Manchester United (Red Devils) | Special Thread

MANCHESTER UNITED NA KILICHOTOKEA MWAKA 1999.

Na Tom Thomas

Mwaka 1999 unabaki kuwa mwaka bora kwenye historia ya Manchester United. Mafanikio yaliyopatikana yanaufanya kuwa mwaka bora na wa kipekee sana. Ni mwaka ambao klabu ilifanikiwa kushinda mataji makubwa matatu. UEFA Champions League, Premier League na FA Cup. Hakuna klabu nyingine iliyowahi kufanya hivi.

Mafanikio haya yalimfanya Kocha wa Manchester United wakati huo, Alex Ferguson atunikiwe heshima maalumu na utawala wa Kifalme nchini Uingereza chini ya Malkia Elizabeth II. Heshima iliyomfanya atambulike kwa jina la Sir Alex Ferguson.

Mafanikio haya hayakupatikana kirahisi. Manchester United walipitia njia ngumu sana kuyapata. Haikuwa kazi rahisi kushinda kila ubingwa ilioupata. Hii ni sababu nyingine inayoufanya mwaka huu uonekane kuwa wa kipekee sana.

PREMIER LEAGUE.
Manchester United walianza harakati za kuutafuta ubingwa huu kwa kucheza mechi ya nyumbani dhidi ya Leicester City. Ikiwa haijashinda ubingwa wowote msimu uliokua umepita, walilazimisha sare ya magoli 2-2 ndani ya uwanja wao wa Old Trafford.

Mpaka dakika ya 78 Leicester City walikua mbele kwa magoli mawili. Magoli ya Emile Heskey na Tony Cotee. Magoli mawili ya Teddy Sheringham na lile la dakika ya 90 la Kiungo David Beckham yaliinusuru Manchester United isipoteze mchezo wake huu wa kwanza wa ligi.

Mechi ya pili ugenini dhidi ya West Ham mambo bado yalikua magumu. Mechi ilimalizika kwa sare ya 0-0. Manchester United walisubiri hadi mechi ya tatu dhidi ya ‘vibonde’ Charlton Athletic ili waweze kupata ushindi wao wa kwanza. Ushindi wa magoli 4-1. Magoli mawili ya Ole Gunnar Solskjaer na Dwight Yorke aliyefunga magoli mawili mawili pia.

Mechi ya tano ugenini dhidi ya Arsenal, walipokea kichapo cha kwanza. Arsenal wakiwa ndani ya uwanja wao Highbury walipata ushindi wa magoli 3-0. Hali ikawa mbaya sana kwa Manchester United ukizingatia mchezo uliokua unafuata ulikua dhidi ya wapinzani wao Liverpool.

Walifanikiwa kushinda mechi hiyo iliyofuata dhidi ya Liverpool. Kuanzia hapo wakaendeleza rekodi nzuri ya kufanya vizuri kwenye mechi zilizofuata. Walipoteza mechi mbili tu tangu siku hiyo, mechi dhidi ya Sheffield Wednesday na ile dhidi ya Middlesbroug.

Mzunguko wa pili, mechi nne kabla ya msimu kumalizika, Arsenal walikua wanaongoza Ligi. Manchester United wakiwa nafasi ya pili, Chelsea akishika nafasi ya tatu. Manchester United walicheza mechi ya ugenini dhidi ya Liverpool. Ilikua ni mechi muhimu itakayotoa mustakabli kuelekea ubingwa.

Dakika ya 60, Manchester United walikua wakiongoza kwa magoli 2-0. Liverpool walipambana sana ndani ya uwanja wao wa nyumbani. Mpaka dakika 90 zinamalizika, matokeo yakawa 2-2. Liverpool walisawazisha kwa magoli ya Jamie Redknapp la lile la dakika za mwisho la Kiungo Paul Ince.

Wakati huohuo, Arsenal wao walishinda mechi yao dhidi ya Tottenham Hotspur, Chelsea pia waliifunga Leeds United goli 1-0. Mbio za ubingwa zilikua kali sana. Arsenal akiendelea kuongoza ligi. Mechi tatu zikabaki.

Mechi iliyofuata ilikua dhidi ya ‘wagumu’ Middlesbrough. Kumbuka mechi ya kwanza, Manchester United walipoteza nyumbani Old Trafford. Mechi hii ilikua ndani ya uwanja wa Riverside Stadium. Mechi ngumu iliyomalizika kwa Man United kupata ushindi wa goli 1-0. Goli la Dwight Yorke.

Arsenal wao walipoteza mechi iliyofuata dhidi ya Leeds United, kitendo kilichoipa nafasi kubwa Manchester United kushinda ubingwa. Mechi iliyofuata, Manchester United walihitaji ushindi kutangaza ubingwa. Haikua hivyo. Mechi ilimalizika kwa sare. 0-0 dhidi ya Blackburn Rovers. Ikawa imeshindikana.

Ikabidi isubiriwe hadi wiki ya mwisho ili iamue ni nani atakua bingwa kati ya Arsenal na Manchester United. Mechi hizo za mwisho Manchester United walicheza dhidi ya Tottenham Hotspur, Arsenal dhidi ya Aston Villa.

Magoli ya Andy Cole na David Beckham yaliipa ubingwa Manchester United kwenye ushindi muhimu wa magoli 2-1 licha ya Arsenal kupata ushindi pia. Msimu ukamalizika Manchester United wakatwaa ubingwa kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya Arsenal walioshika nafasi ya pili.

FA CUP.
Njia waliyopita Manchester United kwenye FA Cup ilikua ngumu vilevjle kama ile ya Premier League. Walicheza dhidi ya timu ‘ngumu’. Middlesbrough, Chelsea, Liverpool na Arsenal kwenye hatua za mtoano pamoja na Newcastle United kwenye fainali.

Walianza harakati za kuwania ubingwa huu kwa kucheza dhidi ya Middlesbrough. Kumbuka Middlesbrough walishinda mechi ya Old Trafford kwenye ligi. Mechi hii ilikua ndani ya Old Trafford tena. Sekunde chache baada ya kipindi cha pili kuanza Andy Townsend aliifungia Middlesbrough goli la kwanza, baadae Man United walirudi na kupata ushindi wa magoli 3-1.

Hatua iliyofuata ilikua dhidi ya Liverpool. Kwenye mechi hii, dakika ya tatu ya mchezo, Michael Owen aliipatia Liverpool goli la kuongoza. Mpaka dakika ya 87, Manchester United bado walikua nyuma kwa goli hilo moja huku wakiwa wamepoteza nafasi nyingi za kufunga.

Wakati mpira ukielekea kumalizika. Dwight Yorke akaipatia Man United goli la kwanza, dakika ya 88 kabla ya Ole Gunnar Solskjaer kufunga goli la pili dakika ya 90. Mechi ikamalizika. Manchester wakasonga mbele. Mechi iliyofuata ilikua dhidi ya Fulham. Ilimalizika kwa ushindi mwembamba wa goli 1-0.

Hatua ya sita. Manchester United walicheza dhidi ya Chelsea. Mechi ya kwanza nyumbani Old Trafford, mechi ngumu iliyowashuhudia Paul Scholes na Roberto Di Matteo wakitolewa nje kwa kadi nyekundu. Mechi ikaisha kwa sare. 0-0. Ikabidi ichezwe mechi nyingine Stamford Bridge. Mechi iliyomalizika kwa Man United kupata ushindi wa magoli 2-0. Magoli ya Dwight Yorke.

Hatua iliyofuata ilikua ni ya nusu fainali. Mechi dhidi ya Arsenal. Mechi ya kwanza, Old Trafford ilimalizika kwa sare, 0-0 baada ya dakika 90. Zikaongezwa dakika 30 pia matokeo yalikua vilevile. 0-0. Ikaamuliwa mechi nyingine ichezwe siku tatu baadae.

Mechi ya pili iliyochezwa April 14, 1999 inabaki kuwa mechi kali kuwahi kuzikutanisha Arsenal na Man United. Ni mechi iliyochezwa ndani ya uwanja wa Highbury. Alianza David Beckham kufunga goli la kwanza kabla ya Dennis Bergkamp kusawazisha.

Mshambuliaji wa Arsenal Nicolas Anelka alifunga goli lakini halikuruhusiwa kwani mwamuzi alisema Anelka alikua ‘offside’. Dakika ya 74, Kiungo wa Manchester United Roy Keane alitolewa uwanjani kwa kadi nyekundu na kuwafanya Man United wabaki 10 uwanjani kwenye mechi hii ngumu.

Dakika ya 90, beki Phil Neville alimchezea faulo kiungo wa Arsenal Ray Parlour ndani ya eneo la box. Mwamuzi akaamuru ni penati. Golikipa Peter Schmeichel akaicheza penati ya Dennis Bergkamp. Mechi ikamalizika kwa sare, 1-1.

Zikaongozwa dakika 30. Ndani ya dakika hizo Kiungo wa Manchester United, Ryan Giggs alifunga moja kati ya magoli yake bora kabisa kwenye maisha yake ya soka. Alifunga goli baada ya kukimbia na mpira kutoka nyuma akiwapiga chenga wachezaji wa Arsenal kisha kumfunga golikipa David Seaman. Mechi ikaisha kwa ushindi wa goli 2-1. Man United wakafuzu hatua ya fainali.

Mechi ya fainali dhidi Newcastle United ndani ya Wembley ilikua ni ya mwisho kabla ya uwanja huo kufungwa. Mechi ilimalizika kwa Man United kupata ushindi wa magoli 2-0. Magoli ya Teddy Sheringham na Paul Scholes. Manchester United wakashinda ubingwa wa pili.

UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Kwanza kabisa, Manchester United walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kupangwa kundi moja dhidi ya Bayern Munich na Barcelona. Klabu nyingine ilikua ni Brøndby kutoka Denmark. Lilikua ni ‘kundi la kifo’.

Manchester United walimaliza mechi za makundi wakiwa na pointi 11. Wakipata sare nne, mbili dhidi ya Bayern Munich, mbili dhidi ya Barcelona. Walipata pointi sita dhidi ya Brøndby. Bayern Munich waliongoza kundi, Man United wakashika nafasi ya pili. Nafasi iliyofanya wafuzu hatua ya robo fainali.

Ilikua ni dhidi ya Inter Milan. Mechi ya kwanza, Old Trafford iliisha kwa Man United kupata ushindi wa magoli 2-0. Mechi iliyofuata kule Milan ikamalizika kwa sare 1-1. Mechi ya nusu fainali ilikua dhidi ya Waitaliano pia, Juventus.

Mechi ya kwanza, Old Trafford, Kiungo na nahodha wa Juventus Antonio Conte aliianza kwa kufunga goli la kwanza. Mpaka dakika 90 zinamalizika, bado Juventus walikua mbele kwa goli 1-0. Kwenye dakika za nyogeza, Ryan Giggs akafunga goli la kusawazisha kutokana na pasi ya David Beckham.

Mechi ya pili kule Turin. Mpaka dakika ya 11, Juventus walikua mbele kwa magoli mawili ya Filippo Inzaghi. Manchester United walihitaji kufanya ‘come back’ na kupindua matokeo. Mwisho, mechi ikamalizika kwa ushindi wa magoli 3-2. Magoli ya Roy Keane, Dwight Yorke na lile la ushindi dakika za mwisho la Andy Cole. Wakaingia fainali.

Fainali. Mechi dhidi ya Bayern Munich ndani ya Camp Nou mjini Barcelona. Kumbuka Bayern Munich na Manchester United walikutana kwenye makundi, mechi zote mbili zilimalizika kwa sare. Mechi hii ya mwisho ilikua ni ya kuamua nani ashinde ubingwa wa Ulaya.

Manchester United iliwakosa viungo wake muhimu, Roy Keane na Paul Scholes. Hivyo ilibidi David Beckham acheze kama kiungo wa kati pamoja na Nicky Butt. Hii ilikua ni mechi ya mwisho ya golikipa Peter Schmeichel kama mchezaji wa Manchester United. Mechi iliamuliwa na ‘referee’ bora kabisa kuwahi kutokea duniani. Muitaliano Pierluigi Collina.

Dakika ya sita tu mchezo. Mario Basler akaipatia Bayern Munich goli la kwanza. Goli liliodumu hadi dakika ya 90. Zikaongezwa dakika tatu. Manchester United wakapata kona alipigwa na David Beckham dakika ya 91. Mpira wa kona uliokolewa vizuri, ukamkuta Ryan Giggs aliyepiga krosi kuelekea ndani ya box, mpira ukamkuta Teddy Sheringham aliyefunga goli la kusawazisha.

Dakika mbili baadae, Manchester United wakapata kona nyingine iliyopigwa na David Beckham tena, ni kona iliyozaa goli la pili na la ushindi lillofungwa na Ole Gunnar Solskjaer. Mechi ikamalizika kwa Manchester United kupata ushindi wa magoli 2-1. Ushindi ulioipa ubingwa wa pili wa UEFA Champions League.

