Manara: Yanga wakijaza uwanja naacha kazi Simba

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
KUELEKEA katika kilele cha Wiki ya Wananchi ya Yanga ambayo itafanyika leo Jumapili uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mtani wao Haji Manara ambaye ni Ofisa Habari wa Simba ametupa kijembe kwa watani zao hao.

Kilele cha Wiki ya Wananchi kitaendana na utambulisho wa wachezaji wao pamoja na mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Kariobang Sharks inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya.

Manara amesema wiki hii kumekuwa na matukio makubwa ya timu mbili kongwe nchini ambapo Simba wanaendelea na wiki yao itakayofikia kilele Agosti 6, Jumanne watakapocheza na Power Dynamos ya Zambia.

Klabu zote mbili zinaendelea na shughuli za kijamii kuelekea kilele chao ambapo Simba hufanya maadhimisho hayo kila mwaka wakati Yanga hii ni mara yao ya kwanza kufanya shughuli hiyo.

"Kama ikitokea siku ya leo Jumapili ambapo Yanga watafikia kilele cha wiki yao idadi ya mashabiki sijui kama inaweza kuwa wengi kufikia idadi ya mashabiki ambao wataingia siku ya Jumanne ambayo tutafanya hitimisho la Simba Day"

"Naomba niweke vizuri hapa kama ikitokea mashabiki wa Yanga wakawa wengi na kujaza uwanja siku ya leo watakapocheza mechi yao ya kirafiki, kuliko ile ambayo wataingia katika hitimisho ya siku yetu ambayo itakuwa Jumanne naacha kazi Simba.

"Katika kuhakikisha hili tunawakumbusha tu wanakumbuka ambacho tulikuwa tunafanya katika mechi zetu za Kimataifa msimu uliopita, basi tunauhakika wa kujaza mashabiki robo tatu siku hiyo kuliko ile ambayo wataingia siku yao," amesema Manara.
 
Hakika mlio hudhuria uwanjani, mnastahili pongezi za kila aina. Tunawaona live bila chenga kupitia Azam sports2. Uwanja umependeza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom