alumelunda
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 830
- 1,014
InapendezaPANGA halikwepeki Manchester United. kocha wa kikosi hicho, Ole Gunnar Solskjaer amekuwa mkali na kusisitiza atawaondoa wachezaji wengi kwenye dirisha lijalo la usajili.
Hata hivyo, unaambiwa hivi kocha huyo huenda akagusa wachezaji wote, lakini si kinda Anthony Martial, ambaye mmiliki mwenza wa timu hiyo, Joel Glazer anamwona kama Pele wa Man United.
Martial kujituma kwake kwenye kikosi hicho kumetiliwa mashaka na makocha wote Jose Mourinho aliyeondoka na huyu wa sasa Solskjaer jambo linalotia wasiwasi mkubwa wa hatima ya Mfaransa huyo kuendelea kubaki Old Trafford msimu ujao.
Hata hivyo, kutokana na kuwa mchezaji kipenzi cha bosi, Martial anaweza kuwa salama. Januari mwaka huu, Martial alisaini mkataba mpya hadi 2023 ambao utamshuhudia akiweka kibindoni Pauni 200,000 kwa wiki.
Makamu Mwenyekiti wa Man United, Ed Woodward naye anamwona Martial ni silaha ya siku za baadaye. Kipindi kile Mourinho alitaka kumwondoa ili kumleta winga Ivan Perisic, lakini mabosi Glazer na Woodward wakamtaka Martial kwenye timu.
Kutokana na hilo, Kocha Solskjaer atakuwa na orodha yake ya wachezaji kadhaa ambao hataguswa akiamua kuwaondoa kwenye kikosi hicho ili kupunguza bili ya mishahara na kuwanasa wachezaji wengine wapya watakaokuwa na faida kwenye timu.
Ripoti zinadai kuna orodha isiyopungua wachezaji wanane wataachana na maisha ya Man United kwenye dirisha lijalo la usajili, huku ikidaiwa kuna sura tano mpya zitatua hapo kabla ya Julai Mosi watakapoanza mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao.
Wachezaji Antonio Valencia na Ander Herrera hao hawatakuwapo Old Trafford msimu ujao, lakini panga la Ole huenda likapitia pia majina ya mastaa kama Matteo Darmian, Marcos Rojo, Eric Bailly, Juan Mata, Romelu Lukaku na Alexis Sanchez.
Kuna taarifa pia zinazomtaja Paul Pogba kuwa ni miongoni mwa mastaa watakaofunguliwa milango ya kutokea licha ya Bosi Woodward kumtaka mchezaji huyo aendelee kubaki Old Trafford kwa sababu za kibiashara.
Ole hataki mzaha na ndio maana kwenye orodha ya wakali wanaotajwa kwamba watapigwa panga Old Trafford kuanzia sasa wote ni mastaa wakubwa.
Mkuu embu nipe rejea aliposema ananunua wa bei rahisiAliyesema hivyo ni OGS, kwamba atanunua wachezaji wa bei rahisi ili atengeneze kikosi cha namna hiyo.
Kwa case hiyo, means at minimum msimu ujao utakuwa mgumu zaidi, hivyo kama ni kuanza kuona matunda ni ule msimu mwingine. Ndiyo maana nikasema msimu ujao ni wa tabu kwenu.
Swali: Je, mna huo uvumulivu? Imagine sisi huu msimu wa nne umekata hatujapata kitu lakini tumo tu tumekubaliana kwamba Klopp anajenga timu. Mungu asaidie tupate hiyo UEFA.
Tunaisubiri mkuu mida midaNitaitafuta, jioni nitaiweka hapa.
Mkuu embu nipe rejea aliposema ananunua wa bei rahisi
Wanatajwa
Pepe (Kati ya £45mil-£70mil)
Fernandes (Kati ya £60-£85mil)
Maguire (£75milion)
Sancho (£100)
Koullibaly (£75-100milion)
Daniel James (£15milion)
Conselo (£50milion)
Wan Bissaka (£40 million)
Reece (£45 million)
Hivi kusema anataka Wachezaji wenye vipaji na wenye njaa ya mafanikio tafsiri yake ni wa bei rahisi. Halafu si kila mchezaji wa bei kubwa ni mzuri, wengine ni virusi tu
Sawa mkuuProbably ni misinterpretation, nitaitafuta hiyo article ambayo OGS aliponda wachezaji kwenye bei na majina makubwa.
Akisema atajikita kusajili low profiled players.