Msimu ukamalizika. Manchester United wakatengenezea historia ya kuwa klabu ya kwanza kushinda mataji makubwa matatu ndani ya msimu mmoja nchini England. Hii ni rekodi ambayo inadumu hadi leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilichogundua siyo sis pekeyetu tulistruggle kweny gem gem hiz za kati kati ya wiki, vigogo wengi hali tete
Utd 2-2 burnley
Newc 2-1 city
Tot 0-1 Watford 55'
Liver 1-1 Leicester 50'
Bournemouth 2-0 Chelsea 68'

Sent using Jamii Forums mobile app
upo sahihi muheshimiwa lakini tunapaswa kwanza tupambane na hali yetu ndipo baadae tumuangalie adui yetu nini anafanya au anafanywa na adui mwengine.
kwa wakati huu ambao inaonenekana dhahiri kwa majirani zetu wawili kuna sintofahamu inayoendelea kurindima sisi ndio tunapaswa tuitumie nafasi hiyo kama wao walivyoitumia wakati wa jose mourinho.

bwana yule alituachia timu tukiwa nyuma kwa alama 11 dhidi ya chelsea lakini kwa msimamo wa sasa chelsea wametuacha kwa alama 2 ndani ya mwezi mmoja wa utawala wa OGS.

tunapaswa tushinde kwanza ndipo tumuombee adui yetu chelsea apoteze dhidi ya bournermouth.
tushinde kwanza dhidi ya leicester city ndipo tumuombee adui yetu arsenal apoteze dhidi ya manchester city siku ya jumapili.

wakuu mumemuonaje kijana wetu wa zamani joshua king performance yake hapo jana?
kwenye mechi 21 amefunga magoli 8.
 
Martial kasaini mkataba mpya mpaka 2024 Fellaini anaenda zake china

Sent using Jamii Forums mobile app
kwa maoni yangu ni maamuzi mazuri yaliofanywa na klabu kwa kukubali kumuongezea mkataba mpya anthony martial na pia kukubali kumuuza marouane fellaini ambaye mwanzo wa msimu alikubali kusaini mkataba mpya wa muda mrefu.
Ifike wakati viongozi wa juu wa klabu wasionyeshe mioyo dhaifu kwenye ishu ya contract renewal kwa waajiiriwa hususan wale ambao hata kama wataondoka klabuni hawataleta athari kubwa sana, fikiria leo hii josep guardiola ameshaonyesha kila dalili za kumuondoa vicent kompany kwenye utawala wake
  • kupewa mkataba mpya kwa anthony martial iwe ni kichocheo zaidi kwa klabu kuwatimizia mahitaji yao david degea, ander herrera na paul pogba.
  • kuondoshwa kwa marouanne felllaini pia iwe kichocheo kwa klabu kufanya maamuzi ya kuwaondoa wachezaji kama matteo darmian, antonio valencia, marcos rojo. Hata kama wataondoka muda huu hawatoleta athari kubwa ukilinganisha na wachezaji kama ander herreara.
Ashley Young ameendelea kunizodoa na kunifuta mavumbi ya ujinga lakini si mchezaji wa kuendelea kumtegemea acheze kila siku hivyo basi anapaswa aongezewe mkataba mdogo huku klabu ikifanya mkakati wa kutafuta mbadala wake, kiupande wangu naamini dirisha lijalo la usajili ndilo tutakalompimia ed woodward kwenye ishu zote zinazohusu uendeshaji wa klabu hususani ndani ya uwanja, tutajua mbivu na mbichi ifikapo mwezi June hadi August.

kila la kheri lord fellaini huko uendako, kwa mshahara atakaopokea nitamuomba aniunganishe kwenye dili la kumsafirishia mende, nge, tandu na wadudu wengineo ambao ni chakula muhimu nchini China.
 
Jezi hiyo inanikumbusha binge la gemu tulioshida 4 - 3 dhidi ya Man City Michael Owen akifanya maajabu dakika za mwisho
 
Hakika katika mapambabo kunahitaji ujasiri, kujituma na kutokata tamaa, wakina Rashford wajifunze vitu kutoka kwa mashujaa wa 1999
 
pound million 400 kwa wachezaji watano ni wastani wa paundi millioni 80 kwa kila mchezaji hivyo sidhani kama bajeti hiyo inawezekana kwa msimu mmoja ikiwa ndani ya misimu mitatu klabu imetumia paundi millioni 400.
Hata mimi pia natamani tusajili takribani wachezaji watano ifikapo msimu ujao lakini maamuzi ya mwisho kwa kiasi kikubwa yanategemea repoti ya mwalimu na mpaka muda huu hajajulikana mwalimu mpya, usishangae anaweza kutafutwa mwalimu mpya ghafla akaja na maamuzi ya kutaka kufanya kazi na wachezaji kama vile antonio valencia, matteo darmian, marcos rojo, phil jones n.k
hahahahahahahahahaahaaaaaaa.

