Mamluki washindwa kupenya uchaguzi wa ndani CCM

Mamluki washindwa kupenya uchaguzi wa ndani CCM

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
21,178
Reaction score
37,475
Uchaguzi wa ndani wa CCM umewaweka kando wagombea wote waliotoka upinzani.

Wagombea wote waliounga mkono juhudi wamejikuta wakishindwa kupenya katika chujio la uchaguzi wa ndani wa CCM na kubandikwa majina ya jebehi kama wakuja, mamluki na nk.

Uchaguzi wa wenyeviti unatarajiwa kufanyika mwezi November 2019.

Kwa hakika wale wote waliounga mkono juhudi wamejikuta wakishindwa vibaya na kuonekana kituko.
 
Kama ni kweli chama kubwa mnastaili pongezi
Wasipenye hata kwenye ubunge wasije kuwasaliti huko mbeleni. Hawaaminiki hao

Kumbukeni, the one who tells something about me is the very one who tells me everything about you.
Sasa hapo ni kanyaga kanyaga kanyaga kanyaga in platinum's voice
 
Tutajie majina yao na wanapatikana mitaa gani

Walitangaza lini kuunga juhudi?
 
Kuna mzee aliwahi kuwa mwenyekiti wa wilaya chadema..kachukua fomu kugombea uenyekiti wa kitongoji ile anafika ofisini wakafunga na kumwambia umechelewa...
 
CCM ya sasa imerudi kwenye ubora wake kama ile ya Mzee Yusufu Makamba...

Kila mgombea ametoa rushwa tofauti ni Kiwango.

Kwa hiyo kuwa ccm inapambana na rushwa ni Hadaa ya Magufuli kwa wananchi wanyonge?
 
Kwa hiyo kuwa ccm inapambana na rushwa ni Hadaa ya Magufuli kwa wananchi wanyonge?
Maneno ya Katibu Mkuu kuhusu Uchaguzi Mkoa wa Dar yanathibitisha hilo, hapo ni Dar serikali yote ipo hapo.

Je huku Nakaguruwe, Nakapanya,Namtumbo hadi Ileje nani emeona figisu zake.
 
Kwani mwenyekiti si anapambana na rushwa? Imekuwaje tena?
Mzee Warioba alisema Mapambano ya Rushwa yanachagua baadhi ya kada....

Mwenyekiti anapambana na Rushwa ile anayoiona yeye, Ukimwonyesha wewe anaipotezea au unaitwa kuhojiwa umejuaje.

Sifa zote zimwendee yeye binafsi
 
Back
Top Bottom