United ni sawa na Madrid, Barca, PSG sio club ya kujenga timu ni club inayohitaji mafanikio kwa njia yoyote ileHahahahahhah Manchester United haina muda wa kusubiri wa kujenga timu kwa miaka 3 o f 4 United hawana upuuzi huo United sio Liverpool mkuu timu ikikosa kombe hata misimu 3 kocha haulizwi United wanahitaji wachezaji wakubwa ,timu ishinde Trophies then wafanye Business wapige pesa
Manchester united wanataka kushindana na Barcelona na Madrid kuanzia ndani ya uwanja kwa maana ya kushinda mataji na nje ya uwanja kwa maana ya Biashara ndio level za unitedUnited ni sawa na Madrid, Barca, PSG sio club ya kujenga timu ni club inayohitaji mafanikio kwa njia yoyote ile
Tatizo linaanzia hapo kwa viungo kwani wakina scholes hawakuwa waingereza? Siku wakiwa na mechi mbaya basi ni kukaba na kublok mipira kitu ambacho pogba hawez yeye lazima azungukwe tu kila siku tunajenga timu kumu unlock pogba hahaha
After turbulent seasonEd ameahidi mpunga wa kutosha kusajili, embu tusubiri tuone View attachment 1099426
Nilichogundua we ni haters wa Mourinho, hapa ninajadili na mtu mweny chuki na mtu fulani, Et Mou ni kocha mwenye uwezo mdogo, kocha yupo kwenye top five ya makocha bora af unamwita vitu vya kipuuzi......we vip, kwanza ukitaja jina la Jose lazima utaje jina la Guardiola mana ndo the only one anayemyumbisha jamaa, uwanjan na kwenye mataj, tuchukulie Guardiola asingekuwepo Man city, EPL last season angechukua nani? Pochetno???..Tena siku nyingine acha kulinganisha "Kipara" Pep Guardiola na vitu vya kipuuzi kama Mourinho...
Sitakai soka la sasa ni kumwaga Pesa .. Nitajie na unilinganishie achievements z Mou na Guardiola katika kipindi cha miaka yao miwili katika timu zao .. Kama utafiti wako utaonesha Wamelingana au Mou kamzidi Guardiola Mimi nitaacha kuwa member na kuomba life bad humu jamii forum..
Lakini pia kumbuka kiasi alichotumia Guardiola ndani ya miaka miwili pale city ndio kiasi sambamba na kile kile alichotumia Mou united ... Kwanini matokeo chanya yaonekane city ?? .. Hapa sasa tunakuja kumdaka kocha .. Kocha ana uwezo mdogo ... Tena uwezo mdogo mno.
Haina haja ya kutoana mapovu kujua ubovu wa mou , rudi nyuma kidogo ulivyo guru my sh wa Chelsea kwa ibu.. Timu aliiacha ikiwa katikati ya msimamo ( Mid of the table )...
Mou anauzika sokoni kwa CV Na achievements zake kwenye soka .. Ni sawa na wakina Rafael Benitezi muda wao umeshakwenda na maji...
Unasema Guardiola natumia 1 billion pound, nikuulize hiyo amount ameitumia kwa miaka miwili ?? Unadhani ndani ya miaka miwili asingefanya vizuri city wangekuwa na hamu ya kumuongezea Pesa za kusajiri ???
Mkuu mpira ni mchezo wa wazi Fanya kazi upewe hela ... Mou aliikuta timu Nafasi ya sita na kaiacha Nafasi hiyo hiyo . Hakuna alichoongeza zaidi ya kutafuna Pesa ..
Wilfried Zaha anataka kuondoka crystal palace. Cha ajabu ni kua Crystal palance wanataka £100m kwa klabu inayomtaka zaha.
Wamuuze tu. United ana 25% yake hapoWilfried Zaha anataka kuondoka crystal palace. Cha ajabu ni kua Crystal palance wanataka £100m kwa klabu inayomtaka zaha.
Jose ameongea mambo mengi sana ambayo sasa hivi watu wameanza kuyaaminiNilichogundua we ni haters wa Mourinho, hapa ninajadili na mtu mweny chuki na mtu fulani, Et Mou ni kocha mwenye uwezo mdogo, kocha yupo kwenye top five ya makocha bora af unamwita vitu vya kipuuzi......we vip, kwanza ukitaja jina la Jose lazima utaje jina la Guardiola mana ndo the only one anayemyumbisha jamaa, uwanjan na kwenye mataj, tuchukulie Guardiola asingekuwepo Man city, EPL last season angechukua nani? Pochetno???..
Wakat Jose anafukuzwa kazi wote tulimunyoshea kdole kwamba tatizo ni yeye, ila sa hv nan anamnuoshea kidole jamaa, wengi sa hv wameturn back kuinyoshea kidole board na players, ni kweli watu wengi tuna dislike mbinu zake uwanjani, lakn tatzo la man u ni zaid ya Jose na hili yeye alilisema waz,....Ko kumbe tatzo la Man u sio mbinu za kocha tuu ni accumulation of problems...
Pote inajulikana kuwa ukimwajir Mou timu yako itakuwa ya kupak basi, sasa kwa nin usimpe support ya kutosha atimize malengo yake badala yake unaanza kumnanga ili afeli umfukuze kazi, Na ulimwajir ukijua hilo, huo si ni unafiki.....
Msimu wa kwanza Guardiola alisajili wachezaji wanane, na hakupata chochte zaid ya kuingia top 4, Rumours za kufukuzwa kazi zilikuwa nje nje lakn board ilimpa full support, msimu wa kwanza pesa iliyotumika ni Pound 186Mill,....Tafta ya Mou alitumia sh ngap...Mou akachukua Europa nafkli na FA
Msimu wa pili Guardiola alspend Pound 276Mill,....akachukua ndoo ya EPL, Tafta uone Mou alispend sh ngap....akaishia nafas ya pili, .....
Jose alijua kabisa mapungufu yaliyopo hvyo kuingia msimu wa tatu alihtaj kukiongezea nguvu kikosi ili kukabili kasi ya Man city na Liver....kilichofanyika tunakijua, akaonekana anafuja hela, ooh mbinu yake ya kupaki basi, kwanza kaishia nafs ya pili msimu uliopita na mengne mengi...
Guardiola akamwaga tena Pesa Pound mill 63, Sjui hata United ilitumia sh ngap....alaf mtu anademand matokeo mazur uwanjani how comes? unaweza kufight na best managers kama Klopp na Guardiola wenye kila aina ya silaha wanayotaka, huku ww silaha unazozitak hupati, unaletewa Pogba na Sanchez, et lengo wanakuforce ubadili mbinu ucheze mpira wa kuintertain mana wachezaji hao sio wa kupaki basi, et una rashford na Lingard huo si utani kabisaa...anyway mambo ni meng na mda ni mchache...
Kwa misimu miwili tu Guardiola alitumia zaid ya pound mill 525,....
Mou amespend pound 390 Mill in total....
Wewe ni mcheza FOREX mzuri sana, na njia hyo ya kujipatia kipato imekufikisha hapo ulipo japo wengine wanakudharau kwa kusema FOREX ni utapeli. ko usimdharau Mou kwa style yake ya kupaki basi, ndo ilipomfikisha hapo alipo, na akienda timu yyte lazima aondoke na vikombe, sa unaanzaje kumwita kocha kama huyo uwezo mdogo.... Jamaa ana mapungufu yake ndio, ila sio kumshusha hadhi kias hcho aisee....
Ole kwangu mm sio kocha bora na nadhani timu yetu itamshinda kama haiijamshinda bado.Haha haha
Naona watu wenye imani haba wameanza kumkumbuka yule mmakonde wa Mtwara "Jose Mourinho" kwa timu kutokufanya vizuri muda huu.
Niweke kitu sawa. Matatizo ya sasa hayafuti udhaifu wa Mou. Mou ni kocha mbovu... Timu kuendelea kuwa mbovu haimuondolei ubovu wake.
Issue kubwa ni kocha Ole ameshindwa kuchanga karata zake vyema mechi 10 za mwisho ...
Huyo mou alivyotimuliwa Chelsea kocha aliechukua mikoba yake aliweza kuivusha timu na kuiepusha na kushika Nafasi za 10+...
Niliwahi kusema humu kwamba ni lazima tuwe timu kama Barcelona , Chelsea au Madrid kwamba kocha ukizingua unafukuzwa kabla mambo hayajaharibika....
Leo watu wanamkumbuma Mou ila wamesahau mechi ya mwisho na Liverpool , ambayo tulichezea kipigo "heavy" na kupelekea huyu mmakonde kutimuliwa pale Old Trafford.. Katika mechi hiyo aliwaweka benchi Pogba, Martial , Lukaku, Valencia , Herrera... Hahaha
Ole mimi nakupa Nafasi na nitapima uwezo wako kwenye pre season matches na kwenye transfer zako .
Otherwise , GGMU.