Manager wa TRA Handeni mjini ni tatizo

Manager wa TRA Handeni mjini ni tatizo

Wakuu sijawahi kukutana na mtu mkorofi mtata na mwenye visasi kiasi hiki. Biashara imekuwa ngumu sana mpaka nawaza kuifunga tu asije akanipeleka jela bure maana amepania kupeleka jela wafanyabiashara 6.

Wakuu miezi kadhaa nyuma maduka yote Handeni mjini tuligoma kufungua mpaka mkuu wa wilaya alipokuja kusuluhisha.

Maana huyu Manager amekuwa akipiga faini za hovyo na mgumu sana kumsikiliza mtu. Mtu unakuta anapitia tatizo la kawaida kama mashine kuzingua ndani ya siku hiyo hiyo au siku moja tu tayari hakuelewi. Imekuwa ni kukomoana na amepania hilo zaidi baada ya ule mgomo na yeye kubakishwa bado.

Sasa jana ofisini kwake aliwatishia wafanyakazi wa chini yake kupunguza kiasi cha mshahara na mlinzi mmoja kupoteza mafao akijinasibu uwezo anao. Kosa ni mfanyakazi mmoja kutoka kwa haraka ni mdada nahisi ni shida za kiafya alienda msalani akachukua muda. Anaelezwa amepata shida kiafya kaenda msalani haelewi anaona anadanganywa. Aisee

Sijawahi kukuta ofisi ina manager wa staili hii aisee

Dar es salaam nimeingia ofisi kadhaa za TRA nimehudumiwa vyema sana lakini hapa Handeni tunakomolewa. Sijui tufanyeje ahamishwe maana baada ya ule mgomo wote tulioongea vimbelembele tuna kimbembe.

Ktk mkoa wa Tanga Handeni nasikia na Pangani mzunguko wa Hela uko chini sana.
Korogwe na Mheza ni sababu ya kuwa kwenye main road junction.
Rushoto wana Neema tu labda tuseme hivyo.
Handeni labda itakapoisha barabara hiyo ya Kilindi Songe Singida yamkini.
 
Hili pendekezo la kuhamishwa ni la kuusambaza ugojwa, si sawa.
Msumbufu wa aina hiyo ni wazi ni mhaini na mchonganishi wa Serikali kwa wananchi wake.

La msingi hapo kama inavyonadiwa siku zote;
'Serikali sikivu, basi, achunguzwe na ikidhihirika ni kweli apigwe chini mazima.
Nasema achunguzwe sababu wakikurupuka wakati mwingine watu wana maugomvi yao wakataka kuharibiana.

Nawasilisha.
 
Hadidu za rejea ziwe ni zipi wakati wa kuchunguzwa?

Jamaa ameshasema mashine yake ilipata hitilafu,
Kwa hiyo anakiri kuwa ni kweli hajatumia mashine ipasavyo kwa mujibu wa sheria.
Ambayo ni makosa yanayopelekea adhabu.
Na kimsingi hata huko kusema kuwa mashine ilikuwa na hitilafu ni kuuma maneno tu.
Sema tu inahitajika subira na hekima kwa hiyo officer lakini in the first place hapo hana kosa, yeye ame enforce sheria tu.
 
Ktk mkoa wa Tanga Handeni nasikia na Pangani mzunguko wa Hela uko chini sana.
Korogwe na Mheza ni sababu ya kuwa kwenye main road junction.
Rushoto wana Neema tu labda tuseme hivyo.
Handeni labda itakapoisha barabara hiyo ya Kilindi Songe Singida yamkini.
Handeni papo vizuri kibiashara panakua
 
Hili pendekezo la kuhamishwa ni la kuusambaza ugojwa, si sawa.
Msumbufu wa aina hiyo ni wazi ni mhaini na mchonganishi wa Serikali kwa wananchi wake.

La msingi hapo kama inavyonadiwa siku zote;
'Serikali sikivu, basi, achunguzwe na ikidhihirika ni kweli apigwe chini mazima.
Nasema achunguzwe sababu wakikurupuka wakati mwingine watu wana maugomvi yao wakataka kuharibiana.

Nawasilisha.
Tayari anavisasi na tulioongea
 
Wakuu sijawahi kukutana na mtu mkorofi mtata na mwenye visasi kiasi hiki. Biashara imekuwa ngumu sana mpaka nawaza kuifunga tu asije akanipeleka jela bure maana amepania kupeleka jela wafanyabiashara 6.

Wakuu miezi kadhaa nyuma maduka yote Handeni mjini tuligoma kufungua mpaka mkuu wa wilaya alipokuja kusuluhisha.

Maana huyu Manager amekuwa akipiga faini za hovyo na mgumu sana kumsikiliza mtu. Mtu unakuta anapitia tatizo la kawaida kama mashine kuzingua ndani ya siku hiyo hiyo au siku moja tu tayari hakuelewi. Imekuwa ni kukomoana na amepania hilo zaidi baada ya ule mgomo na yeye kubakishwa bado.

Sasa jana ofisini kwake aliwatishia wafanyakazi wa chini yake kupunguza kiasi cha mshahara na mlinzi mmoja kupoteza mafao akijinasibu uwezo anao. Kosa ni mfanyakazi mmoja kutoka kwa haraka ni mdada nahisi ni shida za kiafya alienda msalani akachukua muda. Anaelezwa amepata shida kiafya kaenda msalani haelewi anaona anadanganywa. Aisee

Sijawahi kukuta ofisi ina manager wa staili hii aisee

Dar es salaam nimeingia ofisi kadhaa za TRA nimehudumiwa vyema sana lakini hapa Handeni tunakomolewa. Sijui tufanyeje ahamishwe maana baada ya ule mgomo wote tulioongea vimbelembele tuna kimbembe.
Sidhani kama ana mamlaka kisheria ya kuwafanyia lolote. Anaweza akawabambikia tuhuma za uongo za kutolipa Kodi, ila masuala hayo hayaishii kienyeji kama anavyotaka na kwa bahati mbaya naona kama nanyi mnaingia katika mtego wake. Mna wanasheria? Je mnalipa kodi? Hairuhusiwi hata kuwafungia biashara zenu! Nchi hii imezidi matamko ya mtu, sheria zinadharauliwa!
 
Ktk mkoa wa Tanga Handeni nasikia na Pangani mzunguko wa Hela uko chini sana.
Korogwe na Mheza ni sababu ya kuwa kwenye main road junction.
Rushoto wana Neema tu labda tuseme hivyo.
Handeni labda itakapoisha barabara hiyo ya Kilindi Songe Singida yamkini.
Ni nini unachojaribu kutueleza? Na kwa usahihi ni Muheza na Lushoto.
 
Kama unabisha njoo ufungue biashara.
Nina biashara Dar na handeni na pia nasimamia biashara kadhaa za familia.

Njoo handeni . Mashine izingue siku hiyo hiyo upigwe faini siku hiyo hiyo kama ni haki.

Lingine jirani alikosa bidhaa flani akaja kuchukua kwangu yaani kaniazima baadae akileta mzigo anirudishie bidhaa . Hivyo aliyetoa risiti kwa mreja ni jirani . Walivyokuta hilo tunamweleza aawapi tumepigwa faini.
Duuh . Dar hizi changamoto hakuna kabisa na sijawahi kukutana nazo
Kwanini sasa

Tena nikisimamia biashara kubwa kuliko sasa.

Ishu ya watendaji wenzie ni kweli . Ubabe ubabe
Ndugu yetu, jirani kapelea bidhaa, je kachukua au kanunua kutoka kwako? Wewe hutaki kufanya biashara? Si unamuuzia halafu akipata mzigo wake, na wewe kama unauhitaji unanunua kutoka kwake? Vitu vingine tuache kufanya kienyeji.
 
Nyie si ndio tunawategemea kwa uchawi huko mpaka tunakujaga kununua sasa vipi mnalalamika tena kwa case ndogo kama hii, vipi mabusha yameisha stoo?
 
Handeni si ndio jirani na Kwamsisi? Mna feli wapi?
 
Rudia Tena kusoma mtiririko mzima Halafu niambie ambapo hujaelewa
 
Duuh pole.
Nafikiria mzunguko wa Pesa ulivyo chini huko Handeni kwenyewe Halafu upigwe adhabu ya shillingi 1,500,000/- sipati picha.
Chanika mzunguko wa Hela ni Mdogo sana.
mimi nishauri tu ama unastahili kutoa risiti wewe toa tu halafu tuone kama watakuja na sababu nyingine kuliko kutukutoa maana nao wanafata sheria na wasipofanya hivo nadhani kuna sehemu wanapimwa kama sikosei CAG.
 
Ndugu yetu, jirani kapelea bidhaa, je kachukua au kanunua kutoka kwako? Wewe hutaki kufanya biashara? Si unamuuzia halafu akipata mzigo wake, na wewe kama unauhitaji unanunua kutoka kwake? Vitu vingine tuache kufanya kienyeji.
Wewe kichwa maji kweli , sasa hapo kuna tofauti gani sasa watu wa ofisini kwenye mambo ya biashara sio lazima mchangie .

Mimi nimuuzie mteja wa jirani yangu kwa huyo mteja kukosa kitu kimoja tu kati ya vingi alivyonunua kwa jirani na jirani akubali utengenezeke ukaribu kati yangu mimi na huyo mteja. Si ndio nitamwiba. Wafanyabiashara tuliokiushindani hatuwezi kuruhusu mteja kufika kwenye biashara ya mpinzani hiyo nafasi tunaiminya kwa kila namna.

Dar hiyo ipo sana na hamna tatizo
 
mimi nishauri tu ama unastahili kutoa risiti wewe toa tu halafu tuone kama watakuja na sababu nyingine kuliko kutukutoa maana nao wanafata sheria na wasipofanya hivo nadhani kuna sehemu wanapimwa kama sikosei CAG.
Mashine mbovu na kadhibitisha hilo . Sasa nawezaje kusema mbovu bila ushahidi
 
Kama unatumia mashine utajua kuna wakati inazingua , na unakuta labda ni leo tu hujatoa risiti imegoma , namna ambayo kwa wale waelewa wanakuelewa inaenda kurekebishwa unaruhusiwa kutumia ya mkono . Sasa mtu mpaka jana yake ulitoa risiti fresh ni siku hiyo tu uliyokutwa ndio mashine iliharibika hakuelewi faini 1500000 hivi tutatoboa kweli.
1,500,000 ?? per day aise
 
Back
Top Bottom