaimarisha sekta nyingine za kiuchumi zenye kutoa ajira kama vilesekta za ujenzi na uzalishaji viwandani, pamoja na kupanua wigo wa kinga yajamii ili kuongeza ushiriki wao kwenye shughuli za uchumi na hivyo kuinua Patola wananchi na kuongeza kasi ya kupunguza umaskini wa kipato.
Mwenendo wa Bei​
62.​
Mheshimiwa Spika, wastani wa mfumuko wa bei kwa mwaka 2012uliongezeka kwa asilimia 16.0 ikilinganishwa na asilimia 12.7 mwaka 2011.Upandaji huu wa bei ulitokana hasa na kupanda kwa bei ya mafuta ya petrolikatika soko la dunia na kupanda kwa bei za chakula kulikotokana na mahitajimakubwa ya chakula katika baadhi ya nchi jirani. Ikumbukwe kwamba chakulapeke yake huchangia asilimia 47.8 ya bidhaa na huduma zinazotumika katikaukokotoaji wa fahirisi ya bei kwenye kapu la bidhaa za walaji, ikifuatiwa nausafiri (asilimia 9.5) na nishati (asilimia 9.2). Makundi haya ni muhimu sanakatika kuchochea mwelekeo wa bei za bidhaa na huduma mbalimbali. Katikakukabiliana na kasi ya kupanda kwa bei za bidhaa na huduma, Serikali ilichukuahatua kadhaa zikiwemo:(i) Kuhakikisha kuwa kunakuwa na ugavi mzuri wa chakula unaoendana namahitaji nchini;(ii) Kupanua kilimo cha mazao ya chakula na kuongeza upatikanaji wapembejeo za kilimo zikiwemo mbolea, madawa na mbegu bora;(iii) Kuimarisha miundombinu ya usafirishaji; na(iv) Kupandisha kiwango cha riba ya Benki Kuu inayotozwa kwa mikopoiendayo kwa taasisi za fedha nchini kutoka asilimia 7.58 hadi asilimia 12.58.63. Mheshimiwa Spika, hatua hizi ziliwezesha kupunguza kiwango chamfumuko wa bei kutoka asilimia 18.7 mwezi Aprili 2012 hadi asilimia 9.4 mweziAprili 2013.
Mafanikio katika Sekta mbalimbali​
64.​
Mheshimiwa Spika, Serikali ilitoa jumla ya shilingi bilioni 826.1 kwa ajiliya kuwezesha upatikanaji wa umeme na kutekeleza miradi mbalimbali yakimkakati. Baadhi ya miradi iliyotekelezwa ni pamoja na: kuanza ujenzi wabomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ikijumuisha ujenzi wa kituocha kupokelea gesi Kinyerezi; kukamilisha ujenzi na kuanza kuzalisha umemekwa kutumia mafuta mazito katika vituo vya Ubungo - Dar es Salaam (MW 105)na Nyakato - Mwanza (MW 60); kuendeleza miradi ya umeme vijijini katikamikoa 16; na kuendeleza upembuzi yakinifu katika miradi ya Makaa ya Mawe –Mchuchuma na Liganga. Aidha, hadi kufikia mwezi Desemba 2012, kiasi chaumeme kilichoingizwa kwenye Grid ya Taifa kilikuwa MWh 5,759,756ikilinganishwa na MWh 5,153,400 mwaka 2011, sawa na ongezeko la asilimia11.8.65. Mheshimiwa Spika, sekta ya maji iliendelea kupewa kipaumbele katikamwaka 2012/13 kwa kuendeleza ujenzi wa miradi ya maji katika vijiji 682 kupitiampango wa vijiji kumi kwa kila Halmashauri; uboreshaji wa mamlaka za majimijini; na ujenzi wa miundombinu ya maji, ikiwemo bomba la maji la Ruvu Chinihadi Dar es Salaam. Ili kutekeleza miradi ya maji, Serikali ilitoa jumla ya shilingibilioni 106.6 katika ngazi ya Wizara na shilingi bilioni 98.4 katika ngazi yaHalmashauri.66. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/13, Serikali ilitoa jumla ya shilingibilioni 537.40 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya tiba, kinga na ustawi wajamii. Fedha hizo pia zilitumika katika kuendeleza ujenzi na ukarabati wamiundombinu ya afya; kuimarisha stadi na kujenga uwezo wa rasilimali watu; nakuanza ujenzi wa Chuo Kikuu cha Afya, Mlonganzila - Dar es Salaam.67. Mheshimiwa Spika, Serikali ilitoa jumla ya shilingi bilioni 2,421.5 katikasekta ya elimu kwa ajili ya kugharamia shughuli mbalimbali katika shule zamsingi, sekondari, elimu ya watu wazima, vyuo vya ufundi stadi, na vyuo vyaelimu ya juu. Baadhi ya shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na: ulipaji wamishahara kwa wakati; kuajiri walimu wapya 27,773 (walimu 13,633 wa shule yamsingi, 14,060 wa sekondari na 80 wa vyuo vya ualimu) na kuwalipa stahili zao;kugharamia uendeshaji mashuleni (Capitation); kutoa mikopo kiasi cha shilingibilioni 326.1 kwa wanafunzi 96,350 wa elimu ya juu; kuanza ujenzi wa maabarakatika shule mbili kwa kila Halmashauri 132 ambapo kiasi cha shilingi bilioni102.3 kimetolewa; ununuzi wa vitabu vya kiada na ziada 27,159,106 kwa ajili yashule za msingi; na kuendelea kuboresha miundombinu ya kutolea elimu katikangazi zote nchini.68. Mheshimiwa Spika, Serikali ilitoa jumla ya shilingi bilioni 1,044.2 kwa ajiliya kujenga na kukarabati barabara za lami; kufanya matengenezo maalumu naya kawaida kwenye barabara za changarawe; kuboresha barabara za wilayapamoja na kujenga na kukarabati madaraja. Aidha, fedha hizo zilitumika kwa ajiliya kuanza ujenzi wa vivuko vitatu na maegesho; kukarabati vivuko vitano; nakufanya upembuzi yakinifu wa kujenga barabara na vivuko katika maeneomengine nchini. Vilevile, Serikali iliendelea na ujenzi na ukarabati wa barabaraza Dar es Salaam na miji mingine mikuu ili kupunguza msongamano wamagari.69. Mheshimiwa Spika, sekta ya uchukuzi ilipewa jumla ya shilingi bilioni181.8 kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo: kuanzisha usafiri wa treni yaabiria jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari naadha ya usafiri jijini Dar es Salaam; kuboresha na kurejesha huduma za treni zaabiria na mizigo katika reli ya kati na TAZARA; na kuendeleza miradi ya ujenziwa viwanja vya ndege vya Songwe, Katavi, Mwanza, Kigoma na Tabora.