Manchester United (Red Devils) | Special Thread

hivi huyo rasford mpaka afike miaka 30 ndo atakuwa mzuri ? kila siku sababu
 
Vitu vingine tukiandika tupunguze mahaba.
 
Vitu vingine tukiandika tupunguze mahaba.
Sio mahaba Huo ndo UKWERIII "in jiwes voice" Rash ni key player ata akifunga goli mbili mashabiki uchwara wote watasahau mapungufu yake na kurudisha matumaini pia SHAW aise SHAW ni key player kabsaaa jamaa nikimuona uwanjani roho inazuuzika kabsaa Sema sasa linanenepa Mnoo yani saivi linaelekea kilo billion mbili na nusu mpaka anaonekana mzito kama Papa Molinga
 
Vitu vingine tukiandika tupunguze mahaba.
UCL msimu uliopita Group stage Tena Bahati nzuri PSG tulikuwa same Group.

-Rashford Goli 6 mechi 6 tena Hakuanza mechi nyingi aliingia sub, dakika alizocheza ni 416 tu ina maana kila dakika 69 Rashford alikuwa akifunga Goli.

-Mbape goli 8 Mechi 10 dakika 900 alicheza hivyo alifunga goli kila dakika 112. Walikutana Kama mechi 4 under ole na Unajua nini Kilitokea.

-Haaland Mechi 8 Goli 10, ndani ya dakika 706 Goli kila baada ya dakika 70.

Msimu wa Juzi na msimu wa Jana Rashford anafunga Goli 20+ kwenye msimu na Kutoa Assist 10+ zaidi Goal comtribution 30. Misimu yote miwili Aliwazidi wachezaji kibao ikiwemo kina Mane.
 
hivi huyo rasford mpaka afike miaka 30 ndo atakuwa mzuri ? kila siku sababu
Tatizo Lenu mnakuwa na Reactionary views, sababu Jamaa Form imeshuka baada kurudi kutoka majeruhi Basi mna Assume Hana Kitu. 2019/2020, 2020/2021 si Foden wala si Mane waliokuwa Level ya Rashford,
 
Mkuu Rashford msimu huu ameanza na Majeruhi Hakucheza mwanzo wa Msimu na Alivyorudi Kacheza Mechi chache under Ragnick most of time out of position. Je ni kigezo kweli hichi cha Kumjudge Mchezaji?

Ukimtoa Ronaldo nani Man U pale anajua Ku fight? Mechi inaisha dakika za majeruhi kuforce Goli? Juzi tu Hapa na Leicester kaingia alikuwa anatuinua Dakika za Mwisho kama Sio Elanga kumkwatua, Msimu huu huu aliofanya Vibaya Katuinua Vs westham na Burnley kama kumbukumbu zipo sahihi
Ana Goli 4 so far za Dakika ya Mwisho akitupa point 3 muhimu.

Na Sio Hilo Value Kubwa ya Rashford kwangu ni Big Matches,




Timu 6 ambazo Rashford anazionea sana ni Leicester, Chelsea, Liverpool, Man city, Totenham na Liverpool. Timu pekee kubwa ambayo haipo hapo ni Arsenal tena nayo Kawafunga Goli 2 na Assist 3.

Rashford ana Goli 59 Tu lakini ukiangalia zaidi ya nusu ya magoli yake ni vs hao wakubwa.

Leo hii mkuu Bavaria Man U wanakupa Kitita hata pound milioni 100 tafuta Mchezaji ambaye Atatuokoa hizo Big matches na Afunge kama Rashford utamleta nani?
 
Tatizo Lenu mnakuwa na Reactionary views, sababu Jamaa Form imeshuka baada kurudi kutoka majeruhi Basi mna Assume Hana Kitu. 2019/2020, 2020/2021 si Foden wala si Mane waliokuwa Level ya Rashford,
mbona sanchez hakupewa huo muda na majeruhi sio sababu wengi tumeona wanarudi vizuri ye kila siku anaboronga ila anatetewa
 
mbona sanchez hakupewa huo muda na majeruhi sio sababu wengi tumeona wanarudi vizuri ye kila siku anaboronga ila anatetewa
1. Sanchez kacheza misimu miwili
2. Sanchez hatoki Academy yetu
3. Mshahara mkubwa kuliko wachezaji wote
4. Sanchez hajawahi ku prove akivaa Jezi ya Man Utd.
 


Rashford ni winga kwa asili. Assuming he is so good kama unavyodai kwanini namba akaichukua Greenwood na sasa Elanga? Na Sancho akaletwa kwa ajili ya ishu hizo hizo za wings.

Kwakua ni goal scorer mzuri as you say na amecheza ST mara nyingi sasa kwanini same position imewatesa united mpaka akanunuliwa ighalo, Cavani na sasa ronaldo?

Anakaa benchi kufanya nini? Umewahi ona Mbappe au Haaland anakaa benchi mechi muhimu na siyo majeruhi? Rashford kashakaa mara ngapi? Unasema psg wanamtaka hata kesho. Walipeleka ofa ya bei gani kwa united ikakataliwa?

Rashford anatakiwa awe 1v1 na kipa mara ngapi ili ascore goli moja? Mbappe na Haaland wanahitaji nafasi ngapi?

Mbappe na Haaland wamewahi letewa watu wa kujaza nafasi zao na wao wakakaa benchi kwa ajili ya ujio wa hao watu? Akija Icardi hapo united unaamini atakosa namba kwakua Rashford yupo?
 
Kumuweka Rashford level moja na Mbappe na Haaland ni mahaba yaliyopitiliza.

Watu wengi wanaotegemea stats kujenga hoja hua hawaangalii mechi. Ndiyo maana wakati mnamuambia Chief-Mkwawa kwamba timu haiperform (Kipindi cha Ole) yeye alikua bize kuleta xG na conversion rate ya timu. Mwisho wa yote waangalia mechi walikua sahihi.

Timu kubwa duniani zimeshamtaka Mbappe na Haaland. Lini zimemtafuta Rashford?
 
Una Accuse wenzako hawaangalii mpira na hata position anayocheza rashford huijui. Na Rashford si winga wa Asili, winga wa asili ni yule anaetanua width na kutia majaro, Rashford ni inside forward ama ukipenda Wing forward ni Aina za washambuliaji wanaotoka pembeni na kuingia Ndani.

Hakuna hata mmoja uliomtaja anacheza namba ya Rashford, Labda Sancho ambaye nae si kwamba anacheza Namba ya Rashford bali ni versatile pande zote.

Ole alikuwa anacheza 4-2-3-1 na Rashford alikuwa akicheza Kushoto mwa Uwanja, Namba yake alikuwa Akicheza Yeye au Martial ama Pogba sometime.

Na Wote Mbappe na Haaland stats zao zipo inflated na Ligi wanazocheza, Lacazette, Aubameyang, Batshuayi na wengine kibao at some point wamewahi kuwa na Goli za kutosha hizo ligi, ndio maana nikatumia UCL kutoa data Nzuri.

Hao PSG walimtaka Rashford sio mara Moja na Tuchel alibeep sana wakati ule.

Na si kila Kocha Anatumia Mchezaji yoyote kila kocha ana mfumo wake na mbinu zake, Sebastian Haller alikuwa kimeo west Ham anakimbia kimbia tu ila At right system Pale Ajax sasa Hivi Anachuana na Lewandoski na Benzema.

Ragnick mfumo wake alikuwa anacheza 4222 mechi nyingi za mwanzo Bila winga na namba 10 wawili ni Mfumo unaofit Mtu kama sancho zaidi Kuliko Rashford, unataka Technique kuliko pace.
 
Kwa Hio haiperform misimu miwili ya Ole tukamaliza nafasi ya 3 na ya 2.

Ilikuwaje ikawa haiperform na tukamaliza nafasi za juu.

Msimu uliopita tumefunga magoli 121, hakuna Kocha wowote post fergie aliefunga Magoli kama Hayo, yalitoka wapi hayo magoli?
 
Mimi sijaaccuse, nimesema.

Nimeandika Rashford ni winga kwa asili siyo wa asili. Winga wote siku hizi wana cut in na kujaribu kuscore au kuassisst.

Kama hujanielewa ni kwamba;

Rashford alikua anawekwa kulia. Akatolewa akawekwa Mason na Sasa ni Elanga.

Angeweza wekwa kushoto ila akaletwa Sancho na Ole kamchezesha sana Pogba pembeni huku Rashford yupo.

Hoja yangu ni kwamba hata namba yake ya asili haaminiki nayo.

4 2 2 2 unasema haihitaji pace inataka tech pekee? Hii formation inataka wings ziwe na pace na skills na forward yenye decent pace na huku DM awepo kitasa na ochestrator. Haya Rashford hana pace? Kwanini alikua hagewi namba to the extent Bruno akawa anawekwa wing?

Katika kuweka namba 10 wawili mbona Ralf kashawaweka Rashford na sancho kama namba 10 wawili dhidi ya chelsea? Akarely kwenye pace za hawaw wawili and it paid off. Isipokua poor finishing na decision making ya Rashford ikanyima ushindi.

Hoja ya ligi ya Mbappe na Haaland ni nyanya ni hoja dhaifu. Thiago katoka ligi aliyopo Haaland. Hazard alitokea ligi aliyopo Mbappe. Messi kaifuata ligi aliyopo Mbappe na hana output aliyozoeleka nayo same na Wijnaldum.
 
Assuming timu ilikua inaperform kama unavyosema.

Kwanini ole ameondoka?
 
Rashford hajacheza kulia tofauti na msimu huu makocha wote Kuanzia LVG, Mou mpaka Ole anatumika kushoto ama Kati. Labda kwenye mechi kidogo aende kulia ila hajawahi kucheza mfululizo hio namba
Angeweza wekwa kushoto ila akaletwa Sancho na Ole kamchezesha sana Pogba pembeni huku Rashford yupo.
Lini Pogba akacheza pembeni na Rashford yupo? Pogba alicheza kushoto Rashford alipofanyiwa Operation ya Mgongo. Na Ole hakumnunua Sancho kuja kumuweka Benchi Rashford, 2 different players ambao wanacheza pamoja.
Hoja yangu ni kwamba hata namba yake ya asili haaminiki nayo.
Acha kuongea usivyovijua hio 4222 haina winga. Na kubase Argument zako kwa kocha wa Muda kumuelezea Rashford wakati yupo zaidi ya miaka 6 ni useless.
Katika kuweka namba 10 wawili mbona Ralf kashawaweka Rashford na sancho kama namba 10 wawili dhidi ya chelsea? Akarely kwenye pace za hawaw wawili and it paid off. Isipokua poor finishing na decision making ya Rashford ikanyima ushindi.
Uongo unaendelea lini Ralf kacheza na Chelsea? Toka Ralf awe kocha wetu hatujawahi kucheza na Chelsea.
Hoja ya ligi ya Mbappe na Haaland ni nyanya ni hoja dhaifu. Thiago katoka ligi aliyopo Haaland. Hazard alitokea ligi aliyopo Mbappe. Messi kaifuata ligi aliyopo Mbappe na hana output aliyozoeleka nayo same na Wijnaldum.
 
Tatizo Lenu mnakuwa na Reactionary views, sababu Jamaa Form imeshuka baada kurudi kutoka majeruhi Basi mna Assume Hana Kitu. 2019/2020, 2020/2021 si Foden wala si Mane waliokuwa Level ya Rashford,

Kwahiyo Rashford aliwahi kumzidi Mane sio?

Kweli wewe ni Chief manake hakujawahi kuwa na Chief mwenye akili ndiyo mana waliishia kuuliwa na Wajerumani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…