Mangula akutana na moto wa UKAWA

Mangula akutana na moto wa UKAWA

kibogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
9,739
Reaction score
4,746

Mangula-June19-2014.jpg


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Philip Mangula

Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wamempuuza Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula, ya kutafuta mwafaka ili warejee katika Bunge Maalum la Katiba.

Juni 10, mwaka huu, Mangula alizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kama Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha cha Demokrasia Tanzania (TCD) na kueleza kuwa kituo hicho kitaandaa mkutano wa faragha kwa viongozi wa vyama vya siasa na kuwaalika watu mashuhuri ili kutafakari hali na mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba na kutafuta suluhu kabla halijaingia awamu ya pili ya majadiliano Agosti 5, mwaka huu.
Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kauli ya Mangula hawaitambui kwa kuwa ilitakiwa kutolewa na Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo, kusisitiza msimamo wa Ukawa kuwa hawatakuwa tayari kurejea bungeni ikiwa rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Jaji Warioba itajadiliwa kama ilivyo bila kubadilishwa.
Profesa Lipumba ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF, alisema kauli iliyotolewa na Mangula Ukawa hawaitambui kwa kuwa ameingilia majukumu ambayo hayamhusu na kuongeza kuwa kitakachowashawishi kurudi bungeni ni kujadiliwa maoni yaliyotolewa na wananchi kwa Tume ya Jaji Warioba ambayo yanapendekeza muundo wa serikali tatu.
"Tunashangaa kuona mtu anaingilia jukumu la mwenyekiti, TCD ina kanuni na sheria zinazoiongoza, tutarudi kuendelea na mjadala mpaka wabunge wa CCM watakapoheshimu maoni ya wananchi yaliyopendekezwa kwa Tume ya Warioba," alisema Profesa Lipumba.
"Wana-Ukawa ni waelewa sana, hawataki kudharau wananchi kwa kile walichokipendeza katika mikoa mbalimbali, tukikubali kurejea tutakuwa tunakiuka haki ya msingi ya kuheshimu maoni ambayo kwa kiasi kikubwa yanalenga kuleta mabadiliko makubwa," aliongeza Profesa Lipumba.
Aliongeza kuwa kinachotakiwa rasimu iliyowasilishwa na Warioba ijadiliwe bungeni na baada ya wabunge kuchangia na baadaye ipelekwe kwa wananchi waamue ni muundo gani wa Muungano wanaoutaka.
Bunge hilo lilikumbwa na mgawanyiko Aprili 16, mwaka huu baada ya wajumbe wa Ukawa inayoundwa na vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi kususia kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wake ambao waliulalamikia wakisema kuna ubaguzi na uchakachuaji wa Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba.
Bunge hilo lililoanza Aprili 18, mwaka huu hadi Aprili 25 lilipoahirishwa, lilijadili sura mbili tu ya Kwanza na ya sita ambazo zinazungumzia jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na muundo wa Muungano.
Ukawa wanataka jina liwe shirikisho na serikali tatu wakati CCM wanataka jina la Jamhuri ya Muungano na serikali mbili.
Hata hivyo, Cheyo alipoulizwa, alisema katiba ya TCD inaruhusu makamu mwenyekiti kuzunguzia jambo lilote pale mwenyekiti anapokuwa na majukumu na kueleza kuwa siku hiyo yeye (Cheyo) alikuwa katika vikao kamati ya Bunge.
LISSU AWAPA ANGALIZO WASULUHISHI
Wakati huo huo; Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amesema viongozi wa dini na wanasiasa wanaosuluhisha Ukawa kurudi bungeni watambue sababu zilizowatoa bungeni ndipo wajumbe wake watarudi bungeni na kujadili maoni ya wananchi.

Lissu alisema kitakachowakomboa wananchi ni kuunga mkono rasimu ya Jaji Warioba ambayo ndio maoni ya wananchi kuhusu Katiba mpya.
Hata hivyo, amesema CCM hawataki huku na kwamba kutokana na kutokubali kwao, vyama upinzani vimeamua kushirikiana ili kuwaeleza wananchi kuhusu mwenendo wa Bunge hilo.
Lissu aliyasema hayo wakati akiwahutubia wakazi wa Jimbo la Iringa katika soko la Kihesa.
"Sisi vyama vya upinzani tuliamua kuondoka bungeni kwa sababu kungeendelea kukaa kule bungeni na kuendelea kujadili Katiba mpya mwisho wa siku CCM wangepitisha na kusema kuwa haya yote tuliyajadili na vyama vyote vya upinzani vikiwemo, lakini sisi kama Ukawa tuliondoka na kama wanataka turudi bungeni na kuendelea kujadili kuhusu katiba hiyo wakubali maoni ya Jaji Warioba na siyo ya CCM.
Alisema baada ya vyama vya upinzani kuunda Ukawa, kumezuka maneno mengi ya propaganda kutoka chama tawala yanayojaribu kuwakatisha tamaa wananchi, akifafanua kuwa propaganda hizo ni hofu ya CCM kuogopa muungano wa wapinzani.
"Siku zote mtu mkweli huwa anapigwa mawe kwanini, kila kinachosemwa na UKAWA wanapinga na tunayojadili ni ya msingi na yenye tija kwa taifa, lakini jambo la CCM hata kama sio la msingi linapitishwa, sisi Ukawa hatutakubali kabisa," alisema Lissu.
 
