Maneno mazito ya Mtatiro kwa Prof. Lipumba

Maneno mazito ya Mtatiro kwa Prof. Lipumba

Hadi sasa nina kizunguzungu maana sijui huyu professor anawaza nini?lakini muda haungopi!ushauri wangu CUF muwe makini sana katika maamuzi yenu.
Uamuzi sahihi ni kumkataa huyu mtu, kwani alipo kuwa cuf alisha wahi kupata wabunge tanzania bara kama sasa ambao wamepatikana wakati yupo nje ya chama?
 
Lipumba usikubali kuachia uenyekiti, wakumbushe mateso uliyopata kwa kupigwa mabomu, kuvunjwa mikono, hadi kusachiwa pochi, saa yako ya thamani, na miaka yote ya umri wa mtu mzima ulioupoteza kwa ajili ya CUF halafu hawa watoto waje kukuletea ubabe! Usikubali.
 
Uamuzi sahihi ni kumkataa huyu mtu, kwani alipo kuwa cuf alisha wahi kupata wabunge tanzania bara kama sasa ambao wamepatikana wakati yupo nje ya chama?
Umesema kweli kabisa waliomtuma kutoka ndo waliomtuma kurudi sasa CUF wawe makini sana.
 
sophist, nimekusoma Mkuu. wakati una Maneno na yanasikika ingawa ubongo wa wengi wenye masikio hutambua jioni, ambao huwa mwanzo wa tungo shurutia.
 
Na hao ndio wenye bendi wengine wooote wacheza shoo, wakiamua sasa wanapiga sebene Mtatiro and etal ni kunengua tu. Hiko chama bila Seif na Lipumba lazima kiyumbe.

Mawazo ya kizamani hayo mkuu. Mawazo kama yako ndo yametufikisha hapa tulipo katika hali halisi. Hata Makazini wazee wamefikia muda wa kustaafu kutokana na mindset zao eti wanaomba waongezewe muda eti kwa sababu bila wao taasisi itakufa. Huo ni mtazamo hafifu usio na mantiki yoyote. Siamini kama taasisi inajengwa na mtu mmoja. Naomba ufahamu kuwa hao wa chini unaowadharau ndio wachapakazi katika taasisi yoyote. Ni sawa kama utakavyo dharau walioko kwenye production line kwenye kiwanda. utendaji wa hawa watu ndio unaojenga jina la kiwanda. Lipumba na Maalimu Seifu kuwa viongozi siyo kumaanisha kuwa bila wao CUF itakufa. Taasisi haijengwi na Meneja, Mwenyekiti au Mkurugenzi. Taasisi inajengwa na watu wote walio ndani ya hiyo taasisi wenye malengo na madhumuni yanayofanana.
 
Nashindwa kumshangaa huyu Profesa Lipumba najiuliza hivi kweli ni msomi aliyebobea? binafsi yangu sidhani ana nia njema na chama cha CUF je! kuna kitu alisahau ktk chama?.Kwa mawazo yangu kawadhalilisha sana wanachama wa hiki chama kwamba hakuna anayeweza kukiongoza hicho chama zaidi yake.hivi vijana mko wapi si mgombee hiyo nafasi au kuna agenda ya siri tusiyoijua kuhusu hiki chama?.
 
Aliyesababisha yote haya ni mfalme Mbowe.
Alikiuka makubaliano ya UKAWA na kuanza kusimamisha mgombea kila sehemu cuf iliposimamisha mgombea.

Hadi Mbatia aligeuka mpiga debe Wa chadema badala ya Nccr.

Je mlitaka na Lipumba awe mpiga debe Wa chadema badala ya cuf??

Ndio maana Prof alijihuzuru.
 
Lipumba usikubali kuachia uenyekiti, wakumbushe mateso uliyopata kwa kupigwa mabomu, kuvunjwa mikono, hadi kusachiwa pochi, saa yako ya thamani, na miaka yote ya umri wa mtu mzima ulioupoteza kwa ajili ya CUF halafu hawa watoto waje kukuletea ubabe! Usikubali.
Kwani alifukuzwa
 
Huyu msomi wangu wa Tabora nae, uelekeo kakosa nini, achukue kadi ya CCM sababu kwa sasa tunaye nahodha wa kuweza kujivunia.
 
Intelligentsia: Lipumba ni mtu wa system. Wakati anajiondoa uenyekiti mwaka jana, system ilihitaji hivyo. Lengo linafahamika. Prof. Lipumba alijitahidisana kuvuruga UKAWA kuanzia January hadi Julai (2015), na alikuwa amefanikiwa ila kukatokea tukio la kisiasa lisilotegemewa - Lowasa kujiunga CHADEMA. Mipango ya awali yote ikabidi ibadilike.

Kutumika akiwa ndani ikashindikana. Mkakati wa muda mfupi ukabuniwa. Kwamba atoke kuona iwapo ingesaidia kuleta haueni kwa CCM. Sina uhakika iwapo alifanikiwa au la.

Lakini sasa system inamwitaji tena. Anatakiwa kutatua tatizo la Zanziar. Kwa mkakati wa muda mfupi, Jecha aliweza kufanikisha. Mkakati wa muda mrefu umeshindikana kupata fixer. Lipumba anatakiwa, akiwa ndani, siyo nje ya CUF, kuokoa jahazi la Zanzibar. Mapalala, Nyaruba, Awesi Dadi na wengineo (Enzi za Komandoo Amour) waliweza kufanya hivyo wakiwa nje ya CUF lakini hawakufanikiwa sana. Sasa anatakiwa key brain ku-run system ya utawala Zanzibar.

Kwa kuanzia Prof. Lipumba ana assignment ya kuhakikisha analeta vurugu katika uongozi wa CUF. Atatengenezewa wafuasi na washabiki wanaotaka arudi. Unaweza kushangaa ilikuwaje hao washabiki na wafuasi wake famfe walishindwaje kumzuia asiondoke CUF wakati alitakiwa awepo kuhakikisha chama hakiyumbi! Wakati wa Kampeini kuelekea uchaguzi 2015.

Mgogoro wa uongozi unaweza kusogeza mbele, siku kadhaa hata mwaka, kwa utawala wa Zanzibar kuishi kwa muda huo wakati CUF wanaumana wao kwa wao. Ni mkakati ule ule uliotumika enzi za akina Marando na kundi lake vs. Augustino Mrema (NCCR-Mageuzi: 1996-67). Makundi yote (NCCR-Mageuzi) yalishindwa. Mkapa na CCM waliweza kupeta uchaguzi Mkuu mwaka 2000.

Na ikitokea Prof. Lipumba akafanikiwa kuwa Mwenyekiti wa CUF, hatua itakayofuata ni kuendeleza mgogoro baina yake (wafuasi wake) na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad. Kwa hiyo tutakuwa tunaendelea kusikia habari za kamati Kuu ya CUF (Lipumba) imemfukuza uanachama Maalim Seif S. H, au Kamati Kuu ya CUF (Seif S. H) yamvua Madaraka na kunfukuza uanachama Prof. Lipumba.

Hali itaendelea hivyo hadi 2020. Kila mtu atakuwa amechoka, lakini si haba kwa Prof. Lipumba. Lakini pia tutarajie kauli za Mwenyekiti Prof. Lipumba kukubaliana na matokeo ya uchaguzi Zanzibar 2015 hivyo kuunga mkono Serikali ya Dr. Sheini. Msisahau kuwa kila statement huwa inalipiwa, si haba.

Huu si utabiri, ni intelligentsia.
Tusubiri.


Hivyo ulichokisema ndicho kipo kichwani kwangu, na pia anaweza kukigawa Chama cha bara lipumba cha zbz Ni seif kufikia hapo msajili wa vyama vya siasa atakifuta Chama cha cuf kwa kuwa Kuna cuf mbili na kwa maana nyingine suala la uraisi znz litakuwa limekufa automatically
 
Lipumba usikubali kuachia uenyekiti, wakumbushe mateso uliyopata kwa kupigwa mabomu, kuvunjwa mikono, hadi kusachiwa pochi, saa yako ya thamani, na miaka yote ya umri wa mtu mzima ulioupoteza kwa ajili ya CUF halafu hawa watoto waje kukuletea ubabe! Usikubali.

hivi jamaa wa mwendokasi anapewa lini panga la l.u.m.u.m.b.a?? nasikia huko kwenu moja haikai wala mbili haikai....!!!! hivi yale maneno ya gwajima yangekuwa feki i hope olesendeka angetoa press jana ....
 
MACCM yalimtumia kama ndom kisha yakamtosa, sasa njaa imeanza kufanya vitu vyake.

Mkuu BAK rejea comment namba 19 ya mchangiaji mmoja humu, utagundua kwamba sio ametoswa na ccm.. Amepewa assignment mbaya zaidi, ambayo itakuwa na impact mbaya zaidi kwa cuf na upinzani kwa ujumla.. Hii ni calculated move from ccm.. I pray & hope hii hujuma ishindwe.. Maana mwisho wake ni kuzidi kufifisha upinzani.. Utaanza kusikia sasa hivi mgogoro cuf..
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom