Maneno gani uliyokuwa unayatumia zamani?

upupu

JF-Expert Member
Apr 15, 2008
614
198
Wakuu, ni maneno gani Uliyokuwa unayatumia zamani, either utotoni ila siku hizi huyatumii tena, iwe kwa kubadili mazingira au mfumo wa maisha, au mabadiliko ya umri!?
Mi neno moja wapo ni "GIJA" ikimaanisha teke
La pili ni "UMERO” likimaanisha uroho

Ongeza maneno mengine na maana zake,
 
ndindi (yaan nimekula nimeshiba sana kiasi ukigonga tumbo na na kidole unasikia ndindi so kiufupi unasema "nipo ndindi " kama ukikalibiswa kula au ile nipo DIDA
 
Wakuu, ni maneno gani Uliyokuwa unayatumia zamani, either utotoni ila siku hizi huyatumii tena, iwe kwa kubadili mazingira au mfumo wa maisha, au mabadiliko ya umri!?
Mi neno moja wapo ni "GIJA" ikimaanisha teke
La pili ni "UMERO” likimaanisha uroho

Ongeza maneno mengine na maana zake,
lazima utakuwa mtu wa pwani hasa pwani ya "waja leo....." hahaa.

Dingirizi, boflo,
 
Njagu=polisi,NOMA=ubaya,NGUNA=ugali,DINGI=baba,MAZA=mama,MKWANJA=hela,BLUU=noti ya 10000,NIPE TANO=niunge mkono.
 
Mambo mpwito
Mambo Bam bam
Mambo Shega
Wowowo
Ndopa
Bitozi Nyangema
Ametoka Chicha
Kishtobe
Pensi Nyanya
Mkuda
Mamen nigger
Anamwaga ung'eng'e
Mnuso( wali)
Kudisa/kudinda
Manyigu (ukoko wa wali)
Raba mtoni
Kaboka mchizi
Fidodido leo ndio Kiduku
 
1-"Mambo?" Unajibu "Dukinaa" au "Dole tupu"

2-Ukitaka kumtisha mtu unamwambia "Utabana ngenge" au "Utapotea maboya"

3-Kufanya matusi = Ngono

4-Ubeche = Wali
 
Back
Top Bottom