Maneno mazito ya Mtatiro kwa Prof. Lipumba

respect wa boda

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
4,556
3,838
NGOJA NIWAELEZE UKWELI!

Kama mzee wetu anao washauri, wamwambie kuwa "DALILI ZA MVUA NI MAWINGU". Na kwamba, NGOMA ivumapo sana hupasuka na tena ajulishwe kuwa VITANI hakuna michezo ya KUJIFICHA na KUONEKANA baadaye, jana niliwaambia kuwa najua CUF inao watu makini wanaojua nini haki ya PROFESA LIPUMBA na nini haki ya CUF kama chama. Kwa wale ambao hawakuelewa ujumbe wangu wa jana nilikuwa namaanisha viongozi wa CUF watakuwa upande wa chama, hawatafuata matakwa ya mtu, na dalili zimeanza kuwa hivyo. Mwisho wa siku mshindi wa mchezo huu ni CHAMA na WANACHAMA wenye UTII na COMMITMENT kwa chama chao, na siyo MTU!

Kuna watu nasikia wanasema WATAGAWANA MBAO, ukweli ni kuwa CUF ni taasisi imara na haiwezi kuwa na MBAO za kugawana. Kutakuwa na machaguo mawili tu, aidha kuondoka na mtu au kubaki na chama, wale watakaobaki na chama watabaki na mbao zote, na wale watakaoondoka na mtu hawatandoka na hata kipande cha ubao - kwa sababu mchezo huu hautahitaji hasira. Siasa ni maisha halisi ya watu, vyama vikiruhusu zigeuke kuwa mchezo wa KOMBOLELA, zitakosa maana na hapa lazima ieleweke, kwamba kuna mambo ambayo vyama vya upinzani vikiyaruhusu yaendelee kutendeka, vitakuwa vinafanya ujinga wa kiwango cha PhD na Uwendawazimu wa Kiwango cha MWENDOKASI!

Profesa Lipumba ambaye kila mtu anamheshimu sana, apishe kwenye uongozi ili chama kijiandalie ZAMA mpya. Nawarejesha kwenye nukuu yangu ya mwaka jana wakati anajiuzulu, kwamba "Kamanda wa vita akiuawa katikati ya vita, siyo muda wa kuanza kulia na kuomboleza, siyo muda wa kulaumiana, anatafutwa askari mwingine na kutwaa bunduki yake, mapambano yanaendelea mbele".

Ninaamini kuwa, CUF inao watu wenye sifa za kuwa wenyeviti wa chama na tena kisiasa wapo watu bora sana. Chama kisiogope kufanya maamuzi sahihi kwa ajili yake na siyo kwa ajili ya mtu. Na iwe fundisho kwa wanasiasa kuwa HISIA za wafuasi wa vyama hazichezewi, na iwe FUNDISHO kwa viongozi wa kisiasa kwamba MISIMAMO na KUTOYUMBA ni wajibu wao usiokwepeka.

Katika mgogoro huu wa kutengenezwa makusudi, wanachama imara wanajua wajibu wao, wasimame upande wa chama, wasimame upande wa taasisi, maana taasisi itakuwepo siku zote. Mtu na watu watapita haraka na kunyauka kama maua.

Namshauri Prof. Lipumba, kwa namna yoyote ile, asikubali kutumikia matakwa ya kundi lolote lile, iwe ndani ya chama au nje ya chama. Asikubali kuwa sehemu ya kuanzisha mgogoro na vurumai kubwa ndani ya chama, asikubali kuwa chanzo cha kuleta sintofahamu kama hii, namtambua Mwenyekiti wangu kama mtu makini na muumini safi wa dini ya kiislamu na huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani, hebu na ajitafakari upya ikiwa NIA yake ni salama kwa ajili ya wanachama wa CUF na nchi yetu.

