Mangula akutana na moto wa UKAWA

Mangula akutana na moto wa UKAWA

image.jpg image.jpg Tatizo alikuwa kavaa hivi .......
 
Mimi naona CCM waipitishe tu katiba kama wanavyoona inafaa ili ijulikane kabisa kuwa ni katiba ya chama tawala. Hii itarahisisha hoja ya kuifanyia mabadiliko makubwa huko mbeleni ili iwe katiba halsi ya wananchi.
 
watu tuna mitazamo tofauti sana, UKAWA ndiyo wa kuwaomba watanzania msamaha , kwa nini walitoka bungeni baada ya kuona wamezidiwa hoja na kusahau kuwa wametumwa na wananchi na siyo maslahi yao binafsi?
hoja ya kumtukana warioba kwakweli sisiem ilishinda!
 
watu tuna mitazamo tofauti sana, UKAWA ndiyo wa kuwaomba watanzania msamaha , kwa nini walitoka bungeni baada ya kuona wamezidiwa hoja na kusahau kuwa wametumwa na wananchi na siyo maslahi yao binafsi?
Hoja ipi hiyo waliyozidiwa na ccm? Hiyo yakupiga chini maoni ya wananchi? Kimsingi sishangai kwa mtazamo wako maana watanzania tuna tabia yakumsifia hata jambazi, ni gonjwa la taifa hilo kuna wachache wamepona lakini wengi bado na wewe ni mmoja wao.
 
Na wasirudi tu kwani hata wakirudi wanaendekeza matusi tu. wanawafunzisha tabia mbaya vijana wetu
Hakuna dhambi mbaya kama unafiki, ni ukweli ulio wazi kwamba ccm ni mabingwa wa matusi bungeni, hata mmoja wao aliwahi kutukuna tusi zito na spika akajifanya hasikii, kinacho wasumbua wote wenye mahaba na mapenzi ya dhati kwa ccm na serikali yake ni upofu, waswahili walisema kwenye mapenzi hata chongo huitwa kengeza, huoni kasoro. Hayo mnayoyaita matusi ni pale mnapo ambiwa vitu kwa lugha kali na pasipo kupepesa macho (laivu kavu) na kwakuwa mmezoea lugha ya kubembelezana basi mnachanganyikiwa.
 
Back
Top Bottom