Maneno ya huyu mzee yalinishangaza kidogo

Maneno ya huyu mzee yalinishangaza kidogo

Gepard

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2021
Posts
291
Reaction score
385
Tulikuwa tupo mahali tunapiga one two. Npo na rafiki yangu, mzee wake na wazee wengine watatu. Baba yake rafiki yangu (mzee) anapesa pesa pesa. Story nyingi tulipiga ila kuna jambo lilinishangaza. Alimwambia kijana "ntafurahi siku ukija na mwanamke na mtoto nyumbani na nikithibitisha ni wakwetu ntakujengea na ndoa tutafanya kubwa nitasimamia mana naamini wewe ni rijali".

Nkamuliza mzee kwanini unamwambia kijana ivo🤔 akasema hata baba yako nadhani atafurahi ukifanya hivyo, wakati hata baba yangu hamjui. Huyo mzee professionally ni daktari wa binadamu. Najiuliza ni ulabu ulimkolea au nini. Kwanini hataki kijana wake aoe kwa harusi halafu ndio apate mtoto ambayo hata kidini ndio vizuri.

Mwenye mawazo mapana karibu.
 
Hapo hakuna tatizo kijana. Kwani mzee amemwambia mwanae afanye yake mapema yeye atamwezesha katika hizo harakati.

Huoni mzee ana nia yakumtoa kijana wake kwenye uhuni na kumuingiza kwenye taasisi ya ndoa? Kuhusu mtoto kuzaliwa kabla ya ndoa au baada ya ndoa hiyo haibadilishi chochote, akizaliwa kazaliwa tu.
 
Waafrika ukioa maana yake mwanamke wanamtegemea azae!! Sasa iwapo baada ya NDOA mwanamke hazai hapo ndio ndoa nyingi huvunjika. Sasa naona kwa uzoefu wake huyu Mzee anaona kuepuka ndoa kuvunjika kwa sababu ya kukosa watoto angalau basi kijana wake apate mtoto kabla ya kufunga ndoa!
 
Mzee ana mashaka na kijana wake pamoja na wewe. Hawaamini kama mko fiti ndo sababu ya kukujumuisha na wewe.
 
Pengine labda anaona mambo ya kusubiri subiri after marriage ni kupoteza muda

Pengine labda ulabu ulimkolea akaropoka

Pengine anaona ufahari kwa kijana kumzalisha mwanamke kabla ya ndoa kudhihirisha urijali
daah kweli umewaza mengi zaidi, ahsnte, wewe mkuu unaona n vema lakini?
 
Anataka kuhakikisha kwanza kama yaliyomo yamo... anaogopa mwanae asije akaoa mwanamke ambaye hatampatia mtoto. Nimejaribu kuelewa mawazo yake sio kwamba nakubaliana nae
Umeyaelewa vzuri mkuu, ila kwanini boss sikuizi watu wasio na uwezo wa kuzaa na kuzalisha wanaongezeka kwa kasi boss? Na kwanini hukubaliana na hivyo?
 
Hapo hakuna tatizo kijana. Kwani mzee amemwambia mwanae afanye yake mapema yeye atamwezesha katika hizo harakati.

Huoni mzee ana nia yakumtoa kijana wake kwenye uhuni na kumuingiza kwenye taasisi ya ndoa? Kuhusu mtoto kuzaliwa kabla ya ndoa au baada ya ndoa hiyo haibadilishi chochote, akizaliwa kazaliwa tu.
Mkuu hiyo dp yako inaonesha unafuatilia sana greek mythology.
 
Umeyaelewa vzuri mkuu, ila kwanini boss sikuizi watu wasio na uwezo wa kuzaa na kuzalisha wanaongezeka kwa kasi boss? Na kwanini hukubaliana na hivyo?
Sijui tatizo ni nini. Sikubaliani naye kwa sababu mtoto akizaliwa ndani ya ndoa kuna asilimia kubwa kuwa atalelewa na wazazi wote wawili maana tayari wapo ndoani ila akizaliwa nje ya ndoa probability ya hao wa zazi kuingia ndoani ni 50/50, hivyo kuna hatari ya mtoto kulelewa na mzazi mmoja
 
Huyo mzee huwezi mpigia simu umuulize hilo swali akupe jibu pana?
 
Umeyaelewa vzuri mkuu, ila kwanini boss sikuizi watu wasio na uwezo wa kuzaa na kuzalisha wanaongezeka kwa kasi boss? Na kwanini hukubaliana na hivyo?
hizi takwimu umetoa wapi ? au umeoteshwa ?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom