Maneno mazito ya Mtatiro kwa Prof. Lipumba

Maneno mazito ya Mtatiro kwa Prof. Lipumba

Mawazo ya kizamani hayo mkuu. Mawazo kama yako ndo yametufikisha hapa tulipo katika hali halisi. Hata Makazini wazee wamefikia muda wa kustaafu kutokana na mindset zao eti wanaomba waongezewe muda eti kwa sababu bila wao taasisi itakufa. Huo ni mtazamo hafifu usio na mantiki yoyote. Siamini kama taasisi inajengwa na mtu mmoja. Naomba ufahamu kuwa hao wa chini unaowadharau ndio wachapakazi katika taasisi yoyote. Ni sawa kama utakavyo dharau walioko kwenye production line kwenye kiwanda. utendaji wa hawa watu ndio unaojenga jina la kiwanda. Lipumba na Maalimu Seifu kuwa viongozi siyo kumaanisha kuwa bila wao CUF itakufa. Taasisi haijengwi na Meneja, Mwenyekiti au Mkurugenzi. Taasisi inajengwa na watu wote walio ndani ya hiyo taasisi wenye malengo na madhumuni yanayofanana.

Hivyo vyama majina yamegandana na wenye vyama ukiwetenganisha.
 
Hiki kimeo chenu CCM haihusiki na hizi sinema zenu na magear yenu, nyie jihukumuni wenyewe na msala wenu.
Lipumba atawasumbua sana CUF na UKAWA kwa ujumla. Kosa kubwa alilofanya LOWASSA ni kuchagua watu wa kuwahonga akawasahau wenye chama kama Lipumba,
 
ndio hapa utajua mbowe ambaye hajasoma ana akili nyingi kuliko huyu profesor ........... big up mbowe we unajua una akil piga hela siku zoteeee chaga dom
 
Mzee atuachie chama abaki mwanachama wa kawaida hataki akaanzishe chama chake kama anajiamini yeye ndo kila kitu
 
Kwa kweli CUF inayumba. Hebu fikiria CUF-Znz itadumaa kisiasa kwa muda wa miaka mitano. CUF Makao makuu haina uongozi wa juu. Maamuzi hayafanyiki kwa kufuata kanuni na sheria. Hivi mnafikiriaje hatma ya CUF kwa sasa?

Sawa, mgeni (mkimbizi) ghafla alikuja na baadhi yetu tulimuamini haraka bila tafakuri ya kina lakini kumbe ni hadaa.......

Nusra inatakiwa haraka ipatikane, kwa yeyote anae itakia mema CUF.
Huu si wakati wa porojo tena, wana CUF ni lazima wajipange, vinginevyo jahazi linakwenda mrama. Chonde Chonde.

CUF haiwezi kwenda mrama kwa watu wasiojiheshimu kama Lipumba aendelee kulipigania tumbo lake sio kutuvurugia CUF
 
Lipumba ni mtu wa mikakati ya uvurugaji upinzani anayetumiwa na ccm,huwezi ukajitoa kwenye pambano la mwisho na dakika ya mwisho Kwa kisingizio kisicho na mashiko,kisha unawatelekeza wenzio na nakutoa siri Kwa adui halafu baada ya vita kuisha eti unarudi tena kinyumenyume
 
Kafanyaje?
Alijiuzulu uenyekiti wa CUF kwa hiyari yake mwenyewe ikiwa imepita karibu miezi 10 sasa, lakini katika hali ya kushangaza sasa kaandika barua ya kuomba kutengua ile barua yake ya kujiuzulu na kutaka eti arejee kwenye nafasi yake jambo ambalo sijawahi kusikia kihoja kama hiko,ndio maana wengi wetu tunamuona kama mtu aliyechanganyikiwa
 
mtatiro ndo nani kwenye cuf , hadi pro kuamua kurudi kuna kundi kubwa sana lililoenda kumuomba arudi kundi na hao ndo wenyewe chama

Kwa nini hilo kundi(kama lipo) huyo Prf Lipumba hakuwapa /hakukipa nafasi ya kukisikiliza na kuufanyia kazi ushauri wakati ule alipo jiondoa Cuf!?
 
Lipumba MNAFIKI, MSALITI..!! ana akili ya MWENDOKASI..!!

Maalim Seif kashasema atafute uenyekiti chama kingine sio CUF... au abaki kama mwanachama wa kawaida..!!
 
Kwa nini hilo kundi(kama lipo) huyo Prf Lipumba hakuwapa /hakukipa nafasi ya kukisikiliza na kuufanyia kazi ushauri wakati ule alipo jiondoa Cuf!?

Mkuu mark my words kuna siku hata huko cdm fukuto litaanza ,juu ya ujio wa wa edo usione watu wamenyamaza kimya ,na kumtii m/kiti kila asemalo ,ukaona watu wanafurahia ,kuna siku watamwambia tu ukweli
Na usihoji kijingajinga kuwa walikuwa wapi siku zote mpaka sasa ,ndo wanze kuhoji ,kwa sasa wanachama wa chama cha CUF wanaona neno ukawa linatumika na CDM kuhalalisha maamuzi ya kafu iwe wameshirikishwa au laa ,utasikia neno UKAWA UKAWA ,ili hali maamuzi ni ya CDM ,na mbatia akiwa kwa pembeni akiwa kama mshenga
 
NGOJA NIWAELEZE UKWELI!

Kama mzee wetu anao washauri, wamwambie kuwa "DALILI ZA MVUA NI MAWINGU". Na kwamba, NGOMA ivumapo sana hupasuka na tena ajulishwe kuwa VITANI hakuna michezo ya KUJIFICHA na KUONEKANA baadaye, jana niliwaambia kuwa najua CUF inao watu makini wanaojua nini haki ya PROFESA LIPUMBA na nini haki ya CUF kama chama. Kwa wale ambao hawakuelewa ujumbe wangu wa jana nilikuwa namaanisha viongozi wa CUF watakuwa upande wa chama, hawatafuata matakwa ya mtu, na dalili zimeanza kuwa hivyo. Mwisho wa siku mshindi wa mchezo huu ni CHAMA na WANACHAMA wenye UTII na COMMITMENT kwa chama chao, na siyo MTU!

Kuna watu nasikia wanasema WATAGAWANA MBAO, ukweli ni kuwa CUF ni taasisi imara na haiwezi kuwa na MBAO za kugawana. Kutakuwa na machaguo mawili tu, aidha kuondoka na mtu au kubaki na chama, wale watakaobaki na chama watabaki na mbao zote, na wale watakaoondoka na mtu hawatandoka na hata kipande cha ubao - kwa sababu mchezo huu hautahitaji hasira. Siasa ni maisha halisi ya watu, vyama vikiruhusu zigeuke kuwa mchezo wa KOMBOLELA, zitakosa maana na hapa lazima ieleweke, kwamba kuna mambo ambayo vyama vya upinzani vikiyaruhusu yaendelee kutendeka, vitakuwa vinafanya ujinga wa kiwango cha PhD na Uwendawazimu wa Kiwango cha MWENDOKASI!

Profesa Lipumba ambaye kila mtu anamheshimu sana, apishe kwenye uongozi ili chama kijiandalie ZAMA mpya. Nawarejesha kwenye nukuu yangu ya mwaka jana wakati anajiuzulu, kwamba "Kamanda wa vita akiuawa katikati ya vita, siyo muda wa kuanza kulia na kuomboleza, siyo muda wa kulaumiana, anatafutwa askari mwingine na kutwaa bunduki yake, mapambano yanaendelea mbele".

Ninaamini kuwa, CUF inao watu wenye sifa za kuwa wenyeviti wa chama na tena kisiasa wapo watu bora sana. Chama kisiogope kufanya maamuzi sahihi kwa ajili yake na siyo kwa ajili ya mtu. Na iwe fundisho kwa wanasiasa kuwa HISIA za wafuasi wa vyama hazichezewi, na iwe FUNDISHO kwa viongozi wa kisiasa kwamba MISIMAMO na KUTOYUMBA ni wajibu wao usiokwepeka.

Katika mgogoro huu wa kutengenezwa makusudi, wanachama imara wanajua wajibu wao, wasimame upande wa chama, wasimame upande wa taasisi, maana taasisi itakuwepo siku zote. Mtu na watu watapita haraka na kunyauka kama maua.

Namshauri Prof. Lipumba, kwa namna yoyote ile, asikubali kutumikia matakwa ya kundi lolote lile, iwe ndani ya chama au nje ya chama. Asikubali kuwa sehemu ya kuanzisha mgogoro na vurumai kubwa ndani ya chama, asikubali kuwa chanzo cha kuleta sintofahamu kama hii, namtambua Mwenyekiti wangu kama mtu makini na muumini safi wa dini ya kiislamu na huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani, hebu na ajitafakari upya ikiwa NIA yake ni salama kwa ajili ya wanachama wa CUF na nchi yetu.

Binafsi nisingelipenda kuona mgogoro mwingine mkubwa CUF, ambao matokeo yake sote tunayajua, kwamba chama ndicho kitashinda na kitabaki salama salmini, na kwamba watu wachache ndiyo wataumia na kufedheheka, akiwemo mtu anayeheshimiwa sana na aliyewahi kushiriki kukijenga chama hiki kwa nguvu zake na akili zake zote.

Mtatiro J

Copy and paste From Mtatiro Facebook Wall.

My Take

Tanzania bado hatujaishiwa vijana wajasiri na wasema kweli wenye uthubutu wa kumwambia Mfalme uko Uchi. Asante Comrade

BACK TANGANYIKA

Hivi Prof hakuyajua haya. Wakati mwingine usomi hausaidii kuwaza nje ya kisanduku!
 
Jana niliona kwenye TV Mzee Lipumba akijieleza akiwa amezungukwa na kikundi kidogo sana cha mashabiki! Hapo hapo nikawaza kwa nini Mzee huyu aliyekuwa anaheshimika ameamua kujidhalilisha. Wale waliokuwa wamemzunguka na baadaye kumshangilia hawakuonyesha kuwa wanachama wa CUF ambao tulikuwa tukiwaona kwenye mikutano ya chama hicho. Watu hawa walionekana kama kikundi cha watu waliokodishwa kufanya shughuli ya ushabiki! Maskini Mzee Lipumba! Bora akapumzika tu kuliko kujidhalilisha!
 
Prof lipumba angejikita kwenye kutumia elimu yake ya uchumi kufundisha vijana wetu huko vyuo vikuu mambo ya siasa ashaweka doa halitoki kabisa hata likifuliwa kwa dawa ya jiki
 
Hivi huyu Prof, ndumi la kuwili alisahau nini CUF? namshauri aendelee 'kutumia alizopewa' kama zimeisha awarudie wakampe nyingine! Anataka kuja CUF akapige deal jingine msikubali hata chembe!
 
Back
Top Bottom