(picha treni ya Mwakyembe)70. Mheshimiwa Spika, kuhusu kuimarisha utawala bora, Serikali ilitoa jumlaya shilingi bilioni 27.0 kwa ajili ya mchakato wa marekebisho ya Katiba ikiwa nipamoja na kukusanya kura za maoni katika mikoa yote 30 ya Tanzania Bara naZanzibar na shilingi bilioni 40 kutekeleza mradi wa vitambulisho vya Taifa. Aidha,shughuli zingine muhimu zilizotekelezwa ni kukamilisha rasimu ya awali yakatiba mpya, kuchapisha nakala za rasimu ya katiba mpya na kuzisambaza kwawadau mbalimbali nchini pamoja na kuendesha mikutano ya Mabaraza yaKatiba.(picha ya katiba)71. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na upungufu wa chakula kwenyebaadhi ya maeneo nchini, Serikali ilitoa jumla ya shilingi bilioni 42.87 mwaka2012/13 zilizotumika kununua tani 53,269.70 za nafaka kwa ajili ya kuongezachakula cha hifadhi ya Taifa. Aidha, Serikali ilisambaza chakula cha msaadakwa wananchi wenye mahitaji katika Halmashauri 47 na kuuza jumla ya tani16,653 kwa wasagishaji wa nafaka ili kurahisisha usambazaji wa unga wasembe na hatimaye kupunguza mfumuko wa bei nchini. Vilevile, uzalishaji wachakula katika msimu wa mwaka 2012/13 ulifikia tani milioni 13.34ikilinganishwa na mahitaji ya chakula ya tani milioni 11.97.(chakula cha msaada)72. Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio hayo, changamoto bado ninyingi, ambazo ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa mapato kutoka vyanzovya ndani na upatikanaji wa mikopo ya nje yenye masharti ya kibiashara kwawakati na hivyo kuchelewa kupeleka fedha kwenye sekta husika. Changamotonyingine ni: madai ya wakandarasi, wazabuni, watumishi na watoa huduma wandani na nje; kuimarisha miundombinu; kupata thamani ya fedha katika ununuziwa umma; kuongeza ubora na tija katika uzalishaji; kutumia fursa za kijiografiakatika ukuzaji wa uchumi; upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika;kusimamia deni la Taifa; kudhibiti mfumuko wa bei na mabadiliko ya tabianchi.73. Mheshimiwa Spika, changamoto nyingine ni: huduma za jamii hususanelimu, afya, na maji bado hazijafikia viwango vinavyotarajiwa; kuongeza fursa zaajira; kukuza ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi (PPP); na upatikanajiwa huduma za mikopo ya kilimo. Changamoto hizo zitaendelea kutafutiwaufumbuzi hatua kwa hatua katika kipindi cha muda wa kati na muda mrefu.Aidha, Serikali imejipanga kukabiliana na baadhi ya changamoto hizi katikamwaka 2013/14.
IV. BAJETI YA MWAKA 2013/14​
74.​
Mheshimiwa Spika, bajeti ya mwaka 2013/14 itazingatia vipaumbelevilivyoainishwa kwenye: Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2013/14 na mfumompya wa utekelezaji wa vipaumbele vyenye matokeo makubwa na ya haraka(Big Results Now – BRN); Awamu ya Pili ya Mkakati wa Kukuza Uchumi naKupunguza Umasikini (MKUKUTA II); Malengo ya Maendeleo ya Milenia 2015;Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010; na programu za maboresho katikasekta ya umma. Lengo likiwa ni kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.
Shabaha na Malengo ya Bajeti kwa Mwaka 2013/14​
75.​
Mheshimiwa Spika, bajeti ya mwaka 2013/14, imejielekeza katika kufikiashabaha na malengo ya uchumi jumla yafuatayo:-(i) Pato halisi la Taifa linatarajiwa kukua kwa asilimia 7.0 mwaka 2013,na asilimia 7.2 mwaka 2014;(ii) Kuendelea kudhibiti kasi ya upandaji bei ili ibaki kwenye viwango vyatarakimu moja, ambapo mfumuko wa bei unatarajiwa kushuka zaidi kufikiaasilimia 6.0 Juni 2014;(iii) Kuongezeka kwa mapato ya ndani yatakayofikia uwiano na Pato laTaifa wa asilimia 20.2 mwaka 2013/14 ikilinganishwa na matarajio yaasilimia 17.7 kwa mwaka 2012/13;(iv) Kuwa na nakisi ya bajeti (ikijumuisha misaada) ya asilimia 5.0 yaPato la Taifa mwaka 2013/14;(v) Kudhibiti ongezeko la ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3)katika wigo wa asilimia 15.0 Juni 2014 utakaowiana na malengo ya ukuajiwa uchumi na kasi ya upandaji bei;(vi) Kuwa na akiba ya fedha za kigeni itakayoweza kukidhi mahitaji yauagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi kisichopungua mieziminne mwaka 2013/14;(vii) Kupunguza tofauti ya viwango vya riba vya kuweka na kukopa; na(viii) Kuimarisha thamani ya Shilingi na kuwa na kiwango imara chaubadilishanaji wa fedha kitakachotokana na mwenendo wa soko la fedha.
Misingi ya Bajeti ya Serikali kwa kipindi cha mwaka 2013/14​
76.​
Mheshimiwa Spika, ili kufikia malengo yaliyoainishwa hapo juu, misingiya bajeti ya Serikali kwa kipindi cha mwaka 2013/14 ni hii ifuatayo:(i) Kuendelea kuimarisha na kudumisha amani, usalama, utulivu nautengamano;(ii) Kuendelea kuboresha viashiria vya uchumi jumla na maendeleo yajamii vikiwemo Pato la Taifa, biashara ya nje, fedha, mapato na matumizina viashiria vya huduma za jamii;(iii) Kuongeza mapato ya ndani kwa kuimarisha vyanzo vilivyopo nakubuni vyanzo vipya vya mapato;(iv) Kuboresha usimamizi wa fedha za umma;(v) Kuimarisha mfumo wa IFMS na kuhakikisha unatumika kuwekamihadi ya huduma na bidhaa kabla ya malipo;(vi) Kuzingatia vipaumbele vilivyopo katika Mpango wa Kwanza waMaendeleo wa Miaka Mitano hasa vipaumbele vyenye matokeo makubwana ya haraka pamoja na MKUKUTA II;(vii) Kuboresha mfumo wa utekelezaji wa vipaumbele na uwajibikaji;(viii) Kuendelea kuimarisha sera za fedha ili ziendane na sera za bajetizitakazosaidia kupunguza mfumuko wa bei na tofauti ya riba za amana naza mikopo; na(ix) Kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ikiwa nipamoja na kuvutia ushiriki wa sekta binafsi katika uchumi.
Sera za Mapato​
77.​
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Serikali inakusudia kuchukuahatua mbalimbali za kuimarisha mapato ya ndani yanayotokana na kodi nayasiyo ya kodi. Sera za mapato zinajumuisha kupanua wigo wa kodi kwakubainisha vyanzo vipya na kuimarisha usimamizi wa ukusanyaji wa mapatokutoka vyanzo vilivyopo. Aidha, hatua zaidi zitachukuliwa kudhibiti nakupunguza misamaha ya kodi. Kwa ujumla, sera na hatua zitakazotekelezwakatika mwaka wa fedha 2013/14 zinalenga kuimarisha uwezo wa Serikalikukusanya mapato ya ndani ili kupunguza utegemezi kutoka nje, na kupunguzakutegemea kodi zinazotokana na biashara za kimataifa ambazo zimeanzakushuka kutokana na kuongezeka kwa biashara za ushirikiano wa kikandakatika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusinimwa Afrika.78. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mikakati ya pamoja ya kuongezamapato ya Serikali, napenda kuchukua fursa hii kukushukuru wewe binafsi kwahatua uliyochukua ya kuunda Kamati ya Spika ili kuishauri Serikali kuhusuvyanzo vya mapato ambapo mapendekezo yake yamezingatiwa katika Sera zaMapato kwenye Bajeti ya mwaka 2013/14.79. Mheshimiwa Spika, Serikali itatekeleza baadhi ya mapendekezoyaliyotolewa na Labs ya kubuni vyanzo vya mapato. Baadhi ya mapendekezohayo ni kuanza kuuza vitalu vya misitu na uwindaji kwa njia ya mnada nakufanya tathmini ya mali na ardhi ili kuimarisha makusanyo ya tozo ya mali nakodi ya ardhi. Hatua nyingine za kumairisha makusanyo ya mapato yasiyo yakodi tayari zimeshatangazwa kupitia bajeti za Wizara husika.(Picha ya Wanyama)80. Mheshimiwa Spika, Serikali katika mwaka wa fedha wa 2013/14itatekeleza mikakati mbalimbali ya kuimarisha ukusanyaji wa mapato ilikupunguza utegemezi. Moja ya hatua muhimu itakayotekelezwa katika mwaka2013/14 ni kuangalia upya misamaha ya kodi kwa lengo la kuipunguza. Hatuanyingine zitakazochukuliwa ni pamoja na:(i) Kupunguza misamaha ya kodi kwa kufuta msamaha wa kodi yaongezeko la thamani kwenye huduma za utalii. Aidha, Sheria ya Uwekezajiitafanyiwa marekebisho ili kupunguza misamaha ya kodi na kubakizamisamaha yenye tija na yenye kuchochea uwekezaji mkubwa katika sektaza uchumi za kimkakati;(ii) Kuendelea kuunga mkono jitihada za kuanzishakituo kimoja chakutoa huduma bandarini (one stop centre) katika bandari. Aidha, Serikaliitaendelea kutekeleza mpango wa kuanzisha One Stop Border Posts katikamipaka kwenye vituo vya Holili, Mutukula, Sirari, Horohoro, Kabanga,Tunduma, Rusumo na Namanga;(iii) Kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa Serikali wakiwemo waMamlaka ya Mapato ili kupata ujuzi wa kuthibiti mbinu za kukwepa kodizinazotumiwa na makampuni makubwa hasa katika sekta za mawasiliano,madini na gesi ukiwemo ujuzi wa kukagua uhamishaji wa gharama yaani“transfer pricing” hivyo kudhibiti mianya ya kupotea kwa mapato;(iv) Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendela kuimarisha matumizi yamashine za kieletroniki za kutoa risiti (Electronic Fiscal Devices-EFDs)
ambazo zimeunganishwa moja kwa moja na Mamlaka kwa mtandao wakompyuta ili kuhakikisha kuwa Serikali inapata mapato yake stahiki. Aidha,Mashine hizi zinasimamiwa kupitia mtandao wa kielektroniki ambapohupeleka moja kwa moja taarifa kwenye hifadhi kuu ya Mamlaka kila siku.(v) Kuwajengea uwezo watumishi kwa kutoa mafunzo ya muda mfupi namrefu ndani na nje ya nchi, hususan katika sekta ya gesi, mafuta na madiniili kusimamia ipasavyo mapato yatokanayo na rasimali hizo; na(vi) Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania itaanzisha mfumo mpyaujulikanao kama​
Revenue Gateway ambao utaanza kutumika rasmikuanzia tarehe 1 Julai 2013. Mfumo huo unalenga kuboresha mifumoiliyopo ya ulipaji kodi na upatikanaji wa taarifa za malipo ya kodi kwa njiaya mtandao. Aidha, mfumo huo utarahisisha uhamishaji wa fedha kutokakwenye benki za biashara hadi Mfuko Mkuu wa Serikali. Vilevile, mlipakodiatalazimika kujisajili kwa ajili ya kufanya malipo kupitia tovuti ya Mamlakaya Mapato Tanzania kabla ya kulipa kupitia mfumo wa Tanzania InterbankSettlement System (TISS). Mtumiaji wa mfumo huuatanufaika kwa kupatataarifa kwa njia ya barua pepe kuhusu malipo yake ya kodi aliyofanya.81. Mheshimiwa Spika, Sera za mapato katika mwaka 2013/14, zinalengakukusanya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi ya shilingi bilioni 11,154.1 sawa naasilimia 20.2 ya Pato la Taifa. Kati ya kiasi hicho, mapato ya kodi ni shilingibilioni 10,412.9, na mapato yasiyo ya kodi ni shilingi bilioni 741.1.0. Mapatoyanayotokana na vyanzo vya Halmashauri ni shilingi bilioni 383.5 sawa naasilimia 0.7 ya Pato la Taifa.
Mikopo ya Ndani​
82.​
Mheshimiwa Spika, Serikali bado ina changamoto ya kugharamia miradiya maendeleo kwa kutegemea mapato ya ndani. Ili kukabiliana na changamotohiyo, Serikali itakopa shilingi bilioni 1,700 katika mwaka 2013/14 kutoka soko landani. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 552.3 sawa na asilimia moja ya Pato laTaifa ni kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo na kiasi cha shilingi bilioni1,147.6 ni kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za Serikali za muda mfupizinazoiva.
Misaada na Mikopo ya Masharti Nafuu​
83.​
Mheshimiwa Spika, Washirika wa Maendeleo wamekuwa wakichangiakatika bajeti ya matumizi ya kawaida na maendeleo. Katika mwaka2013/14,Serikali inatarajia kupata misaada na mikopo yenye masharti nafuukiasi cha shilingi bilioni 3,855.2 kutoka kwa Washirika wa Maendeleo. Kati yafedha hizo, misaada na mikopo ya kibajeti ni shilingi bilioni 1,163.1; misaada namikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni shilingi bilioni 2,191.6; na mifuko yakisekta ni shilingi bilioni 500.84. Mheshimiwa Spika, kutokana na juhudi zao za kuchangia maendeleoyetu, naomba kuwatambua na kuwashukuru Washirika wa Maendeleo yetukama ifuatavyo: Nchi za Canada, China, Denmark, Finland, Hispania, India,Ireland, Italia, Japani, Korea ya Kusini, Marekani, Norway, Sweden, Ubelgiji,Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Ujerumani, na Uswisi, pia taasisi mbalimbali zaKimataifa ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Dunia, BADEA,Global Funds, OPEC Fund, Saudi Fund, Umoja wa Ulaya, Shirika la Fedha laKimataifa (IMF) na Mashirika ya Umoja wa Mataifa. Tunawashukuru sana natunathamini michango yao.
Mikopo ya nje yenye Masharti ya Kibiashara​
85.​
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia mahitaji makubwa ya kuendelezamiradi ya maendeleo kwa mwaka 2013/14 na changamoto za upatikanaji wamapato ya ndani, Serikali itakopa kutoka nje mikopo yenye masharti nafuu yakibiashara shilingi bilioni 1,156.4, sawa na Dola za Marekani milioni 700. Mikopohiyo itatumika kugharamia miradi ya maendeleo kama ilivyoainishwa kwenyeMpango wa Maendeleo wa mwaka 2013/14. Uamuzi wa kuendelea kukopa kwamasharti nafuu ya kibiashara unazingatia uhimilivu wa Deni la Taifa uliopo.
Sera za Matumizi​
86.​
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Serikali itatekeleza sera zamatumizi zifuatazo:-(i) Kuwianisha matumizi na mapato yanayotarajiwa;(ii) Nakisi ya bajeti (ikijumuisha misaada) haitazidi asilimia 5.0 ya Pato laTaifa;(iii) Mafungu yatazingatia viwango vya matumizi vitakavyoidhinishwa naBunge;(iv) Kutenga fedha za kutosha katika kutekeleza miradi ya vipaumbelevilivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo; na(v) Kuzingatia Sheria ya Fedha za Umma na Sheria ya Ununuzi wa Umma.87. Mheshimiwa Spika, matumizi ya kawaida kwa mwaka 2013/14yanalenga katika kufanikisha maeneo yafuatayo: kugharamia nyongeza yamishahara pamoja na kulipa mishahara kwa wakati; kuboresha huduma zakiuchumi na maendeleo ya jamii; kukamilisha mchakato wa upatikanaji waKatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; kuendelea na utoaji wavitambulisho vya Taifa; kukamilisha uchambuzi wa takwimu za sensa ya watu namakazi; maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015; na kuendelea kulipamadeni ya ndani na nje yaliyoiva pamoja na madai mbalimbali ya watumishi nawazabuni yaliyohakikiwa.88. Mheshimiwa spika, katika bajeti ya mwaka 2012/13, Serikali ililengakupunguza matumizi yasiyo ya lazima katika maeneo mbalimbali kama vilesemina, usafiri wa ndani na nje, ununuzi wa samani, maonesho mbalimbali nakatika magari. Matokeo ya hatua hizi yameleta mafanikio kadhaa ikiwemoyafuatayo: semina na warsha zimepunguzwa; manunuzi ya magari mapyayamepunguzwa na yananunuliwa kwa kibali cha Waziri Mkuu tu na ukubwa wainjini umepunguzwa na kubaki zenye ukubwa uliokubalika (cc 3,000 au chini yahapo); maonyesho pia yamepunguzwa mfano maadhimisho ya wiki ya utumishiwa umma hayakufanyika mwaka 2012/13; ununuzi wa samani kutoka njeumepungua.89. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Serikali itaendelea kudhibitimatumizi yake katika maeneo mbalimbali ikiwemo kutumia malipo ya simu kablaya huduma; kutumia utaratibu wa ununuzi wa magari wa pamoja ambaoutapunguza gharama za ununuzi; kupunguza matumizi ya magari ya Serikalikwa kuanzisha utaratibu wa kuwakopesha magari watumishi wa Serikaliwanaostahili; kuoanisha kanuni za ununuzi wa umma za Serikali Kuu na Serikaliza Mitaa kwa lengo la kuimarisha ununuzi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;na kuhimiza matumizi ya samani zinazotengenezwa nchini.90. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa matumizi ya maendeleo, bajetiitazingatia kutekeleza vipaumbele vya Mpango wa Kwanza wa Maendeleo waMiaka Mitano ambao mwaka 2013/14 unaingia mwaka wa tatu wa utekelezajikama ifuatavyo:
(i) Miundombinu​
: - miundombinu ya nishati; usafirishaji (barabara, reli,viwanja vya ndege, usafiri wa majini ); TEHAMA; maji safi na maji taka naumwagiliaji;
(ii) Kilimo​
: – ikijumuisha mazao ya chakula na biashara, malighafi yaviwandani, ufugaji, uvuvi na misitu;
(iii) Viwanda​
: – vinavyotumia malighafi hususan za ndani, na kuongezathamani, viwanda vikubwa vya mbolea na saruji, viwanda vya kanda maalum zakiuchumi, kielektroniki na TEHAMA;(iv) Maendeleo ya rasilimali watu na Ujuzi kwa kutilia mkazo sayansi,teknolojia na ubunifu;(v) Uendelezaji wa huduma za utalii, biashara na fedha; na
(vi) Huduma za jamii​
: kuimarisha upatikanaji na ubora wa huduma za jamii.91. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Serikali itaendelea kuboreshamfumo wa ugawaji wa fedha kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kwakuzingatia sera ya ugatuaji wa madaraka na raslimali. Aidha, Serikali itaimarishamifumo ya ndani ya mapato na matumizi kwa kutoa miongozo mahsusi yaukaguzi wa ndani, kuimarisha utendaji wa kamati za ukaguzi, kutoa mafunzo yausimamizi na uimarishaji mifumo ya udhibiti wa ndani kwa Wakurugenzi waHalmashauri. Vile vile, Mamlaka za Serikali za Mitaa zitawezeshwa kuainishauwezo wa pato la kila Halmashauri na fursa zilizopo katika ukusanyaji wamapato ya ndani; na kujenga uwezo wa Halmashauri katika matumizi ya mfumowa IFMS; kuhuisha baadhi ya vyanzo vya mapato ya ndani ili kuongeza mapato;kuboresha mfumo wa uthamini wa majengo kwa kutumia kanuni za jumla;kuhamasisha Halmashauri kutumia teknolojia rahisi ya mitandao ya simu zamkononi katika kufanya malipo.92. Mheshimiwa Spika, ili kuwezesha Wizara, Idara zinazojitegemea, Mikoana Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza majukumu yao, Serikali itahakikishakwamba mafungu yanapata fedha kama ilivyoidhinishwa na Bunge lako tukufu.Kwa hali hiyo, Serikali itaongeza juhudi za kukusanya mapato ya ndani,kuharakisha majadiliano na Washirika wa Maendeleo na wakopeshajimbalimbali katika kutafuta mikopo na misaada kwa wakati. Ninatoa wito kwaWizara, Idara zinazojitegemea, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaakuhakikisha kwamba wanatimiza masharti na taratibu za kupata fedhazilizoidhinishwa na Bunge.