Binafsi nisingelipenda kuona mgogoro mwingine mkubwa CUF, ambao matokeo yake sote tunayajua, kwamba chama ndicho kitashinda na kitabaki salama salmini, na kwamba watu wachache ndiyo wataumia na kufedheheka, akiwemo mtu anayeheshimiwa sana na aliyewahi kushiriki kukijenga chama hiki kwa nguvu zake na akili zake zote.

Mtatiro J

Copy and paste From Mtatiro Facebook Wall.

My Take

Tanzania bado hatujaishiwa vijana wajasiri na wasema kweli wenye uthubutu wa kumwambia Mfalme uko Uchi. Asante Comrade

BACK TANGANYIKA
 
Nadhani ukisoma katikati ya mistari anamaanisha Lipumba anaungwa mkono na mmoja wa waasisi wa Chama ili arudi na nadhan atakua Maalim
 
mtatiro ndo nani kwenye cuf , hadi pro kuamua kurudi kuna kundi kubwa sana lililoenda kumuomba arudi kundi na hao ndo wenyewe chama
 
Nadhani ukisoma katikati ya mistari anamaanisha Lipumba anaungwa mkono na mmoja wa waasisi wa Chama ili arudi na nadhan atakua Maalim

Na hao ndio wenye bendi wengine wooote wacheza shoo, wakiamua sasa wanapiga sebene Mtatiro and etal ni kunengua tu. Hiko chama bila Seif na Lipumba lazima kiyumbe.
 
Mtu kama Lipumba anadhalilidha taaluma yake kibaya zaidi anawakilisha wasomi wengi nchini waliotayari kuacha taaluma zao kutumika kisiasa kuwa profesa ni mibaraka unatakiwa uwe role ya model kwa kizazi kinachokuja. Profesa Ibrahim anawakilisha wasomi wengi wanadhalilisha taaluma zao kwa ajili ya siasa
 
Dr. Mwakyembe antuasa kuwasikilkiza wasomi wetu na 'kuwapuuza wasiosoma' ambao kimsingi tunatengeneza kama 90% ya Tanzania. Sasa yeye ana PhD na hapa tunamuongelea msomi mwingine na mtu aliyesemekana kuwa miongoni mwa wachumi bora duniani na ngazi yake kisomi ni Profesa ambaye ni zaidi ya Mwakyembe!
Naona ni makosa makubwa andapo tutawaamini 'wasomi' wa namna hii, ni bora mara 100 kujiamini sisi wenyewe ambao 'hatujasoma' kuliko kuwaamini vigeugeu kama hawa maana watatupeleka makaburini kama mabehewa.
 
Kwa kweli CUF inayumba. Hebu fikiria CUF-Znz itadumaa kisiasa kwa muda wa miaka mitano. CUF Makao makuu haina uongozi wa juu. Maamuzi hayafanyiki kwa kufuata kanuni na sheria. Hivi mnafikiriaje hatma ya CUF kwa sasa?

Sawa, mgeni (mkimbizi) ghafla alikuja na baadhi yetu tulimuamini haraka bila tafakuri ya kina lakini kumbe ni hadaa.......

Nusra inatakiwa haraka ipatikane, kwa yeyote anae itakia mema CUF.
Huu si wakati wa porojo tena, wana CUF ni lazima wajipange, vinginevyo jahazi linakwenda mrama. Chonde Chonde.
 
Dr. Mwakyembe antuasa kuwasikilkiza wasomi wetu na 'kuwapuuza wasiosoma' ambao kimsingi tunatengeneza kama 90% ya Tanzania. Sasa yeye ana PhD na hapa tunamuongelea msomi mwingine na mtu aliyesemekana kuwa miongoni mwa wachumi bora duniani na ngazi yake kisomi ni Profesa ambaye ni zaidi ya Mwakyembe!
Mkuu mchumi bora duniani? Hiyo siyo siasa tu mkuu,
Mbona katika orodha ya wachumi bora 20 Duniani hayumo?
Angalia hapa:20 Most Influential Living Economists | Super Scholar
 
Intelligentsia: Lipumba ni mtu wa system. Wakati anajiondoa uenyekiti mwaka jana, system ilihitaji hivyo. Lengo linafahamika. Prof. Lipumba alijitahidisana kuvuruga UKAWA kuanzia January hadi Julai (2015), na alikuwa amefanikiwa ila kukatokea tukio la kisiasa lisilotegemewa - Lowasa kujiunga CHADEMA. Mipango ya awali yote ikabidi ibadilike.

