Maneno haya yanachanganya matumizi yake

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Nimekuwa nikichanganyikiwa hasa katika matumizi ya maneno haya

1. Mahindi mabichi: yanachomwa au yanabanikwa?
2. vitumbua: vinachomwa au vinakaangwa?
 
Nafikiri ili kitu kikaangwe hakina budi kutiwa kwenye mafuta, vitumbua haviwekwi kwenye mafuta ila mafuta huwa yananyunyuziwa tu.

Kuhusu mahindi na mimi pia nina utata.
 
Nafikiri ili kitu kikaangwe hakina budi kutiwa kwenye mafuta, vitumbua haviwekwi kwenye mafuta ila mafuta huwa yananyunyuziwa tu.

Kuhusu mahindi na mimi pia nina utata.

Gurta ..hahahahhah lol
hilo jina lako limenikumbusha nyumbani sana lol
mmhhh haya bwana
sasa na hisi weye ni Garma au Ako...
 
Nimekuwa nikichanganyikiwa hasa katika matumizi ya maneno haya

1. Mahindi mabichi: yanachomwa au yanabanikwa?
2. vitumbua: vinachomwa au vinakaangwa?

mahindi mabichi yanachomwa na vitumbua vinakaangwa
 
Nimekuwa nikichanganyikiwa hasa katika matumizi ya maneno haya

1. Mahindi mabichi: yanachomwa au yanabanikwa?
2. vitumbua: vinachomwa au vinakaangwa?

Namuunga mkono Gurta kwa upande wa vitumbua.
Nataka kujibu kwa upande wa mahindi mahindi hayabanikwi bali yanachomwa,kwa sababu kitu kinachochomwa huwa hakikauki kwa hiyo nasema hivi mahindi hayabanikwi kwa sababu mahindi mabichi huchomwa na sizani kama kuna mtu atakayekula mahindi mabichi ya mkausho kwa mimi sijawahi hata siku hindi la mkausho.Kwa kumalizia nyama hubanikwa nyama ikichomwa haiwezi kuiva vizuri.Neno 'kubanika' linafanana na 'kukausha'

...........ASANTE............
 
Nimekuwa nikichanganyikiwa hasa katika matumizi ya maneno haya

1. Mahindi mabichi: yanachomwa au yanabanikwa?
2. vitumbua: vinachomwa au vinakaangwa?

Namuunga mkono Gulta kwa upande wa vitumbua.
Nataka kujibu kwa upande wa mahindi mahindi hayabanikwi bali yanachomwa,kwa sababu kitu kinachochomwa huwa hakikauki kwa hiyo nasema hivi mahindi hayabanikwi kwa sababu mahindi mabichi huchomwa na sizani kama kuna mtu atakayekula mahindi mabichi ya mkausho kwa mimi sijawahi hata siku hindi la mkausho.Kwa kumalizia nyama hubanikwa nyama ikichomwa haiwezi kuiva vizuri.Neno 'kubanika' linafanana na kukausha

...........ASANTE............
 
Nimekuwa nikichanganyikiwa hasa katika matumizi ya maneno haya

1. Mahindi mabichi: yanachomwa au yanabanikwa?
2. vitumbua: vinachomwa au vinakaangwa?

Mahindi mabichi yanaweza:

A) Kuchomwa
B) Kukaangwa
C) kupikwa
D) Kuchemshwa

Vitumbuwa vinatumbuliwa, havichomwi wala havikaangwi na ndio maana vikaitwa vitumbuwa!
 
Kuchoma kwa kiingereza ni burning kwa hiyo mahindi huwa hayachomwi bali ubanikwa kwa maana ya ku-roast, vitumbua hukaangwa kwa maana ya frying because frying is using cooking oil. Hupo hapo!
 
Kuchoma kwa kiingereza ni burning kwa hiyo mahindi huwa hayachomwi bali ubanikwa kwa maana ya ku-roast, vitumbua hukaangwa kwa maana ya frying because frying is using cooking oil. Hupo hapo!
Tuache kasumba. Kwani kiingereza ndio nini? Si ni lugha sawa na Kiswahili? Na kwa kukuchanganya zaidi, burning tafsiri yake sio kuchoma ni kuunguza. Ukweli niuonavyo mahindi huchomwa. Watu husema mahindi ya kuchoma na sio ya kubanikwa. Unasemaje hapo mzee KONDOO?
 
tuache kasumba. Kwani kiingereza ndio nini? Si ni lugha sawa na kiswahili? Na kwa kukuchanganya zaidi, burning tafsiri yake sio kuchoma ni kuunguza. Ukweli niuonavyo mahindi huchomwa. Watu husema mahindi ya kuchoma na sio ya kubanikwa. Unasemaje hapo mzee kondoo?
uko sahihi
 
Nafikiri ili kitu kikaangwe hakina budi kutiwa kwenye mafuta, vitumbua haviwekwi kwenye mafuta ila mafuta huwa yananyunyuziwa tu.

Kuhusu mahindi na mimi pia nina utata.

Karanga je hufanywaje? Maana nazo hatuweki mafuta
 
karanga,zinakaangwa
kukaanga si lazima utumie mafuta ata chochote tu
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom