Wizi wa mchana kweupe kutoka manispaa ya ilala


K

kiwososa

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
1,108
Likes
109
Points
160
K

kiwososa

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
1,108 109 160
Ni takribani mwaka mmoja sasa na zaidi tangu Serikali kupitia manispaa ya ILALA ilivyotangaza kuuza viwanja maeneo ya Kinyerezi jijini Dar es salaam na kukusanya mabilioni ya shilingi kutoka kwa watanzania masikini kama malipo ya fomu za maombi ya kuuziwa ardhi. Kulingana na tangazo la hawa mabwana, ilitakiwa ndani ya siku 14 majibu ya waliopata viwanja yawe yametoka na kutakiwa kulipia viwanja hivyo mara moja Cha kushangaza leo ni zaidi ya mwaka na nusu hakuta matokeo ya maombi yaliyowekwa hadharani wala maelezo yoyote toka uongozi wa manispaa ya ilala kwamba kulitokea kitu gani kwenye sakata lile!!!! Na watanzania tulivyo wasahaulifu wala hakuna anayekumbuka wizi huu uliofanywa na serikali tena mchana kweupe!!!!! Sasa nauliza ule ulikuwa mradi wa serikali kuibia wananchi ama kilikuwa ni kitu gani??!!! Meya wa ILALA JERRY SILAA tuambie kuna nini kinaendelea hapa!!!! wananchi tuamke kudai heki zetu na tukemee kwa nguvu zote udhalimu huu na unyangànyi wa waziwazi unaofanywa na viongozi wa serikali!!
 

Forum statistics

Threads 1,274,136
Members 490,601
Posts 30,502,217