Mange Kimambi ameshindikana kudhibitiwa kabisa?

Kwa upande mwingine yupo sahihi maana anatoa fundisho la kuacha kujirekodi/kupiga picha za utupu, ameona fursa ametumia fursa maana mazimbukuku ya teknolojia yako mengi kila siku yanapiga picha na kujirekodi video za utupu, wapenzi mnapopendana akili itangulie alafu hisia ndo zifate, ubaya wengi mnatanguliza hisia matokeo yake ndo mnapigishana mapicha na kuchukuana mavideo ya utupu yakishavuja akili ndo inakuja.
You are very stupid guy hii ishu ni mbaya sana sababu unaweza ukawa Lodge na mpenzi wako mkajikuta kwenye Mange App watu wataanza kurekodi mambo ya lodge na kumpa Mange coz analipia hizo connection you shall see katika miezi ijayo idadi ya connections zinaweza zikawa nyingi sana

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Wale watoto nawahurumia sana ila inaonekana siku hizi hawapelekeshi atakavyo watakua wameshapata elimu ya kujikomboa,ndo maana amebaki kulalamika kuhusu yule mkubwa kujiamulia style za nywele atakavyo. Bhoke ndo alimkimbia hataki hata kurudi kumsalimia

Zari alimkomesha kwenye kutukana watoto wa wenzie. Faiza alimkomesha kwenye kuita wenzie single mothers without child support. Kumbe kipindi anamsakama faiza nae alikua anapitia yale yale ya usingle mother akijua hakuna mbongo atakaye fahamu wakaibuka wabaya wake wakamuumbua akajitokeza hadharani kuachika😂😂😂😂. Natamani warudi tena kutuonyesha mengine ili akome daah rachel temu ndani ya fekero alitisha sana.
Dooh! nimejikuta naionea huruma familia yake yote, ulikua ni usiku wa kutisha sana kwao,

Kwa hii acha awe na hasira na kila Mtu nawaza hata wale Watoto wake sijui kama wanapona kufokewa fokewa tena speaking of Watoto tangu aanze mambo ya App siku hizi hawapost kabisa Watoto wake,

Na Zari ndio hua anamnyoosha
 
Nauliza huyu Mwanamama anayeitwa Mange Kimambi ameshindwa kabisa kudhibitiwa kwa Tabia zake za Kutukana, Kudhalilisha, Kuumiza na hata Kuharibu Maisha ya Watu??

Tangu aanze haya Mambo ya Kutukana Watu ni Zamani sana kuanzia kwenye Blog yake, akaenda Instagram akaitukana sana Serikali iliyokuwepo Madarakani na sasa kahamia kwenye App akiendeleza yale yale,

Huko kwenye App nasikia ameweka Kipengele maalum kabisa cha kuweka Videos za Kudhalilisha Watu, Serikali ya awamu ya Sita imefungia sites zote za Porn ajabu kwenye App ya Mange kuna Videos za aina hizo.

Watu Wamelia, Wameharibu Heshima, Wameharibu Kazi, Wamekosa Kutokujiamini tena mbele ya Jamii, Wamepata Misongo ya Mawazo, Wengine hadi Jela wameenda,

Je Serikali imemshindwa? Au inaona ni sawa anayoyafanya? Hakuna Wanasheria wa kuliweka hili suala lake kisheria??

Binafsi nasikitishwa sana nionapo Mtu anadhalilishwa kwa faragha zake, inafika muda hata Mke na Mume ndani tutaanza kutokuaminiana, Mtu aweza akavujisha videos kwa Mange ili apatiwe Pesa,

Mange ni sikio la Kufa hata akisemwa vipi ni kama ameshakubali liwalo na liwe as long as Pesa inaingia ndio maana nauliza hakuna jinsi ya kumshtaki kisheria hiyo tabia yake ikomeshwe?
Kwa nini mnajirekodi picha na video za utupu? Tulieni muilambe dawa simbilisi nyie
 
Yule manzi serikali haina kosa tena maana ishafungia APP yake mpaka uwe na VPN.... ila ndo hivyo wadau wa kupenda udaku na zile ponoo wanalipaa mahelaaa tuuu...!! yule manzi ikipita mwaka na ile app kama hajafikisha mil 200 cash aisee kuna mkono wa mtuu...
200m?... Hyo hela ameitengeneza ndan ya week mkuu.. yule ni nuksi...
 
Back
Top Bottom