uzuri ni kwamba ujio wa Ole Gunnar Solskjaer ndani ya klabu umekuwa ni ujio wa furaha kwa pande zote zenye kuunga mkono juhudi za manchester united za kurudi kwenye ubora, kama tungelikuwa tupo na bwana yule kivyovyote kwa hali tuliokuwa nayo ingelazimika klabu kumtimizia mahitaji yake kwa gharama yoyote ile nyakati hizi lakini hali imekuwa tofauti.
vile vile kama ujio wa OGS ungelizidi kuendeleza jinamizi la kufanya vibaya wahusika wakuu wangelilazimika kuhangaika kutafuta wachezaji kwenye dirisha gumu la usajili la mwezi January na kumfanya jose mourinho awe ni mshindi kwenye pambano la nani alikuwa sahihi.

Mourinho kwa nyakati tofauti alituaminisha ya kwamba baadhi ya world class wapo ovyo sana kiasi ambacho alifikia hatua ya kuwaweka benchi jambo ambalo halikuwa sahihi lakini kiupande wa pili wa shilingi madai yake ya kuwa klabu inahitaji mabadiliko ya kuleta wachezaji wapya na kuongozwa kisasa kama wanavyofanya wapinzani wetu yanaendelea kuwa hai mpaka kesho ndio maana sijawahi kupinga mawazo ya ujio wa director of football.

kama ulivyoandika hapo juu ni muda muafaka kwa klabu kufanya maandalizi ya msimu ujao ili kurudisha imani iliofifia kwa miaka 7 tokea aondoke gaffer, kama tunavyofikiria sisi tuliopo uswahilini na viongozi pia natamani wawe na fikra zaidi ya hizi za kwetu za kuleta mabadiliko kwa kuanzia kuwauza wachezaji wasio leta athari kubwa sana msimu huu na kuzifanyia uchunguzi wa kiufundi repoti za skauti waliozagaa pembe zote za dunia.

mipango mibovu pamoja na machaguo ya ovyo yakiongozwa na familia ya glazer ndio yametufikisha hapa tulipo, ahsante sana OGS kwa kuturudishia kile ambacho tulikuwa tunakikosa kwa muda mrefu, nataka niamini ujio wako pamoja na mike phelan hautokani na nguvu ya familia ya glazer bali ni mkono wa mwanadamu mgumu aliyejenga emperor kwa miaka 26 aliyodumu kama mtawala..

ahante ed woodward kwa kuweza kuzuia deal za ovyo zilizokuwa zinategemea kuigharimu klabu lakini bado mpaka leo sijaelewa kilichokufanya ukimbilie kumpa mkataba mpya jose mourinho mwezi january huku ukiwa huna mipango ya kumtimizia mahitaji yake.
 

Attachments

  • 1548970246079.png
    144.1 KB · Views: 24
Hatari sana aisee maana naona mnaipiga first eleven yote na mishahara ya 200k+++++++

Antony Martial now on 250,000 British pounds per week wage
Source ya taarifa yako?

Mshahara haujatajwa so far

By the way, tumia hela upate hela

Spurs walikuwa na ceiling ya £100,000 per week, ulipofika mkataba wa Kane (wakati huo United wanamtolea macho, huku Madrid wanamzengea) ikabidi wapande hadi 270K ndio Kane akasaini.

Kwa Dele wamevuka ceiling. Kwa Ericksen wanajidai wabahiri, amegoma kusaini mkataba mpya, Aldeweherd alishaamua kuondoka.

Baki na hela zako bank uendelee kuwa na status ya kushika bunduki, badala ku shoot....endelea kushika bunduki

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Source hii hapa

Anthony Martial signs new deal with Manchester United until 2024


Halafu Eriksen mbona Skysports wanasema yuko juu ya 100k?
 
Source hii hapa

Anthony Martial signs new deal with Manchester United until 2024


Halafu Eriksen mbona Skysports wanasema yuko juu ya 100k?
Ericksen yupo kipindi cha kujadili mkataba mpya, hawataki kumpa anachotaka. Kwa sasa analipwa £70,000 per week.

So option ya kwanza ni kumuacha aondoke kwa hela ndogo (maana mkataba wake una expire summer ya 2020) na wazibe nafasi kwa kununua mchezaji mwingine kwa £50+mil (hapo hatujazungumzia mshahara atakaodai).

Option ya pili ni kulipa mshahara mchezaji kulingana na kiwango alichonacho lakini pia kwa kuangalia soko. Kwa soka LA sasa ukijidai unang'ang'ania policy ya club kulipa mshahara kiduchu si tu hutawezi kusajili World Class Players, bali pia hutaweza ku keep wale ulionao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu damushin shukrani sana kwa nondo zilishoshiba haswaaa.... Je kwa upande wako unaona nani anafaa kuwa manager wa timu kuelekea msimu ujao kati ya poch na ole?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu damushin shukrani sana kwa nondo zilishoshiba haswaaa.... Je kwa upande wako unaona nani anafaa kuwa manager wa timu kuelekea msimu ujao kati ya poch na ole?

Sent using Jamii Forums mobile app
dah! hii heshima ulionipa ni nzito kuliko ndevu za lionel messi.
ujio wa pochettino na faida zake kwa mtazamo wangu.
  • ana uzoefu na ni muumini wa mpira wa kisasa ambao tumekuwa tukiulilia kwa muda mrefu
  • ni muumini wa kuwapa nafasi wachezaji vijana na hili tumelishuhudia kwa wachezaji tofauti.
  • ana rekodi nzuri sana kwenye suala la kusajili wachezaji, ukiangalia wachezaji wengi aliowasajili tokea yupo southampton hadi tottenham hotspurs wameendelea kufanya vizuri na wengi wao ni wale aliyowasajili kwa fedha chache.
athari yake kubwa ninayoiona ni kurudi tena kwenye zama za kuachana na falsafa, misingi na utamaduni wa klabu iliojengwa miaka mingi iliopita, naamini kama pochettino atawasili msimu ujao hatopendelea kuchaguliwa benchi lake la ufundi hivyo basi atakuja na timu yake ya ufundi, inamaana tutaanza tena upya kama alivyofanya david moyes, LVG na jose mourinho.
halafu pia siamini kama pochettino atadumu kwa muda mrefu klabuni bila ya kuwa na fikra za kurudi tena spain kufundisha

kwa uoni wangu sioni dalili yoyote ya kuondolewa ole gunnar solskjaer mwishoni mwa msimu hata kama atashindwa kupata nafasi ya nne, kuna nguvu tatu zina mlinda kwa sasa ambazo ni legends aliocheza nao kwa mafanikio makubwa, waliyopendekeza apewe nafasi baada ya kuona jahazi linazama na nguvu ya mwisho ni ya mashabiki wale wa karne ya 20 ambao bado wanaendelea kumuona ni shujaa aliyetakasika kwa kile alichokifanya pale nou camp.

silaha yake nyengine kubwa aliyokuja nayo ni kurudisha utamaduni wa manchester united wa kucheza mpira wenye kueleweka, makocha waliopita kila mmoja alikuja na falsafa yake isiyoendana na damu ya manchester united, wakati wa jose mourinho tulishinda mechi nyingi sana chini yake kuliko mwalimu yoyote yule lakini nidhamu yetu ya ushindi ilikuwa ni ya kiwango cha chini sana.
hata ukiangalia benchi lake la ufundi ni uthibitisho tosha jinsi gani klabu imeshajiandaa kuishi na OGS kwa sababu limejaza watu wanaoendana na utamaduni wa manchester united, siamini kama ujio wa mike phelan ni kwa muda wa miezi sita tu halafu atafute mlango wa kutokea.

kama ishu ni kuwapa nafasi majina makubwa basi klabu tayari imeshapitia hatua hiyo lakini bado tuko pale pale, ukiangalia upande wa pili imemchukua miaka mitatu jurgen klopp kuifikisha liverpool hatua iliopo muda huu cha umuhimu ni kuwepo uaminifu.

Solskjaer, Phelan, Karrick na McKenna ni timu ambayo inahitaji kutafutiwa mwanadamu mwenye uelewa mkubwa wa soka la kisasa na hii ndio kazi ya kwanza anayopaswa aifanye ed woodward.
nasubiria majibu yake siku ya jumapili baada ya kupoteza alama mbili kwa mara ya kwanza tokea awe mwalimu wetu, leicester city ni kipimo chengine cha ukweli.

kuna mlevi mwenzangu ameniuliza hapa hivi ole gunnar solskjaer aliikuta manchester united ikiwa nafasi ya nne?
 
Kiukweli haikua kazi rahis

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…