Maneno ya faraja kwako .. soma tafadhali

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Yawezekana umepita katika hali ngumu ya maisha, kiasi kwamba umetamani usingekuwepo au upotee urudi mambo yakiwa safi, wakati mwingine umejuta na kusema laiti kama nisingezaliwa labda kwa vile huna wazazi au umeumizwa na mpendwa wako au umewapoteza watu uliokuwa ukiwategemea na mara zote unadhani hakuna anayekupenda wala kukujali. Utakapowaza haya hakika hutakuwa na furaha, na ndio maana unajribu kutafuta furaha sehemu nyingi lakini bado mawazo yanarudi palepale. Napenda kukuhakikishia mpendwa unayesoma hapa, yawezekana ukapata furaha na amani kwa maana hauko peke yako. Yesu anakupenda na anakuwazia mema kumbuka kumkaribisha moyoni mwako ili awe rafiki yako. Yeye ni rafiki wakweli wengine wanakucheka wanafurahi jinsi unavyoshindwa lakini Yesu atakupitisha katika majaribu yote kwa maana majaribu tunapitia ili tuweze kufika pale Mungu anapotaka majaribu ni mtaji au ni mtihani ili kushinda inabidi kupitia hayo. Mungu anakupenda anajua kila unachohitaji chukua hatua sasa jifunze kuomba mwenyewe, ukimwambia Mungu siri wa moyo wako hakika utaona faraja na utapata FURAHA ya kweli.
 
Huu upako huu kweli umekutembelea Tutor B
Endelea na huo upako mkuu na kushusha maneno ya faraja kwa wale waliopondeka mioyo na kukata tamaa ya maisha wajue kuwa kuna mtetezi wao
 
Last edited by a moderator:
Huu upako huu kweli umekutembelea Tutor B
Endelea na huo upako mkuu na kushusha maneno ya faraja kwa wale waliopondeka mioyo na kukata tamaa ya maisha wajue kuwa kuna mtetezi wao

Nafurahia kuendesha mahubiri ndani ya Jamii forum; kuna wengi jana hawakwenda makanisani lakini ofisini wamekutana na neno la Mungu kupitia Tutor B.
 
Umesema kweli tupu.Kila jaribu linamlango wa kutokea na kila gumu ni dalili ya jambo jema na kubwa ambalo Mungu anataka kukupatia hivyo anakupitisha mahali ili kuona kama utaweza kubeba changamoto zake na endapo upo tayari kupokea.
Ukimuita Mungu naye hujibu kwa wakati wala hawahi wala kuchelewa.hakika ukimjua Mungu hutoona shida yeyote na magumu yatakuwa majaribu ya kawaida sana utakayoyaona mlango wake wa kutokea.

Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikia sauti yangu na Dua zangu,kwa maana amenitegea sikio lake,kwahiyo nitamwita siku zangu zote ZAB 116:1-2
Yawezekana umepita katika hali ngumu ya maisha, kiasi kwamba umetamani usingekuwepo au upotee urudi mambo yakiwa safi, wakati mwingine umejuta na kusema laiti kama nisingezaliwa labda kwa vile huna wazazi au umeumizwa na mpendwa wako au umewapoteza watu uliokuwa ukiwategemea na mara zote unadhani hakuna anayekupenda wala kukujali. Utakapowaza haya hakika hutakuwa na furaha, na ndio maana unajribu kutafuta furaha sehemu nyingi lakini bado mawazo yanarudi palepale. Napenda kukuhakikishia mpendwa unayesoma hapa, yawezekana ukapata furaha na amani kwa maana hauko peke yako. Yesu anakupenda na anakuwazia mema kumbuka kumkaribisha moyoni mwako ili awe rafiki yako. Yeye ni rafiki wakweli wengine wanakucheka wanafurahi jinsi unavyoshindwa lakini Yesu atakupitisha katika majaribu yote kwa maana majaribu tunapitia ili tuweze kufika pale Mungu anapotaka majaribu ni mtaji au ni mtihani ili kushinda inabidi kupitia hayo. Mungu anakupenda anajua kila unachohitaji chukua hatua sasa jifunze kuomba mwenyewe, ukimwambia Mungu siri wa moyo wako hakika utaona faraja na utapata FURAHA ya kweli.
 
Dah,
mkuu neno jema kwangu, Mungu hataruhusu jaribu kumzidi uwezo mja wake, zuri zaidi, atamfanyia mlango wa kutokea jaribuni.
 
Umesema kweli tupu.Kila jaribu linamlango wa kutokea na kila gumu ni dalili ya jambo jema na kubwa ambalo Mungu anataka kukupatia hivyo anakupitisha mahali ili kuona kama utaweza kubeba changamoto zake na endapo upo tayari kupokea.
Ukimuita Mungu naye hujibu kwa wakati wala hawahi wala kuchelewa.hakika ukimjua Mungu hutoona shida yeyote na magumu yatakuwa majaribu ya kawaida sana utakayoyaona mlango wake wa kutokea.

Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikia sauti yangu na Dua zangu,kwa maana amenitegea sikio lake,kwahiyo nitamwita siku zangu zote ZAB 116:1-2

Ahsante kwa nyongeza ya neno kukazia uzi huu.
 
Kuna watu wametafsiri maisha: KWAMBA MAISHA NI MTIRIRIKO WA MATATIZO WENYE CHECHEMBA NDOGONDOGO ZA RAHA.
Definition hii tunaionaje wale ambao tunaitambua neema ya Bwana Yesu?

Wengi wanafurahia kwenda mbinguni peke yake, wanasahau kuw kuna vita ya kupigana kuipata Kanani yako hapa hapa duniani.
Kwamba tuna hakika ya kushinda vita yeyote inayokuja mbele yetu kwa kuwa mshindi na mpiganaji mkuu, Yesu kristo ameshatushindia vta vyote!
 
kuna watu wametafsiri maisha: Kwamba maisha ni mtiririko wa matatizo wenye chechemba ndogondogo za raha.
Definition hii tunaionaje wale ambao tunaitambua neema ya bwana yesu?

Wengi wanafurahia kwenda mbinguni peke yake, wanasahau kuw kuna vita ya kupigana kuipata kanani yako hapa hapa duniani.
Kwamba tuna hakika ya kushinda vita yeyote inayokuja mbele yetu kwa kuwa mshindi na mpiganaji mkuu, yesu kristo ameshatushindia vta vyote!
ubarikiwe mpendwa katika bwana.
 
Back
Top Bottom