Maneno ya mwisho ya Steve Jobs, bilionea ambaye alikufa akiwa na umri wa miaka 56 kuhusu maisha

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,863
20,715
Maneno ya mwisho ya Steve Jobs, bilionea ambaye alikufa akiwa na umri wa miaka 56 kuhusu maisha.

“Nimefikia kilele cha mafanikio katika ulimwengu wa biashara. Katika macho ya wajinga, maisha yangu ni mafanikio. Hata hivyo, kando na kazi yangu, nilikuwa na furaha kidogo sana. Mwishowe, utajiri ni ukweli tu ambao nimeuzoea.

Katika wakati huu, nikiwa nimelala katika kitanda changu cha hospitali, na kukumbuka maisha yangu yote, ninatambua kwamba umaarufu wote, na utajiri ambao nilijivunia sana, umebadilika na kuwa duni mbele ya kifo kilichoko mbele yangu.

Unaweza kuajiri mtu aendeshe gari lako au kupata pesa kwa ajili yako, lakini huwezi kuajiri mtu wa kubeba ugonjwa na kufa kwa ajili yako.Vitu vilivyopotea vinaweza kupatikana. Lakini kuna jambo moja ambalo haliwezi kupatikana wakati limepotea, "maisha".

Tukiwa katika hatua yoyote ya maisha, baada ya muda tutakabiliana na siku ambayo pazia litafungwa mbele yetu. Penda familia yako, mwenzi wako na marafiki. Watendee mema,watunze.

Kadiri tunavyozeeka na kuwa na hekima zaidi, tunatambua polepole kwamba kuvaa saa ya $300 au $30 zote mbili hutoa wakati mmoja.Tuwe na pochi ya $300 au au ya $30, kiasi cha pesa kilichoko ndani ni sawa.Tunaendesha gari la $150,000 au gari la $30,000, njia na umbali ni sawa, na tunafika mahali pale pale. Iwe nyumba tunayoishi ni futi za mraba 300 au 3000, upweke ni uleule. Kwa jinsi hiyo utatambua kwamba furaha yako ya kweli ya ndani haitokani na vitu vya kimwili vya ulimwengu huu,bali na Mungu.

Iwe unasafiri kwenye ndege daraja la kwanza au daraja la uchumi, ndege ikishuka, unashuka nayo. Kwa hiyo natumai unagundua kuwa unapokuwa sawa na Mungu, una marafiki, kaka na dada, ambao unazungumza nao, unacheka nao, unaimba nao, unazungumza juu ya kaskazini kusini na mashariki au mbingu na dunia, hiyo ndio furaha ya kweli!

Na huu ndio ukweli usiopingika wa maisha: Usiwasomeshe watoto wako kuwa matajiri, wafundishe kumjua Mungu,Yeye atawapa utajiri. Kwa njia hiyo watakuwa na furaha ya kweli. Kwa njia hiyo pia watakapokuwa wakubwa watajua thamani ya vitu na sio bei.

Maisha ni nini? Ili kuelewa maisha vizuri, kuna maeneo matatu:

~HOSPITALI
~ GEREZANI
~ KABURINI

Hospitalini utaelewa kuwa hakuna kitu bora kuliko AFYA.
Ukiwa gerezani, utaona kwamba UHURU ni kitu cha thamani sana.
Kwenye kaburi, utagundua kuwa MAISHA sio chochote.
Ardhi tunaokanyaga leo ndio paa letu la kesho.

Habari mbaya: tulikuja HATUNA kitu na tutaondoka bila KITU. Kwa hiyo tuwe wanyenyekevu na kumshukuru Mungu kwa kila jambo.
========================
NB
Tafadhali peleka ujumbe huu kwa watu wengine, ili wapate taarifa hii muhimu.

96% ya watu hawatapeleka ujumbe huu kwa wengine, lakini kama wewe ni mmoja wa 4% waliosalia, peleka ukweli huu kwa wengine. Mungu akubariki sana.
 
Painful kwa wenye dhambi
Lakini hata wewe sio mkamilifu mkuu.Kumbuka unapomnyooshea mwenzio kidole,vidole vingine vinne vinakuelekea wewe.Acha ufarisayo mkuu.

Biblia inasema katikà 1 Yohana 1:8
8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
9 Bali tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
 
Yupo sawa kuhusu MUNGU kwanza.

Pia, Utajiri ni muhimu, muhimu sana. Asikudanganye mtu. Tuutafute utajiri, na tumuombe sana MUNGU atupe utajiri.

Raha iliyoje bibi yako akiugua mkamsafirisha na ndege binafsi ya familia kwenda hospitali huku ndugu na marafiki mkiwa mpo nae.
 
Nimejifunza kwamba:
Usiwasomeshe watoto wako kuwa matajiri. Wafundishe kumjua Mungu, kwa njia hiyo watakuwa na furaha ya kweli. Kwa njia hiyo, watakapokuwa wakubwa watajua thamani ya vitu na sio bei.
Kuna kujifunza na kulifanyia kazi (ku practice) Wengi wetu huwa tunaishia kujifunza kwenye nadharia tu basi (kwamba tunaishia kuelewa maana). Kujifunza kwa 100% pia kunahitaji ku practice na ku analyse outcomes.
 
Back
Top Bottom