Mangula: Lowassa bora uondoke kuliko kuivuruga CCM

Mangula: Lowassa bora uondoke kuliko kuivuruga CCM

ACHEBE

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2008
Posts
348
Reaction score
76
Mangula makamu mwenyekti wa CCM Taifa amepigilia msumari mkali kwenye ndoto ya Edward Lowassa kwa kumwambia bora aondoke kwani hata simamishwa na CCM kama mgombea wake wa Urais kwani matendo anayofanya yanampoyezea sifa ya kuwa mgombea wa CCM labda chama kingine!

Kayasema hayo leo mchana Lumumba CCM Sub HQs!

-------------------------

Waungwana, kupitia taarifa ya habari ya channel ten makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(ccm) ametoa tamko kali kwa kusema chama hakitasita kumchukulia kiongozi yeyote hatua kama atagundulika anatoa rushwa ,anatoa michango mbalimbali kama harambe kweny maeneo mbalimbali bila idhini ya chama watachukuliwa hatua na pia ameonya makundi yote yanayokigawa chama waataitwa na kuhojiwa. Swali je hawa watoa michango hawajulikani mpaka wafanye uchunguzi, haya makundi hawayajui. Tujadili

------------------------------

CCM WAAMUA KUMTELEA UVIVU LOWASSA MBIO ZA URAIS 2015

Unaweza kusema sasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kumfungia kazi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa baada ya jana Makamu Mwenyekiti wake (Bara), Phillip Mangula kusema kuwa wanachama wake walioanza mbio za kuwania urais mwaka 2015 watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Mangula alisema kama wanachama hao wasipochukuliwa hatua watakifanya chama hicho kupoteza mvuto katika medani ya kisiasa nchini;

"Wapo watu wanataka waichanechane CCM kwa sababu ya uroho wao wa madaraka, uroho wa udiwani, ubunge na hata urais. Kuna makundi ndani ya chama kazi yake ni kuwabomoa wenzao, kamwe hatuwezi kuyafumbia macho."

Akifafanua hilo Mangula alisema: "Tutawaita wote walioonyesha nia ya kuutaka urais 2015 na kuwahoji kwanini wanafanya hivyo wakati muda bado haujafika. Tumeshawachunguza katika mikutano wanayoifanya, tumebaini kuwa wanatoa misaada na kusafirisha watu, tunajua dhamira yao ni nini."

Mangula ametoa kauli hiyo ikiwa imepita siku moja tangu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye kusema mwanachama yeyote wa CCM anayetangaza nia ya kuwania urais kabla ya muda mwafaka kutangazwa atapoteza sifa za kugombea.

Nape alitoa kauli hiyo baada ya Lowassa siku mbili zilizopita, kutangaza nia ‘kimtindo' akisema anaanza rasmi safari aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake, ambayo pia itatimiza ndoto za Watanzania za kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika.

Lowassa ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, alitoa kauli hiyo katika ibada ya shukrani ya kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Monduli.

Mangula aliwashukia vigogo wa chama hicho wanaoutaka urais jana katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Kamati ya Siasa tawi la Ofisi ndogo za chama hicho Lumumba, wakati akitoa salamu za mwaka mpya kwa wanachama wote wa CCM nchini.

Ataja kanuni za uongozi

Katika mkutano huo Mangula alisaidiwa kusoma kanuni za uongozi na maadili ya chama hicho, kutolea ufafanuzi mambo mbalimbali na Katibu Tume ya Udhibiti wa Nidhamu ya Viongozi wa CCM na wanachama taifa, Masoud Mbengula.

Moja ya kanuni hizo inasema "Ni mwiko kwa kiongozi wa CCM kutumia dini yake au kabila au rangi au jinsia au eneo analotoka, kama sifa ya kushawishi wapiga kura wamchague ama yeye mwenyewe ama mgombea anayemuunga mkono."

Mangula alisema kwa mujibu wa kanuni za chama hicho, mwanachama anayefanya mambo kinyume na kanuni huitwa msaliti na hafai kuendelea kufumbiwa macho kwani anaweza kukiangamiza chama wakati wowote.
 
Masikini dili limebuna lowessa kawadai wachungaji nama shekhe pesa zako.
 
Hongera Mangula kama kweli yametoka kinywani mwako, lakini nauliza mbona CCM mnamhamasisha ZZK adai haki yake CDM? Vivyo hivyo hata Lowasa nae anadai haki yake ya kugombe 2015. Patamu hapo haya ni mawazo yangu binafsi sina mrengo wa mtu au chama.
Haki haiji bila wajibu!
 
Wanasiasa,wanasiasa wanasiasa wana-make headlines,si mangula,si lowassa,walopigia kelel kupanda kwa bei ya umeme,wala si Nape,,,
so sad,wachumia tumbo
 
Nilijua tu kuwa papara za Lowasa zinazotokana na uchu wa madaraka uliopitiliza zitamponza.
 
Mangula makamu mwenyekti wa CCM Taifa amepigilia msumari mkali kwenye ndoto ya Edward Lowassa kwa kumwambia bora aondoke kwani hata simamishwa na CCM kama mgombea wake wa Urais kwani matendo anayofanya yanampoyezea sifa ya kuwa mgombea wa CCM labda chama kingine!

Kayasema hayo leo mchana Lumumba CCM Sub HQs!

Ngoma ya segere ndani ya chama kubwa immeansa
 
Nadhani huu ni wakati wa CHADEMA nao kumtumia Lowassa ili kuisambaratisha CCM!!!
 
Hongera Mangula kama kweli yametoka kinywani mwako, lakini nauliza mbona CCM mnamhamasisha ZZK adai haki yake CDM? Vivyo hivyo hata Lowasa nae anadai haki yake ya kugombe 2015. Patamu hapo haya ni mawazo yangu binafsi sina mrengo wa mtu au chama.
Haki haiji bila wajibu!

umesomeka mdau,labda #teamzitto na #teamlowassa zitajibu
 
Lowasa ni fisad mkubwa No 1, tanzania hakuna asiyemjua lowasa, kwan ni mnafiki anaingia makanisan eti na misikitini kumwaga misaada wakat jimbo lake maji shida tu!! Wamasai wanaenda kutafuta maji na punda zao
 
Teh teh teh!We babu mangula kwa nyinyi maccm tayari mnamgombea urais?
 
Mangula makamu mwenyekti wa CCM Taifa amepigilia msumari mkali kwenye ndoto ya Edward Lowassa kwa kumwambia bora aondoke kwani hata simamishwa na CCM kama mgombea wake wa Urais kwani matendo anayofanya yanampoyezea sifa ya kuwa mgombea wa CCM labda chama kingine!

Kayasema hayo leo mchana Lumumba CCM Sub HQs!

kama mbaya na iwe mbaya tu.
 
Waungwana, kupitia taarifa ya habari ya channel ten makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(ccm) ametoa tamko kali kwa kusema chama hakitasita kumchukulia kiongozi yeyote hatua kama atagundulika anatoa rushwa ,anatoa michango mbalimbali kama harambe kweny maeneo mbalimbali bila idhini ya chama watachukuliwa hatua na pia ameonya makundi yote yanayokigawa chama waataitwa na kuhojiwa. Swali je hawa watoa michango hawajulikani mpaka wafanye uchunguzi, haya makundi hawayajui. Tujadili
 
Vipi ile miiezi sita aliyotoa kwa walioingia hakmashauri kuu kinyemela??? Hana lolote huyu
 
Back
Top Bottom