Wanahaki ya ukataa kurudi kwenye meza ya mazungumzo na c.c.m,maana kauli mfu za mangula hazikulenga kuleta mwafaka hata kidogo.
 
Ushauri kwa hawa viongozi wa c.c.m.
-kauli zao zimekuwa ni mbaya na chafu kwa umma hivyo wakili na kutuomba radhi watanzania wote tulioipigani na kuitolea maoni yetu rasimu zote mbili za katiba.
 
LISSU anaamini ndoa yao na CCMB ni salama kweli au naye anajifariji?
 
Ushauri kwa hawa viongozi wa c.c.m.
-kauli zao zimekuwa ni mbaya na chafu kwa umma hivyo wakili na kutuomba radhi watanzania wote tulioipigani na kuitolea maoni yetu rasimu zote mbili za katiba.

watu tuna mitazamo tofauti sana, UKAWA ndiyo wa kuwaomba watanzania msamaha , kwa nini walitoka bungeni baada ya kuona wamezidiwa hoja na kusahau kuwa wametumwa na wananchi na siyo maslahi yao binafsi?
 
Na wasirudi tu kwani hata wakirudi wanaendekeza matusi tu. wanawafunzisha tabia mbaya vijana wetu
 
CCM ni majority so why they cannot opt to continue na kuandika katiba mpya na kuwaacha UKAWA out kwa kuwa wanajiona wanaweza bila UKAWA ?

Si wamalizie kazi na waende kwenye maoni shida wapi hadi kusumbuka na na UKAWA ?
 
watu tuna mitazamo tofauti sana, UKAWA ndiyo wa kuwaomba watanzania msamaha , kwa nini walitoka bungeni baada ya kuona wamezidiwa hoja na kusahau kuwa wametumwa na wananchi na siyo maslahi yao binafsi?
Ni kweli Mkuu. Wanachokifanya UKAWA kwa sasa ni kujizika wenyewe
 
CCM ni majority so why they cannot opt to continue na kuandika katiba mpya na kuwaacha UKAWA out kwa kuwa wanajiona wanaweza bila UKAWA ?

Si wamalizie kazi na waende kwenye maoni shida wapi hadi kusumbuka na na UKAWA ?
CCM ni mzazi wa vyama vyote. Hata nyumbani kwako ukiona mtoto hataki chakula lazima ufanye jitihada kumbembeleza. Huwezi kusema mwache afe na njaa
 
CCM ni majority so why they cannot opt to continue na kuandika katiba mpya na kuwaacha UKAWA out kwa kuwa wanajiona wanaweza bila UKAWA ?

Si wamalizie kazi na waende kwenye maoni shida wapi hadi kusumbuka na na UKAWA ?

wanawaonea huruma tu , unafikri wakikataa Katiba haitaandikwa, subutu!
 
Wanahaki ya ukataa kurudi kwenye meza ya mazungumzo na c.c.m,maana kauli mfu za mangula hazikulenga kuleta mwafaka hata kidogo.

kusema wanarudi meza ya mazungumzo ni kauli mfu? bongo za w tz zimelala kweli. Na angesema hawabembelezi, hiyo kauli ingeitwaje?
 
Nina maoni tata kidogo.
-hii c.c.m naamini imefika mwisho kuwahudumia watanzania maana sioni wakuikubali na kuisifia zaidi ya shetani,maana maovu yao ni zaidi ya mauaji kwa watanzania.
 
Ninatabiri:
-anguko la c.c.m linakuja na litaletwa na wao wenyewe kutokana na uchu wa kutafuna mali za umma na ubinafsi wao.
R.i.p c.c.m!
 
watu tuna mitazamo tofauti sana, UKAWA ndiyo wa kuwaomba watanzania msamaha , kwa nini walitoka bungeni baada ya kuona wamezidiwa hoja na kusahau kuwa wametumwa na wananchi na siyo maslahi yao binafsi?
Hoja ya Nape nayo ni hoja?wabunge wa ccm na akili zao wamekubali kufuata akili ya mtoto wa mwenge wakaacha maoni ya watanzania.Eti serikali 2 zilizoboreshwa halafu husemi umeboreshaje
 
Back
Top Bottom