Ilikuwa ni April 19 mwaka 2000 katika dimba la Old Trafold...
Real Madrid waliwakilishwa na:
Casillas,
Salgado,
Karanka,
Campo,
Carlos,
McManaman,
Muheshimiwa Redondo,
Helguera,
Savio,
Raul,
Morientes.
Subs:
Illgner, Dorado, Anelka,
Baljic, Geremi, Karembeu, Julio Cesar.
Pale katikati Referee alikuwa ni Perluigi Gigi Collina toka katika viunga vya Tuscan nchini (Italy).
naikumbuka mechi hii Manchester UTD walichutamishwa sebleni kwao na kukubali kulalwa goli 3-2.
Katika mechi hii washabiki wa Man UTD na Wa Madrid woote walilipuka kwa pamoja kushangilia goli la 3 alilolifunga Raul Madrid.
Goli hili lilitiwa ladha na nakshi kwa chenga ya maudhi aliyopigwa beki wa Mnchester UTD Henning Berg na kiungo mbishi, sugu, anayejuwa mpira, na kipenzi cha waargentina hapa namzungumzia Muheshimiwa Fernando Redondo.
Mpaka mwisho wa mchezo Madrid waliwaandamisha Man UTD na kuendeleza utemi na ubabe kwa KILABU hiki cha Uingereza.
Teh teh usimchukie Sisimizi...Sukari haimalizi