Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,092
- 866
Mange Kimambi anaonekana kuwa na tabia ya kutaka kila siku yeye ndiye awe kwenye trend. Wengine wanapopata attention kubwa, badala ya kufurahia mafanikio yao, mara nyingi huonekana kuanza kuwashambulia.
Nakumbuka Wema Sepetu alipata mtoto, Mange alimpinga hadi kufikia kutaka mtoto huyo apewe jina la “Kifo”. Baadaye, Zuchu na Diamond Platnumz walipopata mtoto, "MwanaKukua", naye aliwakosoa Watanzania waliokuwa wakimpa mtoto huyo support.
Sasa Dudu Baya anaendesha kampeni ya kuhamasisha Watanzania kulinda migongo yao, lakini Mange bado anaipinga. Niffer naye amejitolea kumsapoti Mtanzania mwenzake, Jihan, anayeshiriki Miss Grand, lakini kwa sababu Niffer amekuwa akitrend, naye amekuwa akishambuliwa.
Sasa kosa la Niffer ni nini? Kumsaidia Mtanzania mwenzake?
Mange anapaswa kuelewa kwamba si kila siku lazima yeye awe kwenye trend. Leo ni wakati wa Dudu Baya, kesho Niffer, na siku nyingine ni mtu mwingine.
Wakati wako ukipita, ukubali wengine nao wang’ae. Mwanga wa mwingine haupunguzi mwanga wako.