Kutumika akiwa ndani ikashindikana. Mkakati wa muda mfupi ukabuniwa. Kwamba atoke kuona iwapo ingesaidia kuleta haueni kwa CCM. Sina uhakika iwapo alifanikiwa au la.

Lakini sasa system inamwitaji tena. Anatakiwa kutatua tatizo la Zanziar. Kwa mkakati wa muda mfupi, Jecha aliweza kufanikisha. Mkakati wa muda mrefu umeshindikana kupata fixer. Lipumba anatakiwa, akiwa ndani, siyo nje ya CUF, kuokoa jahazi la Zanzibar. Mapalala, Nyaruba, Awesi Dadi na wengineo (Enzi za Komandoo Amour) waliweza kufanya hivyo wakiwa nje ya CUF lakini hawakufanikiwa sana. Sasa anatakiwa key brain ku-run system ya utawala Zanzibar.

Kwa kuanzia Prof. Lipumba ana assignment ya kuhakikisha analeta vurugu katika uongozi wa CUF. Atatengenezewa wafuasi na washabiki wanaotaka arudi. Unaweza kushangaa ilikuwaje hao washabiki na wafuasi wake famfe walishindwaje kumzuia asiondoke CUF wakati alitakiwa awepo kuhakikisha chama hakiyumbi! Wakati wa Kampeini kuelekea uchaguzi 2015.

Mgogoro wa uongozi unaweza kusogeza mbele, siku kadhaa hata mwaka, kwa utawala wa Zanzibar kuishi kwa muda huo wakati CUF wanaumana wao kwa wao. Ni mkakati ule ule uliotumika enzi za akina Marando na kundi lake vs. Augustino Mrema (NCCR-Mageuzi: 1996-67). Makundi yote (NCCR-Mageuzi) yalishindwa. Mkapa na CCM waliweza kupeta uchaguzi Mkuu mwaka 2000.

Na ikitokea Prof. Lipumba akafanikiwa kuwa Mwenyekiti wa CUF, hatua itakayofuata ni kuendeleza mgogoro baina yake (wafuasi wake) na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad. Kwa hiyo tutakuwa tunaendelea kusikia habari za kamati Kuu ya CUF (Lipumba) imemfukuza uanachama Maalim Seif S. H, au Kamati Kuu ya CUF (Seif S. H) yamvua Madaraka na kunfukuza uanachama Prof. Lipumba.

Hali itaendelea hivyo hadi 2020. Kila mtu atakuwa amechoka, lakini si haba kwa Prof. Lipumba. Lakini pia tutarajie kauli za Mwenyekiti Prof. Lipumba kukubaliana na matokeo ya uchaguzi Zanzibar 2015 hivyo kuunga mkono Serikali ya Dr. Sheini. Msisahau kuwa kila statement huwa inalipiwa, si haba.

Huu si utabiri, ni intelligentsia.
Tusubiri.
 
Sasa si unajua sisi wazee wa 'd,d,d,f' aka vi.la.za, hivyo ndivyo tuliambiwa na baadhi ya wasomi na sisi tuwakatalie na kuwapinga kama nani!?
Hawa wasomi ni shiiida sana, hata wanayotufundisha wao hawafanyi!! Na bado tunawaita wasomi kwa sababu ya idadi ya vyeti walivyobeba.Badala ya Ujuzi walionao.
 
Back
Top Bottom