Mandela hakustahili tuzo ya Mo Ibrahim?

Mandela hakustahili tuzo ya Mo Ibrahim?

sinafungu

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2010
Posts
1,527
Reaction score
868
dunia nzima imezizima kwa msiba wa kiongozi huyu mstaafu. sijui vigezo vinavyotumika kumpata kiongozi bora wa ngazi ya urais aliyestaafu, lkn nawauliza wenye kujua huyu mzee naye ni kama hawa wengine hakuwa na sifa............?
 
Watampa sasa akiwa kaburini ale Graca
 
HAKUSTAHILI KWASABABU KUBWA MOJA"tata madiba was above mo ibrahim prize"
 
jibu maswali haya kisha tuendelee na mjadala.
1 tuzo ya mo-ibrahim imeanzishwa mwaka gani?
2 je waliposema watawatuza marais wastaafu walioongoza vizuri waliweka/wameweka vigezo gani vya muda gani tokea marais wastaafu(time limit mfano marais waliostaafu miaka miwili au mitano ilopita au wote waliostaafu hata kama mtu kastaafu mwaka 1966?)

ukijibu haya, nitapata cha kuchangia
 
dunia nzima imezizima kwa msiba wa kiongozi huyu mstaafu. sijui vigezo vinavyotumika kumpata kiongozi bora wa ngazi ya urais aliyestaafu, lkn nawauliza wenye kujua huyu mzee naye ni kama hawa wengine hakuwa na sifa............?

Vigezo vya mtu kushindania na kuteuliwa mshindi wa tuzo ya Mo Ibrahim ni hivi vifuatavyo;-
  1. Awe kiongozi mstaafu wa nchi ama serikali toka bara la Africa
  2. Awe ameachia ofisi/madaraka kwa muda wa angalau miaka mitatu(3) nyuma
  3. Ni lazima awe kiongozi aliyepata kuchaguliwa kidemokrasia
  4. Awe ametumikia uongozi ndani ya muda wake wa kikatiba
  5. Awe ameonyesha uongozi wa mfano/wa kipekee

Check zaidi hapa Ibrahim Prize | Mo Ibrahim Foundation

Kumbuka tuzo ya Mo Ibrahim ilianzishwa mwaka 2007 na Nelson Mandela aling'atuka madarakani mwaka 1999. Moja kwa moja utaona Mandela hakukidhi kigezo nambari 2 hapo juu.
 
Mkuu i salute you for this very comprehensive information. It has closed the matter! However if it was'nt for the time limit i believe Mandela and Nyerere would invariably get the prize!
 
Back
Top Bottom