Mfumo Mpya wa Uandaaji na Utekelezaji wa Vipaumbele vya Miradi yaMaendeleo​
93.​
Mheshimiwa spika,kama ilivyoelezwa hapo awali kwenye hotuba yaWaziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu, Mh. StephenMasatu Wassira (Mb), Serikali imeainisha maeneo ya kimkakati ambayoyatafungua fursa ya mapinduzi ya kiuchumi na kuleta matokeo makubwakiuchumi na kijamii kwa muda mfupi. Maeneo hayo ni utafutaji wa mapato,kilimo, maji, elimu, nishati na miundombinu ya uchukuzi. Serikali imedhamiriakutekeleza miradi kwenye maeneo hayo katika kipindi cha muda wa kati.Utekelezaji madhubuti wa vipaumbele hivi utafanikisha kufikia malengo ya Diraya Taifa ya Maendeleo 2025 ya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati.94. Mheshimiwa spika, ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi yamaendeleo, Serikali imeweka mikakati ya kuongeza nidhamu ya kupanga nakutekeleza miradi ya mendeleo ili kupata matokeo yanayowiana na thamanihalisi ya fedha. Kwa kuzingatia hilo, Serikali imeainisha maeneo makuu sitakama nilivyoeleza hapo awali ambayo yatazingatiwa katika kipindi cha miakamitatu ijayo. Aidha, kama mnavyofahamu, Serikali imeunda chombo(Presidential Delivery Bureau) kitakachoratibu, kufuatilia na kutathminiutekelezaji wa miradi katika sekta zilizobainishwa.95. Mheshimiwa spika,katika mwaka 2013/14, Serikali imeweka kipaumbelekatika kutatua kero ya maji kwa wananchi ambapo shilingi bilioni 747.6zimetengwa kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya maji mijini na vijijini. Katikakipindi cha muda wa kati, Serikali itaendelea na juhudi za kuimarisha upatikanajiwa maji safi na salama.96. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha miundombinu ya uchukuzi ambayoinajumuisha barabara, reli, madaraja, bandari na viwanja vya ndege, Serikaliimetenga shilingi bilioni 2,169.0 katika mwaka 2013/14 ikilinganishwa na shilingibilioni 1,940.0 mwaka 2012/13. Kati ya fedha hizo zilizotengwa mwaka 2013/14,shilingi bilioni 196.8 ni kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya reliikilinganishwa na shilingi bilioni 134.2 zilizotengwa mwaka 2012/13, sawa naongezeko la asilimia 46.6. Aidha, Serikali imedhamiria kuongeza bajeti nakuchukua hatua za kuishirikisha sekta binafsi katika kuimarisha miuondombinuya reli.97. Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza sekta ya nishati na madini, juhudizitaelekezwa katika kuongeza uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umemeambapo jumla ya shilingi bilioni 1,116.3 zimetengwa kwa ajili hiyo ikilinganishwana shilingi bilioni 731.8 mwaka 2012/13, sawa na ongezeko la asilimia 52.5.(Picha ya nguzo ya umeme)
Sekta ya Fedha​
98.​
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Serikali itachukua hatuazifuatazo katika kuboresha sekta ya fedha:-(i) Kutunga sheria ya Mfumo wa Malipo nchini kwa ajili ya kuwa na utaratibuwa usimamizi wa mifumo ya malipo nchini ili kuboresha matumizi ya kielektronikikatika kufanya malipo, hususan kwa kutumia simu za mikononi, huduma zabenki kwa njia ya mtandao, vituo vya mauzo na mashine za kutolea fedha(ATM);(ii) Kuandaa Sera ya Bima ya Taifa; na(iii) Kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Taasisi ndogo za Fedha, 2002.99. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2013/14 Serikali itaendeleana hatua za kuboresha sekta ya hifadhi ya jamii kwa kutekeleza kazi zifuatazo:-(i) Kuandaa kanuni na miongozo ambayo itajikita katika kuboresha sekta yahifadhi ya jamii na kuifanya kuwa endelevu na yenye mchango katikamaendeleo ya wanachama wa mifuko na nchi kwa ujumla;(ii) Kusajili mifuko, mameneja uwekezaji (Fund Managers) na watunza mali(Custodians) kwa ajili ya kutenganisha majukumu kwenye uendeshaji wa Mifukoili kuleta ufanisi zaidi; na(iii) Kutoa elimu kwa umma kuhusu sekta ya hifadhi ya jamii.
Mikakati ya Kukabiliana na Changamoto​
100.​
Mheshimiwa Spika, kutokana na changamoto nilizozieleza awali, serikaliimeandaa mikakati ya kukabiliana nazo katika mwaka 2013/14 kama ifuatavyo:kuhusu suala la tija katika kilimo, Serikali itaboresha mfumo wa kilimo, mifugona uvuvi uwe wa kibiashara badala ya ule wa kujikimu; kuimarisha miundombinuya umwagiliaji; kuongeza upatikanaji na utumiaji wa pembejeo za kilimo;kuimarisha huduma za ugani; upatikanaji wa mikopo kwa wakulima, kusimamiaupatikanaji wa masoko; na kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta yakilimo.101. Mheshimiwa Spika, kuhusu matumizi ya fedha za umma, Serikaliitaendelea kuwajengea uwezo watumishi wa kada za uhasibu, ununuzi, uhakikimali na ukaguzi wa ndani. Aidha, Serikali itaimarisha, usimamizi wa mali zaSerikali na kufanya uhakiki wa mali za Serikali katika Wizara, Mikoa naHalmashauri ili kuboresha daftari la mali za Serikali na kubaini mali zisizokuwana tija kwa ajili ya kuzifuta.102. Mheshimiwa Spika, katika hatua za kudhibiti matumizi, Serikaliitapunguza matumizi kwenye maeneo mbayo hayataathiri utoaji wa huduma zamsingi. Aidha, Serikali itapitia kanuni za ununuzi ili kuhakikisha kuwa hudumana vifaa vinavyonunuliwa vinaendana na thamani ya fedha. Serikali itaendeleakuhamasisha matumizi ya TEHAMA katika kupunguza gharama za uendeshaji.103. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Sheria ya ununuzi wa umma,kumekuwepo na kanuni za ununuzi tofauti kati ya zinazotumika katika SerikaliKuu na zile zinazotumika katika Serikali za Mitaa. Uzoefu uliopo unaoneshakuwa kanuni hizo zimekuwa na changamoto nyingi za kiutekelezaji. Ili kutatuatatizo hilo, Serikali imepanga kuoanisha kanuni za ununuzi wa ummazinazotumika katika Serikali Kuu na zile zinazotumika katika Serikali za Mitaa.Hatua hii itaboresha usimamizi na udhibiti wa ununuzi wa umma. Ili kuhakikishaununuzi wa umma unatekelezwa kulingana na Sera na Sheria husika, Wizara yaFedha itasimamia shughuli hiyo.104. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha usimamizi wa Deni la Taifa, Serikaliinakamilisha taratibu za kuanzisha Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa ndani yaWizara ya Fedha ambayo itaanza kazi mwaka 2013/14. Aidha, Serikali inapitiaupya Mkakati wa Kusimamia Deni laTaifa wa mwaka 2002 pamoja na kuifanyiamarekebisho Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada ya mwaka 1974iliyorekebishwa mwaka 2004, ili kutambua uanzishwaji wa Idara ya KusimamiaDeni la Taifa kwa mujibu wa Sheria na kuiboresha ili kwenda na wakati.105. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kwamba Bajeti ya Serikaliinatekelezwa kama ilivyokusudiwa, Serikali itawajengea uwezo watumiaji waMfumo wa Malipo (IFMS) kuhusu maeneo yaliyoboreshwa katika toleo la Epicor9.02; kuhakikisha mihadi na malipo yote yanafanyika kwa kutumia mfumo waIFMS; na kufanya ukaguzi wa ununuzi kwenye Wizara, Idara zinazojitegemea,Taasisi na wakala wa Serikali, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha,Serikali itaweka utaratibu wa kuibua miradi, kuifanyia upembuzi yakinifu nakuichambua kabla haijatengewa fedha katika bajeti ya mwaka husika ilikuhakikisha kuwa miradi inatekelezwa kwa wakati na Serikali inapata thamanihalisi ya fedha.106. Mheshimiwa Spika, kuhusu kutumia fursa za kijiografia katika ukuzaji wauchumi, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya usafirishaji hususanbarabara, reli, bandari, na viwanja vya ndege; kuongeza upatikanaji wa nishatiya umeme; kuboresha huduma za utalii; kupunguza gharama za kufanyabiashara nchini ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje; na kuimarisha ulinzi nausalama katika ngazi zote.107. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Serikali itaendelea kudhibitimfumuko wa bei kwa kuhamasisha uzalishaji na usambazaji sawia wa mahitajimuhimu kama vile chakula, mafuta ya nishati, sukari, vifaa vya ujenzi nahuduma za usafiri. Aidha, Serikali itasimamia na kuratibu upandaji wa bei kwakutumia sera za uongezaji wa bidhaa na huduma katika soko ili kukidhi mahitajina kupunguza ushindani unaochochea upandaji wa bei. Vilevile, Serikaliitaimarisha thamani ya shilingi kwa kutumia sera za fedha.108. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko yatabianchi, Serikali itaimarisha kamati za kisekta za kuratibu mifumo ya kuhimilina kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi. Aidha, Serikali itaendeleakutekeleza Mkakati wa Taifa wa Mabadiliko ya Tabianchi; kuhimiza wananchikutumia nishati mbadala; kuhamasisha wananchi kupanda mazaoyanayostahimili ukame; kutumia chakula kilichopo kwa tija na uangalifu ilikukidhi mahitaji ya msingi; kuchukua tahadhari ya upatikanaji wa umeme wauhakika; na kuelimisha wananchi wachukue tahadhari za mabadiliko yatabianchi pamoja na kuepuka uhaba wa chakula.
V. KUBORESHA MFUMO WA KODI, ADA, TOZO NA HATUA NYINGINE ZAMAPATO:​
109. ..........................................................................................................................................................................​
VI. SURA YA BAJETI KWA MWAKA 2013/14​
110.​
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia sera za uchumi jumla pamoja namisingi na shabaha ya bajeti, sura ya bajeti itakuwa kama ifuatavyo; Serikaliimepanga kukusanya jumla ya shilingi bilioni 18,249 kutoka kwenye vyanzo vyandani na nje. Mapato ya kodi na mapato yasiyo ya kodi yanatarajiwa kufikiashilingi bilioni 11,154.1 sawa na asilimia 20.2 ya Pato la Taifa. Aidha, mapatokutokana na vyanzo vya Halmashauri yanatarajiwa kufikia shilingi bilioni 383.5sawa na asilimia 0.7 ya Pato la Taifa.111. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14 Washirika wa Maendeleowanatarajiwa kuendelea kutupatia misaada na mikopo ya jumla ya shilingi bilioni3,855.2. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 1,163.1 ni misaada na mikopo yakibajeti na shilingi bilioni 2,692.1 ni mikopo na misaada kwa ajili ya miradi yamaendeleo, na Mifuko ya Pamoja ya Kisekta shilingi bilioni 500.4.112. Mheshimiwa Spika, ili kuziba nakisi ya bajeti, Serikali inatarajia kukopakutoka katika vyanzo vya ndani na nje shilingi bilioni 2,856.3. Kati ya fedha hizo,shilingi bilioni 1,147.6 ni kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za Serikalizinazoiva na shilingi bilioni 552.3 ambayo ni asilimia moja ya Pato la Taifa; nashilingi bilioni 1,156.4 ni mikopo yenye masharti ya kibiashara.113. Mheshimiwa Spika, kuhusu matumizi, jumla ya shilingi bilioni 18,249zimekadiriwa kutumika katika mwaka 2013/14, kwa ajili ya matumizi ya kawaidana ya maendeleo. Kati ya hizo matumizi ya kawaida ni shilingi bilioni 12,574.9ambayo yanajumuisha shilingi bilioni 4,763 kwa ajili ya mishahara ya watumishiwa Serikali, Taasisi na Wakala za Serikali; Mfuko Mkuu wa Serikali shilingi bilioni3,319.2, na Matumizi Mengineyo shilingi bilioni 4,492.6.114. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2013/14 jumla ya shilingi bilioni 5,674zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo, ambapo kiasi cha shilingibilioni 2,982 kitagharamiwa kwa fedha za ndani. Kati ya kiasi hicho, shilingibilioni 552.3 zinatokana na mkopo kutoka vyanzo vya ndani, shilingi bilioni1,156.4 ni mikopo ya masharti ya kibiashara, shilingi bilioni 386.2 ni mikopo yakibajeti, na shilingi bilioni 887.1 zitatokana na asilimia 8 ya mapato ya kawaida.Kiasi cha shilingi bilioni 2,692.6 kitagharamiwa kwa fedha za nje, misaada namikopo ya miradi ya maendeleo ikijumuisha Mifuko ya Pamoja ya Kisekta.
