Mamlaka ya Mahakama Kifedha (Pecuniary Jurisdiction)

Apr 26, 2022
64
97
Imeandaliwa na kuletwa kwako na Zakaria (lawyer by profession).

Leo napenda tujifunze “Pecuniary Jurisdiction” 💸 ya Mahakama mbalimbali nchini Tanzania. 🇹🇿

Awali ya yote, tufahamu nini maana ya Pecuniary Jurisdiction? Haya ni mamlaka au mipaka ya Mahakama katika kusikiliza na kuamua kesi, kwa kuzingatia kiwango au kiasi cha fedha au thamani ya kitu.

Kuna mipaka ya kiasi/kiwango cha fedha kwa kila Mahakama. (Hivyo, kabla hujafungua kesi ni muhimu ujue thamani ya madai yako ili ujue unatakiwa kwenda Mahakama ipi).

Nitaelezea Pecuniary Jurisdiction kuanzia Mahakama ya Mwanzo (Primary Court), kisha Mahakama ya Wilaya (District Court), Mahakama ya Hakimu Mkazi (Court of a resident magistrate) na mwisho nitamalizia na Mahakama Kuu (High Court).

1: PECUNIARY JURISDICTION OF THE PRIMARY COURT (MAHAKAMA YA MWANZO):

The pecuniary jurisdiction of the Primary Court in respect of civil suits is specifically provided under section 18(1)(a)(ii) and (iii) of the Magistrates’ Courts Act [CAP. 11 R.E. 2019] hereinafter referred to in short as MCA, which is Tshs. 50,000,000/= (fifty millions) for Immovable properties and Tshs. 30,000,000/= (thirty millions) for movable properties.

Ukomo wa mamlaka ya Mahakama ya Mwanzo katika kesi za madai ni shilingi 50,000,000/= (Milioni Hamsini) kwa mali isiyohamishika na shilingi 30,000,000/= (milioni thelathini) kwa mali inayohamishika.

2: PECUNIARY JURISDICTION OF THE DISTRICT COURT AND RESIDENT MAGISTRATES COURT (MAHAKAMA YA WILAYA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI):

(Ikumbukwe kwamba Mahakama hizi mbili zina Mamlaka sawa/Concurrent Jurisdiction).

The pecuniary jurisdiction of the District Courts and Courts of Resident Magistrates in civil cases (for non commercial matters) is Tshs. 300,000,000/= (three hundred millions for immovable property and 200,000,000/= (two hundred millions for movable property).

Mahakama ya Wilaya na Mahakama ya Hakimu Mkazi zina Mamlaka ya kusikiliza kesi za madai (yasiyo ya kibiashara) yasiyozidi shilingi 300,000,000/= (milioni mia tatu) kwa mali isiyohamishika na shilingi 200,000,000/= (milioni mia mbili) kwa mali inayohamishika). Section 40(2)(a) & (b) and section 41(1) of the MCA.

However, in COMMERCIAL CASES the pecuniary jurisdiction of the District Courts and Courts of Resident Magistrates is TSh. 100,000,000 (one hundred million shillings) for immovable property & TSh 70,000,000 (seventy million shillings) for movable property.

Mahakama ya Wilaya na Mahakama ya Hakimu Mkazi zina Mamlaka ya kusikiliza kesi za madai ya KIBIASHARA yasiyozidi shilingi 100,000,000/= (milioni mia moja) kwa mali isiyohamishika na shilingi 70,000,000/= (milioni sabini) kwa mali inayohamishika. Section 40(3)(a) & (b) of the MCA.

-Also, they have pecuniary jurisdiction in administration of small estates, which does not exceed TSh. 100,000,000 (one hundred million shillings). Kwa kiswahili, Mahakama ya wilaya na Mahakama ya Hakimu Mkazi, zina Mamlaka ya kusikiliza shauri la mirathi lisilozidi shilingi 100,000,000 (milioni mia moja). As per Section 6 & 2 of the Probate and Administration of Estates Act, CAP 352.

His Lordship (Jaji) Mlyambina J., yeye anakwambia, “current value of a small estate is an asset or assets whose total value do not exceed TZS 300,000,000.” Make reference to Beatrice Brighton Kamanga & Amanda v Ziada William Kamanga, Civil Revision No. 13, 2020, page 11. (My efforts to search for the amendments in respect of that position, ended in vain).

3: PECUNIARY JURISDICTION OF THE HIGH COURT (MAHAKAMA KUU):

Jurisdiction of the High Court starts immediately where there is no other court specified or immediately after the maximum pecuniary limits of the district and resident magistrates’ courts. (Pecuniary jurisdiction ya Mahakama Kuu, huanzia pale Mahakama za chini zinapoishia).

In light of Article 108(2) of the Constitution of Tanzania and the provision of section 2(1) of the Judicature and Application of Laws Act [CAP. 358 R.E. 2019], the High Court is vested with UNLIMITED Jurisdiction over all civil and criminal matters. It has power over any matter not even expressly provided for by the law.

Mahakama Kuu imepewa mamlaka yasiyo na mipaka kwenye kesi za jinai na madai. Ina mamlaka ya kusikiliza kesi zote ambazo ziko nje ya Mamlaka ya Mahakama za chini yake na pia ina mamlaka ya kusikiliza masuala yote ambayo hata sheria haijatamka wazi yapelekwe Mahakama ipi.

Therefore, the High Court’s Pecuniary jurisdition is on those matters that are outside the pecuniary jurisdiction of the courts subordinate to it.

Hivyo, tunaweza kusema kwamba, (minimum) Pecuniary jurisdiction/limit ya Mahakama Kuu ni pale kinapoishia kiwango cha Mahakama za chini yake (mfano kiwango cha mwisho cha Mahakama ya Wilaya na Mahakama ya Hakimu Mkazi ndipo kiwango cha Mahakama Kuu kinapoanzia).

Kwa lugha rahisi, Pecuniary jurisdiction ya Mahakama Kuu ni UNLIMITED/haina ukomo.

MWISHO.

Zingatia maelezo haya ni kwa mujibu wa sheria zilizokuwa zinatumika mpaka siku ya kupost hili andiko. (Hivyo unaposoma leo andiko hili soma na marekebisho ya sheria yaliyopo sasa hivi)

Imeandaliwa na kuletwa kwako na Zakaria . 0754575246 (WhatsApp).
 

Ofisi Nje Kama Watu Wanakula Raha, Kumbe Oops

Yaliyomo Yamo

 
Back
Top Bottom