Mandela road kuna nini leo?

Mmwaminifu

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
1,129
302
Heshima zenu wakuu.
Nimekuja mjini kuungana na familia kwa ajili ya sikukuu ijayo.

Toka saa kumi na mbili nimetoka ubungo ila hadi saa hizi bado sijafika hata buguruni.

Ni utaratibu wa kila siku au leo imekuwa mpya?
 
Kwa mandela road kwa mida hii ni kawaida sana hio.

Unaeza kuta foleni linaanzia Tabata Matumbi mpaka Ubungo.

Kama unatokea Ubungo kwenda Buguruni mida kama hii ni bora ukapita magomeni usalama pale uka drop ukachukua gari la kutokea Usalama mpaka Buguruni, hii ruti hainaga foleni sana
 
Watu wa mikoani bana utawajua tu! Pole mkuu vumilia tu utafika nyumbani salama yawezekana mbele kuna ajali manake hiyo barabara ya Mandela huwa yapitisha malori makubwa kwenda huko mikoani ulikotoka.
 
Heshima zenu wakuu.
Nimekuja mjini kuungana na familia kwa ajili ya sikukuu ijayo.

Toka saa kumi na mbili nimetoka ubungo ila hadi saa hizi bado sijafika hata buguruni.

Ni utaratibu wa kila siku au leo imekuwa mpya?
Foleni ya hiyo barabara ni jipu uchungu mkuu, nlitoka riverside saa 7 mchana nkafika buguruni saa 10 mchana. Sahvi angalau yanayoenda ubungo yanatembea
 
Watu wa mikoani bana utawajua tu! Pole mkuu vumilia tu utafika nyumbani salama yawezekana mbele kuna ajali manake hiyo barabara ya Mandela huwa yapitisha malori makubwa kwenda huko mikoani ulikotoka.
Na watu wa mjini utawajua tu. Asante
 
Haaa haaaa haaaaa. Jaribu ungo pia unafaa kwa usafiri naniharaka. Ushauri tu au familia uihamishe Dar itakusaidia kuepukana na foleni. Ahsante.
 
Haaa haaaa haaaaa. Jaribu ungo pia unafaa kwa usafiri naniharaka. Ushauri tu au familia uihamishe Dar itakusaidia kuepukana na foleni. Ahsante.
Dah! Ushauri mzuri sana aisee. Ntaanza na swala la kuhamisha familia kwanza. Hilo la ungo ntakufata unipe ushauri. Kama unajua wapi wanatoa training mkuu. Hahahahaaa
 
Heshima zenu wakuu.
Nimekuja mjini kuungana na familia kwa ajili ya sikukuu ijayo.

Toka saa kumi na mbili nimetoka ubungo ila hadi saa hizi bado sijafika hata buguruni.

Ni utaratibu wa kila siku au leo imekuwa mpya?[/QUO
Kuna mwanamke TAZARA traffic light hamna kitu kabisa. Buguruni sokoni hadi TAZARA tumekaa masaa 3.
 
Sio Kweli Kuwa Malori Ndio Ambayo Yanasababisha Hizo Foleni Mabarabarani!! Mbona Kuna Njia Hayo Malori Hayaruhusiwi Kupita, Lkn Foleni Iko Pale Pale Tu!!! Tatizo La Foleni Ktk Miji Mikuu Na Majiji Ni Matokeo Ya Mipango Miji Na Miundombinu Mibovu Tu!! Hakuna Nchi Ambayo Inapokea Malori Mengi Kama KONGO DRC!! Tena Makubwa Kuliko Haya Yaliopo TANZANIA!! Mbona Hakuna Mafoleni Ya Kijinga!! Haya Rwanda Kwa Kagame, Hakuna Foleni Za Hovyo!! Kama Ni Ambayo Iko Juu Kutengeneza Barabara Zake Nyingi, Hasa Za Michepuko Zilizo Bora Ni Rwanda!! Kila Kona Kuna Barabara Za Michepuko!! Sasa Sio Kuiga Kufagia Tu Mitaa Yetu J, mosi Na Tuige Na Mifumo Huu, Tupunguze Misongamano!! Haiwezekani Mtu Anataka Kwenda Buguruni, Yupo Mburahati, Eti Analazimika Kupita Ilala Au Tabata Au Mbagala Kwenda G/mboto Lazima Uende Hadi Tazara, Chang'ombe Mtoni Ndio Afike Mbagala!!! Hii Ni Mif. Ya Njia Za Michepuko Nyingi Mno Zinazohitajika Nchini!! Otherwise Foleni Hata Zijengwe Flyover Ngapi, Misongamano Itaendelea Tu, Kama Flyover Rwanda Ziko Kitambo Tu, Lkn Kagame Anajenga Barabara Za Michepuko Lukuki!!!
 
Heshima zenu wakuu.
Nimekuja mjini kuungana na familia kwa ajili ya sikukuu ijayo.

Toka saa kumi na mbili nimetoka ubungo ila hadi saa hizi bado sijafika hata buguruni.

Ni utaratibu wa kila siku au leo imekuwa mpya?
Sisi tumezoea ulichotakiwa umuulize mwenyeji wako angekupa ratiba nzuri baada ya kufika UBT ungepitia pale riverside ungepata moja mbili then ukaondoka na foleni usingeiona.
 
Mandela road ni kawaida sana,kibaya zaidi foleni yake ni bora ingekuwa inasogea kidogo kidogo foleni yake unaweza kukaa nusu saa hujasogea hata nchi 1.
 
Watu wa mikoani bana utawajua tu! Pole mkuu vumilia tu utafika nyumbani salama yawezekana mbele kuna ajali manake hiyo barabara ya Mandela huwa yapitisha malori makubwa kwenda huko mikoani ulikotoka.
Unajiona mjanjaa?
 
Sisi tumezoea ulichotakiwa umuulize mwenyeji wako angekupa ratiba nzuri baada ya kufika UBT ungepitia pale riverside ungepata moja mbili then ukaondoka na foleni usingeiona.
Asante sana kwa ushauri mkuu. Itakuwa vizuri sana hiyo aisee!

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom