Maneno ya Afande Sele kwa Paul Makonda kuhusu Madawa ya kulevya

Mr Suprize

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
858
937
Kaandika kupitia ukurasa wake wa facebook

"Katika hili sakata la MAPAPA na MAPUNDA ya Unga kama kweli braza Paul yupo serious na sio 'Matango Pori'kama tulivyoona ktk masakata mengine,huenda hata wale WASAFI wakaonekana wachafu...kila la kheri Mr Paul....RiP Da Amina...wacha parry ianzeee....."
 
Hivi ganja nayo si madawa ya kulevya? Afande Sele ww sio muathirika wa haya madawa.
 
wasafi kwamaana ya wcb au wale waliokuwa hawana skendo hizo za madawa sasa watakuwa nazo? kama sijamuelewa
 
Afande ameongea mnaona anaongea bange,tasnia ya bongo flava hapa bongo kwa asilimia kubwa ni ngada oriented,kama mnabisha makonda awe serious tu na hili na muda uwepo pia tutashuhudia mengi
 
Binafsi nilivyomwelewa Afande Sele ni kwamba Muda si Mrefu hata wale ambao tunazani ni Watu Safi kana kwamba wanapata pesa zao halali kwa kazi zao, Basi nao wanaweza kuingia ktk upande wa pili, ambao ni wachafu akimaanisha wanahusika na biashara.
Lakini Ijulikane Wazi kwamba kwa kiasi kikubwa ukitaja jina lolote Mind Zetu huanza na lile linalofahamika kwanza,
Kwa mfano aliposema Vanessa Mind zetu zinamwangalia zaidi Vanessa Mdee lakini ukweli ni kwamba mpaka atajwe complete name,
Vivyo hivyo afande aliposema WASAFI wengi kwenye Mind ni WCB but anaweza kuwaruka vilevile,
Ukweli ni Kwamba Wanamziki wengi na watu Mashuhuri duniani hujikuta ktk business hii hasa baada ya Maisha kuanza kuwapiga, Mfano halisi ni whitney houston na mtoto wake (R.I.P)

But hatuna haja ya kunyosheana vidole, Serikali inajua who is who ktk hii business maana ni sakata ambalo lipo na ni la Muda Mrefu,

Halafu kama Mtu anatumia hiyo kitu Mwisho wake huwa ni aibu.
So ni vyema sio tu tusijaribu bali hata hata kuwaza kujaribu maana mwisho wake si salama
 
HARAKA YA NINI NGOJENI TUONE MWISHO WA HILI SAKATA DAR. MIKOA MINGINE NAYO INA MAMBO YAKE SI LAZIMA UNGA .
 
Cocaine inaurahibu wa ajabu sana. Unapoanza kutumia it feels like you can conquer the world. Inakupa drive kutenda kwa kujiamini zaidi. Kifupi ni kwamba cocaine inauwezo kukurudisha katika original thoughts. Na hapa ndipo creativity ilipo. Ndiyo maana watu wa sanaa wanatumia ili kuonge ubunifu wao. Lakini tukumbuke cocaine ni sumu.....baada ya muda inadhuru mwili. Halafu akili itaanza kukosa umakini kwasababu mwili umejaa sumu. Ukiongezea na watu wanavyowasema vibaya watumiaji basi wanapata sana matatizo yakushuka moyo (depression). Ili kukabiliana na ukali na maneno ya kudhihakiwa inabidi watumie kiwango kikubwa zaidi. Hapa wengi wanakufa kwa overdose.

Binafsi nadhani vita ya madawa ya kulevya haitafanikiwa kwasababu tumeweka juhudi zetu katika mlengo hasi kila kitu utasikia kampeni kupinga matumizi, kampeni kukamata watumiaji, kampeni kuongeza vituo vya waathirika. Hii yote inatengeneza ukinzani na hatimaye watumiaji wanazidi kuongezeka. Ngumu kung'amua hili inatakiwa kuangalia kwa makini......where the mind focus the energy flows.

Kutatua hili, tujitahidi kuwekeza kwenye mambo yanayomsaidia kijana kujifahamu zaidi na kudhamini utu wake zaidi. Cocaine au Heroin inakunyanganya afya ya nafsi yako na afya ya mwili wako.
 
Back
Top Bottom