Mapato Shilingi MilioniA. Mapato ya Ndani 11,154,071​
(I) Mapato ya Kodi (TRA)​
10,412,937
(ii) Mapato yasiyo ya Kodi​
741,134B. Mapato ya Halmashauri 383452C. Mikopo na Misaada ya Kibajeti 1,163,131D.Mikopo na Misaada ya Miradi yaMaendeleo ikijumuisha MCA (T) 2692069E. Mikopo ya Ndani 1699860F.Mikopo yenye Masharti yaKibiashara 1156400JUMLA YA MAPATO YOTE 18248983MatumiziG. Matumizi ya Kawaida 12574949
(I) Deni la Taifa 3,319,156(ii) Mishahara 4,763,196(iii) Matumizi Mengineyo 4,492,566Wizara 3,738,316Mikoa 49,701Halmashauri 04,549​
H. Matumizi ya Maendeleo 5,674,034​
(I) Fedha za Ndan 2981965(ii) Fedha za Nje 2692069​
JUMLA YA MATUMIZI YOTE 18,248,983VII. HITIMISHO​
115.​
Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza hapo awali, bajeti ya mwaka2013/14 imelenga kutekeleza Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa miakamitano; Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010; Awamu ya Pili ya Mkakatiwa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA II); Malengo yaMaendeleo ya Milenia 2015; na kuanza kutekeleza maeneo ya vipaumbeleyaliyoainishwa katika Labs. Madhumuni ya mipango na mikakati hii ni kufikiamalengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.116. Mheshimiwa Spika, suala ambalo ningependa kulisisitiza ni sote kwapamoja kuongeza ushirikiano katika kusimamia majukumu na matumizi ya fedhana rasilimali zetu vizuri ili kuongeza ufanisi. Masuala yote tuliyoyajadili katikabunge hili ni ya msingi sana, hivyo kama yakifanyiwa kazi kwa ufanisi tutafikiamatarajio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambayo yanalenga kuitoaTanzania katika kundi la nchi maskini na kuingia katika kundi la nchi zenyeviwango vya kati vya mapato na hali bora ya maisha.117. Mhesimiwa Spika, bajeti hii imelenga pia kuongeza makusanyo yamapato, hasa ya ndani kwa kuanzisha vyanzo vipya na kuboresha vilivyopo.Lengo likiwa ni kujitosheleza kwa mapato yatakayowezesha kutekelezwa kwamiradi mbalimbali ya maendeleo na kuboresha huduma kwa wananchi. Katikakikao hiki cha Bunge la bajeti, waheshimiwa wabunge walipendekeza kuongezafedha kwa baadhi ya mafungu ili kuyawezesha kutekeleza majukumu yaokikamilifu. Napenda kilihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa Serikali sikivu yaChama cha Mapinduzi imezingatia kwa kiasi kikubwa mapendekezo hayo. Ilikutekeleza mapendekezo hayo, imelazimu kufanya maboresho zaidi katika kodina tozo mbalimbali kwani isingewezekana kugharamia mapendekezo hayo bilakuathiri upande wa kodi. Hivyo, waheshimiwa wabunge naomba mnielewekatika hili na kuniunga mkono ili mafungu yaweze kutekeleza majukumu yaokikamilifu na kufikia malengo tuliojiwekea.118. Mhesimiwa Spika, Serikali kwa upande wake inaendelea kuboreshamiundombinu ya kiuchumi, kifedha na kijamii ili kuongeza fursa za ushiriki wawananchi katika uzalishaji na kuboresha hali zao za maisha. Bajeti, inalenga piakuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika, kuendeleza ardhi nakuunganisha nchi yetu kwa njia ya miuondombinu ya barabara, reli na viwanjavya ndege na mawasiliano. Hii itasaidia pia kutumia vyema fursa za kijiografiazinazotokana na kupakana na nchi zisizokuwa na bahari. Aidha, bajeti hiiinalenga kufungua fursa za kuchumi na kijamii kwa ajili ya maendeleo endelevukupitia mfumo mpya wa utekelezaji wa miradi ya kipaumbele ambapo italetamatokeo makubwa kwa haraka.(picha ndege)119. Mheshimiwa Spika, bajeti ya Serikali kwa mwaka 2013/14 imezingatiamapendekezo ya Kamati ya Bajeti na Kamati za Kisekta za Bunge kadiri hali yafedha ilivyoruhusu. Ushauri uliotolewa na Kamati hizo na hoja mbalimbalizilizotolewa na waheshimiwa wabunge zilifanyiwa kazi kadiri ilivyowezekana.Aidha, kwa utaratibu huu mpya wa mzunguko wa bajeti ambao ulipitisha bajetiza mafungu mbalimbali, maelelezo yangu haya ni kuhitimisha mjadala wa bajetiya Serikali kwa mwaka 2013/14.120. Mheshimiwa Spika, yote niliyoyasema yanawezekana iwapo kila mmojawetu na wananchi kwa ujumla tutatimiza wajibu wetu, kila mmoja kwa nafasiyake, kwa kushiriki na kuwajibika kikamilifu katika kutekeleza sera na mipangotuliyojiwekea.
121. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
 
Back
Top Bottom